Kigogo Mwingine wa CCM Arusha amfuata Millya Chadema

M4C
Mwenye macho haambiwi tazama!
Mtu yeyote atakayejigamba mbele za watu wenye upeo wa kufikiri kuwa yeye ni mwanachama wa chama cha mapinduzi atakuwa na roho ngumu sana kipindi hiki
 
hapa ni tume switch on bluetooth, wanatutafta wenyewe, we are expecting more makini people from magambaz territory.....
Viva M4C

Nakubaliana na wewe, kwamba wale MAKINI ndio tuwachukue. Ila nina wasiwasi sana kuwapata watu makini kutoka CCM kweli? Yan wangekua makini wangesubiri mpaka wasutwe ndiyo wakimbie? Hawa mi nashauri wasipewe cheo chochote hadi baadae ya kukaa chamani kwa muda wa miaka 5, unaweza kukuta ni wafuata upepo na wameshagundua ccm inafika mwisho sasa wanataka kutafuta mahala pa kupitia kushika uongozi. TUWE MAKINI SANA NA HAWA VICHWA MAJI WANAOHAMIA CDM, WASIJE WAKALETA MTAFARUKU KWENYE CHAMA MAKINI (CDM). TUUTUMIE UMAKINI WETU KUWAPA PROBATION PERIOD YA MIAKA 5 (MILIMWONA SHIBUDA ALITAKA KUHARIBU CHAMA, KAMA SIYO UMAKINI WA VIONGOZI WA CDM, TUSINGEKUA HAPA LEO)
 
Maneno kuntu mkuu wangu....
 
More 2 come stay tune, CDM is the better home!Unganisha nguvu kwa ukombozi wa Nchi yetu
 
Hadi mwaka uishe.....mengi yatasikika na kuonwa....ccm byeeeeeeeeeeeeeeeee..................
 
kama kawa wengine mnasubiri nini . wenzenu wamenasa dume nyie mnanasa galasa poleni sana
au mnasubiri hongo mmalizie ujenzi ambao haukukamilika 2010. mambo ya uchaguzi 2015 ni tofauti sana. ccm hata wahonge vipi hawapiti kutokana na msukumo uliopo sasa
Jinamizi la viongozi na Chama cha Mapinduzi (CCM) la kukihama chama hicho limeendelea kushika kasi, baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha, Justine Genda, naye kutangaza kukihamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Genda ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Karatu Mjini, alitangaza uamuzi huo jana wilayani Karatu na tayari ameshapokelewa na viongozi wa Chadema katika hafla iliyohudhuriwa na Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Karatu Titus Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Thomas Darabe.

Genda alisema ameamua kujiunga na wanaharakati wa kupigania haki na kuleta mabadiliko na kuongeza kuwa kwa sasa fursa hiyo inapatikana Chadema.

"Nimeamua kuhama CCM na kujiunga na Chadema na nina matumaini makubwa kwani nimeona kuwa Chadema kuna fursa ya kumuwezesha kila mmoja kutoa mchango wake katika mchakato mzima wa mabadiliko na ni chama kinachoweza kuleta ukombozi wa kweli katika taifa," alisema Genda.

Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi ya Chadema mwanachama huyo, Lazaro aliwataka wanachama na viongozi zaidi wa CCM na vyama vingine wanaotaka mabadiliko ya kweli kujiunga na Chadema kwani ni chama makini.

Wakati huo huo huko Ruvuma nako Katibu wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Jimbo la Songea mkoani Ruvuma, Joseph Mkondora, amejiengua katika chama hicho na kujiunga na Chadema ambacho alisema ni chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dira ya maendeleo kwa Watanzania.

SOURCE:NIPASHE JUMATATU
 
Movement for change (wireless connection) mpaka Songea!

Nimeipenda sana hyo. Popote inakamata.

Ndugu zangu hawa jamaa wakatae wakubali, sasa wananyolewa kwa wembe!
Mikutano inafanywa kanda ya ziwa then pande mabalimbali za nchi tunaskia watu wakijiunga na CHADEMA!
Kweli hamia wewe, mjomba, shangazi na ndugu zako wote!
 
Back
Top Bottom