Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jinamizi la viongozi na Chama cha Mapinduzi (CCM) la kukihama chama hicho limeendelea kushika kasi, baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha, Justine Genda, naye kutangaza kukihamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Genda ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Karatu Mjini, alitangaza uamuzi huo jana wilayani Karatu na tayari ameshapokelewa na viongozi wa Chadema katika hafla iliyohudhuriwa na Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Karatu Titus Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Thomas Darabe.
Genda alisema ameamua kujiunga na wanaharakati wa kupigania haki na kuleta mabadiliko na kuongeza kuwa kwa sasa fursa hiyo inapatikana Chadema.
Nimeamua kuhama CCM na kujiunga na Chadema na nina matumaini makubwa kwani nimeona kuwa Chadema kuna fursa ya kumuwezesha kila mmoja kutoa mchango wake katika mchakato mzima wa mabadiliko na ni chama kinachoweza kuleta ukombozi wa kweli katika taifa, alisema Genda.
Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi ya Chadema mwanachama huyo, Lazaro aliwataka wanachama na viongozi zaidi wa CCM na vyama vingine wanaotaka mabadiliko ya kweli kujiunga na Chadema kwani ni chama makini.
Wakati huo huo huko Ruvuma nako Katibu wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Jimbo la Songea mkoani Ruvuma, Joseph Mkondora, amejiengua katika chama hicho na kujiunga na Chadema ambacho alisema ni chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dira ya maendeleo kwa Watanzania.
SOURCE:NIPASHE JUMATATU
Ha ha ha haaaaaaaa waacheni wafu wawazike wafu wenzao, hata mjumbe wa mkutano nae ni kigogo? kweli magwanda mnapenda sifa za kipuuzi.
masharti na vigezo kuzingatiwa!!!
CDM ni digitali, ikifikia tarehe 31 Decemba 2012 tunazima mitambo yote ya analogia, kama bado uko huko huwezi tena kutoka. Sumaye aliwahi kuimba bungeni kuwa mambo iko huku, akimaanisha kuwa ukitaka kukwepa kodi uhamie huko analogia, ukitaka kudhulumu mali ya umma uhamie huko analogia. Mimi namwambia watakaodumu huku digitali ni wale wasafi, wasiokwepa kodi, wala wasio wazulumati. DIGITALI BABA, USIKIVU MWANGAVU NA PICHA ISIYO NA CHENGA. PATA KING'AMUZI CHAKO LEO.
Jinamizi la viongozi na Chama cha Mapinduzi (CCM) la kukihama chama hicho limeendelea kushika kasi, baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha, Justine Genda, naye kutangaza kukihamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Genda ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Karatu Mjini, alitangaza uamuzi huo jana wilayani Karatu na tayari ameshapokelewa na viongozi wa Chadema katika hafla iliyohudhuriwa na Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Karatu Titus Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Thomas Darabe.
Genda alisema ameamua kujiunga na wanaharakati wa kupigania haki na kuleta mabadiliko na kuongeza kuwa kwa sasa fursa hiyo inapatikana Chadema.
Nimeamua kuhama CCM na kujiunga na Chadema na nina matumaini makubwa kwani nimeona kuwa Chadema kuna fursa ya kumuwezesha kila mmoja kutoa mchango wake katika mchakato mzima wa mabadiliko na ni chama kinachoweza kuleta ukombozi wa kweli katika taifa, alisema Genda.
Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi ya Chadema mwanachama huyo, Lazaro aliwataka wanachama na viongozi zaidi wa CCM na vyama vingine wanaotaka mabadiliko ya kweli kujiunga na Chadema kwani ni chama makini.
Wakati huo huo huko Ruvuma nako Katibu wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Jimbo la Songea mkoani Ruvuma, Joseph Mkondora, amejiengua katika chama hicho na kujiunga na Chadema ambacho alisema ni chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dira ya maendeleo kwa Watanzania.
SOURCE:NIPASHE JUMATATU
Kigogo kwako nadhan na bila shaka ni mme wako tu!Huyu sio kigogo
Pole.Huyu sio kigogo