Kifo kabla ya uzee, ni mpango wa Mungu?

Nakuita mshenzi kwa kudhihaki Nuru na Kweli tuliyoipokea
Alipodhihaki ni wapi? Yani mtu asipoamini unachoamini wewe ni kosa? Mbona wewe huamin anachokisema yeye na hamna aliyekuhukumu na hata hvyo yeye kauliza tu,kama ungekua na jibu siungemjibu au kama hujaelewa ungemuuliza amemaanisha nini kuliko kumuita mshenzi.
 
Kiukweli limtu linatoka huko litokako limetwika mapombe kreti zima,afu linakimbiza gari mpaka speed za kuazima zingine maana speed za gari zimeisha zote,then linakunja kona ghafla na linabilingita kwenye gari mpaka lina R.I.P kisha ukiwa kwenye msiba unasikia watu wanasema ni mapenzi ya MUNGU,na wakati wa mazishi wanasema alazwe pema peponi.mmmmmh!!!
Ilipangwa afe vile. Asingeweza kukwepa
 
kifo kinaweza kusababishwa either na Mungu au shetani
1. Kifo kinachosababishwa na Mungu kinakua wakati wa mtu kukaa duniani umeisha na hapo biblia inasema ni 70years, umeshamtumikia Mungu kwa uaminifu hivyo Mungu anakuchukua ukapumnzike, akuepushe na moto hii ni pale mtu anaokoka Mara aanguke dhambini yaan ndo maisha yake so Mungu anaweza kukuchukua pale upo safi ili akuepushe na dunia maana unashingo ngumu ila still Mungu anakupenda, pia wakati mwingine ni kwaajili ya utukufu wake rejea 2falme4:8+, Yohana11
2. vifo vinavyosababishwa na shetani.mfano unakunywa mipombe unaendesha gari shetani anakufanyia ajali ili ufe akuchukue maana unakufa katika dhambi au unatumiwa jini linakuua.mtu mwenye Yesu maishani mwake hawezi kuuliwa na jini wala shetani
 
na shetani sahv ana speed kweli ya kuua watu ili apate wengi wa kwenda nao motoni, wake up dears
 
Mungu/umungu ni state ambayo haina mwanzo wala mwisho, ipo beyond time au ni timeless, ni ya milele, ni unity, kwa mungu hakuna tofauti kati ya death and birth,ni hali moja, God is limitless, ipo kila mahali, haina umbo/formless,state ambayo ipo kila mahali na ni kila kitu obvious itakuwa desireless.

Mpango/Plan kwa kifupi ni matamanio ya kufikia lengo fulani, mpango uhusisha muda, ili lengo litimie.

Maumbile/creation,duality,universe ni limit yani ya mwanzo na mwisho, yana mipaka na pia ni illusion au maya(siyo ya kweli).

Tukisema mtu akifa huo ni mpango wa mungu, ni hoja zenye mapungufu makubwa kwenye spirituality. Mungu hawezi kuwa na mpango wowote, mungu kuwa na mpango wowote ina eleleza kuwa mungu ana matamanio(desire) ya kuwa au kutaka kitu fulani,so itakuwa haijakamilika. A state we call God ni absolutely,ni perfect,its everything and beyond that.Hali ambayo imekamilika huwa haitendi, haina mpango.
Haya yote ya kuwa Mungu ana mipango yanaletwa na akili,tukumbuke akili ni limits,ina mipaka(kumbuka mungu hana mipaka).
Mind can never know state we call God, how limit know limitless???
Creation/universe daima yapo kwenye motion, yapo kwenye change of state.

Dini na vitabu vyake vina umuhimu wake,ila tukikuza ufahamu wetu itatusaidia pia. To suggest that a series of words(in the book) can contain an ultimate truth or the essence of God is a very sad idea, the absolute freedom of God means nothing can contain God.
 
Yakupasa kufahamu kuwa Mungu ametuumba kwa makusudi yake anayoyajua yeye mwenyewe

Kila binadamu huwa anashughuli ambayo amekuja kuitimiza duniani ambayo kwa akili zetu wanadamu hatuwezi jua hasa hilo kusudi la mungu ni lipi

Hiyo hata mtoto mchanga akifa huwa kunakusudi flani la Mungu limetimia tayari Na kazi iliyomleta duniani ameahaimaliza ndomaana inabidi afe bila kujali ni ajali au magonjwaa

Katika nnchi zilizoendelea vifo ni vichache kwa watoto chini ya miaka 5 kulinganisha na nnchi maskini lakin hii sababu haitoshi kusema kuwa kifo sio mpango wa Mungu kwani hata huko katka nnchi zilizoendelea kuna kilaaina ya kudhibiti uzembe ili watu wasife lakini bado wanakufa tu. Hii inamaanisha mtu hawezi kukikimbia kifo kwakuwa makusudi ya Mungu yameshatimia hana budi kufa tu.

Kifo ni mpango wa Mungu bila kujali uzembe unaosababishwa na wanadamu wengine.
Hahahahaaaa mkuuu naona unazunguka mbuyu tu, hapo hujajibu mkuu
 
Kifo ni mpango wa mungu amini hvyo

Mkuu, hapana si kila kifo ni mpango wa Mungu, Kama kila kifo ni mpango wa Mungu basi kutakuwa na tatizo kubwa sana kwa Mwenyezi Mungu,

Kwanini nasema hivyo, ukiangalia takwimu za vifo vinavyotokea Africa na hata Mashariki ya kati ya vifo ni kubwa sana than Ulaya na Marekani. Kwa mfano kama kwa Africa kila watoto 10 wanaozaliwa 3 au zaidi hufa kwa magonjwa mbalimbali na kwa wenzetu Ulaya na Marekani ni 10 kwa mmoja.

Sasa kwa hapa tuseme Mungu ana upendeleo? Si hivyo tu, hata Muda wa kuishi kwa sisi wa Dunia ya tatu na wenzetu ni tofauti, kwa Africa most wanaokufa ni vijana ila kwa Ulaya na Marekani vifo vingi sana hutokea kwa wazee.

Swali la kizushi, Je kinachoendelea Syria leo hii ni mpango wa Mungu? Manake kila siku watu wanakufa kwa kupigwa Mabomu ya sumu.
 
Hata hii mada ulioandika ni mpango wa Mungu kukufanya ukaandika hadi kumaliza angeamua angechukua pumzi yake kabla hujamaliza kuandika
 
Umeandikaa vyema sana ndugu yangu. Ahsante

Upeo wa mwanadamu unapogota atamhusisha muumba wake na kila jambo. Kuna m/falsafa ages ago aliwahi kusema ukiona jambo linaaminika sana na watu (kwa maana ya uelewa wa jambo husika) ujue ukweli wake ni kinyume ya huo uelewa wa wengi. Maana yangu ni kwamba mambo yengi tunavyoyaelewa ni kinyume sana na ukweli wake. Mimi ninaamini ktk dini na uwepo wa Mwenyezi Mungu lakini tunakosea na ku-perceive vibaya habari nyingi zilizomo katika vitabu. Ningeandika mengi ila mimi mzito kutype ila mwepesi wa 'kusoma'
 
Hata hii mada ulioandika ni mpango wa Mungu kukufanya ukaandika hadi kumaliza angeamua angechukua pumzi yake kabla hujamaliza kuandika

Mkuu, Acha kupotosha watu. Kama utakubali kuwa kifo au mada hii ameanzisha kuwa ni mpango wa Mungu basi pasi na shaka utakuwa unakubali kuwa Mungu anawapendelea sana Wazungu than sisi weusi.

Why nasema hivyo? Takwimu zilizoko Bara la Africa ni kwamba kila baada ya dakika 10 Mtoto hufa kwa Malaria au Mama Mjamzito hufa wakati wa kujifungua ambayo ni tofauti na wenzetu ambao wameendelea sababu wao ni 100 kwa 1.

Mostly vifo vingi vya Africa huwa vinatokea kwa vijana na watoto than watu wazima ambayo ni differ na wenzetu ambao vifo vingi kwao vitokeavyo ni kwa wazee than vijana na watoto.

Vifo vingi vitokeavyo Africa ni kutokana na uzembe wetu wenyewe na sio mpango wa Mungu.

Hebu fikiria, Mtu keshamaliza muda wake ila anang'ang'ania madaraka na watu wamapigana to death, hivi huo nao utasema mpango wa Mungu?

Mtu anaumwa, hospital ni kilometa 50 toka alipo akifia njiani utasema huo nao ni mpango wa Mungu?

Au kile ambacho sasa hivi kinatokea Syria utasema ni mpango wa Mungu?

Hapana, Naomba Mungu tumpe Heshima yake, sio kila jambo basi tumsingizie yeye.
 
Upeo wa mwanadamu unapogota atamhusisha muumba wake na kila jambo. Kuna m/falsafa ages ago aliwahi kusema ukiona jambo linaaminika sana na watu (kwa maana ya uelewa wa jambo husika) ujue ukweli wake ni kinyume ya huo uelewa wa wengi. Maana yangu ni kwamba mambo yengi tunavyoyaelewa ni kinyume sana na ukweli wake. Mimi ninaamini ktk dini na uwepo wa Mwenyezi Mungu lakini tunakosea na ku-perceive vibaya habari nyingi zilizomo katika vitabu. Ningeandika mengi ila mimi mzito kutype ila mwepesi wa 'kusoma'
Asante ndugu hata kwa huo uzito wako wa kutype tumepata point yako
 
Mkuu, Acha kupotosha watu. Kama utakubali kuwa kifo au mada hii ameanzisha kuwa ni mpango wa Mungu basi pasi na shaka utakuwa unakubali kuwa Mungu anawapendelea sana Wazungu than sisi weusi.

Why nasema hivyo? Takwimu zilizoko Bara la Africa ni kwamba kila baada ya dakika 10 Mtoto hufa kwa Malaria au Mama Mjamzito hufa wakati wa kujifungua ambayo ni tofauti na wenzetu ambao wameendelea sababu wao ni 100 kwa 1.

Mostly vifo vingi vya Africa huwa vinatokea kwa vijana na watoto than watu wazima ambayo ni differ na wenzetu ambao vifo vingi kwao vitokeavyo ni kwa wazee than vijana na watoto.

Vifo vingi vitokeavyo Africa ni kutokana na uzembe wetu wenyewe na sio mpango wa Mungu.

Hebu fikiria, Mtu keshamaliza muda wake ila anang'ang'ania madaraka na watu wamapigana to death, hivi huo nao utasema mpango wa Mungu?

Mtu anaumwa, hospital ni kilometa 50 toka alipo akifia njiani utasema huo nao ni mpango wa Mungu?

Au kile ambacho sasa hivi kinatokea Syria utasema ni mpango wa Mungu?

Hapana, Naomba Mungu tumpe Heshima yake, sio kila jambo basi tumsingizie yeye.
Hata hii reply yako ni mpango wa Mungu kuna ambae anatamani ajibu hivi ila Mungu hakupenda
 
Hata hii reply yako ni mpango wa Mungu kuna ambae anatamani ajibu hivi ila Mungu hakupenda

Ujinga ni kuamini hata ukijichoma kisu/ukinywa sumu na kufa ni mpango wa Mungu.

Shirikisha ubongo wako tafadhari, Ipo siku waweza sema Wizi na Ujambazi ni Mpango wa Mungu. (kidding)
 
Ujinga ni kuamini hata ukijichoma kisu/ukinywa sumu na kufa ni mpango wa Mungu.

Shirikisha ubongo wako tafadhari, Ipo siku waweza sema Wizi na Ujambazi ni Mpango wa Mungu. (kidding)
Hata hii kujiona we unajua sana na unaushirikisha bongo kuliko Mimi pia ni mpango wa Mungu! Kila kinachotokea ni mpango wa Mungu! Hiyo hutokea ili ujifunze!!! Dereva akilewa ma kupata ajali ni mpango wa Mungu ujifunze kua kuna madhara ukilewa na kuendesha gari
 
Acheni masikhara hakuna uzembe... Huo uzembe kausababisha Mungu yani hata jani likidondoka mtini ni kazi ya Mungu.. Every thing is planned from our Lord.. Kila kitu kiko controlled na yeye ni mjuzi anajua afanyalo..
 
Kifo au kufa ni Asili ya Ulimwengu huu ,mimea /miamba/nyota kila kitu kinakufa .Tofauti ni muda tu hichi kinaishi miaka kadhaa na kile kinaishi miaka kadha.Hii habari ya Mungu ni kumsingizia tu sababu baadhi ya vifo vingine husababishwa na Watu wenyewe kwa 'uzembe' kwa 'ujinga' kwa 'upumbavu' pia kwa makusudi.Dhana ya kumhusisha Mungu inakuja tu kama njia ya kumfariji Mtu,tutaendelea kuuwana kwa sababu tulizo zitaja kama bado tutaendelea kuwa na mawazo mgando ya kumsingizia Mungu hata kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu..

Watu wote na vyote vinavyo kufa zipo sababu au chanzo..Ninge pendelea tudili na vyanzo na sio matokeo..
 
naomba kuanzia sasa wote waliosema ni mpango wa Mungu ktk case zisizomhusu Mungu muanze kutubu. pili ukisoma muwe munaelewa TULIPEWA MAMLAKA YA KUTAWALA, sasa kutawa ni kuwa in total control of the universe ambapo katika kuhakikisha hali inakua hivyo yanatokea hayo kama magongwa, kifo n.k ambayo mengi yanasababishwa na human SPIRIT
Tatu elewa kwamba kuna God Spirit, satan spirit and humani spirit that always lead the world, but the two God Spirit, satan spirit do operate kwa kutumia human spirit kwa kadri ya nguvu mwanadamu anayoiruhusu kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom