Kifo kabla ya uzee, ni mpango wa Mungu?

Naona hili neno limekuwa likitumika sana katika kutoa faraja kwa watu, utasikia mtu anamwambia mwenzake, "Pole sanaa ni mipango ya Mungu" ikiwa ni njia ya kumfanya mtu aone hilo jambo ni la kawaida na ni mipango ya Mungu mtu huyo kufa.

Siamini kwamba kila kifo ni mpango wa Mungu.

Imani yangu ni kwamba Mungu katuumba tuishi na tuzeeke tufe.

Mifano ya watu wote walioishi katika njia za Mwenyezi mungu kwenye vitabu vitakatifu inaniambia walizaliwa wakaishi wakazeeka wakafariki wakiwa wenye umri wa kutoendelea kuishi tena. Vifo vya namna hiyo hata mimi naamini ndio mpango wa Mungu.

Mtoto wa miaka minne, ameugua maralia, wazazi wamechelewa kumpeleka hospital au amepelekwa madakatar wakakosea katika vipimo akafa, watu wanasema ni mpango wa Mungu.

Juzi ajali ile ya mabasi ya city boys, dereva badala ya kuendesha kwenye njia yake, kapita njia ya mwenzake watu 42 wakafa tunasema ni mpango wa Mungu kwamba alipanga watu wale 42 wafe siku hiyo.

Unajenga nyumba kizembe zembe mtu anakaa anaangukiwa na ule ukuta unasema ni Mpango wa Mungu.

Nilikuwa naangalia records za vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa upande wa marekani na Tanzania, nikazifanyia comparison, Marekani wana idadi ndogo sanaaaa ya watoto wanaokufa chini ya miaka 5 wakati Tanzania idadi hiyo ni kubwa sana, kwanini? Marekani uangalizi wa watoto wadogo ni mkubwa sana na hata matibabu yake ni ya uhakika wakati Tanzania uangalizi kwa watoto wadogo na matibabu yake ni ya kubahatisha. Je vifo vya hawa watoto ni mpango wa Mungu?

Hivyo hivyo ukiangalia hata hapa kwetu, vifo vya watoto wadogo Masaki na vifo vya watoto wadogo Mbagala utaona kuna ratio ya 1:10 au zaidi ya hapo, Je ni mpango wa Mungu kwamba watoto wengi wafe Mbagala na sio Masaki?

Unaendesha bodaboda kwa speed unaanguka unakufa unasema ni mpango wa Mungu, Mtu katoka huko anaendesha gari lake bila kuwa makini anamgonga raia mwema aliyesimama pembezoni mwa barabara tunasema ni mpango wa Mungu,

Hapana, huo sio mpango wa Mungu, Ni mpango wa binadamu.

Hata katika biblia na Qur'aan ukisoma kama kuna kifo ambacho kilitokea kabla mtu hajazeeka basi fuatilia kuna UZEMBE aliufanya mahali fulani au yeye au wazazi wake wakapelekea akafa.

Kwa kusema hayo, ni imani yangu na ninaomba niwashawishi kwambaa, vifo kabla ya uzee vinaepukika, kutokana na mazingira, kulinda afya yako, namna unavyoishi na watu unaweza kuepuka vifo ambavyo sio mpango wa Mungu.
 
ulichozungumza ni kweli kabsa watu wengi hawafikirii kuhusu hilo,mungu anatupenda saba waja wake tuishi kumtumikia katika maisha ya kiroho
 
Una maana gani mkuu
Kama wewe ni Mkristo na unaiamini Biblia acha nijaribu kukuonyesha imani yangu kwa ishu ya kifo, ni hivi:
Kitabu cha kwanza katika Biblia kinaeleza kwamba Mungu alimuumba mtu wa kwanza, Adamu, na kumpa makao katika paradiso. (Mwanzo 2:7, 15) Baada ya kuumbwa, Adamu alipewa kazi, na vilevile sheria iliyomkataza katakata asile matunda ya mti fulani katika bustani ya Edeni. Mungu alimwambia hivi kuhusu matunda ya mti huo: “Usile, kwa maana siku utakapokula, utakufa hakika.”* (Mwanzo 2:17) Kwa hiyo, Adamu alielewa kwamba angeweza kuepuka kifo. Angekufa tu kama angevunja sheria ya Mungu.

Inahuzunisha kwamba Adamu na mkewe Hawa hawakutii. Waliamua kupuuza mapenzi ya Muumba wao, nao wakapatwa na matokeo mabaya ya uamuzi wao. Alipotaja matokeo ya dhambi hiyo Mungu alisema hivi: “Wewe ni mavumbi nawe utarudi mavumbini.” (Mwanzo 3:19) Walitiwa dosari kubwa, yaani, kutokamilika. Wangekufa kwa sababu ya kutokamilika au dhambi.

Wazao wa Adamu na Hawa, yaani wanadamu wote, walirithi dosari hiyo ya dhambi. Kwa hiyo, dhambi inaweza kulinganishwa na ugonjwa unaorithiwa. Adamu alipoteza taraja la kuishi milele bila kufa, na wazao wake walirithi kutokamilika kutoka kwake. Wanadamu wakaja kuwa watumwa wa dhambi. Biblia inasema hivi: “Hiyo ndiyo sababu, kama vile kupitia mtu mmoja dhambi iliingia katika ulimwengu na kifo kupitia dhambi, na hivyo kifo kikaenea kwa watu wote kwa sababu wote walikuwa wamefanya dhambi.”—Waroma 5:12.
 
Kuna kitu ambacho ni vigumu kukielewa sana na ndio maana ALLAH kuna baadhi ya Aya anasema "kuna mazingatio kwa wenye akili" kwani maneno ya ALLAH ni mazito na hayana mapungufu.Kuna aya ALLAH kasema "kila nafsi itaonja umauti" kuielewa aya hii vizuri ni vigumu kama sio GENIUS,kuna watu wanafikiri kwamba mwili wa mtu ukiteketea kwa njia yeyote basi roho ya huyo mtu inaenda moja kwamoja kwa ALLAH.Nafsi haihusiani na umbo la kiumbe hii inamaanisha kwamba hata kama umbile la kiumbe limeteketea lote kiumbe huyo ataendelea kuishi kama nafsi mpaka mda wake wa kuishi hapa duniani uishe ndio roho yake sasa inapaa inaelekea mbinguni kwa ALLAH.
Rejea kwenye maswala ya ushirikina unaohusu misukule utaelewa ninachomaanisha,mwili unaweza kuchukuliwa kwa nguvu za giza au kishirikina tena ukaliwa nyama mpaka mifupa lakini roho ya mwili husika Ikaendelea kuishi duniani ikisubiri mda wake uishe na ukiisha tu roho inaelekea kwa ALLAH.Wanachokifanya wanga na wachawi ni kuuchukua mwili tu kama wakiwa na nia ya kuutumikisha kama msukule basi roho ikiurudia mwili itakua inarudi katika mwili ule ule ambao uko katika miliki ya wachawi ambapo unatumikishwa katika shughuli zao.Lakini kama mwili ukiliwa nyama na mifupa mpaka ukaisha basi roho itaendelea kuishi bila ya mwili ikisuburi mda wake ufike ndio ipande juu kwenda mbinguni kwa ALLAH.Wachawi hawana uwezo wa kumiliki wala kuichukua roho wanachochukua ni mwili tu so kinachofanya roho kuufata mwili uliochukuliwa na mchawi ni mkataba maalumu uliopo kati ya mwili na roho ambao hakuna mchawi anaweza kuufupisha wala kuurefusha.Ndio mana wachawi wanaotumia mandondocha au misukule kuna wakati inawalazimu kufanya usajiri mpya wa misukule kwani mkataba wa roho kuitumikia ile miili waliyoichukua imeshakwisha so haiwezi kufanya kazi tena kwani roho zake zimesharudi kwa ALLAH baada ya mda wao kufika.
Kuna mkataba maalumu kati ya roho na mwili kuishi pamoja na mwili ndio unatamani kuishi na roho milele lakini roho ikiitwa tu na ALLAH inaitika na hakuna kubisha,kuhoji wala kukimbia.Ndio maana kuna watu wanalala mapema ili kesho waamke waende kwenye mipango yao ya kimaisha lakini wengine hawaamki wanakufa.Hii ikitokea inamaanisha kwamba mtakaba kati ya roho na mwili umeshakwisha na ile mipango ilikua kwaajiri ya mwili tu.Kwahiyo kifo chochote ni mpango wa mungu(ALLAH) kwani kifo ni cha roho na ndio maana hata wale wanaokausha maiti na kuzihifadhi zile maiti hazifanyi kazi kwasababu kinachoishi milele ni roho tu
NB;kuna tofuti ya kufa na kupotea kimazingala pia roho inaweza kuendelea kuishi duniani bila ya mwili mpaka mda wake uliopangiwa na mungu(ALLAH) uishe

QURAN
39:42 "MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri".
21:23 Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo.
56:83 Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,
56:84Na nyinyi wakati huo mnatazama!
56:85 Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.
56:86 Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
56:87 Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
70:4 Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!

Ulichokiwaza wewe ni njia za kufa lakin haijalishi umekufaje ikitoka ROHO tu huitwa KIFO hata kama UTAJIUA[wewe mwenyewe kwa njia uipendayo],UTAULIWA[Na kiumbe chengine] AU UTAKUFA[kwa ugonjwa,ajal au bila tatzo lolote].Main point ni ROHO kutengana na MWILI na kuwa kule KIFO HAKINA SABABU MAALUMU.

N:B
Kama isingekua mpango wa MUUMBA Basi roho zingekuwa na SPARE au RECYCLE kwa wanaouliwa au kujiua.
 
Sikuumba Majini na Watu ila Wapate kuniabudu.

Naishi vizuri tu na Majirani halafu nalogwa Natupiwa Jini na mtu mwenye Husda kisha Nafariki.
Je hapo pia nimefanya Uzembe upi Kwa mujibu wa Biblia??

Ama kweli watu wangu Wanaangamia kwa kukosa Maarifa..
 
Kama wewe ni Mkristo na unaiamini Biblia acha nijaribu kukuonyesha imani yangu kwa ishu ya kifo, ni hivi:
Kitabu cha kwanza katika Biblia kinaeleza kwamba Mungu alimuumba mtu wa kwanza, Adamu, na kumpa makao katika paradiso. (Mwanzo 2:7, 15) Baada ya kuumbwa, Adamu alipewa kazi, na vilevile sheria iliyomkataza katakata asile matunda ya mti fulani katika bustani ya Edeni. Mungu alimwambia hivi kuhusu matunda ya mti huo: “Usile, kwa maana siku utakapokula, utakufa hakika.”* (Mwanzo 2:17) Kwa hiyo, Adamu alielewa kwamba angeweza kuepuka kifo. Angekufa tu kama angevunja sheria ya Mungu.

Inahuzunisha kwamba Adamu na mkewe Hawa hawakutii. Waliamua kupuuza mapenzi ya Muumba wao, nao wakapatwa na matokeo mabaya ya uamuzi wao. Alipotaja matokeo ya dhambi hiyo Mungu alisema hivi: “Wewe ni mavumbi nawe utarudi mavumbini.” (Mwanzo 3:19) Walitiwa dosari kubwa, yaani, kutokamilika. Wangekufa kwa sababu ya kutokamilika au dhambi.

Wazao wa Adamu na Hawa, yaani wanadamu wote, walirithi dosari hiyo ya dhambi. Kwa hiyo, dhambi inaweza kulinganishwa na ugonjwa unaorithiwa. Adamu alipoteza taraja la kuishi milele bila kufa, na wazao wake walirithi kutokamilika kutoka kwake. Wanadamu wakaja kuwa watumwa wa dhambi. Biblia inasema hivi: “Hiyo ndiyo sababu, kama vile kupitia mtu mmoja dhambi iliingia katika ulimwengu na kifo kupitia dhambi, na hivyo kifo kikaenea kwa watu wote kwa sababu wote walikuwa wamefanya dhambi.”—Waroma 5:12.
Asante kwa sababu umekubali kwamba wale jamaa walikufa kwa sababu walitenda dhambi.
 
QURAN
39:42 "MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa"

Mkuu, kwa mstari huo unakubaliana na mimi kwamba sio kila kifo ni mpango wa Mungu maana hata Qur'an inasema kwamba kuna watu wanakufa kabla ya wakati wao, na ikitokea ivyo Mwenyezi Mungu huzishika roho zao hao watu mpaka wakati wao ambao Mungu kawapangia kufa ufike.

Sikuumba Majini na Watu ila Wapate kuniabudu.

Naishi vizuri tu na Majirani halafu nalogwa Natupiwa Jini na mtu mwenye Husda kisha Nafariki.
Je hapo pia nimefanya Uzembe upi Kwa mujibu wa Biblia??

Ama kweli watu wangu Wanaangamia kwa kukosa Maarifa..
Hapo wewe hujafanya uzembe wowote, ila mazingira yako ndo yamekufanya ufe. Yaan soma vizur thread, ni kama mfano niliotoa wa vifo vya watoto wadogo kwa uzembe wa wazazi wao.
 
Ukisoma kitabu kitakatifu cha Biblia,

Mwanzo 6 : 3
Mungu aliyeumba mbingu na nchi anasema.

"BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini"

Katika kitabu cha

Hosea 4 : 6 Mungu anasema

" watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa"

Jibu

Mungu alimwumba mtu na alitaka aishi miaka isiyozidi mia na ishirini akiwa mzee.

Wanaokufa wakiwa vijana wanasababishwa na kukosa maarifa

Mfano,
Vifo vinavyosababishwa na, ajali, kukosa matibabu sahihi, majanga kama njaa, mauaji, vita, ulevi, ujinga, mila potofu, umasikini nk.
Havitokani na mpango wa Mungu.

Olla..!
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom