Kifo cha Swetu Fundikira

Dont play with fire my friend, kwa nyie ambao wala hamjapitia hata JKT mnafikiri it is as easy as you think.
To put it bluntly a soldier is a proffessional legal killer who is to be used at the discretion of the state.
Ni suala la kusikitisha kwa bwana Swetu kupoteza maisha kirahisi hivi,lakini katika mji huu wa fujo nyingi it pays to be civil, you might not know whom you are confronting.


Mkuu Lole,

Maneno yako yamejaa BUSARA tupu. Pana wakati Mtanzania aliniambia kisa cha Kobosile mmoja aliyetaka amtafutie cha moto. Mtanzania alimuambia athari za kutembea na hizi silaha/silaha za moto. Jamaa siku kasikia Dito kauwa, akampa shukurani kuwa na yeye kitu kama hicho kingeliweza kumpata (inawezekana na yeye ni mtu wa kuhamaki mapema).

Haya uliyomalizia ndiyo yamesema yote.
1. Marehemu Swetu angelifahamu anagombana na watu wa namna gani, sidhani kama angelifanya hivyo. Ilitosha kunyamaza na kuombana misamaha na yangeliisha.

2. Hawa wanajeshi na wao wangelitumia BUSARA kidogo tu kuwa hiki kiraia unaweza ukakiuwa bure na ukaishia kushitakiwa uraiani, sidhani wangelihamaki kiasi hicho. Inawezekana kweli jamaa alikuwa ni dead man walking na wao wamefanya kumharakishia tu siku zake. Sasa wameleta simanzi na majonzi kwa familia ya Fundikira na familia zao kwa ujumla.

".....you might not know whom you are confronting."
 
Namshukuru Mungu,
Ndugu zangu,

Yanayotokea nchini mwetu hivi sasa, kama Tanzania ingekuwa ni mwili wa mwanadamu basi kila kukicha tungesikia mtu huyo akisema naumwa kichwa, viungo, nina homa kali, naharisha nk. Ingawa tutakuwa hatujagundua kinachomsumbua mtu huyu ni nini, lakini kelele zake hizi zinatosha kabisa kuonesha kwamba mtu huyu anaumwa!..

Ukitaka kuthibitisha jambo hili, angalia kipindi cha Bunge, Wawakilishi wa CCM au Upinzani wote wameungana pamoja kupambana na matatizo yanayowasumbua Watanzania tofauti na zamani ambapo “ndiyo mzee” zilikuwa nyingi hata mahali zisipostahili.

Hivyo ndivyo ilivyo katika nchi yetu, kelele zote tunazozisikia ni dalili kwamba Tanzania bado inaumwa na inahitaji daktari makini atakayeichukua na kuipeleka chumba cha uchunguzi, kuchukua vipimo vyote ili baadaye tujue tatizo ni nini na kulishughulikia! Je, ni Ufisadi? Je, ni Ukosefu wa Uzalendo? Je, Ni Tamaa ya kujitajirisha? Na magonjwa mengine mengi ya kufanana na hayo.

Ingawa kugundua tatizo na kulishughulikia ni vitu viwili tofauti, bado naamini kama matatizo hayashughulikiwi, Tanzania itaendelea kupiga kelele usiku na mchana! Hakuna tena namna ya kumzuia Mbunge asimjadili Mkapa Bungeni kwa matendo yake au Mwananchi asiandamane kupinga jambo fulani baya linalotokea katika nchi au hata kujadili namna anavyotawaliwa.
Kipindi cha kunyamazisha watu wasiseme kinachowasumbua au kuwatia hofu, kimepita. Ni vizuri sasa viongozi wetu kuanzia ngazi za juu kabisa wakaelewa mahali tulipo na kujishughulisha na kutafuta suluhisho la matatizo yetu pia wakiangalia sana namna ya kututawala, Mtanzania wa miaka ya 2000 ni tofauti sana na Mtanzania wa miaka 1900!

Madaktari makini tulionao wasipojishughulisha na matatizo ya walioko chini, eti wakaziba masikio kwa pamba ili wasisikie kelele na vilio vya watu wanaoteseka, basi haihitajiki shahada mtu afahamu tunakotoka ni kuzuri na tunakokwenda ni kubaya sana katika historia ya nchi yetu. Lakini kitu kimoja kikubwa cha kukumbuka ni kwamba, tuchezeni na kila kitu tulichonacho lakini tusijaribu hata siku moja kucheza na Amani yetu! Hili ni jiwe la thamani ambalo Waanzilishi wa Taifa letu walitutengenezea na kutuachia yatupasa tulitunze sana na kila mtu atimize wajibu wake katika kutunza amani hii.

Najua kila mtu anaweza kudai anazo shida nyingi maishani mwake, lakini ni vizuri kukumbuka kuwa hizo ni shida tukiwa na Amani ya kutosha, hivi tumeshawahi kufikiria kuwa na shida hizo hizo halafu tukawa tunakimbia vita ya sisi kwa sisi au ya Dini na Dini? Jambo hili si ajabu kutokea na bila shaka wapo watu kati yetu wanaotamani ili waweze kutimiza malengo yao ya Kisiasa, Kidini nk.

Ndugu zangu,
Kuna msemo usemao ukitaka kujua umuhimu wa makalio, basi kalia kichwa! Nimetoa mfano huo wa zamani ili mpate kuelewa kwamba baadhi yetu hatuuoni umuhimu wa amani tuliyonayo mpaka siku itakapoondoka na kuanza kuhangaika kuirejesha tukiwa tayari tumekwishachelewa.

Nimeandika makala haya kuwasihi ndugu zangu, Watanzania wenzangu, wanaotoa kauli za kutaka kutuchonganisha ili hatimaye watu ambao kwa miaka yote tumeishi kila mmoja akimwona mwenzake ni ndugu, tuanze kuona tuna tofauti kati yetu ambazo mwisho wa siku zitakuja kusababisha jiwe hili la thamani, AMANI, lipotee.

Nchi yetu ina makabila zaidi ya 120, lakini ina dini kuu mbili; Uislamu na Ukristo, basi! Ingawa zipo nyingine ndogondogo pamoja na ndugu zangu wasiokuwa na dini kabisa, Uislamu na Ukristo ndiyo zinazoonekana kuwa kubwa hapa nyumbani. Hii ina maana tumegawanyika makundi makubwa mawili, wapo Wakristo na wapo Waislamu.

Kama ilivyokuwa nchini Rwanda mwaka 1994, kulikuwa na makabila makubwa mawili, Watutsi na Wahutu ingawa kweli kuna kabila jingine la Watwa, ukweli unabaki pale pale kwamba makabila makubwa ni Wahutu na Watutsi, hata mauaji ya Kimbari yalipotokea yalikuwa ni kati ya makabila hayo makubwa mawili.

Ni kweli katika nchi yangu si jambo rahisi sana kwa vita ya kikabila kutokea, maana chuki za Kikabila hazipo na si rahisi kuzipandikiza kwa sababu ya wingi wa Makabila! Kama kuna hatari inayoweza kupandikizwa na kusababisha mauaji makubwa basi itapitia kwenye mgongo wa Dini ambapo ni rahisi sana kutugawa katika makundi kisha kutuchonganisha ili tuweze kuchinjana! Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, inatupasa tuwe makini sana na jambo hili.

Dini zetu hizi kubwa mbili, zina nguvu sana katika nchi yetu, hata Wanasiasa na viongozi wa juu wanalifahamu jambo hili na mara kadhaa zimewatia hofu kwamba wasipofanya jambo fulani, basi kura za Waumini wa Dini hizo hawatazipata hivyo kuhatarisha nafasi za Wanasiasa katika Madaraka!Hofu hii imefanya Dini hizi kubwa mbili kugeuka kuwa kama Mpiga solo kwenye bendi, ambaye bila yeye muziki haupendezi! Akiudhiwa kidogo tu anasusa na kukaa pembeni, ndiyo maana siku za hivi karibuni Dini hizi zimekuwa zikitoa vitisho kwa Chama Tawala kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu mwaka 2010!

Tukianza na Wakristo, walipopata fununu kwamba misamaha ya kodi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na ya dini ingefutwa, walianza kupanga mikakati ya kuipinga bajeti na wengine kusikika waziwazi wakisema kuwa serikali na chama tawala CCM haiko pamoja nao na kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ndiyo utakaotoa jibu.Kuepuka hatari ya kukosa kura, serikali ilifuta kusudio lake hilo.

Wakiwa wanaanza kupanga mikakati hiyo ya kuipinga bajeti na kuitisha CCM kwenye uchaguzi ujao,tayari viongozi hawa wa dini ya ukristo wako kwenye mkakati wa kusambaza waraka kwa waumini wao kuwaelekeza nani wa kumchagua na nani si wa kumchagua.Mlengwa hapo ni CCM!

Wiki chache tu baadaye, imeibuka hoja ya Mahakama ya Kadhi huko Bungeni Dodoma, serikali imepinga kuanzishwa kwa mahakama hiyo na kusema lazima subira ivutwe kwanza ili ipate kujifunza kutoka kwa wengine waliotangulia kuwa na Mahakama hiyo.

Kitendo hiki kimeoneka kuwakera viongozi wa dini ya Kiislamu, kwani siku chache tu baadaye kupitia Baraza la Waislamu (BAKWATA), walijitokeza na kusema Waislamu hawatakipigia kura Chama cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 kama Mahakama ya Kadhi haitaruhusiwa kuanzishwa nchini, tena wao wakaenda mbele zaidi na kudai serikali ya chama cha Mapinduzi inawapendelea au inaburuzwa na Wakristo.

Nini maana ya malumbano hayo? Ni wapi hasa ambako viongozi wa dini wanataka kutupeleka? Wanataka kutuchonganisha? Ili mimi nianze kuona kwamba nina tofauti na Saidi? Hatimaye kumchukia? Hapana, hili si jambo jema hata kidogo, viongozi wa dini wawe Wakristo au Waislamu wanapaswa kuacha mara moja tabia ya kuwagawa Watanzania kwa misingi ya dini, hili ni jambo hatari sana kufanywa katika nchi yetu iliyozoea amani. Ni vizuri wakaacha kutumia uwezo walionao vibaya.

Isitoshe sitaki kuamini hata kidogo kwamba kuna Mtanzania leo anayeweza kuburuzwa tu na Askofu au Sheikh wake bila kujiuliza faida na hasara za uamuzi huo! Ndugu zangu inatupasa tujifunze kuishi kama ndugu, kutafuta majibu ya matatizo yetu bila vurugu, tofauti na kufanya hivyo tutajikuta siku moja mimi na Mufti au mimi na Pengo tuko Sudan kwenye kambi ya Wakimbizi, sote tukijiuliza tumefikaje huko?

Tukiliona hilo mbele yetu, basi inatupasa tusiendelee na njia hiyo, inatupeleka pabaya! Ni bora kugeuza na kutafuta njia nyingine ya kutatua matatizo yetu badala ya kuanza kupandikiza chuki kati ya makundi ya watu kwa misingi ya dini, hii ni hatari, hii ni sawa na kucheza na moto, lazima siku moja tutaungua!

Pia inatubidi tuwe makini sana na kauli zinatolewa na viongozi wetu, wawe ni wa Siasa, Dini nk. Katika jambo lolote tutakalolifanya Amani yetu lazima ibaki, tusitamani vurugu ndugu zangu, zimewatesa watu wengi sana duniani na mwisho wa siku wakaketi chini kwenye meza ya duara kuongea.

Kama maongezi ndiyo yanayoweza kuleta majibu ya matatizo yetu, kwanini tusiongee leo ili kuepusha matatizo yanayoweza kutokea kesho? Hili linawezekana kabisa kama tutazikubali tofauti zetu na kuishi pamoja kama ndugu tukishughulikia matatizo yanayojitokeza kwa njia ya amani badala ya wachache kupandikiza chuki kwa maslahi yao.

Tukumbuke kitu kimoja kwamba, ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili lakini unaweza kuteketeza mwili mzima! Hivyo ndivyo itakavyotokea kama viongozi wetu wa dini na siasa, wanaoheshimika na kuwa na ushawishi mkubwa katika nchi wataendelea kuzitumia ndimi zao bila busara, LAZIMA SIKU MOJA TUTAANGAMIA.

Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema kile ninachoamini kwamba ni ukweli.
Pasua jipu hili limerudiwa kwa sababu maalum.

http://www.globalpublisherstz.com/pasua_jipu/
 
nasubiri maandamano ya yule mjeshi aliyeua wenzake zaidi ya 10... na ya yule mbongo aliyechomwa kisu pale london... na ya brian mazula, na ya kupaza, na ya kapalata

De Novo, tofauti ni kwamba hawa wanajeshi walioua Mr Fundikira walionyesha "bage" zao walipomchukua kwa hiyo wameua kama wanajeshi, na kwa niaba ya jeshi, kwa hiyo watu wanaweza kuandamana kwenye hii kesi.

Hao wengine uliotaja waliuawa na watu binafsi. Hata yule mjeshi wa USA hakuua kwa niaba ya jeshi. Watu waandamane against nani? Familia za wauaji? Ungejifunza "logic" kwanza kabla ya kujifunza Latin De Novo. Usifananishe mauaji ya watu binafsi na mauaji yanayofanywa na "institutions"
 
Kesi iliishaje?
Walihukumiwa kunyongwa wapo magereza, ila huyo mwanmke Dora taarifa zilitolewa na gereza moja huko Dodoma alipokuwa amehifadhiwa kusubiri kunyongwa (ingawa Tanzania hawanyongi) eti huyo Dora kafariki mwezi uliopita na amezikwa na gereza kam sharia zinavyosema. Ndugu walipewa taarifa hiyo.
 
Walihukumiwa kunyongwa wapo magereza, ila huyo mwanmke Dora taarifa zilitolewa na gereza moja huko Dodoma alipokuwa amehifadhiwa kusubiri kunyongwa (ingawa Tanzania hawanyongi) eti huyo Dora kafariki mwezi uliopita na amezikwa na gereza kam sharia zinavyosema. Ndugu walipewa taarifa hiyo.[/QUOTE

Kaka unavoandika ni kama huna imani kama kweli huyo dada alifariki
 
Walihukumiwa kunyongwa wapo magereza, ila huyo mwanmke Dora taarifa zilitolewa na gereza moja huko Dodoma alipokuwa amehifadhiwa kusubiri kunyongwa (ingawa Tanzania hawanyongi) eti huyo Dora kafariki mwezi uliopita na amezikwa na gereza kam sharia zinavyosema. Ndugu walipewa taarifa hiyo.[/QUOTE

Kaka unavoandika ni kama huna imani kama kweli huyo dada alifariki
Ndugu mwili wa marehemu haujaoneshwa ila kaburi. kwa nini watu wanahoji kuhusu kifo cha Balali?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom