Kifo cha kampuni ya Business Times Ltd

unajua katika kazi ukichanganya na udugu pasipo ujuzi matokeo yake ndio haya, wafantakazi wameanza kudharau familia ya mzee mbuguni na wanakua kama vituko mbele yao.
halafu dogo imma anachanganya kazi na mapenzi, kuna dada mmoja kampiga chini eti anajitia kumtimua, sasa kwa staili hii unadhani kampuni itakwenda wapi kama sio kuzimu?
 
Wakuu hali mbaya ya kiuchumi inaonyemelea kampuni tanzu ya Business Times Limited. Taarifa za ndani zinasema kwamba wafanyakazi wake hawajalipwa tangu mwezi wa kwanza mpaka leo. Kisa family interference into operations. Kwa mujibu wa mfanyakazi huo chama cha wafanyakazi tayari kimetangaza mgogoro na mwajili huyo. This is the shame nakumbuka majira miaka hiyo na Business Times miaka ile. Du kweli la kuvunda halina ubani.....Correspondent wenyewe hawajalipwa kwa miezi mitano.. je tunaelekea wapi......

Na wewe inaelekea umo humo humo.Pole.Lakini kama wewe ni mwandishi wa habari,mm, mbona hata kiswahili chenyewe na uandishi wenyewe wasiwasi?
 
Lusange usinishangaze zaidi. Eti huyo bwana alichanganya mapenzi na kazi? Kwani yeye hajaoa mpaka atembee na wanawake wa kazini anaofanya kazi na wao? Kama anachanganya mapenzi na kazi basi ameua. Kama Sodoma na Gomora ilikufa kwa sababu hiyo, basi hata Business Time Ltd itakufa pia. Mimi nilifikiria penginepo ni tattizo la kifamilia tu ndio linaua kampuni kumbe kuna na mapenzi ya kulazimisha na mtu anapigwa chini kwa kumkatalia mapenzi mtoto wa mmiliki? Huyo dada alyepigwa chini anaitwa nani na amelalamika? Nawafahamu baadhi waliokuwepo siku za nyuma. Si kuna magazeti mengi tu kwanini huyo dada asiombe kazi kwingine? Kama biashara ya mapenzi imeshaingia hapo hapabaki kitu. mkumbushe sodoma na gomora ilivyoanguka pwa, itakuwa business times????????
 
Duh! hii noma! kwan huyo imma mbuguni mkewe hayupo mpaka achakachue nje? tatizo management imezidi kusikiliza majungu. zamani walikuwepo wahariri wazuri sana waliokuwa na uwezo wa kusimamia gazeti na likauzika mitaani. Dogo Aga kwa kupokea majungu bila mpangilio amekuta akipoteza watendaji wake wazuri na kubaki na makapi yasiyoweza kufanya la maana.
Hebu ajifunze kwa hao wanaompelekea umbeya shukrani yao ni kuacha kazi kwa 24 hours, kama walikuwa na mapenzi na kampuni wasingeondoka hapo, kinachowakimbiza hapo ni nini???
Dogo jifunze kupitia hao marafiki zako wa muda wanaokuletea umbeya bila mpangilio.
Imma tulia na mkeo mbona mzuri tu jamani au nini shida??? kama maamuzi mengine mnafanyia home na haya yakurekebishana tabia myafanyie home basi.
Kaeni mjipange vyema kampuni ya business times bado inauzika kwa jina mtaani tatizo ndani kumeoza, rekebisheni madhaifu yenu muweze kusimama upya.
kazi njema.
 
Hata mimi sishangai kusikia Business Times ina hali mbaya. Nina muda mrefu tangu nilipojiondoa katika kampuni hiyo. Lakini nasikia sasa mambo hayaendeshwi kitaalamu. Ukishakuwa mtoto wa mwenye kampuni inatosha kupata nafasi ya kazi. Ukiacha GM ambaye baadhi tu ya wafanyakazi wanasema ana busara na msikivu, kuna mwingine ambaye wafanyakazi wenzake wanadai hawamwelewi kwa sababu haeleweki. Nasikia ingawa huyo mwingine wanayemwita Immma hana taaluma yoyote ya uandishi na wala hajawahi kuandika makala au habari yoyote, yeye sasa ni mhariri mkuu wa gazeti la Darleo. Mtu mmoja akaniambia anahudhuria pia vikao vya jukwaa la wahariri. na sijui kama wahariri wanaokutana wanaulizana taaluma zao. kama yote hayo ni ya kweli, kwanini nishangae ninaposikia BTL iko taabani wakati inaendeshwa na watu wasiojua wanachokifanya? kama ninayosikia ni ya kweli, kuna siku mhariri mkuu wa majira atakuwa mtoto wa mwenye kampuni, na kisha magazeti mengine kama spoti starehe na business times lenyewe. sasa wameanza na darleo, mengine yatafuata. sishangai kila nikisoma majira nakuta halina mhariri bali lina kaimu wake. anayekaimu nafasi hiyo ni John Mapinduzi. Yeye asubiri mhariri mkuu wa Majira atakapokuja kutoka familia ya mwenye kampuni. Nikifikiria hayo hata nikiambiwa nirudi business times nitakataa. Na tangu nilipoondoka 2006 sijajuta. Hiyo ni kazi ya familia. Kama bado kampuni itakuwepo mabadiliko yake yatakuwa hivi: Mkurugenzi wa Business Times Ltd, Baba Mbuguni. Meneja Mkuu, Mtoto Mbuguni, Mhariri Mkuu Majira, Family3 Mbuguni. Mhariri Mkuu Darleo, Family4 Mbuguni, Mhariri Spotistarehe, Family5 Mbuguni, Mhariri Mkuu Business Times, Family6 Mbuguni. Meneja Mkuukiwanda cha uchapaji, Mr1 Mbuguni, nk, nk. Vikao vyote vya utawala vitafanyika nyumbani na maamuzi kufanyika huko huko. Halafu mnashangaa kampuni isife!!!!!!!!!!!!!!!!????????????

Hii kweli inatia uchungu sana, haswa inapohusu kampuni ya wazalendo. Hii kampuni ilikuwa moja ya kampuni za mwanzo za habari Tanzania, na kwa kweli ilileta mapinduzi makubwa katika utoai habari kwa Wananchi, lakini haya yanayotokea sasa hivi ni masikitiko makubwa sana.

Mimi siku zote huwa nalaumu zile elimu zetu za kufaulu kwa PAST PAPERS , na hii ni kwa sababu, baadhi y hawa watoto wa Mzee Mbuguni walipelekwa kwenda kusoma Ulaya na India (Kwa wale walioishi nao Block 41 Kinondoni wanajuwa zaidi), sasa sijui kama walienda kucheza MBOWE kule mavyuoni, au ndioa hayo madhara ya ELIMU za PAST PAPERS ambazo zilikuwa zinawasaidia wanafunzi kupass mitihani tu badala ya kuelimika. Utajiri wa Familia nyingi tajiri duniani huanzia kwenye URITHI, mtihani siku zote ni jinsi ya kuendeleza huo mtiririko.
 
Inasikitisha sana habari hii. Hii ilikuwa ni moja ya makampuni yenye kuletea wazawa heshima kubwa. Tuwaenzi waanzilishi kwa kuwasaidia. Nawashukuru sana mliotua taarifa hii ya kusikitisha. Mchangu wangu kama mtaalam mshauri wa biashara.

Kwanza kuna tatizo la governance au uongozi. Siyo siri kwanza watanzania wengi wetu hatuna mchakato wa kurithishana biashara na mambo wa maana kitaalam. Pili hatuna uwezo wa kujua ni kitu gani cha msingi katika mambo yetu. Tunapenda sifa kuliko kufaidi mambo ya maana. Kwani kuna tatizo gani mtoto wa Tajiri akapata chake na akawa nje ya ofisi.

Nashauri ili yasitokee mambo kama ya Kwacha Transport, Zainabs bus service, Scandinavia, Milo Construction, na wale jamaa wa ujenzi wakina LUKUWI Waliohusika sana na PPF Towers na miradi mingi ya waswahili iliyokuta wafanye mambo yafuatayo. Wenye kuwajua wana familia ya Business times wawaunganishe nami ili kwanza tuwape tiba ya kisaikologia, pili tuweoneshe faida za kampuni kuendeshwa kitaalam, tatu tuwapange ili wafanye kazi kitaalam.

Kwa bahati mumewahi kabla hawajafilisika kabisa. Washauri wenzangu tuwasiline tuwasaidie wazalendo la sivyo hakutakuwa na faida ya JF. Watafanikiwa kwa kufuata kanuni za bishara na kushirikisha wataalam tu. Mbona Mzee Mfugale na Hoteli zake anaonekana anafanya vizuri? Naamini, anafanya kazi na wataalam.

umeongea kwa dhati sana ndugu. Wewe ndo uchukue jukumu la kuunganisha wataalam wenzako kuokoa hili jahazi
 
...... Habari za ndani ni kwamba wafanyakazi wameibuka kidedea na mpunga umetoka kimagumashi.... More to come source anakula sikukuu
 
Kuna taarifa kuwa wafanyakazi waliitwanga barua bodi ya kampuni na kuipa siku kadhaa. Kama mpunga ulitoka labda bodi imejibu. Kama hawakuwa na hela sasa wamezipata wapi? Labda bodi imeshinikiza. Bodi ingeingilia kati pia utendaji wa menejiment ya kampuni. Nani atamwajibisha nani? Kama utendaji ni mbovu, baba anaweza kuwawajibisha watoto? Au watoto wanaweza kuwajibishana wenyewe kwa wenyewe? Huo mpunga ni wa kuahirisha matatizo, lakini matatizo yako pale pale.
 
kweli kaka. Naambiwa na source kwamba baada ya kuonjeshwa asali na ncha ya kisu (yaani kamshahara ka january) mambo yako palepale....mwezi wa nne mshahara hakuna. Jamaa wamekula pini baba,mtoto,watoto
 
chadema walinunue liwe gazeti lao liendelee from there. kwa historia yake, ni aibu kwa gazeti huru la kila siku kufa. na ili kulisaidia lisionje umauti wakati wa uhai wangu ntaanza kuwa nanunua nakala 1 kila siku, hata kama sijavutiwa na chochote. nafanya hivi kwa kuheshimu mchango wa gazeti hili katika mageuzi ya 'nji' (sijui ndo spelling sahihi?) hii!
 
Africa tuna safari ndefu,ni lini tutaweza kufanya kama hawa wageni????????aghhhhhhhhhhhhh
 
Back
Top Bottom