Kifo cha CCM kimetimia

PONGEZI SANA NDUGU 'MATUKUTA JUNIOR' KWA MOYO HUO WA UJASIRI JUU YA MATUMAINI YA CCM HATA IWEJE

Ndugu zangu wana-JF,

Nichukue nafasi hii kumpongeza sana tena sana huyu mtani wetu wa kijani, Ndg Mutakuta Jr, kwa ujasiri wa hali ya juu kuendelea kutetea kile anachokipenda hata darini kama hivi juu ya chama chake cha CCM.

Nasema haimpi mtu yeyote faraja kuja kusikia kwamba 2015 CHADEMA tumeshinda uchaguzi dhidi ya CCM kilicho dhaifu kwa kipindi chote, CCM kilichokata tamaa na CCM kinachoona aibu kujinadi mbele za watu kama alivyofanya hapa huyu mwenzetu Junior??????????

Binafsi, kwangu mimi naamini na kusema hapa kwamba nafarijika sana tena sana ninapogundua kwamba watani wetu wa huko
CCM WANAENDELEA KUJIPA RAHA NA MATUMAINI MOYONI HAKIKA NDIKO UTAMU WENYEWE WA SIASA ZA USHINDANI UNAPOPATA NGUVU YAKE - na huo ndio msimamo wangu ulivyo.
Na ninakuhakikishia hapa kwamba nitatetea HAKI YAKO YA KUSEMA CHOCHOTE HAPA JUKWANI hata kama ninao uhakika ya kwamba kile unachokisema kweli ni upuuzi mtupu na kwamba pengine ni kule katika kujitafutia faraja tu ya muda mfupi moyoni.

Hilo ninalosema nakuhakikishia nitakutetea kwa kila hatua utakapojaliwa pumsi ya kunena zaidi na zaidi mbele ya umati huu wote uliofurika mote hapa jukwaani hata kama mtazamo wako ni kinyume kabisa na cha kwangu huku CHADEMA.

Naam, na hayo ulioyasema nayo ni maneno ya kutumainika maana huna sababu yoyote kujitangazia umauti CCM hadi pale ambapo waheshimiwa wapiga kura watakapotoa maelekezo sahihi kwa muda murua zaidi.

Mtakufa ninyi na CCM itabakia daima kama Chama Dola!!
 
Watanzania wakijitahidi kuona mchawi anafariki, nachelea kusema sifa ya mchawi ni lazima aishi miaka mingi "Kitu mpaka uzeeni kama hakijafanyiwa ya shinyanga na mbeya kwa sasa", Kila anayemtishia uhai wake ujue siku zake zinahesabika kwa namna yeyote ile, Siku anakata roho watu waweza subiri hata siku 3 bado tu anarusha miguu na kufumbua macho.

Hivyo ni vyema kujiandaa vizuri maana bado kuna kazi ngumu mbeleni kama tunavyoona sasa hivi kesi za ugaidi nje nje, kubambikwa kesi ni kawaida sana tu, Rumande ndio hotelini kwa wasema kweli, Ukisema ufisadi na ujangili unaonekana mtovu wa nidhamu kwani hizo ni biashara halali kwa viongozi wetu, Ukisema madawa ya kulevya utaambiwa walioshikwa ni wale mateja wa pale ruvu, Kudhibiti silaha na matumizi mabaya ni kama kuzuia machinga kuuza mapanga, visu na bastola za bandia Dar kwenye foleni.

Ni vizuri kumuuliza kamanda MREMA alikosa hadi kura aliyopiga yeye mwenyewe pamoja na kwenda mahakamani lakini haikupatikana, Pia ushindi siku hizi unatolewa hadi mahakamani kama chama fulani kitaona kura hazikutosha. Tatizo la mahakama zenyewe ndio hizo za kufuta kesi na baada ya dakika 3 unakamatwa tena na kuhamishwa kwa hakimu mwingine anayejua kuendesha kesi, Au kama za Ponda bado hajahukumiwa kama kiongozi wa uvamizi lakini wafuasi muda mwingi tu washaanza kukalia debe.
 
Kuasisi UDINI na Ugaidi hizi kitu wameanzisha ccm na ndio vitawatoa madarakani r.i.p ccm from 1977-2015 God is great.
 
Kwaheri wazee wa zamani. yote ambayo chama cha CCM kinafanya ni dalili zakuondoka madarakani. Nikwanini wanataka kuleta mswada wakuzuwiya maandamano? budget kila mwaka hela hazitolewi kama bunge ilivyoidhinisha? badala yakua bize nakutatua matatizo ya wananchi wako bize nakudhibiti Chadema? Out!!!!
 
ccm bwana walikula mpaka sukita yao we unafikiri wataweza tunza viwanda alivyo anzisha mzee nyerere.....miaka kibao sasa hadithi tu hata kununua kichwa cha treni .....wametuzulumu viwanja kirumba mza na karume ar lakini kazi yao kula u kodi lakini hata kupiga rangi vimewashinda
 
Wapinzani na wananchi kwa ujumla wamekuwa wanasema na kutoa tahadhari ya mambo mbalimbali serikali haisikilizi mambo yakiharibika wanadai tusilaumiane na tusikitike. Kuhusu mihadhara na cd za uchochezi zimelalamikiwa muda mrefu sana, sasa majibu yameanza kutokea wanadai siyo wakati wa kulaumiana. Kwanini usilaumiwe wakati umeonywa siku nyingi huku ulikuwa unabeza kwa dharau. Ccm byeee wamechoka jamani wananchi hatuoni jamani. 2015 tufanye uamuzi wa busara.
 
itakufa na kamwe hatutaizika bali tutaichoma moto kama wahindi. RIP CCM.
 
Tanzania inapita katika kipindi kigumu kwa sasa,kila siku kunajitokeza jambo jipya ambalo linapelekea watu kuwa na taaruki kwa kiasi kikubwa na kuwa habari kubwa katika vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na radio tv magazeti ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii.matatizo makubwa yaliyotikisa nchi hivi karibuni ni pamoja na kuvamiwa na kutekwa kwa mwandishi wa habri w kampuni ya THE NEW COOPERATION ndg.ABSALOM KIBANDA,kuuawa kwa padre mushi,kuchomwa kwa makanisa mkoani dsm,mgogoro wa kuchinja kule Geita hadi kupelekea mchungaji kuuawa na kundi kubwa la waumini wa dini ya kiislam waliomvamia.fujo za wakazi wa mkoa wa mtwara kugomea gesi yao isipelekwe DSM hadi viongozi wa kitaifa kwenda kuzima mgogoro huo ambao umeleta taswira mbaya kwa taifa letu,hadi wananchi waandamane ndo mgogoro utafutiwe ufumbuzi.Kule mkoani LINDI wananchi kuchoma nyumba za viongozi wa chama cha mapinduzi CCM ikiwa ni pamoja na nyumba ya mbunge wa jimbo hilo.kuuawa kwa mwandishi wa habari bwana DAUD MWANGOSI na jeshi la polisi kuhusika na mauaji hayo ya kinyama bila hata na chembe ya huruma.kubwa zaidi ni kulipuliwa kwa kanisa katoliki la mt.joseph mfanyakazi katika kitongoji cha OLASITI nje kidogo ya jiji la ARUSHA na kupelekea vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa hadi baadhi yao kupoteza viungo vyao.Jana maandamo makubwa yamefanyika kuelekea eneo la mazishi katika kanisa hilo yakiongozwa na mh.MIZENGO KAYANZA PETER PENDAwaziri mkuu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na wapendwa wetu kupumzishwa katika nyumba zao za milele.kilichoniuma zaidi watanzania wengi tuna tabia ya kusahau matukio ya nyumba pale tu panapotokea tukio lingine na kulifunika lililotangulia.haya matukio tungekuwa tunayakumbuka basi tungekuwa tunaililia sana nchi yetu ikiwa ni pamoja na maombi.tunakumbuka matukio ya hivi karibuni tu ya nyuma tunayasahau.(chakula cha zamani na kukimbilia cha leo wakati cha zamani kama hakipo basi na kipya hakipo.Nawaomba watanzania tufanye mabadiliko ya kisiasa tujaribu na upande wa pili tuone.kumbuka baba wa taifa alisema asiyekubali mabadiliko,na fikra zake ni ndogo.TUKUBALI MABADILIKO WATANZANIA.:angry:
 
Mkuu umenikumbusha mengi kwa kweli ccm imetufikisha hapa tulipo Mungu inusuru nchi yetu ila kikubwa zaidi watz wenzangu tuungane kuleta uhuru mpya katika nchi yetu na kumng'oa mkoloni mweusi. Sasa basi yatosha.
 
Mkuu kweli umeongea mengi ila watanzania wengi bado tuko kwenye utandawazi lazima tukubali mabadiliko kutoka kwetu wenyewe.
 
Ukweli huu ni dhahili kuwa chama chochote kinachotawala popote duniani, pale kinapoona kuwa utawala wake unaelekea kuangushwa huwa kinakuwa mwanzilishi mkubwa wa uhaini na ugaidi. Kinafanya hivyo ili kuziteka na kuzikoroga akili za watu ili mradi tu wapoteze mwelekeo.
Hivyo kutokana na style hiyoambayo mara nyingi inayoendeshwa na watu wenye nafasi za juu katika serikali inayotawala na wakati mwingine kwa kusaidiwa na mataifa rafiki duniani, ndiyo maana hata CCM wameona wafuate njia hiyo hata ikibidi kupoteza baadhi ya uhai wa wananchi wake, cha msingi kwao ni kubaki madarakani. KAENI CHONJO.
 
Muanzisha mada omba mudi aiweke stick ijadiliwe na kuwafikia watanzania wengi zaidi. ccm ni kama nguruwe nayezaa watoto na kuwala.
 
NINACHOWEZA KUSEMA NI KUWA CCM NCHI ILISHAWASHINDA
USHAHIDI MDOGO KULINGANA NA UWEZO/UPEO WANGU NI HUU HAPA;


  • Viongozi wengi waliopo madarakani hawana upeo/elimu wanaongoza kwa kutumia uzoefu na uchawi
  • Wenye nacho wanaongezewa,wasionacho wanaelekea kuwa na negative (deni la taifa ni la wanyonge,wakati hata hawakukopa)
  • Njaa kubwa inainyemelea nchi,sababu ni mafisadi kujirudishia fedha za EPA kwa kupandisha bei ya pembejeo hasa mbolea
  • Msamaha kwa mafisadi,wakati wanyonge wakiiba kuku tu,miezi 6. sina maana tuibe..
  • Migogoro ya dini
  • Polisi kuwanyanyasa na kuwaua wananchi
  • Kuporomoka kwa kiwango cha Elimu
  • Rushwa serikalini (CCM),polisi,mahakama
  • Maisha duni kwa wananchi kutokana na mfumuko wa bei ....
  • MATUSI MAZITO BUNGENI,BADALA YA KUJIBU HOJA ( MABAVU)

View attachment 94149

Kama wewe unabisha,basi bisha kwa ushahidi.CCm ichukue hatua sasa,hali inaweza kuwa tete
 
Katika karine ya 21 wakati wa digital serekali ya ccm haya ndio mafanikio yake. Nasema CCM itaipeleka Tanzania kaburini kama isipoondolewa madarakani
Mbowe ashuhudia-
 
Back
Top Bottom