Elections 2010 Kibwagizo cha kura alizokataa kikwete kinaboa!

Hivi jamani watu wengine mbona wanachafua JF? Au unataka kufanya watu tusifungue JF the home of Great thinkers? E bana usituchefue tena tafadhali, kama hujui hisabati usirudie kutoa uchafu awko hapa ok.
Umeniharibia siku mzee.
 
Hivi wewe hizi pumba ulizomwaga hapa zinaashiria kuwa husomi contributions za wenzako kabla ya kuchafua hali ya hewa?

Jina lako linaashiria kwamba u mwanamke! Binafsi naamini wanawake wanafikiria b4 ya kuongea! Contribution zipi unazosema msichana?! Hizo contribution za Sh. 315,000 x 400,000?! That is rabish coz' am free thinker na sio mtu wa kukurupuka na kuongea11 Angalia hisabati zilizopigwa na wenzako? Eti mshahara kwa mwaka ni 315,000 x400,000x12!!! Kwani mishahara ipo flat?! Wewe kama una-copy na ku-paste kichwani, mimi huwa na-digest!
 
Mkuu don't tell me you are not Tambwe Hiza or atleast a person working with him at his propagation unit


Ina maana na wewe unakubaliana na hizo hesabu za 315,000 x400,000x12 ?! Ina maana KCC ikiwa Sh.315,000 salary scale itakuwa flat? Yaani mpika chai atalipwa 315,000 na makatibu 315,000? Kweli tuna safari ndefu!!!
 
Hotuba ya raisi ilikuwa wazi, kila mtu ana masikio kusikiliza alichosema, wewe umetia maneno yako ili kujirembesha kwa mafisadi, acha kubwabwaja. Raisi wa nchi hawezi kutoa kauli kama hiyo,wafanyakazi hawabadilishi kura kwa mshahara, muungwana JK alipotoka na hiyo kauli itamtesa maishani mwake milele.

Kama watanzania wana akili sawa na ya kwako basi tumekwisha.Kwanza umesema watanzania sio waaminifu, sijui umetumia vigezo gani kufikia hiyo conclusion, nasema huko ni kuropoka, kama wewe sio muaminifu then dont generalize kuwa watanzania wote sio waaminifu.Umesema kuwa kuna rushwa/ufisadi kuanzania kata hadi ikulu, that is another plain statement ambayo huna any data kuisupport, so kwa hayo mawili nadhani unasukumwa na ushabiki zaidi kuliko akili za kawaida ambazo mungu amekupa. Na kama una macho ya kifisadi hata kama ukipewa data za kujaa chumba kizima bado hutauona ukweli. Sidhani kama data unazihitaji kabla hujafungua macho yako mengine uone ukweli, vua utando wa ghiliba za kifisadi na ushabiki wako kwa CCM na uchafu wao, jivike macho ya uwazi na utambuzi, then utaona jinsi ulivyopumbazika kwa vijisenti unavyopewa kuushabikia uongo na utumwa wa CCM. Wewe ni mtumwa, tena utumwa huu ni mbaya kuliko ule wa enzi zile, utumwa wa fikra na uchovu wa kuchambua hoja na ulegevu wa kutafakari nini hali itakuwa kwa watoto na wajukuu na wajuu za watoto wetu niutumwa mbaya kuliko ugonjwa mbaya na hatari ya malaria na ukimwi.

Kima cha chini cha 350K kinawezekana, hizo ni dola mia 250. Ni hela ndogo kaka, halafu ulivyo mvivu wa kuchambua, hukubother kuhakiki mahesabu ya JK, umebandua na kubandika kama alivyosema. Hebu nijuze, umewezaje kupata trilion 6 kwa mwaka? kama serekali ina wafanyazi 350,000? Excel yangu hapa inaonyesha kuwa kwa mwezi ukizidisha 350,000X350,000 ni 122,500,000,000. Kwa mwaka ni 1,470,000,000,000. Hizo ni trilion 1.47. Sasa kaka unataka tukupe majibu wakati maswali yako umebase kwenye wrong information, kweli tutafika?

Kama wewe ni kuwadi wa kushauri mbona hukumshauri JK atoe kauli zenye hekima.Kugoma ilikuwa ni haki ya mfanyakazi na sidhani kama kwenye mahojiano kulikuwa na swala la kumpa kura JK kama sharti la kuongezwa mshahara, aliibua soo hilo mwenyewe, wacha watu walitumie kisiasa. Hizo hotuba za kuandikiwa na JM ndizo zinamfanya JK aonekane hana maana. Na je lile la kiherehere cha wasichana kupata mimba nalo unalizungumziaje? Hakuna kiongozi wa nchi aliyekwisha sema kuwa kama vipi na kura zenu sizitaki, huo ni uchuro, kwani kama angesema haiwezekani kuwalipa fedha zote hizo kw akuwa serekali haina uwezo kungekuwa na shida gani, yaani kwa kauli yake ni kuwa siwaongezei mshahara na kura zenu sizitaki.Kwanza si raisi wa nchi mwenye mamlaka ya kuongeza mishahara, hivyo kuchaguliwa kwake na kuongezeka kwa mishahara ni vitu viwili tofauti kaka-- lol
Acha, huku ni kutapatapa kwa CCM, mara JK hakusema hivyo (Tambwe) mara wameongeza mshahara kimya kimya, mara TUCTA isiingilie swala la nani watamuunga mkono kwenye kinyanganyiro cha uraisi ni kuvunja sheria-Naibu katibu Mkuu Kazi. If this is damage control mnafanya, then guys mmechelewa sana, it was suppose kufanywa kesho yake baada ya hotuba ya JK. Kama mnaanza damage control baada ya mgombea wa chadema na TUCTA kuonyesha makucha, hiyo sio control bali mnazidi kudamage. Ningekuwa wewe, ningemshauri JK akomae na kauli yake, huo ndio ujasiri, sio kuanza kutafuta watu kama wewe kumsafisha, huo sio ukomavu hata kidogo, ni woga

MPWA umetukana sana na mimi sina budi kukuridhisha kwamba mimi ni juha kweli kweli, nisiyefahamu A wa Be!! Hata hivyo, nambo tujadili kwa kituo hicho kipengele nilichoki-highlight kwa rangi kisha tuambizane kimya kimya ni nani mbumbumbu kati yangu na wewe!!!!
In short sina mengi ninayofahamu kuhusu serikalini lakini huwa sikurupuki na kuandika.
According to Tangazo la Kazi lililokuwa limetolewa na Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma (Daily News April 21,2010) nilikuta the Lowest Grade ni Grade TGOS. A( ambayo salary scale yake ni btn TZS. 104,410 to TZS. 146,570). Grade hii inachukuwa watu kama wasaidizi wa ofisi(wapika chai, wafagizi, and the like) na walinzi! Likewise, fresh graduates wanaanza na Grade D (for non science oriented graduates) ambayo salary yake ni Sh.324,260/= hadi TShs. 401,880) na Grade E (for science oriented graduates) ambayo salary yake ni TZS 408,560/= hadi TZS 505,030! Ikumbukwe, hizo ni grade za chini sana kwenye organization chat! Hivyo basi, tunaposema KCC iwe Sh.315,000/= maana yake ni kwamba Mhudumu wa ofisi alipwe Shs.315,000/=. So, ina maana viwango vingine vibaki vilevile like b4?! Jibu ni kwamba HAIWEZEKANI! Au hata kama vitabaki vilevile, hiyo mantiki ya flat rate ya 315,000/= inatoka wapi?! Jibu lake ni kwamba JF is no longer The Home of Greatest Thinkers, but The Home of Greatest as well as Shallowest Thinkers! Mimi nilinukuu maneno ya JK kwamba endapo KCC itakuwa Sh.315,000 basi bajet ya salary peke yake kwa mwaka itakuwa abt 6 Trilioni! Hesabu zako zinaonesha JK ni muongo kv at TSh. 315,000 plus benefits zinazoenda kwenye pension funds, bajeti ya salary itakuwa haifiki hata Sh. Trilioni 2 (kwa assumption kwamba Employees 400,000 @ 315,000/=!!!!!!!!) Ama kweli, wa-TZ tuna safari ndefu! Ikiwa nawe ni Greatest Thinker, yule aliye Shallowest Thinker atakuwaje?

Yeyote anayehitaji kutoa approximation zake kuhusu bajeti ya salary itakuwaje lazima aangalie yafuatayo!


  • · Kuna grades ngapi za mshahara and their corresponding salary values



  • · Kuna wafanyakazi wangapi kwenye kila Grade



  • · From 104,000 to 315,000 ni increase for abt 200%; kuwe na increase ya % ngapi kwa kila grade iliyosalia!

Ukishapata hayo majibu, ndipo unaanza kukokotoa and not as simple as taking 315,000(KCC) x 400,000(employees)x12(annual budget)!!


Mkuu, mimi na wewe hapo mbumbumbu ni nani? Kwa taarifa yako, sina interest yoyote kwa ama JK, CCM wala serikali yake! Sina ndugu hata mmoja aliye angalau kwenye midle level ama serikalini au CCM! And 2b straight 4wad, sina ndugu yeyote aliye kwenye nafasi yoyote ya uongozi ama serikalini au CCM! Mimi mwenyewe, wala sijui huyo JK anafananaje kv sehemu pekee ambayo nimewahi kumuona ni 4rm TV! Ktk uongozi wote wa CCM na serikali yake; nimewahi kukutana na Mh.Membe peke yake miaka kadhaa iliyopita (2004) and am sure 100% hata leo akiniona hawezi kunikumbuka! Hiyo kadi yenyewe ya CCM wala sijui inafananaje! Nimekupa maelezo yote hayo ili uone tofauti iliyopo kati yangu na wewe! Am sure, wewe unaoongelea ushabiki zaidi kv i guess una some interests na one of political part, in particular CHADEMA! utakuwa ama kiongozi, mwanachama au unafahamiana na wa2 wa huko! Pamoja na kujinadi kwamba hata ukinipa data sitaambua lolote; wewe mwenyewe umesha-prove ubovu wako! Next time, kabla hujaenda kwenye Excel na kufanya irrelavant calculations, unatakiwa kwanza ku-draw logical assumptions na sio kukurupuka na kuingiza minamba kwenye Excel b4 hujafanya reasoning yoyote!
 
Mkuu NasDas UMETUMWA!!
Wote tulimsikia JK siku hiyo wa kumsapoti tulisapoti lakini hakuna rais duniani ambaye anaweza kuendesha mambo yake bila wafanyakazi.
Inahitaji tact na ustadi mkubwa kuwadhibiti wafanyakazi kisiasa.
Ni dhahiri statement ya JK haikumsaidia sana kisiasa
Wafanyakazi hao ndo watu walio karibu naye, madereva, makarani, mamesenja nk.Watu hawa watakuwepo kwa kipindi cha rais yeyote yule.
Tusijaribu kutengeneza the Fifth Column kwa ushauri kama huu usio na mbele wal nyuma

Mkuu Gwakisa, sijatumwa na yeyote and am still firm 2 wht i said!!! Let's be honest banaa, nini hasa alitamka JK kama sio hicho nilichonukuu mimi? Nakumbuka vizuri mkuu, kichwa changu sio karai kiasi hicho! Hakusema hataki kura za w/kazi bali ikiwa sharti la kupata kura hizo ni kuwalipa KCC Sh.315,000/= basi ni heri wasimchague kv hicho kiwango hataweza kulipa! Ingekuwa wewe ungesemaje? Nichagueni na mkinichagua nitawalipa wakati unafahamu hutaweza kufanya hivyo? Achana na calculation za wakali wa hesabu wa primary waliokokotoa kwamba annual salary budget itakuwa 315,000x400,000x12!!!!! Najuaa hata kama ulipata F ya maths, bado utajuwa tu kwamba hizo ni calculation za kimbumbumbu kuliko zote nilizopata kuziona!!
 
"Si hivyo tu, mimi ni mtu ninayeaamini kwamba Watanzania (including na waliomo kwenye uongozi wa upinzani) hatuna uaminifu kabisa!"-QUOTE


Huyu ND anaboa sana hasa anaposema watanzania wote sio waaminifu! Mtu anayeishi nje ya mshahara wake akitegemea wizi na ujanja ujanja wa kazini utamjua tu.......anafikiri wote ndo hivo hivo. Kimsingi ameridhika kuwa wizi na ujanja ujanja ndo mfumo wa maisha ya wafanyakazi Tz. hivyo hata watawala wengine wakija uzi ni ule ule. Wengine tunategemea tu mshahara kaka, ndio maana tunalia uongezwe.

Mzee wa Mjengoni; kidole na jicho bana! Nimesema ni Watanzania wachache sana walio waaminifu!!! Hata kama hutaki huo ndio ukweli wenyewe! Nayasema haya kwa uchungu na wala si kwa kuyaonea ufahari! Na wengi walio waaminifu hawajapata ule mwanya wa kweli wa kudhihirisha uaminifu wao! Inauma sana, lakini huo ndio ukweli wenyewe! Ninachosema mimi, tuachane na dhana kwamba wasio waaminifu ni wale walio CCM tu, bali hili ni gonjwa la wa TZ wengi!
 
NasDaz kama umetumwa na waliokutuma, nenda kawambie JF "hawadanganyiki". Hii ni Blog ya great thinkers ambapo wewe huwezi kujadili baadhi ya maeneo. Unakurupuka kudefend mafisadi. Angalia hapa chini kwenye jedwali, hata kama uli ishia la nne utaelewa tu. Ikishindikana kuelewa basi nenda ukafanyiwe utafiti wa akili huenda zimekaa upande. Mahesabu haya JK angeyachunguza asinge toa hutuba kama ile kwa "wazee wa Dar". Katika hotuba mbaya alizowahi kutoa, ile imeingia kwenye rekodi ya vichwa vya watanzania. Hai itajiki elimu ya chuo kikuu kujua mahesabu haya, achana na watumishi 350,000, tufanye 400,000. Sasa endelea


JEDWALI LA GHARAMA

Maelezo
Kiasi
Miezi
Jumla
Kifupi
Watumishi (Iliyokadiliwa)
400,000
12
4,800,000.00
Million 4.8
Mshahara
315,000/=
12
1,512,000,000,000.00
Trillion 1.512
Akiba( Mifuko Ya Jamii)
315,000 x 15%
12
226,800,000,000.00
Trillion 0.227
Bima Ya Afya
315,000 x 3%
12
45,360,000,000.00
Trillion 0.045
Jumla (Gharama)
371,700.00
12
1,784,160,000,000.00
Trillion 1.784
NB: Trillion ni Million Million ie. 1,000,000,000,000.

Pamoja na michango ya security funds Yaani haifiki hata Trillion 2!
Ukishindwa hesabu hii rahisi, basi akili zako changanya na za mbayuwayu utapata jibu. Maana inawezekana unatumia akili za gong'ota, yaani kila akili yako ikogonga, inaishia kujiridhisha kuwa CCM ni chama kigumu kama gogo la mti!

Naomba kuuliza hivi hawa watumishi wote uliokokotoa wanapata kima cha chini!!
ni swali tuu baba angu!!

 
kima cha chini mwaka jana 104,000 =usd100 (exchange rate of 1usd = 1000), mwaka huu 135,000 =usd90 (exchange rate of usd1 = 1,500). Ndiyo tusema serikali imepatisha mishahara ya watumishi toka usd100 to usd90. Hatudanganyiki!!! kura tutampa anayejali masilai yetu.
 
Back
Top Bottom