Kibongobongo kumiliki milioni 100 kabla ya miaka 30

Milion 100 kuna watu wanashika tena below 25yrs..Kuna chalii mmoja alifeli kabisa Ile division 0 alienda mererani alipata zaidi ya 500milioni na wapi wengi Tu kipindi mererani haina ukuta walishika hizo hela...
Kuna Jamaa mwingine namfahamu alianza na Mali kauli bila mtaji na sasa na biashara ya milion 200++ na yupo kama 33yrs
Kama ni hivo basi kwa hakika inawezekana
 
Anza kumuwekea 200k fixed toka akiwa tumboni akifikisha 25 atakuwa na 60mil za kuanzia maisha. Kama ulimpa principles za biashara by 30yrs atakuwa na kama 200mil hivi. So utajiri wa mtoto wako ni juu yako wewe, kama usipomuandalia njia mwanao atakuwa kapuku kama wewe tu labda abahatike kujitafuta kwa kudra za mwenyezi mungu.


Umetisha
 
Inawezekana.

Ila lazima awe na kipaji yaani gifted. Na asiwe na aibu.

1.Mfano akiwa MC wa sherehe mwenye jina kubwa mapema anapata hizo hela.

2. Akiwa msanii wa muziki mkubwa anapata hizo hela.

3. Akiwa content creater mkubwa toka mapema akafikia kuwa na jina kubwa kama mwijaku anapata hizo hela

Ila kwa kazi ya kuajiriwa haiwezekani
 
Haya wakuu wacha niwasaidie hili. Please note siuzi chochote hapa na nasikitika sijibu dm zozote za msaada au maombi. Kama ni maswali nitayajibu yote hapa kadri ninavyoweza.

Niko katika miaka ya 25-30 na net-worth yangu ni around 450 mil ongeza na punguza kwa sababu vingine sio liquid assets. Ila zaidi ya nusu ni liquid (cash and other assets easily changeable to cash). Imechukua takriban miaka 12 kufika hapa na nilianza kabla ya miaka 18. Kama ningepewa fursa ya kushauri mtoto wangu afikishe 100 mil kabla ya miaka 30 ningempa yafuatayo.

1. Kuanza from zero ni ngumu sana hivyo mpe mtoto advantage ya at least elimu. Kwa mimi nilipata elimu nzuri sana pamoja na watu kutoka maeneo tofauti. Japo sijatoka katika familia ya kitajiri, nilisoma katika shule yenye watoto wa kitajiri na ikanifungua sana akili kupitia kuzungumza nao na kutembea makwao kuona wanavyoishi na kujua wanavyofikiri. Pia nilipata mtaji mdogo (chini ya laki 5) ambao niliupoteza ila siweza sema kuupoteza hakukunifundisha kitu.


2. Mpe mtoto exposure. Kuna exposure ya outdoor na exposure ya indoor.

Outdoor ni kusafiri. Mpeleke mtoto aone maeneo mbalimbali watu wanavyoishi na fungua akili yake. Note kuwa sio kumpeleka tour Dubai bali kufanya vitu kama kumsomesha boarding mkoa mwingine au hata nchi nyingine (Uganda, Rwanda na Kenya gharama ni kama Tz) au kama mtoto ana ndugu katika eneo tofauti na ulilopo mpeleke akae nao katika likizo. Inafungua sana akili na uwezo wa kuelewa mahitaji ya watu na fursa kiujumla. Mimi sikupata hii ila some of the smartest thinkers around me wana hili.

Indoor ni vitabu. Hili nilipata mimi. Himiza usomaji wa vitabu toka utotoni. Kwangu mimi biography na vitabu vya historia/life stories ni pendwa sana kwani vinakupa fursa ya kuishi maisha ya miaka 50 ya mtu mwingine ndani ya kurasa 300. Kila kitabu kinakupanua akili na uwezo wa kuona mambo ambayo wengine hawaoni. Vitabu vyovyote vinafaa kadri mtoto anavyokuwa atajenga matamanio yake mwenyewe vile anavyopenda zaidi.


3. Jenga tabia ya kuwa na bidii na uwezo wa kujisimamia kwa mtoto. Ripoti zangu za shule zilikuwa ni jukumu langu kupresent kwa wazazi na kujieleza. Nguo zangu (hususani za shule) nilianza kufua taratibu nikiwa na miaka 6. Nikichelewa basi la shule ni jukumu langu kuhakikisha nafika shule kwa njia nyinginezo. Uongozi pia ni sehemu ya hili. Kuwa kiranja wa darasa au hata kapteni wa timu ya mpira ni njia ya kujenga bidii na kujisimamia.


4. Mfundishe mtoto principle ya asymmetric risk and reward. Ukweli ni kwamba kuupata utajiri ni risky. Mfundishe mtoto jinsi ya kutambua fursa zilizo na risk ila uwezo wa kupata matokeo makubwa. Risk simaanishi iwe kitu cha hatari au kiwe haram. Bali kiwe kina possibility kubwa ya kushindwa ila akishinda kina manufaa makubwa. Kwa kuanzia vitu hivi ni kama uongozi wa shule nzima (head boy/girl), mashindano ya kitaifa ya riadha au masomo na kuanzisha klabu ya jambo flani shule na kuifanya kubwa. Kama uko open unaweza kumwambia aanza biashara ya kumwingizia pocket money. Vitu hivi vitamfundisha baadae achukue hatua anapoona fursa katika maisha.

5. Mfundishe mtoto kuhusu pesa. Atambue income, expenses, assets and liabilities kabla ya miaka 18. Kitabu cha rich dad na poor dad ni kizuri sana kwa hili. Unaweza kujumuisha na michezo kama Monopoly na Rich Dad The Game. Vitu hivi viliniwezesha niweze kusoma na kuanalyse Income Statements and Balance Sheet za kampuni za DSE kabla ya kuingia utu uzima. Atambue pia jinsi ya kusave na ikiwezekana mfungulie akaunti na kumpatia kadi ya benki akiwa mdogo. Hizi skills ni muhimu sana katika kutambua fursa na kutunza pesa baada ya kuzipata.


6. Mfundishe mtoto kutokuwa na wategemezi mapema. Japo si mara zote, una uwezekano mkubwa zaidi wa kufikisha 100 mil kabla ya 30 ukiwa hauna wategemezi. Wanawake/wanaume wa kuomba pesa sana na kukuegemea na muhimu zaidi kutopata watoto mapema. Kwangu mimi haya ni vema zaidi ikiwa baada ya miaka 25 na nzuri zaidi 30 kwa vitu serious. Hapohapo pia awe msiri katika pesa zake asivutie marafiki wanyonya pesa na ndugu waomba pesa kama mjuavyo katika jamii zetu za kiafrika.


7. Mfundishe mtoto kujifunza kutokana na failure (kushindwa). Safari haitakuwa rahisi. Hivyo pale unapoona mtoto ameshindwa katika jambo mfano kupata matokeo mabaya darasani au kufungwa mchezoni au hata katika mashindano hizi ni moment za kujifunza. Mwambie mtoto afanye tathmini nini hakikuenda sawa na aongee mbinu za kutumia hapo mbele ili mara inayokuja awe na uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa. Kumbuka usimuambie kushindwa ni vibaya kwani utamjengea hofu. Nashukuru kwangu mimi hili halikuwepo na kila ninapokosea najaribu kujifunza na kusonga mbele na nimeshindwa mambo mengi sana aisee haha. Hapa pia mtoto atajifunza kuhandle maumivu pamoja na upweke kwani kwa wengi safari ya mafanikio iko hivi.


8. Jenga audience inayokuamini. Mara zote ambazo nimefanikiwa katika biashara ni kwa sababu ya kujenga audience inyoniamini. Naweza sema hii ni shortcut yangu. Tumia majukwaa ya kijamii na hata maeneo ambayo unaishi au kupitia. Wote hao 'wana pesa zako'. Hii inamaanisha fundisha mtoto kuwa mwaminifu na kutoa value kwa watu kwani hivi ndio vitu vikuu katika kujenga audience. Nimeongeza hii point ni actionable kwa kila mtu hata kama si mtoto.

Hayo ni machache niliyoweza kufikiria kwa sasa, natumai mtapata chochote kitu na kukitumia katika maisha ya watoto wetu au hata wenyewe mkipenda.
Nondo muhim sana Intelligent businessman wakati unaelekea kupata mtoto zingatia haya kaka
 
Milion 100 cash at bank or assets/biashara yenye thamani ya milion 100?

Either of 2, mbona umeweka target ya mbali hivyo? Miaka 30 ni umri wa kuelekea uzee! At that age kama ni malengo au dreams, basi uwe na assets zenye thamani isiyopungua milion 400

Milion 100 iwe target ya kijana wa miaka 25!!
Miaka 25 milioni mia anatoa wapi!
 
Inawezekana ukiwa mjanja na kufanya shughuli zenye kipato kikubwa .

Ukiweza kujibrand online mapema ukiwa na miaka 25 unaanza harakati za kujibrand online . mfano kuwa kama kina mwijaku, hamissa mobetto, baba levo unatengeneza net worth ya milioni 100 kabla ya miaka 30.

Zama hizi hela ipo kwenye entertainment industry. Online entertainment inakutajirisha fasta kama hauna aibu na unajua kufosi vipaji
Branding ya kina mwinjaku na baba Levo Sidhani kama ina afya kwa jamii.
Ni symbol ya utumwa mambo leo na amini nakwambia haiwezi vuka generations moja.
 
Jf raha sana kila mtu tajiri.Ukweli nikwamba maisha ya mtaani tunayaona labda huko dar ila huku vijijini hata milioni tano ni kipengele.njooni usukumani huku hali tete kinyama.
 
Hela hizi mil 100 mnazipata wapi na njaa yote ipo hapo?
Yangu sijawai hata kuiona.
Inaingia na kupotea hukohuko benki.
 
Kuna watu zaidi ya million 60 TZ. Mwenye takwimu za fedha, ni watu wangapi wenye miaka 30 ambao wanamiliki binafsi fedha ama wealth >=TZS 100 million? Au tuseme hivi...kwa watu wote walio umri wa miaka 30 (wake kwa waume), ni wangapi kati ya hao wanamiliki cash ama wealth yenye thamani ya million 100? Kutoa mfano wa mtu mmoja mmoja tena kwa kusikia kwa watu wengine kwamba anamiliki zaidi ya hiyo pesa, siyo kiwakilishi kizuri kwa Tanzania nzima. Kwa mafikirio yangu mimi, hao hawazidi hata 1% ya watu wote wenye umri wa miaka 30.
 
Khaaa jamani humu kuna watu waovyo sana,eti miaka 25 amiliki million 100,hii haiji kichwani kabisa je huyu kijana alimaliza chuo lini,jamani jamani tusilishane matango pori humu sisi sote tunajielewa huwezi miliki million 100 ukapoteza mda humu,kusema la kseli kwangu mimi namiliki nyumba 2,gari 1 pikipiki za boda boda 4 heka 50 huwa nashika million 30 tena nina miaka around 34
Ukiwa una save 1M kwa mwezi ambayo ni ngumu itakuchukua miaka 10 kupata milioni 100😄 hizo nyengeza tuseme niyale matumizi makubwa n.k
 
Hiyo ukute mtoto wa kigogo, serikalini tena fisadi, ingawa wapo lkn familia kama bakhresa na "mo" ?
 
Back
Top Bottom