Rais Dkt. Mwinyi akishiriki Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mei 3, 2023, Zanzibar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Leo Mei 3, 2023 ni siku ya tatu ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani linalofanyika kwenye Ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar, mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.



VIONGOZI WAWASILI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman ameshawasili na kuingia ukumbini.

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amewasili na shughuli inaanza rasmi.

UTAMBULISHO
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Zanzibar, Hassan Khatib Hassan anafanya utambulisho wa Wadau walioshiriki kuwezesha Kongamano husika.

JOYCE SHEBE: Akitoa hotuba ya Maazimio ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe amesema

"Katika Kongamano la Mwaka 2023 washiriki wametoa mapendekezo mbalimbali kwa taasisi na Wadau wengine, sisi washiriki tumeazimia kutetea, kuimarisha, kuhamasisha na kutetea uhuru wa kujieleza wa Vyombo vya Habari kama msingi muhimu wa hai zingine za binadamu zinazochangia kuongeza uelewa wa wananchi kwa pamoja katika shughuli za maendeleo.
Shebe kuimarish.JPG

JOYCE SHEBE: Mwenyekiti wa TAMWA amesema “Mashirika na Wadau wa Habari yawakutanishe Wanafunzi wa kike na Wabunge Wanawake ili kujadili changamoto za ukatili wa kimtandao na kuwajengea uwezo ili watumie mitandao kwa ajili ya utetezi.”

JOYCE SHEBE (Mwenyekiti wa TAMWA) Kutetea na kulinda maslahi ya Nchi katika kulinda Haki za Binadamu kuliko kutanguliza maslahi ya wafadhili, kujenga na kuimarisha mitandao ya Wadau ikiwemo vyombo vya usalama ili kuweza kutatua changamoto za ulinzi na usalama kwa Waandishi wa Habari
Tumeazimia_kuimarisha,_kuhamasisha_na_kutetea_uhuru_wa_kujieleza.jpg

Kuwa na mfumo mmoja wa kuripoti matukio ya ukatili na unyanyasaji na ukiukwaji wahaki za waandishi wa habari pamoja na kanzi data ya maswala hayo tofauti na ilivyo sasa ambapo kila taasisi ina mfumo wake wa kuripoti

JOYCE SHEBE (Mwenyekiti wa TAMWA): Maazimio kwa Vyombo vya Habari, kuweka utaratibu wa kurithisha ujuzi na uzoefu, kuendeleza vipaji vya Waandishi chipukizi watakaoleta mafunzo, fikra mpya na ubunifu wa Kidigitali katika Vyombo vya Habari pasipo kukiuka maadili ya Uandishi wa Habari

Kuboresha maslahi ya Wanahabari ikiwemo mikataba ya ajira, amlipo kwa wakati na malipo na bima ya afya.

Kuongeza mafunzo kwa Wahariri wa Habari, kuendesha mijadala kati ya Wakongwe na Chipukizi pamoja na kuwekeza katika tafiti na kutumia matokeo ya tafiti hizo kwa faida ya jamii.

JOYCE SHEBE (Mwenyekiti wa TAMWA): Kuwekeza kwenye digitali ili kuzalisha maudhui yenye bora, pia kuanzisha madawati maalum ya kuhakiki taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ili kurejesha imani kwa Vyombo vya Habari wakati huu wa zama za digitali ili kuzuia taarifa za chuki.

Kutengeneza na kuimarisha sera na masuala ya Kijinsia na kuanzisha madawati ya kijinsia ili kushughulikia changamoto hizo kwenye vyombo vya habari.

JOYCE SHEBE (Mwenyekiti wa TAMWA): Maazimio kwa Waandishi wa Habari, kuripoti na kupaza sauti kwa wasio na sauti kuhusu Wanawake na makundi maaluma wakiwemo, wenzetu walemavu na wanaoishi katika mazingira magumu. Kujiendeleza na kujisomea ili kuendana na kadi ya digitali.

Waandishi wa Habari Wanawake kutumia fursa ya kidigitali kujiendeleza, kutangaza kazi zao na kutumia fursa zinazopatikana pia washiriki katika matukio muhimu ya kihabari.

JOYCE SHEBE (Mwenyekiti wa TAMWA): Taasisi za Mafunzo zinatakiwa kujumuisha mafunzo ya kidigitali katika mitaala lengo ni kuendana na kasi ya giditali pamoja na kitisho kwa usalama kwa Wanahabari

Maazimio kwa Serikali ya Zanzibar, ione namna ya kuharikisha mchakato wa marekebisho ya Sheria ya Habari na kuwashirikisha Waandishi wa Habari katika mchakato huo wa mabadiliko ya Sheria ili kutoa mazingira mazuri kwa Wanahabari kufanya kazi kwa uhuru.

Pia kutathmini na kurekebisha Sheria za Habari mara kwa mara ili ziweze kuendana na mabadiliko ya digitali yanayotokea kila baada ya muda.

JOYCE SHEBE (Mwenyekiti wa TAMWA): Serikali ione umuhimu wa kuharakisha mchakato marekebisho ya Sheria ya Utangazaji ya Mwaka 2003 ili iendane na uhalisia au kuktadha wa sasa.

Kyle Nunes (Balozi wa Canada): Nilisoma Unandishi wa Habari miaka 30 iliyopita, hivyo najua maana ya kutafuta ukweli wa taarifa na kuifanya Serikali iwe inawajibika.

Kuna madhara makubwa ya kutokuwa na taarifa sahihi, nimefurahishwa kuona kuna mabadiliko makubwa yametokea tangu kipindi nilichoma uandishi na hali ilivyo sasa.

KYLE NUNES (BALOZI WA CANADA): Ni kazi ngumu kwa Mwanamke kuwa Mwandishi wa Habari, wanapata changamoto kubwa sana, wanastahili pongezi kutokana na kukabiliana na ukatili na manyanyaso mengi
bALOZI.JPG

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI: Nimefurahi kusikia maadhimisho haya ya Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yamefanywa kwa ushirikiano wa Wadau mbalimbali wa Habari.

Nawapongeza kwa kauli mbiu ya ‘Kuunda Mustakabali wa Haki’, lengo la siku hii ni kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari na Serikali kukutana na Wadau wote ili kujadili mustakabali wa tasnia.
Mwinyi.JPG

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI: Kutokana na shughuli zilizofanyika inadhihirisha majukwaa haya ni muhimu kuibua changamoto za kisera na kuangalia namna bora ya kuendesha Vyombo vya Habari.

Serikali zote mbili zinathamini na kuheshimu uhuru wa Vyombo vya Habari na uhuru huo umeendelea kukua siku hadi siku.

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI: Taarifa YA Idara Habari – MAELEZO inaeleza kutoka Bara kuna magazeti 312 yaliyosajiliwa Nchini hadi kufikia Februari 20, 2023, wakati kabla ya uhuru wa Tanganyika kulikuwa na magazeti 10 tu.

Taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hadi Februari 2023 kulikuwa na Radio 218, TV 68, Radio za Kimtandao 8, TV za Kimtandao 391, blog na majukwaa 73, cable opareta 53 zimesajiliwa Tanzania Bara.
Mwi Uhuru.JPG

Wakati huo taarifa za wakati wa uhuru zinaonesha kulikuwa na kituo kimoja cha Redio, hakukuwa na televisheni, blog wala majukwa aya mtandaoni.

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI: Upande wa Zanzibar pia kumekuwa na kasi kubwa ya usajili mpya wa Vyombo vya Habari hasa vya kielektroniki kupitia Tume ya Utangazaji.

Takwimu zinaonesha TV 21 za kawaida, 38 za mitandao zimesajili, Redio 27 zikiwemo za masafa ya FM na ya Jamii zimesajiliwa.

Usajili mkubwa wa Vyombo vya Habari umeonekana zaidi Mwaka 2020 na 2023, ni ukweli usiopingika kuwa Sheria Kanuni na Taratibu zetu ndizo zinazoruhusu uwepo wa vyombo hivyo.

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI: Wingi wa Vyombo vya Habari unaongeza uhuru wa kujieleza na uhuru kusambaza habari.

Sheria ya Habari upande wa Zanzibar tayari mchakato umeshaanza ambapo dhumuni lake ni kufuta usajili wa Magazeti na kuwa na Sheria nzuri inayohusiana na masuala ya Habari hivi karibuni

Tanzania inathamini mchango mkubwa Wanahabari kwa kuwa Vyombo vya Habari vimeshiriki katika kutoa elimu na kulinda amani na mshikamano wa kitaifa, pia kuitengenezea taswira chanya kimataifa.

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI: Vyombo vya Habari vimekuwa vikifichua vitendo viovu ambavyo zamani vilikuwa haviripotiwi kama mauaji ya vikongwe na Watoto wenye ulemavu hali ambao imesaidia Serikali kuchukua hatua katika kukomesha vitendo hivyo.

Pia sisi Wanasiasa tumesaidiwa sana na Vyombo vya Habari kufikisha ujumbe kwa Wananchi kuhusu sera na Tanzania tunatotaka kuijenga na kukuza Demokrasia Nchini.

Nitumie hadhara hii kushukuru na kuwapongeza Wanahabari katika ujenzi wa taifa letu.

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI: Vyombo vya Habari vinaweza kutoa mchango bora zaidi endapo Wanahabari mtazingatia uzalendo, weledi na maadili ya utoaji habari, vinginevyo vitaleta madhara makubwa kama ambavyo baadhi ya Nchi zimeingia kwenye machafuko kutokana na habari za kichochezi.

Tunapoadhimisha siku hii tujue hakuna uhuru bila mipaka au uhuru bila wajibu, kwa hiyo tunapotimiza wajibu wetu tuwe wazalendo kwa Nchi yetu.

DIDIER CHASSOT (Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania): Uhuru wa Habari ni chachu ya maendeleo ya nchi pia kutimiza Miaka 30 ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ni mafanikio makubwa na wakati mahususi wa kutafakari tulipotoka, tulipo na tunapokwenda.

Ni muhimu kupunguza vikwazo kwa wanahabari wanaofanya kazi zao za mitandaoni, kuondoa vifungo vya magazeti yaliyofungiwa, kuboresha mifumo ya kisera na Sheria katika Vyombo vya Habari na kushauri mabadiliko ya Sheria ya Sheria ya Vyombo vya Habari kama inavyopendekezwa na Wadau.

DIDIER CHASSOT (Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania): Kwa miaka 30 iliyopita kumekuwa na maendeleo makubwa ya Uhuru wa Habari ikiwemo hapa Tanzania.

Naipongeza Tanzania kuanza kurejea katika Uhuru wa Habari ndani ya Mwaka mmoja uliopita, Serikali na Vyombo vya Habari wote wameshiriki katika hatua hiyo nzuri.
 
Ajabu waandishi wa Tanzania nao watasherehekea hiyo siku, wakati sioni kama wapo huru kuandika yote yanayoigusa jamii yetu kwa uzito stahiki.

Tumejaa waandishi machawa wanaowaiga wenzao duniani kusherehekea siku isiyowahusu, wao wangetakiwa kusherehekea utumwa wao kwa watawala.
 
Leo Mei 3, 2023 ni siku ya tatu ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani linalofanyika kwenye Ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar, mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.
All the best
 
Back
Top Bottom