Siku ya Pili, Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, 02/05/2023 Zanzibar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Siku ya Pili, Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mei 2, 2023 Zanzibar, Kongamano hili linafanyika wenye Ukumbi wa Golden Tulip.



Mjadala unatarajiwa kuanza muda si mrefu kutoka sasa...

BAKARI MACHUMU: MAGAZETI YALIANZA KUWA NA HALI NGUMU HATA KABLA YA UVIKO-19
Mwanahabari wa Kampuni ya Mwananchi, Bakari Machumu anasema “Vyombo vya Habari magazeti na majarida vimekumbwa na hali ngumu ya kiuchumi katika miaka ya hivi karibuni, hali hiyo ilitokea hata kabla ya zama za #UVIKO19, hiyo ni kutokana na wafuatiliaji wengi kuhamia mtandaoni ambapo pia matangazo yalihamia upande huo.”

Amezungumza hayo katika siku ya pili ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inayofanyika, Zanzibar, akiongeza “Pamoja na maendeleo hayo ya kidigitali bado kwa Tanzania magazeti yamekuwa yakitumika kutengeneza ajenda mbalimbali ambazo zinakuwa gumzo Nchini.”
Machumu.JPG


BAKARI MACHUMU: WANAHABARI WANA FURSA YA KUTOA ELIMU KWA WENYE UHITAJI
Akizungumza katika siku ya pili ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inayofanyika, Zanzibar, Bakari Machumu ambaye ni mwanahabari kutoka Kampuni ya Mwananchi anasema “Mwaka 2022 kulikuwa na kikao kilichoandaliwa na Taasisi ya Serikali Mkoani Tanga, mmoja wa Wahariri wetu akaenda kutoa uzoefu wake kuhusu uandishi wa habari wa takwimu na jinsi gani tunavyoufanya.”

Anaongeza “Baada ya mjadala tulipata mwaliko kutoka taasisi nyingine ya Serikali wakiomba kupewa elimu ambayo ilitolewa na inavyoweza kuwanufaisha wao katika majukumu yao.”

Anasisitiza kuwa hiyo elimu hiyo ni sehemu ya fursa ambayo inaweza kuwa moja ya njia ya kuingiza kipato kwa Wanahabari au Vyombo vya Habari badala ya kutegemea chanzo kimoja.

NYONZO: VYOMBO VYA HABARI VITUMIE TETESI ZA MITANDAONI KAMA FURSA
Afisa Program wa JamiiForums, Francis Nyonzo anasema “Kuna dhana kuwa taarifa zinazotolewa na vyanzo vingi mitandaoni sio za ukweli lakini uhalisia ni kuwa ukiendelea kuandika taarifa ambazo hazina ukweli watu watakukimbia sababu hakuna anayependa kusoma habari za uwongo.”

Nyonzo anasema hayo katika Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Zanzibar, ambapo amesisitiza “Uwepo wa dhana hiyo unatakiwa kutumika kama fursa ya taasisi nyingine za habari kuwa na kitengo au utaratibu wa kuhakikisha taarifa zinazoripotiwa mitandaoni zina ukweli au la.”

Ameongeza “Mfano ukiwa na ukurasa wa #Instagram ambapo kazi yako ni kutoa taarifa za ukweli juu ya tetesi zinazosambaa mitandaoni, utapata watu na utakuza mtandao wako, ni suala la kutumia nafasi na kuacha kuwa na hofu kuhusu elimu ya digitali.”
Nyi.JPG


NYONZO: KATIBA INATOA UHURU WA MAONI NA TAARIFA LAKINI BAADHI YA SHERIA ZINAMINYA
Francis Nyonzo ambaye ni Afisa Program wa JamiiForums anasema “Kuna dhana ya kutaka kuwazuia watu kutoa taarifa kwa sababu tu hawana taaluma ya uandishi wa habari lakini Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa kila mtu uhuru wa kutoa maoni na taarifa bila kujali mipaka ya Nchi.

Anaongeza “Upande wa pili kuna Sheria na Kanuni zinazozuia watu kutoa maoni na taarifa kwa kuweka vigezo kadhaa, nitoe mfano mimi ni Mwanauchumi kitaaluma, inamaana sitakiwi kutoa maoni yangu ya uchumi mitandaoni kwa kuwa tu si Mwandishi wa Habari?”
Katiba.JPG


NYONZO: HAUWEZI KUIZUIA DIGITALI, UNATAKIWA KUJUA JINSI YA KUISHI NAYO
Afisa Program wa JamiiForums, Francis Nyonzo anasema “Kumekuwa na dhana kuwa digitali inaweza kuathiri Vyombo vya Habari vya magazeti na majarida, lakini uhalisia ni kuwa hauwezi kuzuia mabadiliko ya teknolojia bali unatakiwa kujua jinsi gani ya kuishi nayo.

Anaongeza kuwa "Kumekuwa na hali ya kupinga katika kila maendeleo ya kidigitali yanapokuja, mfano nilisoma Kitabu cha Martine Sturmer akielezea jinsi ambavyo Serikali ilikataa uwepo wa TV.”

Ameongeza kuwa hali hiyo ndiyo ambayo inatokea hata wakari huu ambapo baadhi wanapinga ongezeko la vyombo vya habari vya mitandaoni na vyanzo vingine vya mitandaoni.
Nyo.JPG


ROSE KIMANI: WAHARIRI, WAANDISHI WA HABARI WAFUNDISHWE KUENDESHA VYOMBO VYAO KIBIASHARA
Rose Kimani ambaye ni Meneja Miradi wa DW Akademie anasema “Unapozungumzia ustahimilivu wa Vyombo vya Habari haimaanishi fedha pekee bali kuna mambo mengi ambayo unatakiwa kuyafikiria kuhusu tasnia nzima ya Uandishi wa Habari ikiwemo ubora wa taaluma yenyewe.”
Amezungumza hayo katika siku ya pili ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani linayofanyika, Zanzibar, akiongeza kuwa elimu inatakiwa kutolewa zaidi kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kuwa na mtazamo wa kuendesha vyombo vyao kibiashara na kisasa zaidi.

ROSE KIMANI: KUNA ONGEZEKO KUBWA LA VYOMBO VYA HABARI VYA MTANDAONI KULIKO MAGAZETI
Meneja Miradi wa DW Akademie, Rose Kimani anasema “Tumefanya utafiti kwa kushirikiana na Aga Khan University kuangalia mambo ambayo yanaweza kuchangia maendeleo chanya katika Vyombo vya Habari ya Afrika Mashariki na kuangalia miundo ya taasisi, mifumo na hali ya kiuchumi.”
Amebainisha kuwa utafiti wao umehusisha Vyombo vya Habari zaidi ya 500 kwa Afrika Mashariki kuanzia Septemba 2020 hadi Agosti 2021 na kubaini kuwa zaidi ya nusu ya Vyombo vya Habari zilivyo hai vimeibuka ndani ya miaka 10 iliyopita huku magazeti mengi yakiwa na umri wa miaka 11 na zaidi
Rose1.JPG


ROSE KIMANI: VYOMBO VYA HABARI VINATEGEMEA MATANGAZO YA BIASHARA KWA 88.9%
Meneja Miradi wa DW Akademie, Rose Kimani anasema utafiti walioufanya katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Aga Khan University kwa Mwaka 2020 hadi 2021 wamebaini kuwa Vyombo vya Habari vingi vinategemea matangazo ya kibiashara kwa ajili ya kujiendesha na ndiyo njia yao kubwa ya kuingiza kipato kwa Asilimia 88.9.

Ametaja vyanzo vingine vya kuingiza mapato walivyobaini ni; maudhui ya kibiashara (70.4%), matangazo ya Serikali 65.2%, Wafadhili 41.1%, harambee (24.9%), Wafuasi wanaojisali 22.2%, Mauzo ya huduma 21.9%, Uuzaji wa nakala 20%, Ruzuku 19.3%, Mauzo ya bidhaa 17.09%, Mikopo/uwekezaji 15.6% na nyinginezo 11.9%.

MSIGWA: DUNIA IMEBADILIKA, KUNA BAADHI YA VITU HATUWEZI KUZUIA KWA SHERIA
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Gerson Msigwa anasema “Kuna jambo lilizungumzwa hapa jana (Mei 1, 2023) limeleta taharuki Nchi nzima wakati sisi tulikuwa tunajengana, ulikuwa ni mjadala tu kuhusu Wachekeshaji wanaofanya vipindi makini kwenye vyombo vya habari waende wakasome."

Anaongeza “Yale yalikuwa ni majadiliano tu, Dunia imebadilika sana, kuna baadhi ya vitu huwezi kuzuia kwa Sheria lazima twende na kasi ya mabadiliko.”
Msi.JPG


BALILE: HATUTAKIWI KURUDI NYUMA KUHUSU MUSWADA WA HABARI
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (#TEF), Deodatus Balile anasema “Kuna watu walitaka tuukatae Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari lakini tukajenga hoja kwa nini hatutakiwi kuukataa japokuwa kweli kuna mambo yanahitaji kurekebishwa.”
Amesema kuna vifungu vingi vinavyotoa unafuu kwa Wanahabari ambavyo mwanzo havikuwepo, hivyo Wadau wa Habari wanatakiw akuukubali japo kuna vipengele vingine vya kurekebisha lakini sio kuurudisha mchakato nyuma.

Ameongeza “Kuna Sheria ambayo ilikuwa inaruhusu Mwandishi ashtakiwe kwa kutoa taarifa za kiongozi wa Serikali, Bungeni au Mahakamani inafutwa, sasa hivi ukimuandika au kumsema kiongozi anatakiwa akakushtaki yeye binafsi.”
Ba.JPG


TABIA: WANAHABARI TURIPOTI MATATIZO YETU IKIWEMO UKATILI WA KIJINSIA
Tabia Makame Mohamed, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) anasema “Waandishi wengi hawana mikataba na hiyo ni moja kati ya haki za msingi ambazo tunazikosa licha ya kuwa tumekuwa tukipiga kelele.”
Anaongeza kuwa “Pia suala la haki ya kijinsia zisiishie katika kutamka mitaani na kwenye habari za wengine bali hata sisi wenyewe Wanahabari tunatakiwa kulisisitiza hilo, kuna mambo kadhaa ya ukatili wa kijinsia umekuwa ukitokea na watu wanakaa kimya.”
Zen.JPG


EILEEN MWALONGO: WADAU WA HABARI WASIACHIE KILA KITU KWA SERIKALI, WATUMIE VIZURI FURSA ZILIZOPO
Afisa Program wa JamiiForums, Eileen Mwalongo anasema “Kitendo cha kushiriki katika Kongamano kinatakiwa kitumike kuwa njia chanya ya kufikisha ujumbe Serikalini na kwa Wadau wote husika ili mapendekezo yafanyiwe kazi.”

Anaongeza kuwa “Ushiriki usiishie katika kuwakabidhi Serikali mapendekezo kisha tuishie hapo, yale ambayo yapo ndani ya uwezo wa wetu tuyafanyie kazi kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi taasisi binafsi na sio kila kitu kusubiri maamuzi ya Serikali, Wanahabari na Wadau wajifunze kutumia fursa zilizopo kwa umakini.”
Ei.JPG
 
Back
Top Bottom