Makala ya BBC: Uchambuzi wa Miaka 30 ya uhuru wa watu wa Afrika Kusini na jinsi wanavyohisi

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
821
1,698
Watu wa Afrika ya kusini wanafanya uchaguzi mkuu wao hapo Mei 29, 2024 ukiwa ni uchaguzi mkuu wa 7 wa kidemokrasia tangu kuanguka kwa utawala wa kikandamizaji na kibaguzi wa wazungu wachache mwaka 1994.

Ifuatayo ni makala fupi iliyoandaliwa na mwandishi Nomsa Maseko wa BBCSwahili kuangazia Waafrika Kusini wanavyohisi kuhusu miaka 30 ya uhuru wao na hapo walivyo sasa

Wewe Mtanganyika unahisi nini katika miaka 63 ya uhuru wetu toka kwa ukoloni wa Mwingereza? Kuna mabadiliko? Uhuru wa kijamii na kiuchumi Tulioupigania tumeupata au mambo yako vilevile pengine kwa ubaya zaidi kuliko wakati wa mkoloni?
===================================
Soma👇👇👇

Huku uchaguzi ukikaribia nchini Afrika Kusini, mwandishi wa BBC Nomsa Maseko anaangazia miaka 30 muhimu ya demokrasia na jinsi nchi hiyo ilivyobadilika tangu kumalizika kwa mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Mama yangu aliniambia alipopiga kura yake tarehe 27 Aprili 1994 ilihisi kana kwamba anapiga "kura ya kutoka jela" - alijisikia kuwezeshwa.

Alikuwa na umri wa miaka 43 wakati huo - na kama mamilioni ya Waafrika Kusini wengine ilikuwa mara ya kwanza kupiga kura.

Ilikuwa ni kilele cha miongo kadhaa ya upinzani na mapambano ya silaha dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi na vurugu la wazungu wachache.

Nilikuwa mdogo sana kupiga kura wakati huo, ingawa niliruhusiwa na maafisa wa uchaguzi kupaka rangi kidole changu, ili nami nipate kujua maana yake na kuungana na weusi walio wengi walionyimwa haki ya kuwa huru, hatimaye kuchagua serikali yao wenyewe.

Ilikuwa ni hali ya wasiwasi siku chache kabla ya uchaguzi kukiwa na hofu kubwa ya kutokea ghasia za kisiasa. Mlio wa gesi ya kutoa machozi mara nyingi ulijaa hewani huko Kwa-Thema, kitongoji cha mashariki mwa Johannesburg ambapo tulikuwa tunaishi.

Wakati wa maandalizi ya upigaji kura mwaka 1994 kulikuwa na hofu ya kutokea ghasia.

Magari ya kijeshi yenye silaha yalipita karibu na nyumbani kwetu mara kadhaa usiku na usiku - ambapo milio ya risasi mara kwa mara ilisikika kwa mbali.

Alasiri kabla ya sikukuu, mimi na marafiki zangu tulikuwa tukicheza barabarani wakati lori jeupe liliposimama likiwa limejaa T-shirt, mipira na bendera za Chama cha Kitaifa.

Hiki ndicho chama kilichoingia madarakani mwaka wa 1948 na kuweka sheria za kibaguzi kuwagawanya wa misingi ya rangi, mfumo uliojulikana kama ubaguzi wa rangi, maana yake "kutengana".


Wengi wetu hatukuwahi kumiliki mpira mpya hapo awali, kwa hiyo tulifurahi kupewa mpira huo bila malipo. Lakini furaha yetu ilikuwa ya muda mfupi.

"Wandugu" - wanaharakati wa kupinga ubaguzi - walizichukua zote, fulana zilichomwa moto na mipira kutobolewa kwa visu vya mfukoni.

Tulikaripiwa na kuambiwa: "Usikubali tena chochote kutoka kwa adui." Huenda tulihuzunika, lakini tulielewa kwa nini.

Asubuhi ya kupiga kura ilikuwa tulivu sana. Kulikuwa na jua - lakini hofu na woga na hofu ilitanda miongoni mwa watu. Hawakuwa bado na imani 100% kuwa hali imebadilika..

Kituo cha kupigia kura kilikuwa mkabala na nyumba yetu - kwenye chuo cha ualimu. Bendera kadhaa za "amani" za rangi ya bluu na nyeupe zilikuwa zikipepea. Mawakala wa vyama vya siasa waliovalia rangi zao tofauti walikuwa wakibisha hodi nyumba moja hadi nyingine, kuwashinikiza watu kupiga kura.

Foleni ndefu zilishuhudiwa, huku vijana kwa wazee wakipanga mstari wakiinua ngumi hewani, wakiimba "sikhululekile", ambayo ina maanisha "tuko huru" kwa Kizulu.

Na nilihisi tofauti - kwa namna fulani kwa kutambua kwamba singehitaji kutazama juu ya bega langu na kujificha wakati wowote polisi wazungu waliokuwa juu ya farasi wakipita.

Hadi leo bado nina hofu ya mbwa wa Kijerumani, waliokuwa wakitumiwa na polisi wa utawala wa kibaguzi kutusaka na wakati mwingine kutushambulia sisi watoto bila sababu wakati wa doria zao.

Lakini kuna ukumbusho chanya wa mapambano ya ukombozi katika kitongoji cha Orlando Magharibi mjini Soweto - kiasi kwamba sekta ya utalii imeendelea huko.

"Miaka 30 iliyopita imekuwa pata potea kwa serikali yetu, tunashukuru kwamba wamekuwa wakijifunza"- Sakhumzi Maqubela, Mmiliki wa mgahawa wa Soweto anasema

Bw Maqubela alifananisha juhudi zake mwenyewe katika miongo mitatu iliyopita na zile za viongozi wa nchi.

"Miaka 30 iliyopita imekuwa ya pata potea kwa serikali yetu, tunaweza kuwapongeza kwa sababu wamekuwa wakijifunza.

"Nimebuni nafasi za kazi 500 hapa na ninafarijika nikijua kuwa juhudi zangu zimeleta mabadiliko."

Miaka ya mwanzo ya demokrasia ilikuwa ya matumaini: baada ya muhula wa kwanza wa Bw Mandela, Thabo Mbeki alishinda uchaguzi uliofuata; asasi za kiraia zilistawi - kama vile vyombo vya habari vya sauti na huru.

Lakini wengi wanahisi kuwa fungate imekamilika kwa chama cha ANC, ambacho bado kiko madarakani na kimegubikwa na madai ya ufisadi na malumbano ya uongozi. Nchi inakabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira, uhalifu wa hali ya juu na wengi bado wanakabiliwa na ukosefu wa huduma za msingi kama maji na umeme.

Kwa mchambuzi wa kisiasa Tessa Dooms, kuna maswali magumu ya kuzingatia katika maadhimisho ya miaka 30 ya uhuru.

"Ni wazi kwamba watu hawahisi na hawaoni kama mabadiliko waliyopigania yamefikiwa" Alisema.

"Kuna baadhi ya mambo ambayo bado yanafanana sana na siku za nyuma... viwango vya juu vya ukosefu wa usawa vinaendelea na hata vimeongezeka katika enzi ya demokrasia."

Mgogoro huo unaonyeshwa na mamia ya madaktari waliohitimu ambao wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mikubwa nchini kote kwa sababu ya ukosefu wa ajira.

"Inasikitisha sana kwa sababu watu wa Afrika Kusini wanahitaji sana huduma za afya lakini tuna mfumo ambao haufanyi kazi ndio maana tuna madaktari 800 waliohitimu ambao hawana ajira," alisema Dk Mumtaaz Emeran-Thomas, ambaye anajikimu kwa kazi ya kujitegemea isiyohusiana na ujuzi wake wa matibabu.

Vijana wanataka mabadiliko na hawana imani kwamba chama tawala cha ANC kinaweza kuleta demokrasia.

Baadhi yao wamepoteza matumaini kiasi kwamba wanasema hawatapiga kura kabisa
.

Bado idadi kubwa ya watu, kama mama yangu, ambaye aliishi enzi ya ubaguzi wa rangi, hawawezi kusahau mafanikio yaliyofikiwa na bado wanaamini mabadiliko yanaweza tu kuapatikana kupitia upigaji kura.

Na nitakapokuwa kazini tarehe 29 Mei, uchaguzi mkuu wa saba chini ya utawala wa kidemokrasia, nitamchukua binti yangu mwenye umri wa miaka sita naye apange foleni katika kituo kile kile cha Kwa-Thema ambako nilipiga kura mwaka wa 1994.
======================================
Makala ni kwa hisani ya: bbc.com/swahili

NB:
1. Ukisoma Makala hii, ni nini maoni yako ukilinganisha na miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika?

2. Ukisoma Aya ya mwisho ktk Makala hii utaona kuwa mtoto wa miaka 7 anapiga kura SA. Hii imenishangaza na kunishitua kuwa kumbe kuna nchi zimepiga hatua kubwa ktk demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi

3. Kwa mnaijua Afrika Kusini, hivi sheria yao ya uchaguzi inaruhusu mtoto wa miaka 7 kupiga kura?
 
Back
Top Bottom