Kibonde clouds fm kuwa mzalendo pia serikali iwe makini na matangazo kama haya

Huyu bwana angekuwa Rwanda nafikiri angekuwa mteja wa mahakama za Gachacha! Nasema hivyo kwasababu, angebisha kutotokea kwa mauaji ya kimbari nchini humo!
 
Duru za kiusalama nilizowahi kuzipata ni kwamba ilibidi vita ile ipiganwe maana duru zinasema kipindi kile Tz ilikua na hifadhi kubwa ya fedha za kigeni na uchumi baada ya hapo uchumi ulikua u-tek off kwa kasi. Lakini shauri ya siasa ya ujamaa, mataifa ya magharibi ingekua pigo na tishio kwao na wakaanza kuchochea ugomvi ili kuucripple uchumi wa Tz. Busara za Nyerere kweli zilifeli, na huu ndio ukweli/
 
Hapo kwenye RED, Nani wakutufungulia madai ya kulipwa kwenye ile vita? Museven ambaye Nyerer alimfadhili kambi huko Kilimanjaro kujimobilize na majeshi yake kwenda kupindua serikali ya Uganda na kutwaa Urais wa kudumu?

M 7 mwenyewe yuko bize kujanga shule huko kagera analipa fadhira.
 
huyu jamaa hanaga akili kabisaaaa,kuna kipindi wanafunzi wa UDSM walitaka wamuadabishe kwa kuropoka...!

katika mapimbi watangazaji hili lipimbi limezidi, kuna kipindi lilitaka aga dunia likanywa madawa likarudi barabarani nikajua huenda litaokoka aaaa wapi,,,,, ni kulopoka tu
 
Nafkiri elimu ya Kibonde ni ya 'magumashi' au 'tia maji tia maji'. Hajui kudadavua mambo, ni mropokaji, hasa pale anapokua anataka umaarufu kwa nguvu.

Mwenye taarifa za elimu yake atusaidie. Tusipate shida kujadili suala ambalo linahitaji elimu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kibonde vuvuzela tu, mbona hilo liko wazi sana.

Watanzania wanamchoraga tu. Siku hizi hata u-mc kazi hapati tena

Ngoja na siku hicho kibarua clouds kitaisha siku moja sijui utaenda redio msoga!


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kuna jamaa yake mmoja yupo Tabata aliwahi kunieleza kuwa Ephraim Kibonde ni mlevi sana na kauli kama hizi bila kujua madhara anayosababisha kwa jamii ni hatari sana kuwa karibu ya pombe wakati uko katika majukumu mazito muda mfupi unaofuata. Nasema ni hatari kwa sababu anguko la elimu linaanzia upuuzi kama huu wa kupotosha ukweli. Kibonde kama si mbumbumbu basi ni mjinga sana hivi amesahau jinsi Watanzania wengi walivyouawa pale Misenyi, kiwanda cha Sukari kilivyoshambuliwa na wafanyakazi kibao kuuawa, Kanisa Katoliki lilivyoshambuliwa watu wakauawa leo kwa kutumia hicho chombo Clouds (Mawingu) unataka watoto wetu waamini kwamba vita vya Kagera mchokozi alikuwa Mwalimu Nyerere na si Idd Amin Dada wa Uganda. Kibonde acha kulewa kabla na wakati wa kazi wewe ni kioo cha jamii, Yesu aliwahi kusema Ole wao Waandishi na Mafarisayo. Ole hizo ni kwa upotoshaji kama huo, Kibonde jaribu kujivika kitu kiitwacho AIBU labda UTABADILIKA.

Kauli kama hizi anatakiwa aonywe na wanausalama si wanasiasa kwani nadhani hajui kama kavuka mipaka anahatarisha Usalama wa nchi kwa kauli za kijinga.

Inatakiwa alazimishwe aombe msamaha na aisahihishe kupitia radio hio hio.
 
Sasa hapa uongo wa Kibonde ni upi? Kwani kuyumba kwa uchumi wa Tanzania kulianzia wapi kama si baada ya vita ya Uganda? Tulipotoka vitani tuliambiwa tufunge mkanda kwa miezi sita hadi leo hatukuwahi kuambiwa tufungue. Sasa uongo wa Kibonde ni upi katika hili?

Ni ukweli usiopingika kwamba Nyerere na Idd Amini walipigana kwa sababu ya interest zao binafasi na si interest za nchi hizo mbili. Nyerere anazijua chokochoko zake kwa Iddi Amini hadi kupelekea Iddi Amini kuvamia Kagera. Conflicts za watu binafsi zikazisababisha hizi nchi mbili kuingia vitani na watu wetu wasio na hati kupoteza maisha. Huu ni ukweli na wala hakuna sababu ya kuficha. Kama Kibonde ni msema hovyo, basi katika hili hajasema hovyo.

Watu wanamsifia Nyerere kwa kung'atuka, lakini wanasahau kwamba alilazimika kufanya hivyo baada ya kuona nchi haiongozeki, imeishiwa haina kitu, ilihali mashariti ya IMF na World Bank alishayakataa. Kuogopa kula matapishi yake, akaona bora kung'atuka. Lakini watanzania wasiojua, wanamwita eti ni mfano wa kuigwa. Nyerere naye ni janga lingine la Taifa, huo ukweli ni lazima usemwe. Umaskini huu kausababisha Nyerere. Alikuwa hashauriki, kichwa ngumu. Alichoamua yeye ndicho hicho hicho. Misimamo yake ya kitoto ndiyo iliyopelekea Oscar Kambona kukimbia nchi. Alikuwa hapingwi yule mzee. Msiyemjua mnasifia tu, kwa kuwa mnasoma kwenye magazeti.

Siasa zake za ujamaa lilikuwa ni pigo lingine kwa uchumi wa Tanzania. Mpango wake wa kuanzisha vijiji vya ujamaa ulisababisha si tu umaskini wa watu binafsi bali pia umaskini kwa serikali, kwa kuwa kitendo hiki kilifuatiwa na njaa kali ambayo ilisababisha serikali kuagiza chakula kingi kutoka nje. Na hii ni kwa sababu watu walishindwa kulima kwa utaratibu waliozoea katika makazi yao ya awali. Alisema waanzishe vijiji vya ujamaa ili kurahisisha upelekaji wa huduma, lakini hadi leo hizo huduma hazikuwahi kupelekwa. Lakini zaidi ya yote sera ya ujamaa ni sera isiyo rafiki wa uchumi.

Kikaja kipindi cha uhujumu uchumi ambapo mamilioni ya pesa yalitupwa mitoni na kufukiwa na mengine kuchomwa moto ili kujinusura na kamata kamata za Nyerere na Sokoine kwa yeyote aliyekuwa na utajiri mkubwa. Hii nayo iliongeza umaskini mkubwa si tu kwa watu bali pia hata kwa nchi. Maana haikusaidia kuboresha uchumi bali kuuangamiza. Lilikuwa ni wazo la hovyo. Badala atafute njia za kukusanya hizo hela ili ziingie serikalini, yeye aliwatishia watu, wakazichoma moto hela.

Kana kwamba hiyo haitoshi, sera yake ya kukifanya kila kitu kiwe chini ya miliki ya serikali ilikuwa ni ya kishenzi. Just imagine miaka hiyo Nyerere kwa muono wake finyu aliona awanyang'anye wananchi mali na kuzifanya za umma, akanyang'anya mashule, nyumba, na viwanda binafsi na kuvigeuza kuwa vya umma. Akawaweka mameneja ambao hawakuwahi kuwa hata shule wakashindwa kuviongoza. Leo tena tunachukua vile tulivyonyang'anya kwa watu na kuwaomba wageni waje waviendeshe. Ujinga huu. Kwanini tusingeviacha kwa wazawa tangu wakati ule? Halafu mtu anamsifia Nyerere?

Wazo lake la kuwafukuza wazungu na wahindi na waarabu pia lilikuwa la kitoto. Alikuwa ana sababu gani ya kuwafukuza watu ambao tulikuwa bado tunahitaji utaalamu wao? Ikumbukwe kwamba baada ya uhuru, tulikuwa hatujitoshelezi kitaalamu katika maeneo mengi zikiwemo hospitali na viwandani. Kwanini asingewapa uhuru wa kuchagua kuwa raia na kufuata sheria za nchi au kuondoka? Hatukuwa na sababu ya kuwafukuza haraka, badala yake tungezitumia mbinu na utaalamu wao katika kujijenga. Lakini Nyerere, sijui kutokana na kujiamini sana akawanyang'anya mashamba yao na miradi yao na kuwafukuza, cha ajabu hayo mashamba na miradi yote ilikufa just in ten years time.

Penye ukweli tuseme ukweli hakuna sababu ya kuuficha. Kibonde yupo sahihi.
 
umefanyia wapi utafiti wako!??

Ndio radio ambayo kila siku tunajaribu kuwakosoa ili waongee kitu kizuri kwa jamii! Kila kitu kinachozungumzwa na Clouds tunakileta humu kukijadili.

Kwani radio zingine zote watangazaji wake ni wazuri? Au vipindi vyao ni vizuri? Imagine, kwa wiki Clouds FM inaandikwa humu JF mara tatu hadi nne.
 
Jana katika kipindi cha jahazi cha radio clouds FM, mtangazaji wa wa kipindi Bw, Kibonde katika kujadiri kigoda cha Mwalimu Nyerere, Kibonde alisema kuwa Baba wa taifa Mwal J.K Nyerere ndiye aliyeleta anguko la uchumi wa Tanzania wakati nchi aliikuta katika hali nzuri sana, aliendelea kusema kuwa Mwalimu kuamua kwenda vitani na Uganda ndiyo chanzo cha umasikini ulipo mpaka sasa. Tena Kibonde aliendelea kuutangazia umma kuwa hapakuwa na sababu ya kwenda vitani kwaani Idd Amin hakuwa ameichokoza Tanzania. Ila Mwalimu alikuwa na sababu zake binafsi. Niliposikia habari hii binafsi niliona ni vibaya na kukosa heshima kwa kumsema baba wa Taifa hili katika chombo cha habari huku hakuna upande wa pili kulisemea jambo hili, Je taaluma ya habari inasemaje? Je ni halali kumsema mtu wakati hakuna upande wa pili wa kulisemea jambo hili. Na kama ni kweli hapakuwa nasababu ya kewnda vitani je Uganda wadai tuwalipe compensation ya kuanzisha viat bila sababu? Kama kibonde amepotoka tunaomba serikali iliweke sawa swala hili kwaani habari inavuka mipaka ya nchi. UTAIFA KWANZA SIASA BAADAE.
kwanza nikuulize ni akina nani walikaa na kuamua nyerere awe baba wa taifa,pili nyerere alikua ni binadam na makosa alifanya,na hili la kwenda vitan lilikua ni KOSA na liliigharim tanzania yapata dola milioni mia 5,halafu nikuulize tena kuwa NYERERE hapaswi kujadiliwa na sisi raia?nani wa kumjadili,,,,,aliyoyasema huyo KIBONDE ULITAKA AYASEME NANI?,,,Yaan unataka tumsifie tuu nyererer,yeye nani?Mwenyewe alishawah kukiri kwenye moja ya hotuba zake za kiswahili kabisa alisema 'SERIKALI YANGU IMEKAA MADARAKAN MUDA MREFU,MIAKA 25 SI KIDOGO,YAPO MAMBO MAZURI IMEYAFANYA NA YAPO MAMBO YA KIPUUZI,LAKINI HAWA WA SASA WANAYAACHA MAZURI NA KUYAFANYA YALE YA KIPUUZI'.SO KAMA ANAKIRI ALIFANYA UPUUZI WHY WEWE UNAAMIN KUWA HE WAS RIGHT,THINK TWICE
 
Kibonde,Gerald hawa wote vichefu chefu kabisa wanatumiwa..mnaiharibu redio ya watu fanyeni tafiti mpaka sasa mmepoteza sana mzuto kwenye masikio ya jamii.
 
Sasa hapa uongo wa Kibonde ni upi? Kwani kuyumba kwa uchumi wa Tanzania kulianzia wapi kama si baada ya vita ya Uganda? Tulipotoka vitani tuliambiwa tufunge mkanda kwa miezi sita hadi leo hatukuwahi kuambiwa tufungue. Sasa uongo wa Kibonde ni upi katika hili?Ni ukweli usiopingika kwamba Nyerere na Idd Amini walipigana kwa sababu ya interest zao binafasi na si interest za nchi hizo mbili. Nyerere anazijua chokochoko zake kwa Iddi Amini hadi kupelekea Iddi Amini kuvamia Kagera. Conflicts za watu binafsi zikazisababisha hizi nchi mbili kuingia vitani na watu wetu wasio na hati kupoteza maisha. Huu ni ukweli na wala hakuna sababu ya kuficha. Kama Kibonde ni msema hovyo, basi katika hili hajasema hovyo.Watu wanamsifia Nyerere kwa kung'atuka, lakini wanasahau kwamba alilazimika kufanya hivyo baada ya kuona nchi haiongozeki, imeishiwa haina kitu, ilihali mashariti ya IMF na World Bank alishayakataa. Kuogopa kula matapishi yake, akaona bora kung'atuka. Lakini watanzania wasiojua, wanamwita eti ni mfano wa kuigwa. Nyerere naye ni janga lingine la Taifa, huo ukweli ni lazima usemwe. Umaskini huu kausababisha Nyerere. Alikuwa hashauriki, kichwa ngumu. Alichoamua yeye ndicho hicho hicho. Misimamo yake ya kitoto ndiyo iliyopelekea Oscar Kambona kukimbia nchi. Alikuwa hapingwi yule mzee. Msiyemjua mnasifia tu, kwa kuwa mnasoma kwenye magazeti.Siasa zake za ujamaa lilikuwa ni pigo lingine kwa uchumi wa Tanzania. Mpango wake wa kuanzisha vijiji vya ujamaa ulisababisha si tu umaskini wa watu binafsi bali pia umaskini kwa serikali, kwa kuwa kitendo hiki kilifuatiwa na njaa kali ambayo ilisababisha serikali kuagiza chakula kingi kutoka nje. Na hii ni kwa sababu watu walishindwa kulima kwa utaratibu waliozoea katika makazi yao ya awali. Alisema waanzishe vijiji vya ujamaa ili kurahisisha upelekaji wa huduma, lakini hadi leo hizo huduma hazikuwahi kupelekwa. Lakini zaidi ya yote sera ya ujamaa ni sera isiyo rafiki wa uchumi. Kikaja kipindi cha uhujumu uchumi ambapo mamilioni ya pesa yalitupwa mitoni na kufukiwa na mengine kuchomwa moto ili kujinusura na kamata kamata za Nyerere na Sokoine kwa yeyote aliyekuwa na utajiri mkubwa. Hii nayo iliongeza umaskini mkubwa si tu kwa watu bali pia hata kwa nchi. Maana haikusaidia kuboresha uchumi bali kuuangamiza. Lilikuwa ni wazo la hovyo. Badala atafute njia za kukusanya hizo hela ili ziingie serikalini, yeye aliwatishia watu, wakazichoma moto hela.Kana kwamba hiyo haitoshi, sera yake ya kukifanya kila kitu kiwe chini ya miliki ya serikali ilikuwa ni ya kishenzi. Just imagine miaka hiyo Nyerere kwa muono wake finyu aliona awanyang'anye wananchi mali na kuzifanya za umma, akanyang'anya mashule, nyumba, na viwanda binafsi na kuvigeuza kuwa vya umma. Akawaweka mameneja ambao hawakuwahi kuwa hata shule wakashindwa kuviongoza. Leo tena tunachukua vile tulivyonyang'anya kwa watu na kuwaomba wageni waje waviendeshe. Ujinga huu. Kwanini tusingeviacha kwa wazawa tangu wakati ule? Halafu mtu anamsifia Nyerere?Wazo lake la kuwafukuza wazungu na wahindi na waarabu pia lilikuwa la kitoto. Alikuwa ana sababu gani ya kuwafukuza watu ambao tulikuwa bado tunahitaji utaalamu wao? Ikumbukwe kwamba baada ya uhuru, tulikuwa hatujitoshelezi kitaalamu katika maeneo mengi zikiwemo hospitali na viwandani. Kwanini asingewapa uhuru wa kuchagua kuwa raia na kufuata sheria za nchi au kuondoka? Hatukuwa na sababu ya kuwafukuza haraka, badala yake tungezitumia mbinu na utaalamu wao katika kujijenga. Lakini Nyerere, sijui kutokana na kujiamini sana akawanyang'anya mashamba yao na miradi yao na kuwafukuza, cha ajabu hayo mashamba na miradi yote ilikufa just in ten years time. Penye ukweli tuseme ukweli hakuna sababu ya kuuficha. Kibonde yupo sahihi.
nachokiona hapa watu wanamshambulia kibonde as kibonde na si kujadili hoja,japo huwa anaongea pumba ila hili la NYERERE KIBONDE amenena,sasa kama kuna mtu ana chuki na kibonde iz fine,lakin yupo sahihi kwa ishu ya jana
 
Kama nchi yetu ina usalama wa taifa basi nafikiri kibonde sitegemi kumsikia akitangaza tena, haya ni matusi kwa ndugu zetu waliopotea katika vita ya uganda. then very simple mtangazaji anapotosha umma kuwa Mwl alichokoza uganda? sawa tumeendelea na demokrasia lakini siyo katika maswala nyeti kama haya. Serikali ni sikivu tunajua itachukua hatua.
Huu upuuzi wa kumtukana Hayati Nyerere umeendekeza Serikali. Maneno aliyosema kibonde ndo yalikuwa yanatawala mihadhara ya kidini, wala serikali haikuchukua hatua kwa sababu wanazozijua wao. Hata walipoulizwa kwa nini serikali inaruhusu kikundi cha watu kuzunguka nchi nzima kikimtukana baba wa taifa, kama kawaida serikali ilikaa kinywa. wenye akili tukajua serikali ina hisa kwenye huo upuuzi.
 
Wakati mwingine tunashindwa kuwa wakweli na tunaongea kwa hisia. Mimi nasikitika sana ninapoona watu wanabeza juhudi za BABA WA TAIFA. Madhira, manyanyaso na uchungu vilivyowapata wazee wetu wa MULONGO, BUNAZI, KYAKA na maeneo mengineyo kupuuzwa ni ukosefu si wa akili na uzalendo pekee bali pia ni uzandiki na ukosefu wa akili. Juhudi za mwalimu kuleta ukombozi haziwezi kubezwa hasa sisi ambao ndugu, marafiki na jamaa zetu waliuawa na nduli. Wanaobeza hawasemi jùu ya viwanda, power stations etc
 
Sasa hapa uongo wa Kibonde ni upi?
Umeandika mengi.Inaonekana ulikuwa umejiandaa au umeikariri hiyo essay kiasi kwamba ukiguswa tu unatema cheche. Sasa hebu fafanua ni jambo gani lilianza kabla ya lingine kati ya haya uliyoyaandika.
1. Vita ya Kagera/Uganda.
2. Kung'atuka kwa Nyerere
3. Kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa
4.Utaifishaji wa mali za watu binafsi
5.Kufukuza wazungu, wahindi na waarabu.
Mimi nimefuata mtiririko wa aya za insha yako. Sasa ili kuweka historia sawa, hebu liambie jukwaa ni kipi kianza na kipi kikafuatia. Hii itatusaidia kujua kama matukio hayo yana uhusiano.
 
Clouds FM ni radio inayosikilizwa na wengi!!!
Pengine wengi hao unaowasema wewe watakuwa ni wavuta bangi ambao wengi wao ni madereva wa daladala na vijana wa vijiweni ambao ndiyo wasikilizaji wakubwa wa Clouds FM radio!!
 
Pamoja na kutompenda kibonde na redio yao . Kuhusu nyerere namuunga mkono. Bwana haambiliki anahusika sana na anguko la uchumi wa nchi hii kwa kuanzisha uhasama na idi amin na kupelekea vita iliyoturudisha nyuma sana kiuchumi. Tulikula sana ugali wa yanga enzi hizo, tulipanga sana foleni za sukari, sabuni na unga.
 
Umeandika mengi.Inaonekana ulikuwa umejiandaa au umeikariri hiyo essay kiasi kwamba ukiguswa tu unatema cheche. Sasa hebu fafanua ni jambo gani lilianza kabla ya lingine kati ya haya uliyoyaandika.
1. Vita ya Kagera/Uganda.
2. Kung'atuka kwa Nyerere
3. Kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa
4.Utaifishaji wa mali za watu binafsi
5.Kufukuza wazungu, wahindi na waarabu.
Mimi nimefuata mtiririko wa aya za insha yako. Sasa ili kuweka historia sawa, hebu liambie jukwaa ni kipi kianza na kipi kikafuatia. Hii itatusaidia kujua kama matukio hayo yana uhusiano.
Hili swali lina interest gani? Kufanya hayo kunamsaidia nani? Unataka kuandika historia, au unataka kuelewa ni kwa namna gani Nyerere alichangia kuanguka kwa uchumi wa Tanzania?
 
Back
Top Bottom