Vita ya maneno kati ya Rwanda na Burundi: Ina maana Ndayishimiye hajui tu kama amekalia kuti kavu?

Akilihuru

JF-Expert Member
May 20, 2022
1,444
2,833
Vipi wakuu.

Ki ukweli inashangaza sana raisi wa nchi ambayo ina jeshi, polisi na serikali, lakini anakosa kupata habari za kiintelejensia kuhusu kile kinachoweza kumtokea mbeleni endapo atataka kutumia mamlaka yake kama raisi kupambana na mtu au nchi inayomshinda kila kitu.

Najua fika kuwa Burundi ni nchi yenye nguvu za wastani kijeshi, hii ni kutokana na uzoefu waliokuwa nao pindi walipokuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka zaidi ya ishirini iliyopita. Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kujiona kuwa wanaweza kuingia vitani na Rwanda hata kidogo. Kufanya hivyo itakuwa ni kujichimbia kaburi yenyewe au raisi Ndayishimiye kukata kuti alilokalia mwenyewe na msumeno.

Katika East Africa nzima ukiitoa Kenya na Tanzania, hakuna nchi nyingine ambayo inaweza kusimama na Rwanda vitani ikashinda, hata hiyo Uganda yenyewe inaweza kuhenyeshwa na kutepeteshwa vibaya, achilia mbali nchi ambazo ni nyepesi kupigwa kama Burundi au Congo.

Kama kuna tatizo lolote kutoka Rwanda, ni vizuri ndugu Ndayishimiye alipeleke hilo swala katika vikao vya EAC community wakae walijadili na kama wakiona inafaa kulichukulia hatua watafanya hivyo bila kupendelea upande wowote maana wote ni wanachama wa EAC, lakini swala la kuingia vitani ni Rwanda, litakiweka kiti chake na maisha yake kwa ujumla hatarini, alafu baada ya kichapo Kagame akiwaruhusu wale waliokimbilia nchini Rwanda warudi wakaendeshe nchi yao, watu wataanza kulalamika kuwa Rwanda ilikuwa inafanya choko choko ili baadae iweke watutsi.

Muda ni huu wa kulishughulikia hili swala kwa njia za kidiplomasia, asingoja kuwa too late, akaja kujuta baadae huku akiwa njiani na familia yake wakitimkia Tanzania kupata hifadhi ya kikimbizi. Burundi ipo uchi sana mbele ya intelejensia ya Rwanda, hivyo ni rahisi kuangamizwa vibaya nchini mwao wenyewe.

Afunge mpaka wake na Rwanda, hilo ni sawa, lakini asithubutu kutuma jeshi likathubutu kuingia Rwanda kwa kisingizio cha kwenda kuwatafuta wabaya wake, ataangamia vibaya mno na sisi kwa vile tuko na yetu ya umeme, uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa 2025 basi hatutakuwa na muda wa kwenda kumsaidia kama tulivyomsaidia kurudi madarakani raisi Ngurunziza katika mapinduzi ya mwaka 2015.
 
Ila bongo Kuna wajuaji wengi ambao sio wafuatiliaji wa mambo na ujuaji unaponza wengi.

Najua umeanza kumjua Ndarishimiye alipoteuliwa kama Katibu mkuu wa Chama tawala nchini humo na Nkuruzinza na historia yake ya nyumba huifahamu

RAIS wa Burundi wa Sasa kabla ya kuingia siasani alikuwa ni mkuu wa majeshi wa nchi hiyo na sidhani kama wewe unayeishi uvinza utakuwa na taarifa za intelijensia za usalama na ulinzi kuliko mtu ambaye amewahi kuwa mkuu wa majeshi wa Taifa.

Tatizo mnajazwa upepo mnajaa kabisa ila nakuhahakishia Rwanda Sasa hivi atatulia mazima maana Tshisekedi anaichemsha dawa yao na aliahidi wakati wa kampeni
 
Mkuu humu JF kuna mashushu wabobevu wa nyuma ya keyboard wanajua kila kitu.
 
Back
Top Bottom