"Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano" - Seif Sharif Hamad

Awali ya yote poleni wote mliofikwa na misiba kwa ajali ya meli. Mwenyezi mungu awape afueni majerhi wote, uvumiluvu na utahimilivu wote walio katika dhiki na awapunzishe kwa amani waliotangulia mbele ya haki, Amina.

Tukioendelea na maombolezo nataraji kipindi rasmi kimepita na maisha yaendelee kwa uwezo wake manani.

Kilichonigusa leo ni suala la mwandishi kutoka gazeti moja la kila wiki anayejitambulisha kama Ahmed Rajabu. Huyu bwana amejikita katika kuelezea siasa za Zbar hasa mambo ya muungano. Anatumia kalamu yake vema sana kujificha nyuma ya mwavuli wa uandishi lakini ukweli ni miongoni mwa wale wasioutaka muungano. Hiyo ni haki yake kabisa japokuwa anapaswa kuwa muwazi.

Ukisoma makala zake nyingi anatumia neno Wzbar wanasema, wanataka wanashauri n.k kana kwamba yeye e ni msemaji wa Wzbar na kwamba anazo takwimu(ingawa hana zozote) za kuetetea hoja zake za kuwasemea Wzbar.

Kinachosumbua zaidi ni pale anaposemea ukumbini akijua kuna baraza analoweza kuwafikia wzbar na watanzania wengine kwa urahisi ili kukidhi haja yake. Pengine ni kuhofia mabaraza kama JF ndiyo maana anaamua kuandika magazetini bila kutakiwa kuulizwa.

Ukweli ni kuwa mwandishi huyu ni msomaji mzuri wa JF na anafuatilia mijadala vema kabisa. Kama nilivyosema makala zake nyingi ni kujibu hoja zitokanazo na mijadala (jambo jema) hasa hapa JF.
Moja ya mijadala anayoitolea majibu kwa kusema wzbar wamesema ni hii mada iliyopo sasa.

Ukisoma kwa undani anajibu post kiaina na naweka makala yake kuonyesha ninachosema kwa mantiki.

Ahmed ana haki kabisa ya kufanya atakavyo ndani ya sheria ikiwa ni pamoja na uhuru wa mawazo.

Ninamuomba ajitokeze hapa tujadiliane (two way traffic) ili tusaidiane kueleza mawazo ya kila upande kwa kina, bila kupotosha au kufanya kama ni mawazo yake binafsi nasi tueleze ya kwetu kwa namna hiyo hiyo na inapobidi kila mmoja awe tayari ku 'acknowledge' mawazo ya mwenzie kama sehemu muhimu ya uandishi.

Soma habari hii ikiwa ni moja tu ya habari zake. Hayo niliyoyawekea wino wa bluu ukitaka nitakupa post zake yalipojadiliwa.

itakiwayo ni ya haki, usawa na yenye uhuru wa kuamua… Ahmed Rajab
14 Sep 2011
Toleo na 203
USIKU wa Jumatano tarehe 11 Desemba mwaka 1963 Wazanzibari walimiminika kwa mkururo kwenye uwanja unaojulikana leo kwa jina la Maisara.

Ilipogonga saa sita za usiku wa kuamkia Alhamisi, bendera ya wakoloni wa Kiingereza iliteremshwa kwenye mlingoti mmoja na bendera ya Zanzibar huru ilipanda kwa maringo kwenye mlingoti mwingine.
Bendera hiyo ya Zanzibar huru ilikuwa ya mji mwekundu na katikati kulikuwa na duara ya kijani iliyokuwa na vikonyo viwili vya karafuu.
Si Wazanzibari wote walioushangilia uhuru huo. Ndiyo maana siku 32 baadaye serikali ya Zanzibar ikapinduliwa na kuwekwa madarakani serikali ya kijamhuri. Na ndiyo maana tukawa na masimulizi tofauti, mengi yenye kupingana au kukinzana, kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar na sababu zake.
Hivyo kuunga mkono au kuupinga uhuru wa mwaka 1963 au Mapinduzi ya mwaka 1964 kunategemea na iwapo mtu alinufaika au alitengwa na kupuuzwa na serikali za vipindi hivyo viwili yaani vya uhuru na Mapinduzi.
Kama siku 105 hivi baada ya Mapinduzi na 137 baada ya uhuru Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikaungana na Jamhuri ya Tanganyika kuunda Muungano wa Tanzania.
Hivyo, baada ya kuondoka kwa utawala Wakiingereza Zanzibar ilidumu kama nchi huru kwa muda wa hizo siku 138 tu.
Leo hii miaka 47 baada ya Muungano iwapo patafanywa kura ya maoni au ya maamuzi ya kuwauliza Wazanzibari ni Zanzibar gani waitakayo katika kipindi cha miaka mitano ijayo kufikia mwaka 2016 nina hakika kwamba ni wachache sana wataoamua kuitetea hali tuliyonayo tangu miaka 47 iliyopita.
Kila ninapoyapima matamshi ya Wazanzibari, wananchi wa kawaida na hata walio kwenye uongozi wa serikali na wa vyama viwili vikuu vya kisiasa Visiwani humo, yaani CCM na CUF, ninaona kwamba Wazanzibari wanataka mabadiliko, wanataka mageuzi makubwa na wanayataka leo kabla ya kesho.
Swali linaloibuka baada ya ugunduzi huo ni: iwapo wanataka mageuzi ni Zanzibar gani basi waitakayo? Igeukegeuke vipi hata iwapoze moyo? Kulijibu swali hilo wengi wanaitaja Tanganyika wakihoji kwamba mtu hawezi kuitathmini hali ya Zanzibar ilivyo sasa bila ya kuzingatia mahusiano yake na mshirika wake kwenye Muungano.
Sifanyi inda kulitaja tena na tena suala hili kwa sababu unapozungumza na Wazanzibari utaona kwamba ndilo jambo kubwa lililowakaa rohoni, limekuwa kama mwiba uliowakwama kooni.
Bila ya shaka wapo Wazanzibari wenye kuutetea Muungano kwa jazba kubwa. Lakini hao ni wachache sana. Walio wengi wanawavumilia kwa vile wanaona kuwa ni haki yao hao wachache kuwa na msimamo wautakao kwenye jamii ya kidemokrasi ambayo hao wengi wanajaribu kuijenga na itayokuwa ya muundo wa Zanzibar waitakayo.
Ukiwauliza watakwambia kwamba wanataka wawe na nchi yenye kuendeshwa kwa kanuni za utawala bora zinazoruhusu uhuru wa mawazo, wa kusema, wa chaguzi huru na za haki na wa kuwa na vyama vya kisiasa wavitakavyo.
Muhimu zaidi, watakwambia, wanataka kuwa na nchi itayokuwa na uhuru wa kujiamulia yenyewe mambo yake ya kiuchumi na ya kijamii bila ya kuingiliwa au kuwekewa mipaka na nchi yoyote nyingine.
Kwa ufupi, nionavyo ni kuwa Wazanzibari wanataka nchi yao ikomboke kisiasa, iwe na maendeleo ya kiuchumi, iwe nchi ambayo wananchi wake wanapata fursa sawa na wanatendewa haki.
Hayo hayajapatikana Visiwani hata katika kipindi cha kimapinduzi ambapo malengo makuu yalikuwa kuuondosha ukabila na kujenga jamii yenye usawa na ya kimaendeleo.
Hii leo ukizungumza na Wazanzibari utaona pia kwamba ndoto yao kubwa ni kukikalia tena kiti chao katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuwa memba kamili wa Umoja huo. Hali kadhalika, wanataka nchi yao iwe mshirika mwenye haki sawa kama nchi nyingine zilizo kwemye jumuiya kama ile ya Afrika ya Mashariki.
Wanaitaka Zanzibar yenye haki sawa kama za jirani zake na kama za nchi nyingine za Kiafrika.
Katika kuulizauliza kwangu nimeona kuwa haya ndiyo mageuzi ya awali wayatakayo Wanzanzibari. Wanataka kuihuisha tena nchi yao. Wanayatoa mawazo yao haya kwa ufasaha mkubwa na bila ya woga.
Hayo ni ya upande wa kisiasa
Ama kuhusu uchumi nimeona kwamba Wazanzibari wengi wanataka wawe wadau wenye haki sawa katika uchumi wao na kwamba wanayapata wanayostahiki kuyapata si kwa upendeleo bali kwa haki na usawa. Wanataka ukomeshwe ule mtindo ulioshamiri katika Utumishi wa Serikali wa kupeana kazi kwa sababu mwenye kutoa kazi na mwenye kuiomba ni marafiki au wana ujamaa au undugu au kwa sababu wote wanatoka chama kimoja cha kisiasa.
Ukiwageukia wafanya biashara utaona kwamba wanachotaka ni kuwepo kwa sekta iliyostawi ya biashara za kibinafsi zenye kutumia njia na nyenzo za kisasa za kufanyia biashara na za uwekezaji.
Zanzibar ya leo haikujengeka hivyo licha ya kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa lakini Wazanzibari wengi niliozungumza nao, walio ndani na nje ya serikali, wanaamini kwamba hiyo ndiyo njia ifaayo ya kuifuata. Hawataki tena pawepo ubaguzi na upendeleo katika Utumishi wa Serikali na wala hawataki idara hiyo ihodhiwe na watu fulani tu wakiwatenga wengine. Nimeitaja Idara ya Utumishi wa Serikali kwa sababu kwa mujibu wa mfumo uliopo sasa idara hiyo ndiyo mwajiri mkubwa wa wafanya kazi visiwani Zanzibar.

Kwa vile idara hiyo ni ya Wazanzibari wote haipaswi hata chembe kujiendesha kwa misingi ya kichama au kwa kufuata ilani za chama baada ya uchaguzi. Hata serikali nayo, hasa serikali ya mseto, haijuzu kutawala kwa misingi kama hiyo.
Serikali inachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba siasa haziingizwi katika Idara ya Utumishi wa Serikali na kwamba wanaoingia kwenye idara hiyo wana fursa sawa na wanaingizwa au kupandishwa vyeo kwa uwazi bila ya ubaguzi au upendeleo.
Watumishi wa idara hiyo wawe wanachaguliwa kwa mujibu wa elimu zao, ujuzi na uzoefu wao wa kazi na uwezo wao wa kufanikisha mambo.
Uchumi wa Zanzibar kabla ya Mapinduzi uliwanufaisha wachache kwa vile hapakuwa na usawa katika ugawaji wa utajiri wa visiwa hivyo. Serikali za baada ya Mapinduzi nazo hazikuweza kuirekebisha hali hiyo na ndio maana Zanzibar ya leo haina usawa. Bado utajiri umeselelea kwenye mikono ya wachache, ingawa wachache hao ni wengine na si wale wa kabla ya Mapinduzi. Wenye nacho ni kasoro ya asilimia tano ya wakaazi wapatao milioni moja. Wanaishi maisha ya raha. Wanamiliki vingi na mengi na hawana wanachokikosa.

Hawa ndio wenye kuwapeleka watoto wao kwenye skuli za kulipia ndani ya nchi ama nje ya nchi na wenye uwezo wa kujilipia kwa matibabu, wao na walio wao, ndani ya nchi ama nje ya nchi.
Wenzao, waso nacho, ndio walio wengi. Hawapati mahitaji ya kimsingi ya maisha ya kila siku — hawana maji, hawana umeme. Hawana mbele hawana nyuma. Wanaishi maisha ya kikabwela.
Hali za hawa walio wengi zitaendelea kusononeka ela ikiwa patafanywa mageuzi makubwa ili uchumi ustawishwe na kumfanya kila Mzanzibari ajihisi kwamba hakutengwa au kupuuzwa katika mfumo wa kiuchumi na wa kijamii wa nchi yake.
Wao ndio walio mbele kupigania waipate Zanzibar yenye jamii iliyo huru na usawa na wanaitaka sasa. Kila mmojawao amechoka na hataki tena kutolewa kafara au mhanga kwa makosa ya watawala wao. Kila mmojawo hataki tena kuwa mwathiriwa na janga la utawala usiojengeka juu ya misingi ya haki na uwazi.
Wanataka pawepo mpango kabambe wa maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii o aina hiyo utaweza kuyatengeneza mazingira yao kama vile ya makaazi na mastakimu, ya usafiri na ya mawasiliano. ambao kwa kipindi fulani kitachotajwa utawapatia hali bora za maisha na huduma bora za afya na elimu. Wanatumai kwamba mpang
Nimegundua pia kwamba Wazanzibari wa leo hawataki kubururwa na kurejeshwa nyuma. Wamekwishausahau usultani na ufalme na hawataki urejeshwe. Wanataka Zanzibar iendelee kuwa Jamhuri bila ya kuwa na Aila ya Kifalme ya vizazi vyenye kurithiana utawala. Wala hawautaki ufalme mamboleo. Kubwa wanalolitetea ni mageuzi katika medani ya kisiasa, mageuzi yatayofanywa kwa msingi wa ushindani wa haki na uchaguzi huru na yatayowezesha kuwapo kwa Idara ya Utumishi wa Serikali itayokuwa na uwezo wa kuwatumikia na isiyokuwa hodhi la kuchota kazi na kuwapa watu kwa sababu eti wana mwelekeo fulani wa kisiasa au wanakifuata chama fulani cha kisiasa. Kwa ufupi, hiyo ndiyo Zanzibar waitakayo Wazanzibari wengi.

Nilipo RED.

Nguruvi3,

Naomba ujuwe kuwa Kazi ya mwandishi yoyote ni kuelimisha na kuipasha habari jamii ikiwa pamoja na kuburudisha jamii husika. Kuna njia nyingi sana za kuwasilisha kwa jamii kwa kujenga hoja kwa kutumia Magazeti, Mikutano ya khadhara au hata kuandika katika mitandao mbalimbali kama huu wa JF. Kwani wote huko wanatoa fursa ya kujibu kwa kutoa khoja nzito na wala si kwa kejeli na matusi.

Mwandishi mahiri yoyote siku zote anaandika makala zake kwa kujenga hoja nzito katika magazeti ili kila mtu asome na kuweza kuhifadhi kama fasihi andishi kwa jamii ijayo. Na kama ikitokea kuwa kuna mtu ameona kuna mushkeri katika khoja zake basi naye ANARUHUSIWA KABISA KUANDIKA MAKALA YAKE KUPINGANA NA HOJA ZILE KATIKA GAZETI LILE LILE ILI KULETA MTIRIRIKO MZURI.

Sasa nawewe Bw Nguruvi3 una nafasi ya kujibu makala hiyo gazetini kama ni mwandishi mahiri. Kwani kwenye magazeti zinatakiwa khoja nzito tu na hairuhusiwi kuandika lugha za kejeli na matusi kama ambavyo zinavyotumiwa humu JF na unaona watu hawajengi khoja zaidi ya kutoa matusi na lugha za kejeli. Kwenye Gazeti utaweza kujipambanua uwezo wako kiandishi lather than JF.

 
Nilipo RED.

Nguruvi3,

Naomba ujuwe kuwa Kazi ya mwandishi yoyote ni kuelimisha na kuipasha habari jamii ikiwa pamoja na kuburudisha jamii husika. Kuna njia nyingi sana za kuwasilisha kwa jamii kwa kujenga hoja kwa kutumia Magazeti, Mikutano ya khadhara au hata kuandika katika mitandao mbalimbali kama huu wa JF. Kwani wote huko wanatoa fursa ya kujibu kwa kutoa khoja nzito na wala si kwa kejeli na matusi.

Mwandishi mahiri yoyote siku zote anaandika makala zake kwa kujenga hoja nzito katika magazeti ili kila mtu asome na kuweza kuhifadhi kama fasihi andishi kwa jamii ijayo. Na kama ikitokea kuwa kuna mtu ameona kuna mushkeri katika khoja zake basi naye ANARUHUSIWA KABISA KUANDIKA MAKALA YAKE KUPINGANA NA HOJA ZILE KATIKA GAZETI LILE LILE ILI KULETA MTIRIRIKO MZURI.

Sasa nawewe Bw Nguruvi3 una nafasi ya kujibu makala hiyo gazetini kama ni mwandishi mahiri. Kwani kwenye magazeti zinatakiwa khoja nzito tu na hairuhusiwi kuandika lugha za kejeli na matusi kama ambavyo zinavyotumiwa humu JF na unaona watu hawajengi khoja zaidi ya kutoa matusi na lugha za kejeli. Kwenye Gazeti utaweza kujipambanua uwezo wako kiandishi lather than JF.

samahani hii ni nje ya topic...! naomba usi generalize vitu. Kama hapa JF kuna watu wanatoa lugha ya matusi haimaanishi wote kwa ujumla wetu tunatoa lugha ya matusi. Tangu lini kwenye magazeti zinatoka hoja nzito tu? mbona tunaona matusi na kejeli kila uchao kwenye magazeti yetu?
Huyo Ahmed Rajabu anakaribishwa kuleta hoja zake hapa pia..!
 
samahani hii ni nje ya topic...! naomba usi generalize vitu. Kama hapa JF kuna watu wanatoa lugha ya matusi haimaanishi wote kwa ujumla wetu tunatoa lugha ya matusi. Tangu lini kwenye magazeti zinatoka hoja nzito tu? mbona tunaona matusi na kejeli kila uchao kwenye magazeti yetu?
Huyo Ahmed Rajabu anakaribishwa kuleta hoja zake hapa pia..!

Acha akili mgando wewe.

Si kila mtu ni member wa JF na si lazima kujiunga na JF ndio uwe muwazi zaidi. Nazidi kukushauri njia aliyotumia Ahmad Rajab ni kufikisha ujumbe wake kupitia gazeti na wewe kama amekuuma basi ni vizuri kupitia gazeti hilo hilo kupeleka khoja zake kupinga ile makala yake ili si tu kuleta mtiririko mzuri wa makala bali pia kuacha kumlazimisha kila mtu kutumia JF kama sehemu ya kupeleka mawazo yake kwa jamii.

Lakini kubwa zaidi ukiandika makala na kupeleka Gazetini unakuwa muwazi zaidi kwa kujipambanua na sio kujificha nyuma ya pazia na mhariri wa gazeti hilo anatumia taaluma yake kuhakiki hoja na lugha yako kabla kuifikisha kwa wasomaji tofauti na hapa JF.

Nazidi kukushauri kama imekuuma jipinde nawe utoe makala yako kwenye gazeti hilohilo ili kuonyesha umahiri wako katika kuandika makala.

Nakupa pole sana
 
Acha akili mgando wewe.

Si kila mtu ni member wa JF na si lazima kujiunga na JF ndio uwe muwazi zaidi. Nazidi kukushauri njia aliyotumia Ahmad Rajab ni kufikisha ujumbe wake kupitia gazeti na wewe kama amekuuma basi ni vizuri kupitia gazeti hilo hilo kupeleka khoja zake kupinga ile makala yake ili si tu kuleta mtiririko mzuri wa makala bali pia kuacha kumlazimisha kila mtu kutumia JF kama sehemu ya kupeleka mawazo yake kwa jamii.

Lakini kubwa zaidi ukiandika makala na kupeleka Gazetini unakuwa muwazi zaidi kwa kujipambanua na sio kujificha nyuma ya pazia na mhariri wa gazeti hilo anatumia taaluma yake kuhakiki hoja na lugha yako kabla kuifikisha kwa wasomaji tofauti na hapa JF.

Nazidi kukushauri kama imekuuma jipinde nawe utoe makala yako kwenye gazeti hilohilo ili kuonyesha umahiri wako katika kuandika makala.

Nakupa pole sana
Nadhani hukupata dhana halisi ya kwanini nimeandika. Kuandika magazetini si tatizo kama umeelewa vema dhana yangu. Moja ya kanuni za uandishi ni kukubali kuwa wazo au mawazo umeyapata kutoka vyanzo vingine, kinyume chake utakuwa umefanya 'plagirism' yaani kuibia kama ni kiswahili hicho ni sahihi.

Ukisoma magazeti mbali mabali utakuta yananukuu source, kwa mfano: abcdef ni kwa mujibu wa gazeti au shirika fulani la habari. Au unaweza kusikia 'kama ab alivosema katika gazeti au blog flani....' n.k n.k.

Hapa JF nadhani wamiliki ndio wenye haki ya mawazo ya wachangiaji. Nimekuonyesha kwa uwazi kabisa sehemu ambazo Mohamed Rajabu ima amezijibu au amezinukuu moja kwa moja kutoka JF.
Basi angalau 'acknowledgement' ya JF na sisi yeye kusema ameongea au amegundua n.k ili hali tunaona wazi kabisa sehemu ya uandishi wake haukutokana na mawazo yake mwenye. Hii haina maana kuwa hakuna mawazo yake, la hasha! ila zipo sehemu amebadili lugha lakini mawazo ni ya wanaJF.

Inaweza kuwa mitandao haina haki lakini haki ya acknoledgement ni ya kiungwana na kiuandishi kwahiyo hawezi kusema hiki si kitabu, au gazeti bla bla bla, bado anadhima ya kushukuru chanzo alikopata mawazo.
Ni kawaida kusikia vyombo vingine vya habari vikesema au kuandika kuwa jambo abcd limeleta utata kama lilivonukuliwa kutoka forum flani au blog,gazeti flani n.k

Ni kwa muktadha huo ndio maana tumeona kuwa kuna haja ya kumwalika hapa tuongee naye ili nasi tusikie mawazo yake binafsi sio kusoma mawazo ya wanaJF kwa jina lake.

Kama unadhani hutumetendei haki, niambie niifumue hiyo makala yake kwa vithibitisho kutoka hapa hapa JF na thread hii kama nilivyowekea wino wa bluu.

Mwisho, tumekuwa na mijadala mizuri tu kila jukwaa hapa JF kwa mafanikio sana, hata kuvuta waheshimiwa na viongozi wa dini na serikali. Mfano ni mwandishi Mohamed Said ambaye amekuwa anajitokeza na tunajadiliana naye. Huwezi kuwa na watu 46,000 ukakosa mzaha hapa na pale,muhimu ni je unaeleweka kile unaschosimamia?
Kwa taarifa hata maoni yanayoandikwa magazetini(yale ya mtandao) huwa yanakejeli.
Endapo haoni haja ya kukutana nasi hewala! lakini aache utaratibu wa kunukuu maoni bila kushukuru chanzo ambacho ni JF.

Hoja kuu hapa ni mbili 1) kushukuru chanzo cha habari zake 2) Kumwalika ili nasi tumsikie kwa upande wake binafsi.
 
Back
Top Bottom