Khaa! ..Hebu na Tujitambue...

Kwahiyo akikupeleka/tembea na wewe tu bila kukuchukua jumla ana heshima kwa wanawake? Labda mama yake mzazi. . .ila sio huyo mke wala hawara..

Unamana gani unaposema kuchukua jumla? sijakupata vema.... Hata hivo tumeona wanaume ni wengi ambao wameoa wanatembea nje... sababu za kutembea huko nje zimetofautiana na ni topic nyingine kabisa. Kwamba akitembea na wewe hali akiwa na mke hamheshim huyo mwanamke? sio lazima... Inaweza ikawa kweli ama lah! Anaweza akawa na mke akatembea na mwanamke mwengine na akamheshimu vile vile... Akaheshim mke na huyo mwanamke pia.
 
Hapo pekundu napakosea neno.

Mara nyingi nimegundua sisi wanawake tunakimbilia kuwalaumu wanawake wa nje wa waume zetu.
Kuna mtu alikua anafikiria kila mbinu za kumkomoa mwanamke wa nje wa mumewe,nikamwambia hiyo siyo dawa wa kupambana naye ni mumeo,akasema kamwe hawezi kugombana na mmumewe bali atawakomesha wanaomuibia mumewe.
Baadhi ya hawa waume wanafanya ndio wakulaumiwa,wengine wanatongoza wanawake huko nje wakisema wako singe na siku hizi wanaume wengi tu hawataki kuvaa pete zao za ndoa,kabla ya kuwalaumu hawa wanawake wa nje tujiulize huwa wanaambiwa nini na waume zetu hadi wanakubali kujiamini kuja hadi vyumbani mwetu,japo wapo wanawake makauzu hata akijua huyu ni mume wa mtu hajali ila wapo ambao wanadanganywa kuwa sina mke na vitu kama hivyo.
Kwenye kesi kama hii wakulaumiwa ni mume tu na sio mtu mwingine yoyote yule.

Halafu mi naona kama hawa wanaume wanapata kichwa maana kosa afanye yeye halafu lawama zielekezwe kwa mwingine no wonder hawacheat tena na tena.
queenkami........kuna watu watakuja kukwambia hapa mwanaume hakosei ila mwanamke ndo anachangia!!
Ngoja waje.......
 
Last edited by a moderator:
Hapo pekundu napakosea neno.

Mara nyingi nimegundua sisi wanawake tunakimbilia kuwalaumu wanawake wa nje wa waume zetu.
Kuna mtu alikua anafikiria kila mbinu za kumkomoa mwanamke wa nje wa mumewe,nikamwambia hiyo siyo dawa wa kupambana naye ni mumeo,akasema kamwe hawezi kugombana na mmumewe bali atawakomesha wanaomuibia mumewe.
Baadhi ya hawa waume wanafanya ndio wakulaumiwa,wengine wanatongoza wanawake huko nje wakisema wako singe na siku hizi wanaume wengi tu hawataki kuvaa pete zao za ndoa,kabla ya kuwalaumu hawa wanawake wa nje tujiulize huwa wanaambiwa nini na waume zetu hadi wanakubali kujiamini kuja hadi vyumbani mwetu,japo wapo wanawake makauzu hata akijua huyu ni mume wa mtu hajali ila wapo ambao wanadanganywa kuwa sina mke na vitu kama hivyo.
Kwenye kesi kama hii wakulaumiwa ni mume tu na sio mtu mwingine yoyote yule.

Halafu mi naona kama hawa wanaume wanapata kichwa maana kosa afanye yeye halafu lawama zielekezwe kwa mwingine no wonder hawacheat tena na tena.

Aksante qeenkami umenifungua macho. Ni kweli kabisa kuwa mwanaume ndie wa kulaumiwa ...especially pale ambapo amakuwa ameificha marital status yake BUT pale ambapo alishaweka wazi kuwa ameoa, na wewe unayeletwa nyumbani unakumbuka kabisa kuuliza ..........Kwani mkeo yu wapi leo hata unipeleke kwako?. inanitia mashaka.

Kigezo kuwa ni kosa la mwanaume kwa kuwa yeye ndo anatakiwa kuelewa kuwa ameoa na anatakiwa kuiheshimu ndoa yake sidhani kama linanivua mie kosa............as long as ninajua kuwa AMEOA, inanipasa niituze heshma na hadhi yangu mimi kama mwanamke...sihitaji kujustify kuwa umekuwa muwazi au but as long as ninajua umeoa na nikakubaliana nawe (hapa naweka stop) sitopenda unipeleke kwenye kitanda cha mkeo!

3963674]Kwa nini unadhani ni aibu ya mwanamke tu? Na si mwanamme ambaye kakuoa tena labda kanisani au msikitini?

Kwa nini unambebesha lawama mwanamke peke yake?

Tena mie wa ambiance nitakasirika zaidi ila kama ni mwanamke decent angalau nitavumilia.

Swali, hivi mwanamke hawezi mpenda mwanamme aliyeoa? Naamanisha kupenda na si kwa ajili ya kujinufaisha na faida yeyote.

Halafu nitaendelea na ninachofikiri.[/QUOTE]
na
............ Mamito, aibu si ya mwanamke tu lakini in a sisterly love and care, tunajidhalilisha sie especially kama tunajua wazi hali halisi kuwa this is somebody's husband................... tukumbuke kuwa yeye atachuikuliwa kama kidume wakati wewe, ambaye umeletwa utachukuliwa kama Ma.laya tu ulokuja kuiba tu.............. kwa nini asikulete wakati mkewe yupo, tukaona u-dume wake wa kumlaza mkewe sebuleni kwenye kochi na kukuacha wewe kimwana ukijivinjari katika kona zote za sita kwa sita??

Mwanamke decent hadi akapendwa atakuwa ameelezwa hali halisi na kama kweli ni decent katu hatokubali kuletwa kwenye kitanda cha mke halali!
 
Kweli tunatofautiana.

Haswaa!! Hicho ndicho kinachofanya katika jamii watu tuwe unsettled... Mengi yanakuwa regarded hayafaii katika jamii, na yale ambayo kila mmoja hataki yamkute, ndio yanaongoza kwa kutendwa. Ni either you face the facts and deal with them the hard way or waendelea kubishana na hali halisi... the hard way pia.
 
Hivi sisterly love kati ya wanawake inazidi mapenzi kati ya wanandoa? Nataka kuwa realistic.

Kama mmeo hajali mapenzi ya ndoa,je hii sisterly love inatafanikiwa kweli?

Ila kweli mwanamke mwenye akili timamu hawezi enda kwenye nyumba anayoishi na mkewe na kulala hapo hapo.
 
Kwahiyo akikupeleka/tembea na wewe tu bila kukuchukua jumla ana heshima kwa wanawake? Labda mama yake mzazi. . .ila sio huyo mke wala hawara.

Alafu MwanajamiiOne ningeona huyo mke (sijui kama ni wewe) nae anajitambua iwapo angeuliza "iweje mume ampeleke hawara nyumbani, kwenye kitanda anacholala na mkewe wa ndoa" kisha ndio aulize "iweje mwanamke akubali kulazwa kwenye kitanda cha mwanamke mwenzie"!!

Kwa kuishia tu hapo ulipoishia inaonyesha fika aliyekumbwa na masahibu hajui jukumu la mumewe kwake, anajali zaidi yule ambae hana makubaliano wala viapo nae.

Aksante Lizzy
Ni kweli yapo mengi lakini nakataa kuamini kuwa kuna any justification ya kucheat openly kiasi cha kuleta nyubani, chumbani, kitandani, kwenye shuka langu. NO MATTER WHAT I HAVE DONE, ndio ulete kitandani?? UMENICHOKA na HUNIHITAJI TENA so SITEGEMEI UNIBEMBELEZE wala KUNIOMBA MSAMAHA zaidi sana unambie...................HAYA NADHANI UMENIELEWA FUNGASHA KILICHO CHAKO SEPA.
 
Asie na akili ni mwanaume/mwanamke ambae haheshimu nyumba yake. Mie nikimkuta mwanamke mwingine nyumbani kwangu ntamuambia hebu toka kwanza manake nyumba ina wenyewe, ntageukia mzoga ninaouita mwenza nijiulize 'how the hell could I end up with a dumb arse of sh*t like u?! And I thought I was smart, da*n me'

Mwali wewe, usimtetee mwenza. Kuna m'baba anamtokea mtu anamuambia mke wangu kafariki, tumetengana, katoroka na mwanaume mwingine na hadithi kedekede. Gombana na mbwa wako, usigombanne na jalala la jirani mwanakwetu!
 
Vipi tena MwanajamiiOne ?

Kwema?

Hivi mnashindwa nini kuielewa dunia?

Mimi hata sishangai kwa sababu najua kila mtu mara nyingi anaamini kwamba mwenye ng'ombe ni yule anayekamua!

Kwa hiyo, huyo anayeletwa kwako lazima atavimba kichwa kwa sababu kapewa promotion. Kwani wewe hupendi kupandishwa cheo?

Babu Dc!!
 
yaani labda nisijue kuwa kuna kiumbe kimelala kwenye our 'matrimonial bed', WALLAH NIKIJUA, mimi sina shida na huyo dada, ntamuacha aende zake, mimi namtaka huyo wangu mwandani! tutaanzia alif tujue pa kuishia, ila atalipa vibaya kuliko mimi nilivyomfuma, NITAMUUMIZA MARA 5 YA ALIVYONIFANYA, taratibu tu kwa vitendo, maneno hayasaidii wanawake wenzangu.
 
Hao ndio wanaume bana.....kiukweli sijashangaa hata kidogo! Ila nna swali kwako km ww ndio muhusika sawa kama ni kesi ya dada yako pia sawa ila nna uhakika utakua najibu.
Baada ya huyo mke kugundua hilo akachakua uamuzi gani???
Mimi sitahangaika na huyo nguchiro aliyeletwa ndani maana sikufunga nae pingu za maisha na wala simfahamu sana2 nitamdharau na kumuonea huruma maana hajui mbele ya safari yake atakutana na masaibu ya aina gani.
Wanaume nyie jamani sikilizeni vilio vyetu basi looh,hamjionei huruma na nuksi zitakazowapata???!!!
 
Hayo maumivu ya mara 5 utatumia nini kuyapima? Na mwisho wa siku wewe utakuwa umeumia mara ngapi?

Babu DC!!
 
Mbona mnasahau kuwa kila kiumbe ni selfish?

Kuna mwanamke ambaye namfahamu. anaweza kuzua sababu yoyote wakati wowote hata kama ni saa 6 usiku aende kuonana na Ex BF wake ambaye amekiri kuwa hataweza kumuacha milele!!

Na huyo ni mwanamume?

Babu DC!!
 
Wanawake wenzangu,
Siku hizi kutembea na mume wa mtu ni jambo la kawaida lakini ndio akulete nyumbani, ulalie the same bed anacholalia na mkewe?? That is too much akhaa!!

Hebu tujiulize kwa nini hakuleti nyumbani hapo wakati mkewe yupo? Jeuri hiyo hana kwa kuwa- ANAMPENDA MKEWE na HAYUKO tayari kumpoteza kwa sababu YAKO. Wewe utabakia kuwa mwanamke wa kupoza MHEMKO wake siku zote na katu hutoifilia hadhi ya MKEWE.

Tahadhari, Chukua Hatua!
Mwanaume anapoamua kuleta kimada nyumbani wakati mkewe hayupo ni kuepusha shari lakini ukweli ni kwamba Huko si kumpenda mkewe bali ni dharau kwa wote wawili. Kati ya wawili hakuna anayependwa wote anawatumia kwa manufaa yake. Wengi wapo kwenye ndoa kama kisingizio lakini mapenzi hakuna. NI HIVI WANAWAKE TUSIJIDANGANYE...Mwanaume akishaleta kimada ndani ya nyumba ujue mwisho wa wote umefika. Huu ni mtazamo wangu.
 
MwanajamiiOne bwana!

Sasa ukimdharau na kum curse huyo Other woman ndio mumeo atatulia?

Kitendo cha mumeo kumleta concubine wake kitandani kwako ni dharau kwako na si huyo hawara!

Na kitu kingine, what make u think kuwa huyo mwanamke ana dreams za kuolewa????

Kudivert lawama from the real monster (mumeo aliyeapa kuwa atakuwa na wewe) na kwenda kwa huyo OW haisaidii sana, it is just a weakness! Face the problem ur husband and not the symptoms!
 
Hayo maumivu ya mara 5 utatumia nini kuyapima? Na mwisho wa siku wewe utakuwa umeumia mara ngapi?

Babu DC!!
DC i guess unahisi kuwa labda nitamcheat ili apate maumivu kama yangu, HAPANA hiyo pia si dawa ni kujiongezea matatizo! labda nikufafanulie moja kati ya ambayo nitamfanyia, kwanza kabisa ni COLD WAR, sitamuuliza yule ni nani, wala walikuwa wanafanya nini kitandani kwangu. sitaitisha kikao na mshenga, wala matron, wala wakwe. ni ADHABU TOSHA KWAKE! mengine nisiyaandike hapa!
 
Kumbe wengine mnaenda mpaa kulalia vitanda vya wake za watu, mnaminyege aisay :biggrin:
 
Mbona mnasahau kuwa kila kiumbe ni selfish?

Kuna mwanamke ambaye namfahamu. anaweza kuzua sababu yoyote wakati wowote hata kama ni saa 6 usiku aende kuonana na Ex BF wake ambaye amekiri kuwa hataweza kumuacha milele!!

Na huyo ni mwanamume?

Babu DC!!

Hebu acha mambo yako banaaa....tunaomba kujua sababu zinazopelekea mwanaume kumduu hawara kwenye kitanda walalacho na mkewe. Ina mana gesti zote zimejaa ama hela ya gesti hana???!!!
Waonee huruma wajukuu zako wana kiu ya kujua nini hasa kinawasukuma kufanya hivyo....nna uhakika huwezi mfanyia hivo Bibi DC
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom