Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.

Sir Leem

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
581
122
Habari zilizo patikana hivi punde ya kuwa Liyumba ametoroka na wadhamini wawekwa rumande baada ya kushindwa kumleta mshatiwa mahakamani!!!!
 
Last edited by a moderator:
Duh!!! Kama ni kweli hii basi mafisadi wote warudishwe rumande haraka sana wakiwamo wale wa EPA na akina Mramba.
 
Whaat? Kazi ipo. Kwani alikuwa anahitajika mahakamani ama ni longo longo tu?
 
Mi nilihoji siku za nyuma kwa nini wanawapa haki za kuwa nje ya dhamana wakati wameiba mali za wananchi?
Watu wakasema ni haki ya mtuhumiwa haya sasa huyooooooo katembea na kiloba cha pesa zote.
 
Yeye peke yake hawezi kufanikiwa bila kukamatwa, vinginevyo vyombo vya dola, Mahakama ikiwemo vinahusika.
 
Aise kama hii ni kweli basi mahakama (jopo la mahakimu husika) wawajibike kwani Mawakili wa Serikali walipinga sana jamaa kupewa dhamana kutokana na sababu kuu mbili
1. Aliwasilisha mahakamani passport iliyokwisha muda
2. Ametoa 1.4% ya dhamana stahili tena katika hiyo 1.4% kuna kuku, mbuzi, kondoo nk

Hapa lazima mahakama iwajibike.
 
Miafrica ndivyo tulivyo.
Haya sasa oooh ni haki ya mshitakiwa ooh lazima apewe dhamana haya sasa mkiambiwa amekufa Congo msishangae.
 
tehe tehe.....si pass yake iliisha muda?
katoroka nje ya nchi au?
 
inawezekana, michezo michafu bongo ipo na huu unaweza kuwa ni mmojawapo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom