Kesho jumatano saa 3 asubuhi maandamano kuanzia kituo cha haki ya sheria tafadhali mwambie mwenzako

Matangazo ya maandamano yametuchosha bila vitendo kwa sababu mengi yanaanzia JF na kuelekea kusikojulikana
 
Kesho maandamano kuanza saa tatu asubuhi mbele ya kituo cha sheria na haki za binadamu kilichopo kijitonyama, nyuma ya chuo cha ustawi wa jamii. tafadhali kabla maafa ya hayajakuwa makubwa tuhudhurie bila kukosa kwa mapenzi mema ya nchi yetu

Allah awaongoze, Mungu awaongoze, Mizimu iwaongoze, Miungu iwaongoze. Uzalendo uwaongoze, upendo Uwaongoze, Budha awaongoze, Jah Awaongoze.....

Beba bango lenye ujumbe wako.

Wewe mchaga25 sijui siku ya leo umekuwaje? mchana nilidhani unamning'inio wa jana maana ulitudanganya kwamba kulikuwa na mkusanyiko mlimani city, sasa hivi tena umekuja na hii ambayo nayo ni yauongo. Acha kushusha heshima yako bana.
 
Bado kuna tishio la mashambulizi ya Al Shabab kwa hiyo si vizuri kufanya maandamano kwa usalama wenu

Al shabab watakayokumbana nayo ni maji ya upupu, sijui kama mchaga25 mwenyewe atakuwepo kesho maana ya pale mlimani city alisema kapigwa virungu eti ikabidi watawanyike
 
Mgomo wa madaktari utaiangusha serikali ya Huyu mpuuzi asiye na soni, anguko limekaribia
 
Inaonesha huna kazi za kufanya.

Wewe si ndio ulileta habari kuwa kuna maandamano sijui watu wamekusanyika Mlimani City, yameishia wapi?

Huyu hana kazi, bila shaka ni vile vijisichana vinavyouza sura pale mlimani city ili kuvizia wanunuzi au ni kavulana kanakovunja vioo vya magani na kuiba vitu vya watu kwenye maeneo ya parking.
 
Mgomo wa madaktari utaiangusha serikali ya Huyu mpuuzi asiye na soni, anguko limekaribia

Kati ya mambo ambayo watu watamkumbukaa JK akiondoka madarakani ni pamoja na uhuru wa kumtukana! inabidi watu mjifunze kuacha tabia hii maana hamjui atakayekuja 2015 atakavyo chukua hatua. Tumieni vizuri hii miaka minne iliyobaki
 
Pukudu,hiyo rangi ya maandishi yako hovyo kabisa!
Either wewe ni mshabiki wa Simba or unachuki na CCM... Hii rangi kwangu inamaanisha Uhai na ule mmea wetu wa kujua mema na mabaya I mean canabis sativa
 
Kova kayaruhusu? Isije kukawa na tishio la al-shabaab,ebu muulize mwema intelejensia yao imewapa picha gani?
 
Pukudu,hujakosea hapo kwenye magamba ndo penyewe kabisaa!
 
kwani polisi watatumwa kuwazuia watu wasidai kurejeshwa kwa huduma za afya? itamaanisha polisi hawataki watu watibiwe!!!!!! kama ni kweli tutajipima utu wetu kwa namna hii.
 
nitakwenda hapo hiyo kesho potelea mbali, liwalo na liwe nimepoteza ndugu yangu wa karibu mbwa shenzi serikali
Pole san a kwa kupoteza ndugu wa karibu. Kinachonisikitisha ni jinsi WATU wamavyoendelea na shuguli zao wakati hakuna huduma ya afya mara ajali au ugonjwa utakapo mpata Mtu. Du kweli akili ya kuona urefu zaidi ya pua wanayo wachache hapa nchini. Hivi wakinamama wajawazito waliokua wanapata huduma muhimbili kwa sababu maalumu sio ndio tuwachimbie makaburi kabisa?
 
kwa akili walizonazo ffu utawaona na wenyewe wanpiga watu,,, yaani wana akili mbovu sana hawa jamaa
 
Kova kayaruhusu? Isije kukawa na tishio la al-shabaab,ebu muulize mwema intelejensia yao imewapa picha gani?
 
Maandamano kuhusu nini hebu kuwa specific

Katika nchi ambayo tuna mambo mengi ya kusababisha kuandamana na kupiga kelele ni hii...hakuna kitu ambacho kipo sawa mpaka sasa...kwa hiyo wewe nenda kaandamane utuwakilishe na sisi wa mikoani.Wakikuuliza waambie nchi aieleweki.
 
Al-shabaab na Boko Haram hawatakuwepo? Naomba Kova atujuze tafadhali.
 
Bado kuna tishio la mashambulizi ya Al Shabab kwa hiyo si vizuri kufanya maandamano kwa usalama wenu
Ukikwepa kufa kwa al shababu utakufa kwa kukosa tiba hospitalin kukana na mgomo wa madaktari
 
Back
Top Bottom