Kero yangu Jukwaa hili

Donn kwa mtazamo wangu uliingia kwa mbwembwe sana tena kwakusudio lakutaka kuonyesha watu unajua sana hii sio sawa uliuliza kuhusu web watu wakatoa maoni wewe ukaanzisha ubishi kwakudanganya sababu za kufungiwa ulipoelimishwa ukatulia japo ulishafanya ligi kwajambo usiloelewa.

Siwezi kusema vibaya hapa msaada upo tena mkubwa pasipo majungu wewe ulipigwa majungu kwasababu uliingia hapa kutafuta umaarufu kimsingi tulia soma nyendo utajua namna yakukaa hapa wengine tumeingia hapa hatujui kitu zaidi ya kufungua thred na kuandika.

Llakini now abcs tunazo hapa hakuna mashindano wala sio sehemu yakutafutia sifa ukiwa unajua utapongezwa na kupongeza tulia.
 
chief, nimekusoma ila nimeanza kuingia JF zamani sana, japokuwa nilikuwa msomaji tu.
 
  • Thanks
Reactions: koo
jf mwisho wa kazi, nimejifunza mengi nimesaidiwa mengi. Jf watu wana mioyo ya kusaidia iwapo umetoa details za kuridhisha. na kama kitu hukijui au huna ufahamu nacho tafadhali usijifanye kukifaham maana utaishia kuabika. Watu wengi wamepost threads hapa kwa kugoogle na kujifanya wanajua mambo wakatupostia maujanja ambayo ama Tz hayafanyi kazi au ni mambo ya zamani ambayo hata wao hawaja yajaribu..
Kuwa mfuatiliaji wa threads mbali mbali na ukipost kitu hakikisha walau umetoa details za kutosha
 
Tatizo kubwa watu hawajui hata jinsi ya kuuliza swali "PC YANGU HAIFANYI KAZI NIFANYEJE??" hajatuambia kitu chochote kuhusu tatizo lenyewe ni nini au PC yake iko vipi, hatufanyi miujiza hapa ni diagnostics kutokana na uzoefu na Google. Na ukiwasaidia wanatokomea, haujui hata kama solution imefanya kazi.

Kitu kingine kinachoudhi ni kuomba msaada kabla hata ya kuweka effort yoyote, "NAHITAJI DRIVER ZA HP" wakati ukiGoogle Hp drivers haukosi jibu kwenye first page ya Google, au mbaya zaidi kuomba msaada wa code wakati hata line moja hajajaribu kuandika kuona wapi amegoma.

salute ya!
 
Back
Top Bottom