Kero wanazopitia watoto wenye mafanikio kiuchumi kwenye familia

Wanaposema wanawake wanapenda sana pesa kikweli hawakosei

Daah! Ila bimkubwa wako jau sana
Anazingätia maokoto sana. Kuna siku kanipanga nimpe hela achimbe kisima, ilikuwa kipindi cha korona. Nikamwambia kwa sasa siko vizuri, ila nilifanya kama kumtega nione kama amebadilika.

Nilimwambia dogo namtumia hela yeye amtumie mama achimbe kisima, tulikubaliana na dogo. Baada ya kutumiwa hela mama akawa hanitafuti tena, baada ya mwezi akanikumbusha tena hela ya kisima tukägundua kumbe anatudanganya. Anavuta maokoto kwa dogo halafu ananiambia hajapewa, na nikimpa mm anaomba kwa dogo pia kwa kazi ile ile.


Shida yake akiomba kwangu ananiambia dogo amekataa kumpa, akiomba kwa dogo anamwambia nimemnyima yaani ni Taflani sana
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Niende moja kwa moja kwenye mada yetu inayosema kero wanazokutana nazo watoto wenye mafanikio ya kiuchumi kwenye familia.

Kama mjuavyo kila familia kuna mtoto au watoto wa jinsia zote kike/kiume ambao wanakuwa wanamafanikio kiuchumi.

Watoto hao wengi wao wamekuwa ni kama jicho kwenye familia, yaani wazazi na ndugu zote wanawaangalia.

Kila jambo liwe la wazazi wenyewe linalohitaji pesa basi watoto hao huwajibika kutoa usaidizi.

Wakati mwingine hata ndugu zao waliopo kwenye familia wamekuwa wakihitaji misaada ya kifedha kutoka kwao.

Pamoja na kuwa watoto hao wamekuwa wakitoa misaada ya pesa nyumbani kwao lakini kuna kero ambazo wanazipitia.

Hizi zifuatazo ni baadhi ya kero wanazokutana nazo;

MANENO MABAYA
Watoto hao wamekuwa wakitoa tena sana kwa kuwasaidia wazazi na ndugu zao ila wamekuwa wakipewa maneno mabaya kutoka kwa baadhi ya ndugu zao Tena wa damu ambayo yanawavunja moyo, mfano wa maneno hayo ni 'anajifanya anahela', anaringa sana na nk .

LAWAMA
Kama kuna kitu ambacho watoto waliofanikiwa kwenye familia wanapata ni lawama, wanalalamikiwa na ndugu na wakati wengine wazazi kwa kuwa wamechelewa kuwapa pesa au kutowapa kulingana na kuwa wakati mwingine mambo yao hayajakaa sawa

CHUKI
Hakuna watu wanaochukiwa na kukitapata kwenye familia kama hawa watoto ambao wamefanikiwa kiuchumi, yaani wanaochukiwa tena pamoja na kutoa misaada yao Bado huchukiwa tu.

WIVU
Hapa kwenye wivu ndio penyewe Sasa, maana ndugu zao waliozaliwa tumbo moja Huwa wanawaona wivu sana ndugu zao kwa kuwashinda kimafanikio, yaani wivu huu ni mkali kama wa Yusufu na nduguze.

Pamoja na kuwa watoto hao waliofanikiwa kwenye familia wamekuwa wakitoa misaada kwa wazazi na ndugu zao ila pia kuna wale ambao huwa hawasaidii.

Ajabu ni kuwa katika hayo makundi mawili ya wanaosaidia na wasiosaidia kero zinafanana kabisa.

Inashangaza maana hata wakisaidia wanapata kero tena zinaumiza zaidi kuliko wale ambao hawasaidii.

Unaweza ongeza kero zingine ambazo zinawapata hawa watoto ambao wanamafanikio kiuchumi.
kweli,ata mtaani ukifanikiwa kuwa na kagari au kanyumba kazuri,subiri chuki!!!
 
Usipo kuwa makini unaweza chukia ndugu zako bure.
Kabisa
Na ukifanyiwa hivyo ukanyamaza tu bila chuki, baada ya muda mfupi tu unawa prove wrong kivitendo.
Na ukija kufanikiwa wanahamia na kwako sasa ndio wanaanza kukuona mtu wa maana. Jaman kuwa na hela ni kuzuri, muhimu sana kutafuta hela watu wanadharau sana acha yaani.
 
Back
Top Bottom