Kero wanazopitia watoto wenye mafanikio kiuchumi kwenye familia

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Niende moja kwa moja kwenye mada yetu inayosema kero wanazokutana nazo watoto wenye mafanikio ya kiuchumi kwenye familia.

Kama mjuavyo kila familia kuna mtoto au watoto wa jinsia zote kike/kiume ambao wanakuwa wanamafanikio kiuchumi.

Watoto hao wengi wao wamekuwa ni kama jicho kwenye familia, yaani wazazi na ndugu zote wanawaangalia.

Kila jambo liwe la wazazi wenyewe linalohitaji pesa basi watoto hao huwajibika kutoa usaidizi.

Wakati mwingine hata ndugu zao waliopo kwenye familia wamekuwa wakihitaji misaada ya kifedha kutoka kwao.

Pamoja na kuwa watoto hao wamekuwa wakitoa misaada ya pesa nyumbani kwao lakini kuna kero ambazo wanazipitia.

Hizi zifuatazo ni baadhi ya kero wanazokutana nazo;

MANENO MABAYA
Watoto hao wamekuwa wakitoa tena sana kwa kuwasaidia wazazi na ndugu zao ila wamekuwa wakipewa maneno mabaya kutoka kwa baadhi ya ndugu zao Tena wa damu ambayo yanawavunja moyo, mfano wa maneno hayo ni 'anajifanya anahela', anaringa sana na nk .

LAWAMA
Kama kuna kitu ambacho watoto waliofanikiwa kwenye familia wanapata ni lawama, wanalalamikiwa na ndugu na wakati wengine wazazi kwa kuwa wamechelewa kuwapa pesa au kutowapa kulingana na kuwa wakati mwingine mambo yao hayajakaa sawa

CHUKI
Hakuna watu wanaochukiwa na kukitapata kwenye familia kama hawa watoto ambao wamefanikiwa kiuchumi, yaani wanaochukiwa tena pamoja na kutoa misaada yao Bado huchukiwa tu.

WIVU
Hapa kwenye wivu ndio penyewe Sasa, maana ndugu zao waliozaliwa tumbo moja Huwa wanawaona wivu sana ndugu zao kwa kuwashinda kimafanikio, yaani wivu huu ni mkali kama wa Yusufu na nduguze.

Pamoja na kuwa watoto hao waliofanikiwa kwenye familia wamekuwa wakitoa misaada kwa wazazi na ndugu zao ila pia kuna wale ambao huwa hawasaidii.

Ajabu ni kuwa katika hayo makundi mawili ya wanaosaidia na wasiosaidia kero zinafanana kabisa.

Inashangaza maana hata wakisaidia wanapata kero tena zinaumiza zaidi kuliko wale ambao hawasaidii.

Unaweza ongeza kero zingine ambazo zinawapata hawa watoto ambao wanamafanikio kiuchumi.
 
Wazazi ndio chanzo cha ndugu kuchukiana , wakishasaidiwa wanaleta ubaguzi .
Very true. Nina experience mbaya sana na mama yangu mzazi. Ana upendeleo wa wazi kabisa kwa mtoto yoyote mwenye hela.

Kuna kipindi nimemaliza chuo, nikapata mchongo flani ila natakiwa niwe na cheti cha shule ya msingi, nikamuomba mama akanichukulie anitume ila akagoma kabisa kuwa hana hela ya kuwapa walimu. The same wiki kuna mdogo wangu alikuwa chuo akamwambia mama anataka hela ya nauli ili arudi likizo. Mama alituma hela within 2 days wakati mimi aliniambia hana hela ya kumpa mwalimu elfu 5 ya naulî ili afate cheti wilayani.

Kufupisha tu, ni kipindi najitafuta ila dogo alikuwa bado ana boom so anamtumia tumia mother.

Nowadays mambo yamebadilka kabisa kisa nimemzidi dogo kipato so mama ananipenda zaidi, japo huwa namchana ukweli aache kutengeneza chuki kwa watoto.
 
Mzazi anaweza kuwa chawa wa mtoto wake mpka ukashangaa kisa maokoto, uzuri mmoja kibao kinageukaga, ila usilipize wewe mchane mpka hiyo tabia ikome.
 
Wazazi ndio chanzo cha ndugu kuchukiana , wakishasaidiwa wanaleta ubaguzi .
Wazazi wanajenga chuki na matabaka utagundua hili kwa mfano panapotokea uhitaji wa fedha kwa ajili ya shughuli hawaangalia mkubwa wa mtoto bali wanaanza kwa yule mwenye uwezo...Taarifa haraka anapew dogo kwamba kunahitajika hiki kwa vile ana pesa na uwezo ,yule mkubwa hajui kitu ...Baadae yule mkubwa ndio anapigiwa simu na dogo wake kuna ishu fulani wazee wameniambia ,Jamaa anajiuliza kwa nn mi nipo hapa nisiambiwe? Wakati huo inawezekana hata dogo anaishi mkoani kabisa.

Mazingira mengine ,ni kutafutana pia ni tatizo hata salama kama hauna kitu mambo yanakata kabisa
 
Siwezi lipiza ni mama yangu mzazi. Ila mara kwa mara namkumbusha na kumwambia yeye ndie anaweza kujenga au kubomoa uhusiano mzuri wa watoto wake.
Wazazi wanakuwa na ubaguzi sana , kama hauna pesa hata kama ni mkubwa ushauri wako kwenye jambo lolote kuhusu familia unapuuzwa wazi wazi .

Wazazi wanashindwa kubalance shobo kwa watoto wenye nacho na wanaojitafuta , ndio chanzo cha wivu ,chuki na lawama.
 
Very true. Nina experience mbaya sana na mama yangu mzazi. Ana upendeleo wa wazi kabisa kwa mtoto yoyote mwenye hela.

Kuna kipindi nimemaliza chuo, nikapata mchongo flani ila natakiwa niwe na cheti cha shule ya msingi, nikamuomba mama akanichukulie anitume ila akagoma kabisa kuwa hana hela ya kuwapa walimu. The same wiki kuna mdogo wangu alikuwa chuo akamwambia mama anataka hela ya nauli ili arudi likizo. Mama alituma hela within 2 days wakati mimi aliniambia hana hela ya kumpa mwalimu elfu 5 ya naulî ili afate cheti wilayani.

Kufupisha tu, ni kipindi najitafuta ila dogo alikuwa bado ana boom so anamtumia tumia mother.

Nowadays mambo yamebadilka kabisa kisa nimemzidi dogo kipato so mama ananipenda zaidi, japo huwa namchana ukweli aache kutengeneza chuki kwa watoto.
Wanaposema wanawake wanapenda sana pesa kikweli hawakosei

Daah! Ila bimkubwa wako jau sana
 
Wazazi wanajenga chuki na matabaka utagundua hili kwa mfano panapotokea uhitaji wa fedha kwa ajili ya shughuli hawaangalia mkubwa wa mtoto bali wanaanza kwa yule mwenye uwezo...Taarifa haraka anapew dogo kwamba kunahitajika hiki kwa vile ana pesa na uwezo ,yule mkubwa hajui kitu ...Baadae yule mkubwa ndio anapigiwa simu na dogo wake kuna ishu fulani wazee wameniambia ,Jamaa anajiuliza kwa nn mi nipo hapa nisiambiwe? Wakati huo inawezekana hata dogo anaishi mkoani kabisa.

Mazingira mengine ,ni kutafutana pia ni tatizo hata salama kama hauna kitu mambo yanakata kabisa
Apo lazima tu uwe na dukuduku moyoni tu , wazazi wa hivi hawajui tu wanavyoharibu familia zao wenyewe , then ndugu wakichukiana wanaoumia ni wao.
 
Very true. Nina experience mbaya sana na mama yangu mzazi. Ana upendeleo wa wazi kabisa kwa mtoto yoyote mwenye hela.

Kuna kipindi nimemaliza chuo, nikapata mchongo flani ila natakiwa niwe na cheti cha shule ya msingi, nikamuomba mama akanichukulie anitume ila akagoma kabisa kuwa hana hela ya kuwapa walimu. The same wiki kuna mdogo wangu alikuwa chuo akamwambia mama anataka hela ya nauli ili arudi likizo. Mama alituma hela within 2 days wakati mimi aliniambia hana hela ya kumpa mwalimu elfu 5 ya naulî ili afate cheti wilayani.

Kufupisha tu, ni kipindi najitafuta ila dogo alikuwa bado ana boom so anamtumia tumia mother.

Nowadays mambo yamebadilka kabisa kisa nimemzidi dogo kipato so mama ananipenda zaidi, japo huwa namchana ukweli aache kutengeneza chuki kwa watoto.
Hii ni hatari sana wazazi wanapogeuka kuwa machawa..
Familia lazima mpoteane...
umasikini ni laana kabisa!
 
WIVU
Hapa kwenye wivu ndio penyewe Sasa, maana ndugu zao waliozaliwa tumbo moja Huwa wanawaona wivu sana ndugu zao kwa kuwashinda kimafanikio, yaani wivu huu ni mkali kama wa Yusufu na nduguze.
Hii kitu ni ukweli kabisa. Niliwahi kosa nafasi ya kwenda nje ya nchi kimasomo kisa tu baba mdogo aliona nitatoboa, akaficha chetu changu cha kuzaliwa. Cheti kimepatikana baada ya wiki 3 deadline imepita. Mungu tu alinisaidia nikatuma maombi hivyo hivyo kwa kuchelewa na nikatoa sababu zuilizonifanya nichelewe, then nikabahatika.

Sasa kuna kipindi huyo baba mdogo alitaka nimsaidie mwanae issue ya kazi, ndio ikabidi aombe msamaha na kusema ukweli. Japo mke wake alishamwambia mama maana hakuwa anaelewana na mume wake. Wivu unakwamisha sana
 
Kama utachunguza kwa bongo watu wanaopota mafanikio kwa kazi au biashara hawataki kuishi sehemu walizozaliwa kotokana na utegemezi mkubwa kutoka kwa ndugu na watu wa karibu.....yaani unakuta mtu ni mwalimu ila majukumu ni mengi.

Swali ,je mtu aache kugharamia familia yake na mke kwa kipato chake kidogo badala yake asaidie ndugu?

Mfano mtu anaweza kuchelewa kujenga kisa kusomesha ndugu huu ni upuuzi siku ukistaafu hauna nyumba utabaki na familia yako tu mke na watoto ,ndugu uliokuwa unawaona wana maana sana kila mtu ana familia yake mda huo hana time na wewe.
 
Wazazi wanajenga chuki na matabaka utagundua hili kwa mfano panapotokea uhitaji wa fedha kwa ajili ya shughuli hawaangalia mkubwa wa mtoto bali wanaanza kwa yule mwenye uwezo...Taarifa haraka anapew dogo kwamba kunahitajika hiki kwa vile ana pesa na uwezo ,yule mkubwa hajui kitu ...Baadae yule mkubwa ndio anapigiwa simu na dogo wake kuna ishu fulani wazee wameniambia ,Jamaa anajiuliza kwa nn mi nipo hapa nisiambiwe? Wakati huo inawezekana hata dogo anaishi mkoani kabisa.

Mazingira mengine ,ni kutafutana pia ni tatizo hata salama kama hauna kitu mambo yanakata kabisa
Daaaah ni kama unajua niliyopitia😅😅. Kuna mtoto wa baba mkubwa yuko tu hapo EWURA yeye mpaka apokee simu yako ni shida. Sms anasoma hajibu, kisa anaogopa kuombwa msaada na ndugu zake wa damu.

Cha ajabu anawapambania sana ndugu wa mke wake na wamejazana kwake, ila ndugu wa damu yake hawataki, anawaita ndugu lawama.
 
Mwenye pesa anastahili heshima hata awe mtoto kwa mzazi, kinachofanya apate pesa na wengine wakese ni kwamba ipo mahala amewajibika zaidi pengine hata kwenye hatari.

Sasa wazazi wanapaswa heshima waelekeze kwa mtoto mwenye pesa kwanza ndipo wengine nafuata

Cha ajabu wao hubaki na upendo kwa watoto mafala na kujaribu kumjengea mtoto tajiri maneno yanayombunja moyo

Wakati mwisho shida ya familia hutatuliwana pesa z huyu tajiri
 
Back
Top Bottom