Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,513
Habari wakuu,
Husika na kichwa cha habari,
Niende kwenye mada moja kwa moja,
Jamii nyingi za kitanzania zimekuwa na dhana potofu hasa kwa watoto wa mwisho, watoto hawa wamekuwa wakidharauliwa bila sababu.
Imekuwa ni kama kasumba sasa kwa baadhi ya jamii ya kitanzania kwa watoto wa mwisho kuonekana hawawezi kujitegemea kimaisha.
Ni ukweli usiopingika kuwa pamoja na kuwa watoto wa mwisho wamekuwa wamelemaa kutokana na mapenzi ya wazazi wao ila bado wapo ambao wanajituma sana na wamefanikiwa.
Watoto wengi wa mwisho wamekuwa wakiogopa kusema kuwa wao ni wa mwisho sababu ya kukwepa kudharauliwa.
Maneno ya kejeli ya hapa na pale huwapata sana watoto wa mwisho, utasikia "mtoto wa mama", hili neno limekuwa kejeli sana kwa watoto hao.
Mijadala mbalimbali inayoendelea mitandaoni pia wachangiaji wake wamekuwa wakitumia kejeli kwa kuwaita wenzao kuwa ni watoto wa mwisho.
Mitaani pia ikatokea kijana akashindwa maisha akawa yupo nyumbani hana cha kufanya, basi hukumbana na kejeli hiyo ya kuwa ni "mtoto wa mama"
Achana na huko tuje ndani ya familia yaani mtoto wa mwisho anadharauliwa, maana yeye anakuta wenzie washatoka kimaisha.
Kama ni wazazi walishastaafu au wameshazeeka, yeye anakuwa ni mtu wa kurandaranda kwa ndugu.
Anapita kwa kaka mara kwa dada kujaribu maisha ili aweze kutoka na yeye, ajabu ni kuwa huko kote anaambulia kudharauliwa kwakuwa tu yeye ni wa mwisho.
Pamoja na hayo yote ila mtoto wa mwisho amekuwa akipendwa na wazazi wake na familia nyingine huwafanya warithi wa Mali hasa wale watoto wa kiume.
Ninavyoandika hapa, mtoto wa mwisho amekuwa hana thamani, anadharauliwa tu pasipo na sababu za msingi kabisa.
Nini hasa kinachofanya mtoto wa mwisho adharauliwe na jamii?