Wazazi na Walezi huu ni ujumbe wenu wa thamani kuelekea siku ya familia duniani

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
611
4,035
Salaam nyingi za upendo kwenu.

Wazazi na Walezi, tunapoelekea kwenye siku ya familia duniani tarehe 15 Mei, 2024, tafadhali tuanze ukurasa mpya wa kuwa karibu zaidi na watoto wetu. Zawadi iliyo bora zaidi kwa mtoto wako kwenye nyakati za Dunia ya leo, ni kuwa karibu naye, tena karibu zaidi.

Kila mzazi na mlezi aombe Neema ya kuwa karibu Sana na mtoto/watoto wake.

NAOMBA Sana mnisikilize hapa kwenye hii video fupi Sana, ukisikiliza ombi langu kwani ni umpe na mwingine asikilize tafadhali🙏🏽

Ni katika kupata taarifa ndiyo tunaweza kupanga hatua zetu thabiti, maana tumepata Neema ya kufahamu.

Nawatakia Heri ya Siku ya Familia Duniani, 2024. 🙏🏽

=======

Dkt. Gwajima: Wazazi au walezi wengi wanagundua watoto wao wamefanyiwa ukatili mwingi kwa kuchelewa, kwasababu hawakujenga tabia ya kuwa karibu na watoto, karibu na wanafamilia.

Watoto wanabakwa, watoto wanalawitiwa mara nyingi tu lakini wanafamilia wanakuwa hawajui. Hii ni matokeo ya wanafamilia kuwa na tabia kuzungumza.

Hivyo tunavyokwenda kwenye siku hii ya kimataifa ya familia duniani tarehe 15 May 2024, ndugu wazazi, walezi, ndugu wanafamilia tukubali tofauti zetu kuimarisha malezi ya watoto kwenye familia na haya yote yatatokea tu endapo tutakuwa na utaratibu wa kuzungumza.

Sawa umependeza, Ila kampeni ya kuwazuia watoto na kuwawekea utaratibu maalumu wa kutazama Tv naona bado haijazinduliwa.

Ningependa kuona wizara yako inatoa mwongozo maalumu wa kuisaidia jamii kuhusu hilo swala.

TV inachangia kwa kiwango kikubwa kushuka kwa maadili ya watoto

Ebu waelimisheni watu haya mambo muhimu.

Pia katika wizara yako mnaweza kuandaa vipindi vya dk 40 kila jumamosi kwa ajili ya kutoa Elimu ya kijinsia , kujilinda, kujitambua na kutoa mafundisho.

Jitahidi Mh najua gharama ni kubwa Ila utaacha legacy na kuokoa hiki kizazi kinachoenda kujifia.
 
Ahsante Sana, nimepokea. Utaona hakika utekelezaji, weekend hii tunaanza kukutana online. Mtaona Tangazo. Shukrani
 
Hebu mama pigana hili suala la watoto kumaliza muda wa masomo wanabakizwa shule ili tu walimu wajipatie hela yao kigezo masomo ya ziada. Muda ambao umewekwa na serikali unatosha kabisa kumuandaa mtoto.yaani madarasa ya mitihani inabakia kuwa kero kwa wanafunzi na wananchi.
Watoto wanashinda na njaa walimu wanachoangalia ni maslahi yao.
Mtoto yupo na mwalimu kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 9 anashindwa kumfundisha eti anaona Kama muda wa saa 10-12 ndio atamfundisha aelewe.
Walimu wanajiamulia lolote ndani ya shule za serikali.
Hii ni keep mno kiasi kwamba mtoto hapati muda wa kupumzika,ajisomee na a digest alichofundishwa.

Nakuomba hili suala uliangalie mtoe suluhisho
 
Salaam nyingi za upendo kwenu.

Wazazi na Walezi, tunapoelekea kwenye siku ya familia duniani tarehe 15 Mei, 2024, tafadhali tuanze ukurasa mpya wa kuwa karibu zaidi na watoto wetu. Zawadi iliyobora zaidi kwa mtoto wako kwenye nyakati za Dunia ya leo, ni kuwa karibu naye, tena karibu zaidi.

Kila mzazi na mlezi aombe Neema ya kuwa karibu Sana na mtoto/watoto wake.

NAOMBA Sana mnisikilize hapa kwenye hii video fupi Sana, ukisikiliza ombi langu kwani ni umpe na mwingine asikilize tafadhali🙏🏽

Ni katika kupata taarifa ndiyo tunaweza kupanga hatua zetu thabiti, maana tumepata Neema ya kufahamu.

Nawatakia Heri ya Siku ya Familia Duniani, 2024. 🙏🏽
Umenikumbusha kitu
 
Habari mama pole na hongera kwa majukumu yaliyotukuka kwa jamii🙏🏾

Tarehe 27/03/2024 nilitoa taarifa kupitia namba yako ya whatsap juu ya tukio la unyanyasi kwa mtoto mmoja wa miaka 11 asomaye darasa la 5 watuhumiwa baada ya tukio walikimbia lakin baada ya wiki km 2 hivi wakarudi kijiji husika na kuendelea na maisha hadi leo hii wapo mtaan bila kuchukuliwa sheria yeyote!!
 
Nipatie RB ya tukio hilo nikusaidie kuuliza kwenye mamlaka husika yenye dhamana na jukumu la upelelezi kisha na wewe utaendelea kufuatilia kulingana na mrejesho nitakaokupa.

Kwa kuwa siwezi kukumbuka namba yako iliyotuma sms, tafadhali rejea tuma tena uandike (JF), Ili nikutambue tafadhali. Shukrani
 
Mhe; sio kwa kupenda ila inalazimu kuwaacha watoto mbali. Umejitafuta ukawa na makazi kona fulani ya nchi.

Ghafla, umepelekwa mbali huko umetengwa na mwenza na familia. Mzee alinisimulia enzi zao sharti uhame na mwenza; leo hii kama vipi chagua kazi au familia!

Ulichoshauri hapa ni theory tu not practical in real sense kwa mazingira ya kazi nyakati hizi!
 
Hebu mama pigana hili suala la watoto kumaliza muda wa masomo wanabakizwa shule ili tu walimu wajipatie hela yao kigezo masomo ya ziada. Muda ambao umewekwa na serikali unatosha kabisa kumuandaa mtoto.yaani madarasa ya mitihani inabakia kuwa kero kwa wanafunzi na wananchi.
Watoto wanashinda na njaa walimu wanachoangalia ni maslahi yao.
Mtoto yupo na mwalimu kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 9 anashindwa kumfundisha eti anaona Kama muda wa saa 10-12 ndio atamfundisha aelewe.
Walimu wanajiamulia lolote ndani ya shule za serikali.
Hii ni keep mno kiasi kwamba mtoto hapati muda wa kupumzika,ajisomee na a digest alichofundishwa.

Nakuomba hili suala uliangalie mtoe suluhisho
Pamoja sana.
HATA HILI SUALA LA WANAFUNZI HASA WA SHULE ZA MSINGI KWENDA SHULE SIKU ZA MWISHO WA JUMA HASA JUMAMOSI LIPIGWE MARUFUKU,HUO NI MUDA WA WAZAZI AMA WALEZI NAO KUFANYA MAZUNGUMZO NA WATOTO WAO.
 
Hongera sana kwa hamasa!
Bila ya kuwekeza muda na rasilimali nyinginezo kwenye familia miongo michache ijayo hakutakuwa na taifa.
Voila ya familia Bora, hata yaundwe maroboti ya kila namna taifa kitafutika. Nchi ni watu, na si wingi wa mitambo; na watu bora hupatikana kupitia familia imara.
Mifano ni mingi na inaongezeka
 
Kesi nyengine zinaishia kwa mjumbe wa nyumba kumi wazazi wanakubali kupewa era ili kesi isiende mbali swala ili la ubakiji linazidi kuwa kubwa
 
Nipatie RB ya tukio hilo nikusaidie kuuliza kwenye mamlaka husika yenye dhamana na jukumu la upelelezi kisha na wewe utaendelea kufuatilia kulingana na mrejesho nitakaokupa.

Kwa kuwa siwezi kukumbuka namba yako iliyotuma sms, tafadhali rejea tuma tena uandike (JF), Ili nikutambue tafadhali. Shukrani
Ni pale ambapo mtu hudhaniwa kana kwamba ni mashine - inaweza kufunguliwa na kufungwa popote ipate kuongeza uzalishaji
 
Back
Top Bottom