Kero hii Uwanja wa Ndege JNIA

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
kwa watanzania wen zangu ambao mmewahi kutumia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Jijini Dar es Salaam kwa safari za nje labda mmewahi kukutana na Kero hizi: Ukiwa una safari usiku, pale kuna wahudumu na walinzi ambao ni Kero sana...Hivi karibuni nilikumbana na kijana amelewa yupo karibu na eneo la kucheck in abiria ndani akanibana "ooh bro. lazima unitoe hata na dola 10 mdogo wako, ninyi wenzetu mnasafiri sana".

Siku si nyingi wakati nasafiri tena kuna walinzi wa Kampuni binafsi Group 4 nadhani naona Mara zote huwa ni wale wale tu hawabadilishwi...wawili wakanibana, kaka haiwezi kutuacha. Hivi Hivi...Nilipofika juu eneo la kusubiria ndege nikakuta kuna msafiri amebanwa na wale walinzi wanao clear passport kabla hujaingia eneo la ku board ndege. Abiria huyo alikuwa na kadi ya chanjo (yellow fever) ambayo juu yake haikuwa na jina wala passport namba yake. walimbabatiza kuwa hiyo kadi si halali na kuwa wao wamekuwa wakipokea kesi Nyingi tu za watanzania kurejeshwa Afrika ya Kusini kutokana na kuwa na kadi feki. Jamaa waliotoa kama 20 Hivi wakamtengenezea kadi nyingine hapo hapo. Nilidhani ni suala geni hili lam kupata kadi ya chanjo hapo...Juzi wakati naelekea tena Afrika ya Kusini, Jamaa wakanibana, " mzee kadi yako Ike expiry, imechkaa,imechanika"...Nikasema sina nyingine ni hiyo hiyo na nimekuwa nasafiri na hiyo hiyo muda wote tokea 2006.
Jamaa wakadai haiwezekani kuniruhusu, nikawauliza sasa inakuwaje?..wakaniambia kama una Tshs. 30,0000 unapata faster....wakanielekeza kwa mmoja wao ambae alikuwa amezishika kadi nyingine mkononi. Nikawwambia ninyi sio mamlaka ya ku clear taaraifa za chanjo za ndui. Cha kushangaza nilipokomaa nikaruhusiwa, nikapata Boarding pass na kwenda ku board...
siku hiyo nilikuwa na Perfume kwenye begi yangu. Nilipofika sikuikuta na begi lilikuwa halijafunguliwa ila mmoja ya zip ilkuwa imevutwa upande.

kuna kero zaidi ya hizi pale Umwanja wa ndege, kama kuna mdau anaweza kufanya investigative story kwenye combo cha habari anaweza kupata habari zaidi pale ..
 
Isee hizi za niache nitoe nyingi sana ila sijui nani anadhibiti haya kama wapo wasikie na wafanyie kazi ni aibu.
 
Pale JNIA kuna mambo mengi sana ya kitapeli na ya ujanja ujanja ambayo yanafanyika kimtindo kwa ushirikiano,ni vigumu kuwagundua ila na wao ni waangalifu sana katika kumchagua mtu wa kumbana.kibaya zaidi tunaadhibiana sisi kwa sisi.Utatuzi wake ni mgumu maana wanaohusika katika sekta hiyo ni kama hawajali vile,Kile ni kiwanja cha ndege kama cha kijijini vile na mambo yetu ya kibongo bongo kama kawaida.
 
Mwezi wa pili waliniibia hard disc(external) gb 1000,walioajiriwa pale wote mambulula kabisa,heri kidogo wadada ukutane sasa babu moja na lirungu lake,uzuri kuhusu documents zangu huwa wakiangalia wananirudishia tu maana lugha yenyewe ya visa hawajui hata jina.

Yaani ile geti ya kwanza kwenye ukaguzi unapoanza pako hovyo kuna yule kakaa karibu na ule mlango wa choo,ukaguzi wa passport unaanza kwake ila alipokaa huwezi hata kumwona utadhani yupo kwenye kibanda cha M-Pesa.

We ukifika pale piga tu English jifanye si mbongo watajitawanya tu ukiendeleza maswali utakuta kila mtu anakupaki kwa mwenzake wanaondoka mmoja mmoja.
 
JNIA hakuna walinzi wa group 4 kama unavyodai pia swala ka kuombwa pesa na walinzi si la kweli kwani walinzi wa JNIA hawana shida ndogo ndogo mishahara yao mizuri labda ulikutana na mfagiaji pia hayo mengine sina uhakika
 
JNIA hakuna walinzi wa group 4 kama unavyodai pia swala ka kuombwa pesa na walinzi si la kweli kwani walinzi wa JNIA hawana shida ndogo ndogo mishahara yao mizuri labda ulikutana na mfagiaji pia hayo mengine sina uhakika

Basi wale wanaochukua mabegi ni waizi sana,waache uwizi.
 
JNIA hakuna walinzi wa group 4 kama unavyodai pia swala ka kuombwa pesa na walinzi si la kweli kwani walinzi wa JNIA hawana shida ndogo ndogo mishahara yao mizuri labda ulikutana na mfagiaji pia hayo mengine sina uhakika

Mkuu nahisi we ni mdau hapo, nilichoandika ndicho kilichonitokea na kinawatokea wengi sana. Hao niliokutana nao more than once ni walinzi katika unifomu, nimeandika Sina hakika ni kampuni gani ila wanavaa mashati meupe na suluari /sketi za kijivu sijui ni Ultimate Security au Group 4 (kama wanalipwa vizuri basi wapunguze njaa za kuwaomba posho abiria na wale wa SWISS Port waeleze waache wizi kwenye mabegi). sijui kama mna wafagizi wenye unifomu za pale ndani.!!!.? Wewe kama ni mdau ebu fuatilia hao walinzi wenu wanaosimama kwenye kaunta za international flights. Na pale juu pa ku clear abiria...rushwa na wizi vinanuka hapo. Hata kama vitendo hivyo vinafanywa na wafagizi bado ni kero kwa abiria..ni nani anaeajiri na kuweka wafagizi wa namna hiyo?. Aibu kwa nchi, mnafungua mabegi ya abiria, ninyi ndio mmepewa dhamana ya kutunza mizigo eti mnaiba!!. Ebu muone aibu wazee...
 
Lazima tuangalie mana wengi wenu mapunda wa unga

Mapunda mmeshindwa kuwakamata mnaiba vipafyumu! hivi mishahara ya hapo haiwatoshi,mnaibisha sana kufungua zipu za mabegi ya watu wakati mapunda mmeshindwa kuwakamata.
Shame on you!
 
Huo uwanja hata wakati wa kuingia(kutua) una usumbufu! Kuanzia kwenye passport hadi mlango wa kutokea nje. Usishangae kusumbuliwa zaidi ya mara nne na maofisa wa usalama/polisi na wafanyakazi wengine hapo.
 
Kama ni wizi karibu kila a/port kuna hiyo shida, sijajua Dubai kama hii ni ishu. Ila kwa sehem nlizoboard in/out kuanzia OR Tambo, Gaborone, hata hapa DIA jana tu kuna jamaa kapigwa camera ya $2000 imeleta soo sana. Cha msingi zile bag zetu tuziwekee kufuli, au ikiwa una sanduku la paswed ni vyema zaidi ingawa kuna baadhi ya sehemu huwa wanayaangusha chini makusudi ili yapasuke.

All valuables ingia navyo kwa handbag maximum huwa ni 4kg..not sure
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom