Kero Kituko Uwanja wa Ndege Zanzibar

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
976
1,526
Naipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, ambapo ni wazi umebadilisha taswira ya uwanja kuwa bora kuliko ilivyokuwa awali. Cha ajabu ni kwamba pamoja na ukarabati huo kuna kero mpya imejitokeza hasa kwa abiria wanaondoka/wanaotoka Zanzibar kuelekea maeneo mengine.

Kero inaanzia pale unapofika uwanjani ili uanze kufanyiwa ukaguzi wa tiketi yako na mizigo yako. Inavyoonekana kwa utaratibu mpya ni kwamba, kuna mageti kadhaa tofauti kwa ajili ya ndege ndogo, ndege kubwa za ndani, ndege za kimataifa, n,k. Kwa lugha nyingine ni kwamba kama wewe ni abiria unayesafiri kutokea Zanzibar kwenda Dar na tiketi yako ni ya ndege ndogo, (Coastal, Auric, ,nk) na pia kuna abiria mwingine anayesafiri kwa kutumia ndege kubwa (ATC, Precision, nk), mtaingilia mageti mawili tofauti, na mtakaguliwa tofauti.

Kero ni kwamba hakuna namna yoyote abiria wanaweza kujua kwamba kwa tiketi hii, au ndege hii natakiwa kuingia geti gani. Hakuna maelekezo, au tangazo wala mtu wa usalama ambaye atasaidia angalau kwa kukaa mwanzoni mwa kuingilia uwanjani, angalau kuwaambia abiria kwamba kwa tiketi yako hii unapaswa kuingilia geti fulani. Kinachotokea ni kwamba abiria anaingia geti la kwanza anaambiwa 'sio hapa, nenda pale', anaenda pale anaambiwa 'nenda kule'.

Cha ajabu na kusikitisha ni kwamba wafanya kazi, watu wa usalama wote wanalijua hili, wanatazama tu jinsi abiria wanavyohangaika kuingia geti hili, kutoka na kuingia geti lile, n,k.

Binafsi niliingia na kutoka mageti mawili (Na pote ni kipande cha kutembea) kabla kulifikia geti ninalonihusu. Au ndio tunahitaji mwekezaji aje kutusaidia na hili kweli?

WAHUSIKA REKEBISHENI HILI
 
Muelekazaji anaenda mskitini mda gani? Acheni kejeri za imani za watu.
Kwenda msikitini ni kejeri kwa imani? Bora ungesema niache kejeri kwa Wazanzibar, lakini siyo kwa imani. Uwe unajifunza kuelewa, siyo unakurupuka tu.

Halafu unaonekana zaidi ya kufika haujui Zanzibar, hivyo tulia ujifunze, usipoelewa ukiza
 
Kwenda msikitini ni kejeri kwa imani? Bora ungesema niache kejeri kwa wazanzibar, lakini siyo kwa imani. Uwe unajifunza kuelewa, siyo unakurupuka tu.
Halafu unaonekana zaidi ya kufika haujui Zanzibar, hivyo tulia ujifunze, usipoelewa ukiza
Kwani misikiti inapatikana tu kwa zazibar lengo lako ni kukejeri imani za watu wanao tumia misikiti kufanya ibaada,
 
Naipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, ambapo ni wazi umebadilisha taswira ya uwanja kuwa bora kuliko ilivyokuwa awali. Cha ajabu ni kwamba pamoja na ukarabati huo kuna kero mpya imejitokeza hasa kwa abiria wanaondoka/wanaotoka Zanzibar kuelekea maeneo mengine.

Kero inaanzia pale unapofika uwanjani ili uanze kufanyiwa ukaguzi wa tiketi yako na mizigo yako. Inavyoonekana kwa utaratibu mpya ni kwamba, kuna mageti kadhaa tofauti kwa ajili ya ndege ndogo, ndege kubwa za ndani, ndege za kimataifa, n,k. Kwa lugha nyingine ni kwamba kama wewe ni abiria unayesafiri kutokea Zanzibar kwenda Dar na tiketi yako ni ya ndege ndogo, (Coastal, Auric, ,nk) na pia kuna abiria mwingine anayesafiri kwa kutumia ndege kubwa (ATC, Precision, nk), mtaingilia mageti mawili tofauti, na mtakaguliwa tofauti.

Kero ni kwamba hakuna namna yoyote abiria wanaweza kujua kwamba kwa tiketi hii, au ndege hii natakiwa kuingia geti gani. Hakuna maelekezo, au tangazo wala mtu wa usalama ambaye atasaidia angalau kwa kukaa mwanzoni mwa kuingilia uwanjani, angalau kuwaambia abiria kwamba kwa tiketi yako hii unapaswa kuingilia geti fulani. Kinachotokea ni kwamba abiria anaingia geti la kwanza anaambiwa 'sio hapa, nenda pale', anaenda pale anaambiwa 'nenda kule'.

Cha ajabu na kusikitisha ni kwamba wafanya kazi, watu wa usalama wote wanalijua hili, wanatazama tu jinsi abiria wanavyohangaika kuingia geti hili, kutoka na kuingia geti lile, n,k.

Binafsi niliingia na kutoka mageti mawili (Na pote ni kipande cha kutembea) kabla kulifikia geti ninalonihusu. Au ndio tunahitaji mwekezaji aje kutusaidia na hili kweli?

WAHUSIKA REKEBISHENI HILI
Hii ni sehemu nyingi inatokeaga kwa watu kubadilisha mfumo kwa kukurupuka bila kujali system and process flow ambayo ilikuwa imewekwa.
 
Back
Top Bottom