Keenja: Sasa tuivunje Dar es Salaam

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,754
MBUNGE wa Ubungo Dar es Salaam, Charles Keenja (CCM), ameishauri serikali kufanya uamuzi mgumu wa kulipanga upya jiji hilo. Amesema hiyo ni njia pekee ya kulifanya jiji hilo kwenda sambamba na hadhi ya majiji mengine duniani.

Kwamba, endapo serikali itathubutu kufanya hivyo, kero za foleni, ujenzi holela, barabara finyu na ukosefu wa mitaro ya kutosha katika maeneo mengi ya Jiji, yatakuwa historia. Alisema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu, yaliyofanyika Dar es Salaam.

“Kwa ujumla, asilimia 80 ya Jiji ni hovyo kabisa na tunajidanganya tunajenga Jiji ambalo naamini kuna siku tutalibomoa, kwa sababu tunakaribisha balaa… “Kero haipo katika foleni tu, kila kitu Dar ni hovyo, ujenzi hovyo, miundombinu hovyo, lakini haya yote yana tiba, tena inayoweza kuwa historia…ni kufanya uamuzi mgumu wa kulipanga upya Jiji.

“Tatizo si pesa, bali uamuzi, sisi hatujaamua na gharama za kutoamua ni kubwa mno, angalia muda unaopotea njiani, uchafuzi wa mazingira unaotokana na moshi na hata matumizi makubwa ya mafuta kwa kusimama kwenye foleni… “Ndiyo, yaweza kuonekana kuwa ni gharama kubwa sana, kweli ni gharama, lakini kuiogopa gharama ni kukaribisha hatari zaidi katika siku za usoni.

Ni bora tuwahi sasa kufanya uamuzi mgumu, kwa sababu sehemu kubwa ya Jiji haijaharibiwa, tuwahi kuijenga,” alisema Keenja, Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Jiji la Dar es Salaam, aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kulirejeshea hadhi jiji.

Na ni kutokana na utendaji huo, haikushangaza kuona akipata ubunge kwa urahisi mwaka 2000 katika Jimbo la Ubungo na baadaye kuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa, kuwa Waziri wa Kilimo na Chakula kuanzia mwaka 2000 hadi 2005.

Akizungumzia foleni, alisema kuna kazi kubwa inayopaswa kufanyika, lakini akashauri bora huduma nyingine za kijamii zisambazwe katika maeneo tofauti ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuzuia safari zisizo za lazima kwenda katikati ya jiji.

“Kuna mengi ya kufanya, lakini tuanzie na kusambaza huduma za jamii. Leo hii mtu ana shida ya kamba ya viatu, lazima afunge safari huko aliko hadi Kariakoo au katikati ya Jiji. “Kwa mtaji huu, msongamano utakosekana? Na ikumbukwe foleni hizi zina gharama kubwa, kuanzia suala la muda, uchafuzi wa mazingira kutokana na moshi na hata matumizi makubwa ya mafuta ambayo yanachangia kuharibu bajeti za watu,” alisema Keenja.

Alionya kuna hatari kadhaa za kiuchumi zinazoweza kujitokeza, kutokana na shughuli nyingi kucheleweshwa na foleni. Katika kuthibitisha jinsi foleni ilivyogeuka kero Dar es Salaam, taasisi moja ya utafiti ya CEP inaonyesha kwamba safari nyingi zisizozidi umbali wa kilomita 16 tu, zinalazimu kutumia hadi saa mbili, achilia mbali muda ambao abiria anapoteza kituoni kusubiri usafiri.

Utafiti huo wa Machi mwaka huu, unaonesha kwamba safari ya kutoka katikati ya Jiji hili la kibiashara linalochangia karibu asilimia 60 ya pato la taifa kwenda Mbezi Beach, ambayo kwa kawaida inapaswa kutumia dakika 98.4, inatumia dakika 194, sawa na saa 3:14.

Muda huo ni karibu sawa na ule ambao mtu anatumia kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro! Utafiti huo wa Machi, unaeleza kuwa kutoka Mbezi Luis kwenda Posta kupitia Barabara ya Morogoro, muda unaotumika ni zaidi ya dakika 91, badala ya 30 za kawaida na safari ya kutoka Posta kurudi Mbuzi Luis, utafiti unaonyesha huchukua zaidi ya dakika 104.

Aidha, dakika 81 zinatumika kwa safari ya kutoka katikati ya Jiji kwenda Uwanja wa Ndege kupitia Barabara ya Nyerere, wakati katika hali ya kawaida zingeweza kutumika dakika 27 tu.

Kwa watumiaji wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, angalau wanaonekana kutopata adha kubwa kwa nyakati fulani za siku kutokana na kile kinachotajwa kuwa njia hiyo hutumiwa na wakubwa wengi.

Mbali ya kupendekeza kuanzishwa kwa vituo vya kibiashara, vitakavyosaidia wakazi wengi wa Jiji kupata huduma huko waliko badala ya wote kuelekea katikati ya mji, Keenja alipendekeza pia kuongeza barabara mbadala na pia kujenga barabara za juu katika makutano ya barabara kuu. “Flyovers ni suluhu mojawapo, lakini pia kuna barabara zinazostahili kuimarishwa ili kuondoa msongamano.

Angalia, anayetaka kwenda Tanga lazima apite Ubungo, hakuna ulazima, ingeimarishwa Barabara ya Bagamoyo, watu wakapita huko Pangani mpaka Tanga… “Lakini hali haikuwa hivyo, kwamba ukitaka kwenda nje ya Dar es Salaam, safari lazima ianzie Ubungo! Tunapaswa kubadilika,” alisema Keenja na kuonya kwamba, mbali ya sababu za kiuchumi na kiafya, hali inaweza kuwa mbaya endapo kunaweza kutokea matatizo yoyote ya amani.

“Hivi yakitokea machafuko leo hii, watu watakimbilia wapi, ni kuangamia tu kwa sababu hatuna barabara…angalia kote, kila pande ya Jiji hali ni hiyo, ndiyo maana nasema, si barabara tu, kila jambo tukiamua kwenda hatua kwa hatua, tunaweza, lakini kwa kusubiri fedha taslimu, kamwe hazitapatikana kwa sababu matatizo daima huwa hayaishi…” Akizungumzia ujenzi holela, licha ya kusikitishwa na jinsi jiji linavyokosa mpangilio, alisema anashangazwa kuona sheria zipo, lakini hazifanyi kazi.

“Ndiyo kuna sheria za mipango miji, lakini hazifuatwi, badala yake watu wanajijengea hovyo hovyo na kuigeuzia kibao serikali kwa kudai huduma kule wanakokuwa…kimsingi serikali ndiyo iliyopaswa kutenga maeneo, kuweka huduma zote muhimu na kuelekea aina ya ujenzi… “Lakini ni kinyume, mtu ananunua kiwanja, anachokoza ujenzi, akiona watu wanaongezeka, wanaanza kudai maji, umeme, barabara na mengineyo bila kujua huko waliko serikali haijapangia bajeti, lakini kwa sababu kosa limeshatendeka, basi wakati ni huu, hatujachelewa ili hapo baadaye tusijute zaidi.

“Kote duniani, mji hupangwa, si kwamba watu wanajipangia, lazima tuwe na Master Plan…Dar ninayoijua mimi ilikuwa na viwanja vya wazi zaidi ya mia moja, lakini sasa havifiki hata 30, watu wanajigawia na kujijengea kiholela, Kariakoo ndio usiseme.”

Kutokana na kukithiri kwa ujenzi holela, ameshauri uandaliwe mradi utakaokwenda awamu kwa awamu, ili kuupanga mji, akitolea mfano Magomeni Mapipa kwamba maghorofa matatu yanaweza kuweka familia nyingi pamoja, huku wakihamishwa kwenda nyumba zao hivyo kutoa mwanya kwa serikali kubomoa nyumba na kuupanga mji kwa mpangilio mzuri wenye hadhi ya Jiji.

“Tukianzia hapa, tutakwenda sehemu nyingi, mwisho wa siku mji utajikuta umepangiliwa vizuri ajabu, ndiyo maana nashauri kwa sababu huku tumeshaharibu, tuanzie kuupanga mji kule ambako hakujaharibiwa… Keenja, ambaye hatatetea jimbo lake hilo wala kugombea jimbo lolote la mkoa wa Dar es Salaam, akidai ana uwezo wa kuliteka jimbo lolote, alishauri pia jinsi ya kuondoa kabisa uchafu Dar es Salaam, kwa kuweka ushirikiano baina ya wanajamii na halmashauri, huku kukiwa na usimamizi wa kweli.

“Ikiwezekana hata makampuni ya kigeni yanaweza kukodishwa, lakini lazima jamii ishirikishwe…wakati nipo Jiji kuna watu wanaosafisha Jiji la London, waliomba kufanya usafi, lakini kwa wakati ule mapato yetu yalikuwa madogo, tukasitisha …” Juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi kuzungumzia suala hilo jana hazikuzaa matunda.

Source: Gazeti la Habari leo


Mnauonaje ushauri huu wadau..........Je utasaidia?....................Tafakari
 
Huyu jamaa mufilisi kwani miaka 10 ya ubunge hata daraja la Golani limemshinda!
 
Arudi kuwa mkurugenzi wa Jiji maana siku zile angalau jiji lilikuwa safi na kulikuwa na mpangilio unaoeleweka.

Give the devil his due.
 
Angelifanya yeye alipokuwa Mkurugenzi wa jiji! Sasa ametoka ndio anaanza kuwaambia wengine! Kwa ufupi ni gharama sana! Ukiweka na ubabaishaji wa Kibongo its completely imposible, can you imagine mandela raod imechukua karibia miaka miwili sasa kibarabara cha KM 10-15, kwa mtindo huu utavunja jiji kweli?
 
Keenja ni mwasaiasa mnafiki sijaona.....
Tena muongo mno.....
Analalamikia viwanja vya wazi wakati ni yeye alieamuru shule ya secondary ya Benjamin Mkapa ijengwe kwenye viwanja vya wazi vya shule ya uhuru ili tu ajipendekeze kwa Mkapa.........

Halafu leo anaongea nini................
Umuhimu wa viwanja vya wazi upo palepale
Hata kama unataka kujenga shule..............
 
Keenja ni mwasaiasa mnafiki sijaona.....
Tena muongo mno.....
Analalamikia viwanja vya wazi wakati ni yeye aleamuru
shule ya secondary ya benjamin mkapa ijengwe kwenye viwanja vya wazi vya shule ya uhuru
ili tu ajipendekeze kwa mkapa.........
Halafu leo anaongea nini................
Umuhimu wa viwanja vya wazi upo palepale
hatakama unataka kujenga shule..............

Chukua tano!!!
Huu ni unafiki tu, amefanya nini yeye zaidi ya kujineemesha, jimbo lake la Ubungo kweli 10 years hebu tuone ni ni kimoja alichofanya katika mtiririko huo aliosema, ok barabara? ipi? ni unafiki tu aende zake ni wale wale.
 
Hapo anajikosha ili watu wamfikirie tena na pengine apewe ulaji. Tena bahati mbaya kikwete hajui kuteua watu wachapa kazi usishangae baada ya kuvunja bunge mtu akateuliwa kuongoza jiji.
 
Anachosesema Keenja ni kweli kabisa Maamuzi magumu yanahitajika. Lakini nakubali kwa aliyesema Keenja ni mnafiki sababu sijui hili wazo la maamuzi magumu limemjia kichwani mwaka huu 2010

Yeye mwenyewe angekuwa wazi kwa kutoa mfano halisi ya maamuzi magumu yenye manufaa aliyoyafanya akiwa na rungu la kufanya maamuzi. Hatakiwi kuongea kwa nadharia tu sababu na yeye mwenyewe amewahi kukalia kiti cha kufanya maamuzi.
 
Hivi mnafikiri walipoamua kuhamisha makao makuu na kwenda Dodoma walikuwa wanafikiria nini? mmepata hawa walafi wanaoangalia mitumbo yao mnafikiri watafanya nini. Dar ni mji ambao unatakiwa kuachwa uendelee kama ulivyo na serikali kuhamia Dodoma mtakuwa mmemaliza matatizo ya foleni etc.
 
Hapo anajikosha ili watu wamfikirie tena na pengine apewe ulaji. Tena bahati mbaya kikwete hajui kuteua watu wachapa kazi usishangae baada ya kuvunja bunge mtu akateuliwa kuongoza jiji.

Kabisa mkuu, keshaona ubunge kachemsha sasa anataka afikiriwe huko ili ale kwa upole... unafiki mtupu....
 
Sawa hilo ni wazo zuri .laikni kwanini yeye alishindwa kufanya hayo maamuzi magumu ili hali alikuwa na madaraka makubwa kabisa...sasa hapo ndo maana tunaona ni unafiki tu wa kisiasa ...kuongea sana ..vitendo ziro.:angry:
 
Whether ni mnafiki au la, swala la kufanya uamuzi mgumu kulunusuru jiji sasa halina ubishi. Wataalamu wa mipango miji hapa JF tupeni solution ya hili tatizo bana, tuache kumshambulia Keenja, haitusaidii kitu.
 
Hayo ya miaka 10 ubunge yaweke pembeni kwanza....Mawazo(ushauri) yake unayaonaje....yatasaidia yaitekelezwa japo kwa uchache?

Mawazo yake yemepitwa na muda, Nyerere aliliona hilo 1973 akasema twende Dodoma, Dar Es Salaam haiwezi kuendelea, Tukakubali na tukachanga hela kufanikisha hilo, hela kibao ikatumika kudevelop infrastructure ya Dodoma na mpaka sasa serikali bado inalipa madeni hayo. Viongozi wengi ( keenja akiwemo) hawakutaka kuhama, wanakumbuka leo almost 40 yeras after. hayuko serious, labda anataka mji ugawanywe ili kuwe na majimbo mengi na ubungo ligawanywe ili apate sehemu ya rahisi kugombea.

Angepiga kelele wakati huo angeeleweka lakini sasa, ni mfamaji haachi kutapatapa.
 
Whether ni mnafiki au la, swala la kufanya uamuzi mgumu kulunusuru jiji sasa halina ubishi. Wataalamu wa mipango miji hapa JF tupeni solution ya hili tatizo bana, tuache kumshambulia Keenja, haitusaidii kitu.

tatizo sio keenja ila ni viongozi hawana dhamira, sheria ipo ya kuwa makao makuu yawe Dodoma, walisema mashirika yote yaenge 25% ya profit kudevelop Dodoma, wakasema tena hakuna kujenga ofisi za ubalozi na za serikali DSM isipokuwa Bandari tu na mashirika ambayo operations zake lazima ni DSM, hakuna aliyesikia. kama hawakusikia 1973 wa kusikia leo ni nani???????????
 
Ukweli ni ukweli tu hata kama ukisemwa na mpiga ramli au awaye yote. Keenja alikuwa na mengi mazuri wakati wa uongozi wa tume ya jiji.
Ilichokisema ni facts, bila kumuangalia yeye alipokuwa mbunge alifanya nini. Ni jukumu letu na tuliowakabidhi madaraka kuona kuwa wanafuata vipi ushauri ili kuondokana na hali mbaya ndani ya jiji letu. Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. HAPA KEENJA AMENENA JAMBO
 
Mimi kwa maoni yangu whether Dar inavunjwa au haivunjwi lakini hili la kutengeneza drainage systems za jiji ili ziendeane na hali halisi ya umati wa watu uliofurika Dar halikwepeki hata kidogo. Hatuwezi kuendelea kuwa na jiji ambalo population yake imeongezeka kwa asilimia kubwa sana ukilinganisha na miaka ya 60 ambapo haikufika hata watu laki mbili na sasa kuna watu zaidi ya milioni 4.

Ni lazima katika bajeti inayokuja zitengwe kati ya shilingi bilioni 500 hadi bilioni 700 kwa miaka mitatu ili kuanza kuboresha drainage systems kuanzia katikati ya jiji na baadaye katika vitongoji vyake vyote na kazi hii ikabidhiwe kwa kampuni ya kimataifa yenye ujuzi na uzoefu wa kufanya kazi kubwa kama hii, hili kama halikufanyika itafikia wakati shughuli za jiji itabidi zisimame kabisa kila kutapokuwa na mvua kubwa na pia kunaweza kutokea upotevu mkubwa wa maisha ya wakazi wa jiji na mali zao.
 
....................kuhamisha ofisi za wizara; serikali, na balozi kwenda makao makuu ya nchi kule Dodoma; kutasaidia kupunguza Msongamano DSM. Serikali ianze kuivunja Dar kwa kutekeleza hilo kwa vitendo. Maana kuna watumishi wengi walikwisha lipwa fedha za uhamisho kwenda Dodoma lakini hadi leo bado wapo Dar katika ofisi zilezile walimohamishwa, na hela wametumia. Na sina shaka watastaafu wakiwa Dar. TUHAMIE DODOMA; DSM TUWAACHIE WENYE MJI WAO!!1
 
Nyerere aliliona hili tangu 1973 na lingefanyika ilivyopangwa Dar isingekuwa na population kubwa kuliko uwezo wake na Dodoma mji ambao uko planned ndio ungemeza population ya watz wengi kwani shughuli nyingi za kiserikali na kibiashara zingekuwa hapo. Lililofanyika sana sana ni mjengo wa Bunge.........
 
Back
Top Bottom