Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,754
- Thread starter
- #21
Naona haya ni sehemu ya majibu(japo si rasmi) ambayo Kingobi kajibu kutokana na maoni haya ya Keenja
Jiji: Hatuhusiki na tatizo la foleni Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji, Bakari Kingobi amesema mfumo wa ushirikiano kati ya halmashauri hiyo, halmashauri za manispaa na Wakala wa Barabara (Tanroads), unakanganya hata wawekezaji, huku akisisitiza kuwa ofisi yake haihusiki na tatizo la foleni Dar es Salaam.
Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazolikabili jiji hilo pamoja na uwezo wake kimapato katika mahojiano maalumu na HABARI LEO, Kingobi alisema kwa sasa majukumu ya Jiji ni pamoja na kuzika watu wanaokufa na kukosa ndugu au wanaokufa kwa magonjwa ya mlipuko.
Alifafanua kuwa fedha inazokusanya jiji ambazo hazijafikia Sh bilioni tano tangu wameanza
kuwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mbali na kuzika watu hao pia zinatumika katika
uzoaji wa takataka na mradi wa gesi ya taka unaoendeshwa eneo la Mtoni na Pugu na kulipa
posho za madiwani katika mabaraza ya madiwani ya jiji.
Akielezea mkanganyiko huo, Kingobi alisema ingawa barabara zote za Dar es Saalam ni za Jiji, lakini katika ujenzi wanaohusika ni Halmashauri za manispaa na Tanroads na wao ni
washiriki tu wa usimamizi.
Alitoa mfano kwamba kuna kipande cha barabara kutoka Bendera Tatu kuja mjini ambacho kuna mamlaka mbili zinazohusika na ujenzi wake ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya
Ilala na Tanroads.
Alielezea kisa cha wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) waliokwenda ofisini kwake kuzungumzia ufadhili wa sehemu hiyo ya barabara, na
kushangazwa waliposhauriwa kuwa watalazimika kuzungumza na Tanroads na Halmashauri ya Wilaya Ilala kuhusu ujenzi wa mradi huo.
Mhasibu anayehusika na matumizi ya Jiji, Fadhili Izumbe, alitaja miradi mingine aliyosema fedha hizo za Jiji zimekuwa zikitumika, ambayo hata hivyo imeshakamilika au haipo chini
ya Jiji ukiwemo Mradi wa Mabasi yanayokwenda kasi Dar es Salaam (DART) ambao sasa upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Kwa mujibu wa Izumbe, mapato hayo pia yalitumika katika ujenzi wa shule ya Benjamin Mkapa ya Kariakoo, kuchangia hisa Benki ya Wananchi Dar es Salaam na ukarabati
wa taa za barabarani kwa mfano katika Barabara ya Nyerere (Pugu Road).
Takwimu ambazo gazeti hili linazo zinaonesha kuwa mwaka 2000 mapato ya Jiji yalikuwa Sh bilioni 7.2, lakini ilihusisha Jiji pamoja na manispaa zake tofauti na sasa kila Halmashauri
ina maeneo yake ya kukusanya mapato.
Takwimu zinaonesha kuwa ukusanyaji wa mapato katika mwaka wa fedha wa 2004/2005, Sh bilioni 3.516, 2005/06 Sh bilioni 3.760, 2006/07 Sh bilioni 3.771, 2007/08 Sh bilioni 4.014 na mwaka 2008/09 hadi Machi ilikusanywa Sh bilioni 2.720.
Mradi mkubwa unaoipatia jiji mapato Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo (UBT) ambacho kilichangia Sh milioni 964.095 katika mwaka wa fedha 2007/2008.
Hata hivyo, miradi mingi ambayo inapaswa kutumia mapato ya Jiji ambayo ilitajwa tayari, ilishakamilika kabla ya awamu hii ya uongozi.
Kwa mfano, Kingobi alisema yapo matumizi mengine lakini hayaonekani kwa wazi katika kulipa mishahara ya maofisa wasaidizi wasiolipwa kwa ruzuku ya Serikali Kuu, miradi yamaendeleo kama wa maboresho ya maeneo ambayo hayajapimwa (CIUP) na Jengo la Machinga Complex ambalo bado halijakabidhiwa kwa Jiji kutoka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Jiji ambayo baadhi ya majukiumu yake yalirithiwa na Halmashauri ya Jiji, Charles Keenja aliliambia gazeti hili kuwa maendeleo ya jiji, yanahitaji
utekelezaji zaidi kuliko maneno matupu yenye mipango lukuki isiyotekelezeka.
Alisema hajui kiasi halisi cha mapato cha mwaka huu kwa halmashauri zote nne (Temeke, Ilala, Kinondoni na Jiji) lakini anaamini mapato yameongezeka zaidi kama Jiji pekee bila halmashauri hizo inakusanya Sh bilioni 4.
"Jiji lina shida kubwa ya maji ingawa serikali inajitahidi kulipatia ufumbuzi, asilimia zaidi ya 75 ya mapato ya nchi hii, yanatoka Dar es Salaam, lakini bado masuala ya miundombinu
ya barabara imekuwa hadithi, mimi niliahidiwa barabara za juu pale Ubungo mpaka nimechoka ni zaidi ya miaka mitatu sasa," alisema Keenja.
Source: Gazeti la Habari Leo