RockSpider
JF-Expert Member
- Feb 16, 2014
- 6,861
- 2,754
Uzuri ni kuwa huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda wote .... hatimae Ukweli uko hadharani ..
Zitto atakuwa nuru ya ACT amenikumbusha Ayatola wa iran
Madaraka makubwa kama ya Mfalme Mswati
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT ZZK atakuwa na madaraka yafuatato
"Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania
i) Atakuwa kiongozi mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.
ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafisa wa ACT-Tanzania
iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii
iv) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama
v) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.
vi) Atasimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-Tanzania
vii) Iwapo kiongozi wa ACT-Tanzania hayupo kwa sababu yoyote ile basi Mwenyekiti wa chama Taifa atakuwa Kaimu kiongozi mkuu wa Chama.
viii) Iwapo kiti cha kiongozi mkuu wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu ulioelezwa katika
(vi) ya ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi Mkuu wa Chama mwingine.
ix) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa
litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya kura za wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.
x) Atakuwa ni nuru na taswira ya ACT-Tanzania"
Tafsiri rahisi hapa ni kuwa hiki chama
ni mali yake na yeye ndio muasisi na mfadhili mkubw wa chama hiki.
Hivi wanachama wa ACT wanawezaje kumpa madaraka makubwa hivi mwanachama aliye na umri wa siku 7 chamani hivi wanamwamini vipi?
Kama ya Mbowe vile.
Kwa mamlaka na madaraka haya walahi anaweza hata kuwatandika viboko wafuasi wake
Tulishasema mara nyingi hapa ZZK anajiona yeye ndio kila kitu. Kudhibitisha hilo hataki tena uenyekiti Bali Amejipa usupreme leader!
Kwa mamlaka na madaraka haya walahi anaweza hata kuwatandika viboko wafuasi wake
Kabisa Mkuu. Yaani ni Ayatollah Khomeini wa act. Majanga. Nilitaka nishangae asigombee wakati chama ni chake kama Cheyo!
hii ni ya kidini zaidi na ndiyo maana walisema wataifuta cuf mikoa ya pwani!