Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania

Bavicha mnaendelea kuitangaza ACT..

Mkuu mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa, lakini kwa muda nimekuwa nikiona michango yako haswa jukwaa hili imekaa ki nafiki nafiki sana, ndiyo zzk anamazuri yake lakini ana mabaya pia na kama huu ni mpango wake sasa demokrasia aliyokuwa anatuaminisha nayo imeishia wapi, angaza zaidi ya bavicha na chadema mkuu, vyote hivi vinamwisho si Tanzania
 
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT ZZK atakuwa na madaraka yafuatato

"Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania

i) Atakuwa kiongozi mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.

ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafisa wa ACT-Tanzania

iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii

iv) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama

v) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.

vi) Atasimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-Tanzania

vii) Iwapo kiongozi wa ACT-Tanzania hayupo kwa sababu yoyote ile basi Mwenyekiti wa chama Taifa atakuwa Kaimu kiongozi mkuu wa Chama.

viii) Iwapo kiti cha kiongozi mkuu wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu ulioelezwa katika

(vi) ya ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi Mkuu wa Chama mwingine.

ix) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa
litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya kura za wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.

x) Atakuwa ni nuru na taswira ya ACT-Tanzania"


Sasa mwenyekiti na m/ mwenyekiti kazi yao nn?

Tatizo lakujifanya wajuaji kumbe matutusa tu.
 
ujuha huu........hivi hadi leo tunao binadamu wanaokubali kuwa watumwa wa fikra? Naomba nirudie kusema huu ni UJUHA,hakuna mahala popote kulikowahi kuwa na katiba ya namna hii.
 
Du kweli zitto ndo mwemye act hapa ata katoto kadogo ukikapa hil fumbo kafukuzwa cdm kaenda act katoa tamko sigombei uenyekiti kaenda kwenye mkutano anatangaza anagombea kiongoz Mkuu wa chama ambaye ndo nuru ya act apa sasa mzito kajipiga chenga mwenyew aibu sana kwake cdm mlikuwa sawa 100% huwez anzisha chama ndan ya chama
 
Back
Top Bottom