Kudadadeki hili li zitto ni bonge la political mafia!
-huu siyo ujamaa bali ni unyamaa !
Kama chadema walivyompa uenyekiti DJ MBOWE
ni kama mfalme mbowe wa Chadema,teh teh vyama vya upinzani ni majanga matupu
Katiba wameikopi kutoka Iran.
ACT ni Tishio kubwa kwa uhai wa CHADEMA.
Mkuu mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa, lakini kwa muda nimekuwa nikiona michango yako haswa jukwaa hili imekaa ki nafiki nafiki sana, ndiyo zzk anamazuri yake lakini ana mabaya pia na kama huu ni mpango wake sasa demokrasia aliyokuwa anatuaminisha nayo imeishia wapi, angaza zaidi ya bavicha na chadema mkuu, vyote hivi vinamwisho si Tanzania
PakavuNateleza weka majukumu ya mwenyekiti
Majukumu ya mwenyekiti wa ACT ni haya yafuatayo. Mods naomba mpandishe hii post Juu.
/*l) Kazi za Mwenyekiti wa Chama Taifa :*/
i)Atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa kiongozi mkuu wa ACT-Tanzania
ii) Atakuwa mlinzi mkuu wa sera zilizopendekezwa na kupitishwa au jambo
lolote litakaloamliwa na kupitishwa na vikao cya chama na kuhakikisha
kuwa ngazi zote za chama zinatekeleza maamuzi yaliyotolewa
na
kuhakikisha kuwa ngazi zote zinafanya kazi ndani ya mipaka ya katiba,
kanuni, sera na maamuzi yoyote yaliyoagizwa na vikao vikuu vya chama
iii) Atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya chama ya kitaifa isipokuwa
vikao vya utendaji
iv)
Atafanya shughuli nyingine za Chama kama atakavyoelekezwa na
Kiongozi Mkuu wa Chama
v) Katika mikutano anayoiongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida
atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura ya wajumbe wanaoafiki na
wasioafika zitalingana
Kama ulivyoona mwenyekiti anaripoti kwa ayatollah ZZK
Hicho kipengele kimechomekwa lini?
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT ZZK atakuwa na madaraka yafuatato
"Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania
i) Atakuwa kiongozi mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.
ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafisa wa ACT-Tanzania
iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii
iv) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama
v) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.
vi) Atasimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-Tanzania
vii) Iwapo kiongozi wa ACT-Tanzania hayupo kwa sababu yoyote ile basi Mwenyekiti wa chama Taifa atakuwa Kaimu kiongozi mkuu wa Chama.
viii) Iwapo kiti cha kiongozi mkuu wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu ulioelezwa katika
(vi) ya ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi Mkuu wa Chama mwingine.
ix) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa
litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya kura za wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.
x) Atakuwa ni nuru na taswira ya ACT-Tanzania"