Kazi ya malezi ya watoto wetu sio ya Walimu tu

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Kazi ya malezi sio ya walimu tu,tunawasikilizisha watoto nyimbo za kina Zuchu nyumbani na mtaani halafu tunataka kwenye sherehe za shule wavaibu na nyimbo za Rose Muhando. Mtawaonea walimu bure tu kwa kukwepa uwajibikaji na kukubali matatizo yanaanzia nyumbani na sio shule,shuleni hamna redio wala tv.

Juzi tulikuwa na Nikki wa Pili ana project inaitwa ubongo clever (kutumia hit songs za nje na ndani kuzigeuza ziwe na maudhui ya masomo ya science zitumike shuleni Kibaha) akatoa mfano "ukienda nyumbani kwa mtu sebule yake inaweza ikakupa majibu kama nyumbani kwa mwanafunzi ni sehemu ya kujifunza pia au la" hawa watoto nyimbo wanazisikiliza majumbani kwao hivyo tatizo la kwanza ni walezi/wazazi wanawapa watoto wao content gani nyumbani.

Wasanii wanafanyabiashara hawana muda wa mtoto wako anasikiliza nini.
 
Back
Top Bottom