Kawambwa, Nahodha na Mwema wakutana na wanafunzi UDSM

Polisi wa kutuliza ghasia wamewapiga mabomu ya machozi wanafunzi wa UDSM. Mkasa huo umekuja mara baada ya kumalizika kikao cha wanachuo na waziri wa Elimu. baada ya wageni wote kuondoka ilikuja zamu ya FFU kuondoka kwenye eneo la tukio lakini wanafunzi kwa vile walikuwa wamepania kulipiza kisasi walianza kuwarushia chupa za maji FFU hivyo nao FFU kuanza kujibu mapigo kwa kupiga mabomu ya moshi kuwatawanya wanafunzi. Hivi ninavyoandika maeneo ya kampasi na uandisi na swimming pool hakutamaniki kwa moshi na watu wametawanyika wakikimbia ovyo.

Ni hayo kwa sasa kutoka mlimani.

Mi bado siamini kwamba eti mabomu ya machozi na maji washa yanatawanya watu wenye nia ya kweli ya kudai wanachotaka. Mbona mabomu na maji washa kule misri na tunisia yalikwisha watu wako pale pale? Kwa stahili hii hatuna wakombozi
 
heee hivi mabooom nchi hii hayajaisha kwakweli yanatumika saaana!
 
Waziri Shukuru katoka salama jamani?

Yaani anachomoka tu nyuma mabomu yakaanzwa kupigwa sijajua reaction ya wanafunzi wanaendela na mgomo au la!

Jana usiku order ilishatoka kwa waiziri kuwa wakiendelea hivi leo basi, most likely chuo kifungwe.... polisi wa chuo hawana nguvu tena kuzuia....

Mwili unasisimka natamani vyanzo hivi vya migomo vitumiwe vizuri kumshinikiza Kikwete aondoke madarakani!!
 
Yaani anachomoka tu nyuma mabomu yakaanzwa kupigwa sijajua reaction ya wanafunzi wanaendela na mgomo au la!

Jana usiku order ilishatoka kwa waiziri kuwa wakiendelea hivi leo basi, most likely chuo kifungwe.... polisi wa chuo hawana nguvu tena kuzuia....

Mwili unasisimka natamani vyanzo hivi vya migomo vitumiwe vizuri kumshinikiza Kikwete aondoke madarakani!!



bomu moja chuo kizima wanatawanyika na kukanyagana? Ingewezekana kama hawa wanafunzi wanaweza kupambana na polisi hadi maandamano yao yaingie uraiani.
 
.....matumizi ya nguvu za dola kwa raia mara kwa mara kutawafanya wawe sugu, wayazoee hayo magari ya maji ya kuwasha na anti-riot bombs (mabomu ya machozi)!! Laiti wangepewa dhamana ya vyeo kwa utendaji wao wangekuwa watu wa busara zaidi wa kutaka suluhu ila kwa vile wanapewa vyeo kama asante, undugu na udini wanatumia akili zilizo matakoni badala ya vichwani.
 
Viongozi na wahusika wa clouds FM, tafadhali tunawaomba muondoeni Kibonde kwenye JAHAZI, watu waliolalamika kuhusu huyu bwana ni wengi sana. Ninapendekeza mpelekeni kwenye Africa Bambataa au Taarabu.


we! we! viongozi wa clouds wanamtumikia kafiri wapate mtaji.ciunajua wame'launch' ka'TV' Kibonde yuko pale kwa jina la jk,ciuliona kwenye kampeni za chichiem
 
Kibonde ameachika kwa bwana wake sasa anatafuta bwana mwingine kiguvu, huyu dada ana matatizo sana antaka awaunganishe watu wengi kwenye mtandao wake wa baba ya muziki.
 
Mheshimiwa kajichanganya,kashindwa kujibu maswal magumu na ya mtego ya wanafunzi,aishiwa kuzomewa na kuimbiwa ashuke jukwaani.Wanafunzi wahoji kama serikali haina hela za kuilipa DOWANS zinatoka wapi?Wataka kesi walizofunguliwa wenzao zifutwe mara moja,wasema mbona mafisadi wanaachiwa?Wamuagiza waziri kutoa tamko papo hapo juu ya madai yao,waziri aogopa kujicomitte,baada tu ya waziri kuondoka wanafunzi waanza kuwashambulia polisi kwa mawe na makopo,polisi nao wajibu kwa mabomu ya machozi,vurumai kubwa laibuka,ila kwa sasa hali kidogo imetulia.Ila wanafunzi walikataa agizo la waziri kuwataka warudi madarasani ilihali matatizo yao yakishughulikiwa.
 
nawasalim wana JF
leo jtatu majira ya saa nane mchana mabomu ya machozi yamelipuliwa UDSM
Personal nlikuwepo ilikuwa hivi:
kin'gora kililia pale UCC,mara nkaliona gari liliombeba IGP MWEMA likipita kuelekea MAJI kwa mwendo mdogo
Dakika nne baadae nkasikia mlipuko wa kwanza, nkatoka njee nkawaona wanafunzi wengi wa kike wakikimbia nadhan walikuwa wanatokea NKURUMAH

KUSHANGAA INAKUWAJE MARA MILIPUKO YA MFULILIZO NKAWAI USAFIRI nkiwa naondoka nkawaona wamama wawili wakipanda kilima kwa shida huku wamefumba macho tukawasaidia mpaka pale MAJI.
 
Naomba wenye taarifa za ziada watupe manake mimi nilikutwa kwenye safari zangu za mishemishe za kujitaftia riziki, pale UCC palikuwa tulivu sana ila gafla pakaaribika sikujua timbwili lilianzaje.
 
Tanzania chuo ni UDSM tu...
Hivyo vingine ni vyuo vya Kata kama zilivyo Sekondari za Kata
ktk watu wenye ubongo usiofanya kazi basi nawe ni mmoja wapo.unaongelea chuo mnachopita kwa 40%,choo SUA tuone kama utanusa hata mwaka wa pili utaishia kulamba pesa ya bodi na kukimbia chuo
usidharau baadhi ya vyuo eti kwa kuwa umesoma hapo,hebu angalia vyuo 100 bora Africa utakiuna sua kipo kileleni hakuna cha udsm wala udom

msema ukweli hapendwi daimaaaaaa:clap2:
 
Naomba wenye taarifa za ziada watupe manake mimi nilikutwa kwenye safari zangu za mishemishe za kujitaftia riziki, pale UCC palikuwa tulivu sana ila gafla pakaaribika sikujua timbwili lilianzaje.

wani na leo wameandamana? si walisema wamesitisha kwa muda au?
 
Wanafunzi wametawanyika , wamekanyagana sana, wamejaribu kutupa mawe, ila kutokuwa wamoja kumewaponza , Engineering ndio wanaonekana bado wana nguvu, kwani wao wana ka-mgomo kao ka tofauti na wenzao, wao wanashinikiza mwanafunzi wa mwake wa nne aliyedisco arudishwe!

machozi tumetoa hata members of staff, tumetafuta maji na kunawa bila kupenda, wanafunzi wamekimbilia maofisini ,mwetu hapa ninao akina dada wanne hivi wanalia tu!!! mapinduzi gharama sana kwa nchi za kiafrika.

Dowans..dowans iliimbwa live....

sijajua chanzo cha mabomu...ila nilisikia shukuru kawambwa akiongea nao naona hawakuelewana , mwanzisha thread atatusaidia.

Madai ya elfu kumi yameanza tangu 2007!

Poleni Sana Kwa nini wanakuja chuoni wakiwa tayari na majibu yao hii mbaya sana watalikoroga kama wanaanza vita na wanafunzi
 
Back
Top Bottom