TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Katibu Myeka wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mzee SAMWEL KASORI ameibuka na kufukua ukweli uliojificha, baada ya baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kulihusisha jina la Mwalimu na mbio za urais.
Itakumbukwa kuwa Feb. 10 mwaka huu, Mbunge wa mbinga Magharibi, John Komba alidai kabla Mwalimu Nyerere hajaaga dunia alimkubali (aliridhika na) LOWASSA. KATIBU Myeka wa Nyerere, Mzee Samweli Kasori amesema, Mwalimu alitilia shaka uadilifu wa LOWASSA na hakuwahi kuridhika na utendaji wake hata kidogo.
Mzee Kasori anaendelea kusema Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa LOWASSA alikuwa ni mmoja wa wagombea nafasi ya urais mwaka 1995 na alienfukiwa kwa hoja nzito ya kutokuwa Mwadilifu na Babab wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere.
Mzee Kasori anasema baada ya kuenguliwa, Lowassa alimpigia simu kumuomba amuombee kwa baba Taifa aende Monduli amsafishe ili asikose Ubunge kutokana na maneno aliyoyasema Dodoma ya kumuengua kwenye kugombea Urais, jambo ambalo lilikuwa vigumu kwake(yeye mzse Kasori).
Baada ya Lowassa kuona Mzee Kasori amekataa akamtumia mzee Rashid Mfaume Kawawa ndipo mzee Kawawa akampigia Simu Mzee Kasori kutekeleza maombi ya Lowassa kwa Mwalimu.
Baada ya purukushani zote za Mzee Kasori kuhakikisha ujumbe unamfikia Mwalimu bila kuzikwza pande zote yaani Lowassa, Mzee Kawawa na Mwalimu, Nyerere alikuja alihitimisha hoja hiyo huku akionekana kukasirishwa sana kitendo hicho kwa maneno yafuatayo:
1. Nyerere alimwambia Mzee Kasori, nenda umwambie Kawawa asiwe mjinga kama LOWASSA
2. Nyerere alipokutana na Kawawa akamuuliza, Rashidi, nilimtuma Mzee Kasori akwambie usiwe mjinga kama LOWASSA, amekwambia?
3. Baada ya swali hilo Nyerere akamwambia, Kawawa, Lowassa ni mtoto mdogo sana kwa Mzee Kasori na kwa maana hiyo ni jasiri sana mpaka amtume mzee anayemzidi. Nyerere akaenda mbali akamwambia Kawawa, kwa vile umeniambia wewe maneno haya naamini angeniambia Mzee Samwel Kasori nisingeamini.
NYERERE akasema ujasiri huu wa Lowassa kwa nini hakuutumia kutuambia ukweli kuhusu mali alizonazo nyingi kuzidi mimi(yeye Nyerere) ambaye nimekuwa rais wenu kwa kipindi kirefu?
4. Mwalimu alihitimisha mjadala wa LOWASSA kumuomba amsafishe Monduli ili asikose urais kwa kumwambia Kawawa, "Bwana Rashidi, nakuomba hivi, Kamwambie Mwenyekiti wa CCM, Mh. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowassa na nitagharamia mkutano huu kwa pesa zangu mwenyewe, kamwe msitumie pesa za Chama wala serikali, Monduli sitokwenda, kwa umri wangu , LOWASSA ni mtoto wangu tena mdogo sana na kwa heshima niliyonayo kwangu na kwa Chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina la bwana Lowassa asikose ubunge.
Mzee, Samwel Kasori anamalizia kwa kusema " MKUTANO ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli.
Alichukia sana tabia za Lowassa. Hadi Baba wa Taifa anafariki, sikuwahi na sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowassa anakanusha alivyolimbikiza mali akiwa tumishi wa CCM na Serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza"
Chanzo: Gazeri la Raia Tanzania