Katibu wa Nyerere: Jina la mwalimu linatumiwa vibaya na kambi ya Lowassa

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Katibu Myeka wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mzee SAMWEL KASORI ameibuka na kufukua ukweli uliojificha, baada ya baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kulihusisha jina la Mwalimu na mbio za urais.

Itakumbukwa kuwa Feb. 10 mwaka huu, Mbunge wa mbinga Magharibi, John Komba alidai kabla Mwalimu Nyerere hajaaga dunia alimkubali (aliridhika na) LOWASSA. KATIBU Myeka wa Nyerere, Mzee Samweli Kasori amesema, Mwalimu alitilia shaka uadilifu wa LOWASSA na hakuwahi kuridhika na utendaji wake hata kidogo.

Mzee Kasori anaendelea kusema Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa LOWASSA alikuwa ni mmoja wa wagombea nafasi ya urais mwaka 1995 na alienfukiwa kwa hoja nzito ya kutokuwa Mwadilifu na Babab wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere.

Mzee Kasori anasema baada ya kuenguliwa, Lowassa alimpigia simu kumuomba amuombee kwa baba Taifa aende Monduli amsafishe ili asikose Ubunge kutokana na maneno aliyoyasema Dodoma ya kumuengua kwenye kugombea Urais, jambo ambalo lilikuwa vigumu kwake(yeye mzse Kasori).

Baada ya Lowassa kuona Mzee Kasori amekataa akamtumia mzee Rashid Mfaume Kawawa ndipo mzee Kawawa akampigia Simu Mzee Kasori kutekeleza maombi ya Lowassa kwa Mwalimu.

Baada ya purukushani zote za Mzee Kasori kuhakikisha ujumbe unamfikia Mwalimu bila kuzikwza pande zote yaani Lowassa, Mzee Kawawa na Mwalimu, Nyerere alikuja alihitimisha hoja hiyo huku akionekana kukasirishwa sana kitendo hicho kwa maneno yafuatayo:

1. Nyerere alimwambia Mzee Kasori, nenda umwambie Kawawa asiwe mjinga kama LOWASSA

2. Nyerere alipokutana na Kawawa akamuuliza, Rashidi, nilimtuma Mzee Kasori akwambie usiwe mjinga kama LOWASSA, amekwambia?

3. Baada ya swali hilo Nyerere akamwambia, Kawawa, Lowassa ni mtoto mdogo sana kwa Mzee Kasori na kwa maana hiyo ni jasiri sana mpaka amtume mzee anayemzidi. Nyerere akaenda mbali akamwambia Kawawa, kwa vile umeniambia wewe maneno haya naamini angeniambia Mzee Samwel Kasori nisingeamini.

NYERERE akasema ujasiri huu wa Lowassa kwa nini hakuutumia kutuambia ukweli kuhusu mali alizonazo nyingi kuzidi mimi(yeye Nyerere) ambaye nimekuwa rais wenu kwa kipindi kirefu?

4. Mwalimu alihitimisha mjadala wa LOWASSA kumuomba amsafishe Monduli ili asikose urais kwa kumwambia Kawawa, "Bwana Rashidi, nakuomba hivi, Kamwambie Mwenyekiti wa CCM, Mh. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowassa na nitagharamia mkutano huu kwa pesa zangu mwenyewe, kamwe msitumie pesa za Chama wala serikali, Monduli sitokwenda, kwa umri wangu , LOWASSA ni mtoto wangu tena mdogo sana na kwa heshima niliyonayo kwangu na kwa Chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina la bwana Lowassa asikose ubunge.

Mzee, Samwel Kasori anamalizia kwa kusema " MKUTANO ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli.

Alichukia sana tabia za Lowassa. Hadi Baba wa Taifa anafariki, sikuwahi na sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowassa anakanusha alivyolimbikiza mali akiwa tumishi wa CCM na Serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza"

20150212_075959.jpg

Chanzo: Gazeri la Raia Tanzania
 
Tusubiri utetezi wa Ocampo four na laki si pesa bila kumsahau John Okello
 
mawazo yanabadilika kila mara,si ajabu nyerere angekuepo leo chaguo lake lingekua lowassa na angempigia kampeni kiroho safi,tusiwe na narrow and static thinking.
TEAM lowassa
 
Last edited by a moderator:
mawazo yanabadilika kila mara,si ajabu nyerere angekuepo leo chaguo lake lingekua lowassa na angempigia kampeni kiroho safi,tusiwe na narrow and static thinking.
TEAM lowassa
Subutu! Nyerere angekuwepo, Lowassa angeshajifia siku nyingi sana, lakini hata hivyo mzimu wake bado unaweza kuondoka naye.
 
tumechoka na habari zahuyu mzee kila siku anafikira atoke vipi. lowassa hamuhitaji nyerere kwenda ikulu. watanzania hatumuhitaji nyerere atuchagulie kiongozi. alishafanya hivyo na bado akafail. sasa ni wakati wa kuchagua mtu tunayemtaka sisi wenyewe ambaye tuta dela naye sisi wenyewe. utajiri wa lowassa si shida. wapo waliingia kama maskini na tumeona jinsi ambavyo wameondoka matajiri kwa kuwaridhisha watoto na wake zao mali nyingi sana kupitia biashara haramu na mikataba ya kifisadi. huyu mzee anazeeka vibaya, tayar muda wake ulishaisha anachofanya sasa ni kutafuta kick kwenye vyombo vya hbr siku si nyingi na yeye atasema nyerere amemtokea kamwambia fulani ndo anafaa kugombea urais. hata nyerere angekuwa hai tusingemruhusu atuchagulie Rais. so mi sidhani kama hapa kuna hoja ya msingi. nachojua. LOWASSA HAHITAJI JINA LA NYERERE KUINGIA IKULU. WATANZANIA WAKIMUHITAJI WATAMPA KURA AINGIE IKULU.
 
Mwalimu amekufa na Siasa zake za Ujamaa na Kujitegemea na Chama chake cha Tanu na CCM ile.
Nchi ilibadilika tukaingia kwenye uchumi wa soko huria ambapo sasa "market forces" ndio determinant ya bei ya bidhaa!, hivyo Azimio la Arusha likazikwa na Azimio la Zanzibar!, CCM ya sasa imebinafsishwa kwa wenye nazo!, imehodhiwa na wenye pesa, hivyo rais wa Tanzania wa 2015 doesn't have to be chaguo la Mwalimu, kwa sababu hata Mwinyi hakuwa Chaguo la Nyerere, Mkapa hakuwa chaguo la Mwinyi, na JK hakuwa chaguo la Mkapa!.

Rais tunayemtaka 2015 sio chaguo la mtu bali ni chaguo la watu!.

Pasco
 
Lizaboni hata wewe unakubaliana na jambo hili? umeshahau nyerere huyu huyu si rafiki wa kikwete ? au adui wa rafiki yako ni ndugu yako? huyu nyerere alimwona kikwete ana akili za kitoto kipindi kile na alitumia tu kauli ya busara kumkataa na leo hii angekuwepo angesema nliwaambia kikwete bado mdogo hajakomaa miaka 20 baadaye. lakini linapokuja suala la nyerere kutumika kumpinga lowassa nawe unashabikia kana kwamba nyerere ni nabii? nyerere alikuwa binadamu mwenye damu na nyama kama mimi na wewe. alikuwa na mitazamo yake na alikuwa na hisia kama wengine.so si kila ambacho alisema nyerere kkilikuwa sahihi. na ndo maana hata alimchagua mkapa ambaye mwishoni alikuja kufanya ufisadi mkubwa sana. huyu alionekana kuwa alikuwa clean.....
hoja za kumtumia nyerere zisitumike . LOWASSA HAMUHITAJI NYERERE KUINGIA IKULU.ANAHITAJI KURA ZA WATANZANIA.
TUACHANE NA HOJA MFU.
 
tumechoka na habari zahuyu mzee kila siku anafikira atoke vipi. lowassa hamuhitaji nyerere kwenda ikulu. watanzania hatumuhitaji nyerere atuchagulie kiongozi. alishafanya hivyo na bado akafail. sasa ni wakati wa kuchagua mtu tunayemtaka sisi wenyewe ambaye tuta dela naye sisi wenyewe. utajiri wa lowassa si shida. wapo waliingia kama maskini na tumeona jinsi ambavyo wameondoka matajiri kwa kuwaridhisha watoto na wake zao mali nyingi sana kupitia biashara haramu na mikataba ya kifisadi. huyu mzee anazeeka vibaya, tayar muda wake ulishaisha anachofanya sasa ni kutafuta kick kwenye vyombo vya hbr siku si nyingi na yeye atasema nyerere amemtokea kamwambia fulani ndo anafaa kugombea urais. hata nyerere angekuwa hai tusingemruhusu atuchagulie Rais. so mi sidhani kama hapa kuna hoja ya msingi. nachojua. LOWASSA HAHITAJI JINA LA NYERERE KUINGIA IKULU. WATANZANIA WAKIMUHITAJI WATAMPA KURA AINGIE IKULU.
Semeni yote, ila maneno ya wazee wenye busara kama mzee Kasori si ya kupuuza hata kidogo. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
 
SAMWEL KASORI Hapa tu alikuwa katibu wa nyerere. sipati picha angekuwa ni mke wa nyerere au mtoto wa nyerere angemtumiaje nyerere kama mtaji wake.
TUMEMCHOKA yeye hana jipya miaka mingi baada ya kifo cha nyerere bado anataka atumie jina lake kusikika.hajasikika akizungumzia mambo ya msingi kama kupinga rushwa,uchakachuaji wa kura,siasa chafu,katiba. yeye anachojua ni kumzungumzia LOWASSA Against nyerere.... mbona hasemi suala la akaunti nje
 
Lizaboni hata wewe unakubaliana na jambo hili? umeshahau nyerere huyu huyu si rafiki wa kikwete ? au adui wa rafiki yako ni ndugu yako? huyu nyerere alimwona kikwete ana akili za kitoto kipindi kile na alitumia tu kauli ya busara kumkataa na leo hii angekuwepo angesema nliwaambia kikwete bado mdogo hajakomaa miaka 20 baadaye. lakini linapokuja suala la nyerere kutumika kumpinga lowassa nawe unashabikia kana kwamba nyerere ni nabii? nyerere alikuwa binadamu mwenye damu na nyama kama mimi na wewe. alikuwa na mitazamo yake na alikuwa na hisia kama wengine.so si kila ambacho alisema nyerere kkilikuwa sahihi. na ndo maana hata alimchagua mkapa ambaye mwishoni alikuja kufanya ufisadi mkubwa sana. huyu alionekana kuwa alikuwa clean.....
hoja za kumtumia nyerere zisitumike . LOWASSA HAMUHITAJI NYERERE KUINGIA IKULU.ANAHITAJI KURA ZA WATANZANIA.
TUACHANE NA HOJA MFU.
Nyerere hakumkataa KIKWETE, alisema muda wake bado, na ndiyo maana muda wake ulipofika, alikuwa rais. LOWASSA ni fisi kabisa.
 
Hii article Mzee kasori aliitoa Enzi zile Lowassa anaachia Uwaziri Mkuu!!! Mzee kasori alikuwa anawasiliana na Samwel Sita kwa karibu sana!!! Inaonekana Sitta alikuwa anamtumia Mzee kasori kuweza kufanikisha Fitna zake!!! Anasahau kuwa Magazeti yote ya 1995 yalimnukuu Nyerere akimfagilia Lowassa kwa sanaa... Fitna kuwa Mwalimu alikuwa anahoji Utajiri wa Lowassa usiolingana na umri wake ALIEMJIBU Mwalimu alikuwa Sitta huyo huyo aliemwambia mwalimu kuwa vyanzo vyake vya habari havikuzingatia Azimio la Zanzibar na kuwa Lowassa amewapangisha Ubalozi wa South Africa kwa rates za Ulaya !!!! ... Mzee kasori anafahamu ukweli huu!!! Mzee kasori anatakiwa aweke bayana Lowassa alipotaka Mwalimu aende Monduli na hatimae Mwalimu akakubali kwenda kufanya kampeni ya jumla Arusha ilitokana na Makubaliano kuwa Lowassa alikuwa MSAFI na kuwa Fitna na Chuki za wahasimu wake akina Sozigwa ndo zilimpotosha Mwalimu!!! Mzee Kasori anatakiwa aweke bayana kuwa baada ya Mwalimu kuujua Ukweli alitaka kurudisha Kadi ya CCM na alikataa katakata kuongea na akina Maokola majogo... Hatimae SURA halizi za akina MKAPA et al zilionekana pale walipo Uza NBC na hatimae kumnyamazisha JKN kama walivyofanya kwa Moringe Sokoine ... Itoshe Kusema LOwassa ni Mpango wa Mungu .. wamejaribu sana kumzimisha lakini mara zote Military Intel huwa inamuokoa ... TataMadiba
 
Last edited by a moderator:
kikwete alikuwa rais si kwa sababu ya kuruhusiwa na nyerere.. nyerere alisema kikwete ana utoto... akili yake haijakomaa.nyerere hakuwah mtaka kikwete, nyerere alimtaka salim ahmed salim.angekuwepo nyerere bado angempinga kikwete .
 
Swali la Kizushi: Ikiwa kweli Lowassa ndai ya CCM alionekana hana maadili na alilimbikiza mali hasiyoweza kuielezea imepatikanaje, ilikuwaje tangia wakati huo hajawahi kukosa Uwaziri (na mpaka akapewa Uwaziri Mkuu)? Au tuseme maadili ni pale tu unapotaka kuwa Rais na mwenyekiti wa Chama? Mzee Kasori, je utajiri ulipimwa kwa kulingnisha Nyerere alicho nacho?
 
Back
Top Bottom