Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,119
- 9,049
Kufunga wakati huu wa ramadhani ni sehemu ya ibada kwa muumini wa dini ya kislam. Nijuavyo au ninavyoamini ibada ni juu mtu na mungu wake. Lazima itoke rohoni kwake maana mbele ya mungu hakuna unafiki. Unaweza ku-pretend kufanya jambo mbele ya binadamu mwenzako lakini sio mbele ya mungu.
Tukirudi kwenye ibada ya kufunga, muumini anatakiwa aoneshe kushinda vishawishi kwa kutokula siku nzima. Lazima itoke rohoni na sio kwa kulazimisha. Sasa hii ya kulazimisha watu inatoka wapi? Kama mtu hakufunga kula (ibada) kinakuhusu nini maana ni juu yake na mungu wake?
Kuna binadamu wengi leo wanaofuata dini kwa mkumbo tu. Utamlazimishaje mtu afuate dini kama haiamini? Bila imani mbona ni kazi bure...itakuwa ni kushindishana njaa tu