Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Nimeyaangalia mabango yote, yaliyobebwa na wafanyakazi, yaliyopita mbele ya mgeni wa heshima, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, sikuona hata bango moja, lililokemea vikali ufisadi mkubwa uliofichuliwa na CAG, Charles Kicheere, wa ufujaji wa mabilioni ya shilingi za pesa za walipa kodi wa nchi hii.
Nimeona mabango Karibu yote, yakihimiza maslahi bora kwa wafanyakazi, ikiwemo kuongeza kima cha chini cha mshahara.
Ni jambo la kushangaza, kuona Katika wafanyakazi wote wa nchi hii, hakuna mfanyakazi yeyote aliyekerwa na ufisadi mkubwa uliofanywa na baadhi ya watumishi wachache wa Umma!
Hivi wafanyakazi, wanajua kweli madhara yaliyofanywa na watendaji hao wachache kuiba mabilioni ya shilingi ya walipa kodi wa nchi hii?
Hivi wafanyakazi wanajua kuwa kama siyo ubadhiifu mkubwa unaoendelea kufanywa huko Serikalini, wangweza kulipwa maslahi bora, hata kwa kima kilichopendekezwa na TUCTA cha shilingi milioni moja kwa mwezi??
Hata kauli mbiu ya mwaka huu, MISHAHARA NA MASLAHi BORA YA WAFANYAKAZI NDIYO KILIO CHETU, haikuweza kutumizwa na Rais kwa sababu ya ubadhirifu mkubwa uliotokea Serikalini.
Swali tunalojiuliza wananchi wa nchi hii, je ufisadi mkubwa unaofanywa huko Serikalini, una baraka ya uongozi wa juu wa hapa nchini?