Kero za Wafanyakazi ambazo TUCTA wataziwasilisha mbele ya Rais Samia siku ya Mei Mosi 2023

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,856
18,271
Habari za leo ndugu wakuu! Nawasalimu kwa jina la JMT. Baada ya salamu naomba niingie kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha.

Wakati siku ya wafanyakazi duniani ikikaribia, naomba niweke wazi kero za wafanyakazi, hasa wa sekta ya umma, ambazo Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania (TUCTA) wataziwasilisha mbele ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan siku ya Mei Mosi 2023, sherehe ambazo kitaifa zitafanyika Mkoani Morogoro.

1. Nyongeza ya mishahara
Hiki ndicho kilio kikubwa cha watumishi wa umma katika nchi hii. Kwa upande wa wafanyakazi wa sekta binafsi, hali sio mbaya sana kwani wengi wao wana mishahara mizuri inayoongezeka kwa uhalisia bila mizengwe yoyote. Kwa upande wa wafanyakazi wa serikali, hali ni mbaya sana. Hata ile nyongeza ya mishahara ya kisheria ya kila mwaka haifanyiki hadi Rais atoe tamko. Tukumbuke kwamba nyongeza ya mishahara ya kila mwaka ipo kwa mujibu wa sheria. Jambo hili liliwahi kusemwa na mbunge nguli marehemu Kasuku Bilago bila kupepesa macho.


Inasikitisha kwamba wabunge mashuhuri kama huyu walifanyiwa mizengwe na Magufuli kwenye uchaguzi wa 2020 ili wasipate nafasi ya kurudi bungeni kutetea wafanyakazi.

Magufuli hakuwapenda wafanyakazi hata kidogo ndio maana alikuwa anawatumbua ovyo bila kufuata utaratibu. Tunajua Mh Dr Samia anawapenda wafanyakazi na serikali yake imeyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyosababishwa na Magufuli. Lakini bado haitoshi.

Tunakuomba mama yetu uendelee kuwatetea watumishi wa umma kwani ndio nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa letu. Watumishi wa umma waliobondeka mioyo kwa sababu ya kutoongezwa mishahara na marupurupu mengine ndio chanzo cha ufisadi unaolitesa taifa. Hatutaki watumishi wa umma waendelee kufanya kazi kwa kinyongo kwa sababu ambazo zipo ndani ya uwezo wako. Kama wasaidizi wako ndio wanakuangusha katika hili, washughulikie ipasavyo na wale wasioweza kwenda na kasi yako, wakupishe.

2. Kupandishwa vyeo vya muundo
Kwa mujibu wa sheria, mtumishi wa umma anapaswa kupandishwa cheo kila baada ya miaka minne. Ilikuwa miaka mitatu lakini iliongezwa hadi minne na yote hii ni kwa sababu ya kutaka kuwakandamiza wafanyakazi wa sekta ya umma. Huyu mtu aliyebuni wazo la kuongeza miaka kutoka mitatu hadi minne mbinguni hafiki ng’o!

Ijapokuwa mtumishi anastahili kupanda cheo kila baada ya miaka 4 lakini maofisa utumishi kwenye halmashauri zetu wamekuwa mwiba ulioshindikana. Hawapandishi watumishi vyeo mpaka Rais atoe tamko. Huku ni kukiuka sheria ya utumishi wa umma waziwazi. Kama haya sio maelekezo ya Rais, basi tunakuomba mama yetu Dr Samia uweze kusikia kilio hiki cha wafanyakazi.

Inasikitisha kuona watumishi hawajapandishwa vyeo kwa miaka zaidi ya 10 wakati sheria inatamka wazi kupanda cheo ni kila baada ya miaka 4! Unakuta mtumishi aliyeajiriwa mwaka 1989 analingana cheo na mtumishi aliyeajiriwa mwaka 2002 kwa sababu tu ya kushindwa kumpandisha cheo kwa wakati. Hii haikubaliki hata kidogo na inakatisha tamaa na kuvunja moyo.

Kwakuwa kupandishwa cheo kwa utashi wa Rais kulianzishwa na Magufuli na kwa kuwa wewe Dr Samia ulishajipambanua kwenda kinyume na ukandamizaji wa Rais aliyekutangulia, basi tunakuomba mama yetu uwasisiteze maofisa utumishi wa halmashauri wawapandishe vyeo watumishi wa umma kwa wakati bila kuchelewa. Asiyeweza kutekeleza hili, akupishe. Huwezi kujua huenda HRO’s wanatumiwa na genge haramu la Sukuma Gang kukukwamisha mwaka 2025 kwa kutaka kujengea chuki kati yako na wafanyakazi wa sekta ya umma.

3. Kufutwa kwa sheria ya kikokotoo
Wafanyakazi, hasa katika sekta ya umma, wanajua fika kuwa mafao yao yameporwa kwa sheria ya kikokotoo ambapo 67% ya mafao yao hayalipwi huku wafanyakazi wakiambulia 33% tu kipindi wanapostaafu! Tunakuomba Mh Rais utamke kufutwa kwa sheria hii kandamizi kwa sababu zifuatazo:

(i) Laana kwa serikali na nchi: Nchi italaaniwa kwa kupora jasho la wafanyakazi wanyonge walioitumikia nchi kwa moyo mkunjufu bila kuchoka. Fikiria mtu anaitumikia nchi kwa zaidi ya miaka 30 lakini akistaafu hana mafao. Hii ni laana kubwa sana ambayo itaendelea kuitafuna nchi hadi Yesu atakaporudi.

(ii) Ongezeko la ufisadi: Kwa kuwa wafanyakazi hawana mafao ndio maana wanaamua kujichotea mafao yao kwa njia ya ufisadi na kuwekeza ili watakapostaafu wawe na miradi ya kufanya, kama ilivyokuwa kabla kupunjwa mafao yao.

Tuwashukuru wabunge wa upinzani ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwatetea wafanyakazi kuhusu unyonyaji wa kikokotoo. Pongezi nyingi zimwendee Mh Esther Bulaya (mbunge wa viti maalumu) kwani amekuwa akikazia sana dhuluma hii huko bungeni, ijapokuwa hapati uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wabunge wengine.


Aidha, pongezi zimfikie mbunge wa zamani wa Tarime vijijini, John Heche, kwa jitihada zake binafsi kutetea wafanyakazi wanaumizwa na kikokotoo hiki batili kabisa kuwahi kutokea katika nchi hii.


4. Uhamisho wa watumishi wa umma
Zamani wakati wa awamu ya kwanza na ya pili ya uongozi wa nchi hii, watumishi wa umma walikuwa wakihamishwa bila mizengwe. Mtumishi alikuwa anaajiriwa kwa mara ya kwanza huko Songea anakuja kustaafia Kagera. Uhamisho kwa watumishi wa umma haukuwahi kuwa kero kipindi hicho. Sasa hivi hata kuhama kituo cha kazi ndani ya halmashauri moja imekuwa ni kero isiyoelezeka. Mwalimu anaajiriwa shule ya Msingi Mchambawima anafundisha hapo kwa miaka 40 mpaka anastaafu. Hii haikubaliki hata kidogo.

Watumishi wa umma wanayo haki ya kuhama kuwafuata wenza wao kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa. Kwa bahati mbaya hata mtumishi akifuata utaratibu wa kisheria hahamishwi ng’o! Matokeo yake sasa wameibuka matapeli na madalali wanaokula pesa za walimu kila kukicha kwa kisingizio cha kuwafanyia mipango ya uhamisho.

Na baada ya uhamisho kuonekana kero ya kiutumishi, baadhi ya maofisa wa serikali wanaohusika na uhamisho wamegeuza hii kero kuwa fursa kwao. Kuna watumishi wanakamuliwa hadi Tsh 1,000,000 ili wafanyiwe mipango ya uhamisho. Na unaweza kukamuliwa hicho kiasi cha fedha na usihame! Uhamisho umekuwa biashara ya magendo inayowaumiza watumishi wa umma, hasa walimu, bila huruma.

Kimsingi na kwa mujibu wa sheria, mtumishi anapopata nafasi ya kuhamia kwenye halmashauri nyingine kwa kufuata utaratibu, anapaswa ahame.

Tatizo serikali nayo imekuwa kama kinyonga kwa kubadilisha matamko kila kukicha yanayolenga kuzuia uhamisho wa watumushi wa umma. Uhamisho sio hisani na hauwezi kuonekana tatizo ikiwa serikali itaacha urasimu wa kuwazuia wafanyakazi kuhama kwa mujibu wa sheria na utaratibu uliowekwa.

Tunakuomba mama Samia uwasaidie watumishi wa umma waliokwama kwenye vituo vyao vya kazi kwa zaidi ya miaka 10 sasa licha ya kuwa na barua halali za uhamisho lakini wanakwamishwa na baadhi ya wasaidizi wako wa ngazi za chini. Hiki kilio cha wafanyakazi cha muda mrefu kimesababisha ndoa za baadhi ya watumishi kuvunjika, watumishi kuacha kazi na hata wengine kujinyonga pale wanaposhindwa kupewa haki yao ya msingi ya uhamisho halali.

5. Kuingilia kazi ya utendaji wa vyama vya wafanyakazi
Ni muda mrefu sasa serikali imekuwa ikichomekea makada kwenye vyama vya wafanyakazi ili kuwavurugia wafanyakazi michakato ya kudai maslahi yao ya msingi. Tunakuomba Dr Samia uingilie kati hili suala ili vyama vya wafanyakazi viwe autonomous na viweze kufanya kazi yake ya msingi ya kutetea wafanyakazi na kujenga uhusiano mwema kati ya serikali na wafanyakazi.

6. Kusiasisha cheo cha ukurugenzi
Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuta cheo cha ukurugenzi wa halmashauri/miji/majiji/miji midogo kikiwa cheo cha kitaaluma. Kwa maana kwamba ili ukifikie cheo cha ukurugenzi unapaswa kuanzia kwenye ukuu wa kitengo, ukuu wa idara hadi uufikie ukurugenzi. Lakini Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2020 aliamua kwa makusudi kusiasisha cheo hiki na kuanza kukigawa kwa makada wa CCM walioshindwa uchaguzi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa sasa hakuna mtumishi wa umma anayeweza kufikia cheo cha ukurugenzi kwa kuwa cheo hiki kimeporwa kwa makusudi na kugawiwa kwa wanasiasa makada wa chama tawala. Nadhani hata CHADEMA watakapoingia madarakani nao wataendelea na utaratibu huu haramu. Hii haifai hata kidogo. Kusiasisha chao hiki kuna madhara mawili hasi kama ifuatavyo:

(i) Kwa kuwa mkuu wa wilaya ni kada na mkuu wa mkoa pia ni kada, mkurugenzi anapoboronga kwa mfano, anapofuja mali za umma, mkuu wa wilaya hawezi kumkemea kwa kuwa ni kada mwenzake. Hali ingekuwa tofauti kama mkurugenzi angekuwa mtumishi wa umma. Lazima tu ashikishwe adabu na mkuu wa wilaya pale anapokengeuka.

(ii) Watumishi wa umma ambao wamezibiwa nafasi ya kuwa wakurugenzi, hasa wakuu wa idara, wanafanya kazi kinyonge na kwa kinyongo cha hali ya juu. Ndio maana unasikia mara kwa mara wakuu wa idara wakilalamikiwa kwa kuwapotosha wakurugenzi kwa makusudi katika uendeshaji wa halmashauri.

Hii ni kwa sababu kada anapochomolewa kutoka huko kwenye siasa na kupachikwa cheo cha ukurugenzi anakuwa hajui lolote kuhusu uendeshaji wa shughuli za serikali kwenye halmashauri. Anakuwa yupoyupo tu ilmradi amezawadiwa cheo cha bure basi anakuwa anabweteka.

Matokeo yake wajanja hutumia mwanya wa umbumbumbu wake kufanya ufisadi na kutafuta rasilimali za umma bila yeye kufahamu. Halmashauri nyingi zinapata hati chafu mwaka hadi mwaka kwa sababu ya udhaifu wa wakurugenzi. Na udhaifu huu hauwezi kukoma kamwe hadi serikali itakapofanya mageuzi kurudisha cheo cha ukurugenzi kwenye mikono ya watumishi wa umma.

Nawasilisha.
 
Pia TUCTA waombe Bodi ya Maslahi Katika Utumishi wa Umma irudishwe kwa vile iliondolewa na kufutwa na majukumu kuhamishiwa Idara kuu ya utumishi kimizengwe. Rais akumbushwe kwa vile alikwishaelekeza irejeshwe. Bodi hizi zinaumuhimu sana nchi za SADC na EAC zina mifumo hiyo kusukuma mishahara. Idara kuu ya utumishi inapaswa ibaki na majukumu yake ya msingi ya kisera. Majukumu ya urekebu iachie taasisi nyingine.
 
Watumishi punguzeni pia ulegelege kwenye kutoa huduma kwa watu, watumishi baadhi ni wavivu jamani aisee! Igine kwa wenzetu wakenya linapokuja swala la kazi hawanaga mzaha iwe hosp au ofsn huwa ni Moto Moto!
 
Hamn kitu hapo serikali haina hizo hela kwa kifundi labda wakakope imf huko
1. Wakifuta mfumo wa posho na kuingiza kwenye mishahara, mishahara inaweza kupanda kuliko kipindi chochote tangu hii nchi ipate uhuru bila hela za ziada na Kodi itaongezeka sana hivyo kuwapa fursa ya kurekebisha kikokotoo cha PAYE na kufanya mishahara ipande tena kwa wote.
2. Magari yote ya serikali/jeshi yakative Bima na workshop zao zifanye kazi kwa weledi sio Kiupigaji....
3. Wakiuza manyumba ya hovyo hovyo yaliyo jengwa na NSSF/PPF ambayo hayana wapangaji na kwa gharama ambazo hazina uhalisia. Kuna magorofa wamejenga kule Arusha naona yapo kwenye ukingo wa barabara tena bila eneo la kutosha la packing???
 
Back
Top Bottom