Kati ya CCM na CUF, chama kipi kitaanza kutokomea kwanza?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wanajamvi tujiulize swali hili maana kwa sasa linaonekana kuwa muhimu hasa baada ya kuonekana kwamba Chadema inakubalika kwa kasi sana hapa nchini -- hasa kwa vijana waliokata tamaa.

Hivi kati ya CCM na CUF ni chama kipi kitaanza kutokomea kutoka medani ya siasa za Tanzania?
 
Niko tayari kuweka hata nyumba yangu dau CCM itaanza kutokomea. dalili hizi za kutukanana wenyewe kwa wenyewe ni dalili tosha kuimaliza CCM. hata hivyo naipa hadi 2015 ndiyo mwisho wake.
 
UKIMWI wa kisisa ukiingia kitandani kwa Wanandoa au hata Kimada, siku na kutangulia kusafiri ahera ndio yabakia busara na Mapenzi ya Mwenyezi Mungu lakini uhakika kwa wote ni wa kufa kwa KUSHIRIKI PAMOJA KULA MABUA NA NGURUWE wala usihangaike saaana kutafute wenye busara wakujibu.

Kila siku naona Chama Kipya kikianzishwa kule Tanzania Visiwani kuchukua nafasi ya mahawara hawa wawili; uje uliulize swali juu ya hili mwaka kesho tarehe na mwezi kama wa leo!!!
 
MHESHIWA PINDA CHINI YA RADAR YA ALIYEWAHI KUMUAMINI: UWEZO TUNAO

Eti umesema Mhe Peter Kayanza Mizengo Pinda aka Mtoto wa Mkulima niliyewahi kumpenda na kumuamini ni JAAAAASIRI??? Ni ujasiri gani tena huo, huyu mtoto wa mkulima nisioifahamu mie???

Nakuambia mimi huyu mtoto wa mkulima siku hizi simuelewi kabisa juu ya lolote lile!! Na kwa kukuthibitishia hilo mwenzenu tayari nimekua nikijihesabia KUMPOTEZA KIPENZI sawa sawa na ninsi nilivyowahi kujihesabia huko nyuma nikiwa sekondari huku nikion CCM ikinilazimisha kumpoteza KIPENZI CHA ROHO YANGU KISIASA MHE AUGUSTINO LYATONGA WA MREMA (the bureaucratic rule arch-rival charismatic leader) na hivi majuzi tena nikalazimishwa KUMPOTEZA KIPENZI MWINGINE JOHN POMBE MAGUFULI kwa kukataliwa kuzingatia sheria mstari kwa mstari kwenye utendaji wake.

Nakuuliza mwenzangu ni ujasiri gani huo ulioigundua kwa huyu aliyewahi kuwa Mtoto wa Mkulima huko nyuma na sasa hivi kabakia tu kuwa Mtoto wa walima bustani ya mchicha Mto Msimbazi Dar es Salaam??

Hakika ili niweze kumtendea haki katika kuanza kwangu kumkataa kule kwanza kulitokea azimio nzito sana katika kikao cha kukata na shoka ambapo wahudhuriaji walikua ni akina (1) Uwezo Tunao mwenye Kupenda, (2) Uwezo Tunao akili na fikra pamoja na (3) Uwezo Tunao jicho la walalahoi. Mkutano huu wa zaidi ya wiki ulikua mkali kweli kweli tena wenye futa nikuvute mkubwa mno.

Lakini labda nianze kwa kuwashukuru sana tena sana ndugu zangu wengine hawa (Uwezo Tunao family) kwa kuafiki mapendekeza ya huyo mjumbe wa pili hapo juu ya kwamba kwanza tufanye utafiti utakaotuelekeza kama kweli bado kuna matumaini yamebakia ndani ya Baba huyu 'Mtoto wa Mkulima' hadi hapa tulipofikia au laa. Katika kutekeleza azima hiyo sote watatu tulichagua kujipa siku 90 kumsoma juu ya kauli zake na kwa kiasi gani zinavyokubaliana na matendo yake katika jamii yetu hii.

Kiukweli kabisa, japo MATOKEO YA UTAFITI WA UWEZO TUNAO FAMILI NA HATIMA YA MHESHIMIWA PINDA A.K.A MTOTO WA MKULIMA utakamilika hapo Aprili 23, hata hivyo dalili za awali hazimpendelei saaana huyu kipenzi changu ambaye nasikitika kuelekea kumpoza hivi karibuni katika kitabu changu cha Wanasiasa ninaowaamini nchini.

Hizo dalili za awali zisizompendelea huyu 'rafiki wa roho yangu, mara baada ya kumsogeza kwa karibu zaidi chini ya drubini yangu kwenye maabara binafsi ya siasa nchini (microscope) kumebainika mambo kadhaa wa kadhaa juu yake huyu mwenzetu. Na endapo dlili hizi zenye gizo totoro hazioonekana kupona kitu basi nawahakikishieni kwamba sitochelewa kupendekeza hapa JF na kote nchini kwamba hicho cheo cha heshima cha 'Mtoto wa Mkulima' nacho tukamnyang'anye kabisa kwa kutoitendea haki ipasavyo.

Kwa mwenzetu, ndugu yetu na Baba yetu wa Taifa Mwalimu Nyerere cheo kile cha heshima toka kwetu wananchi aliendelea kukitumikia hadi dakika ya mwisho aliposema maneno mawili mtatu kwa Mzee Rashidi Simba wa Vita pembeni mwa kitanda chake hospitalini kule Uingereza hivyo hata akaendelea kustahili kubakia nayo hata baada ya safari ya kurudi kwa muumba wake ilipowadia.

Mapungufu mazito tuliyoyaona ni haya na ni bora akayafanyia kazi kwa haraka kabla hatujafunga faili na kuikabidhisha kwa wapiga kura kumpima nayo zaidi pamoja na kwamba keshaahidi kurudi kupumzika nyumbani mara baada ya utumishi wake kama Waziri Mkuu, Mheshimiwa Pinda ni:

1. Kiongozi anayeogopa sana LAWAMA:

Hii tabia imegeuka kuwa jela yake binafsi anayotembea nayo kila mahali kama mfungwa wa hiari. Kwa kukuthibitishia madai yangu haya utagundua kwamba Mhe Pinda siku zote hajawahi kuonyesha OWN INITIATED ACTION BALI NI MZEE WA REACTIONS tu. Nasema akome kukimbizana na upepo kwa mtindo wa zimamoto kwa kila atendalo.

2. Mtaalam wa Kukasimu Madaraka, Mchovu wa Kufuatilia:

Delegating power is a very good sign of a leader who has confidence in colleagues and teamwork spirit. Lakini kama huna muda wa kufuatilia ulioyakasimu, wala uwezo wa kuhakikisha kwamba kweli ulioyakasimu yanaleta matunda ya kugusika kwa mikono na kuonekana kwa macho basi mwenzetu ukae ukijua kwamba wengi huku nje wanajiuliza kiti hicho unachokalia unakiachia wazi lini???

Uthibitisho wa madai yangu; Mzee Pinda alijichagulia kuparamia swala nyeti la Madai ya Katiba nchini na kwa kuelewa kwamba anayo GOODWILL kwetu sie walalahoi tulio wengi basi akaona vema kuchangamkia tenda hiyo.

Lakini, kwa bahati mbaya sana 'Wa Mkulima ' hajagundua siri kwamba goodwill ni goodwill tu na inayo ukomo wake na kwamba kitendo cha kuuchukua swala la katiba na kujirithisha kuuficha ndani ya mfuko wake wa suruali ya nyloni ni jambo la hatari kuliko angeliacha tu swala hili bila kuahidi kulishughulikia kabisa.

Katika hili nasema Mhe Pinda usiombe mtu na au kundi la watu waliyokumini pindi wanapogeuka na kukosa imani kwako - mungalie Ndugu yetu Mhe Kikwete na jinsi alivyotuchukulia for granted imani yote kwake na kura zote katika kipindi chake cha kwanza mpaka akafika mahala na kuona kwamba tuliomuamini baada ya kutusaliti basi ni bora akatumie njia ya mkato KUTUIBIA KABISA KARU nadhani lengo likiwa ni kupata SECOND CHANCE kurekebisha mambo lakini ndio hivyo maji ya kunywa yakishamwagika bora ukayapigie tu deki.

Mheshimiwa Pinda kwa taarifa tu ni kwamba 'Nguvu ya Umma' tunasubiri kwa hamu kuona endapo tena utaipigia danadana swala la Katiba Mpya na Mtume huru za Uchaguzi; Bara na Visiwa hata isipitishwe kwenye bunge hili la mnamo mwezi huu wa April 2011!!!!

3. Group Thinking

Mheshimiwa Pinda ni muumini mkubwa wa kanisa au msikiti wa maamuzi ya kikundi kundi hivi. Hili jambo linampa shida sana kwa kuwa kila mara anakosa ORIGINALITY katika msururu wa mambo ya kutekeleza hivyo jambo linapoenda kombo anashindwa kulitafutia lango la pili kwa kuwa he is NOT never married to the original idea either.

Kwa mtindo huu 'Wa Mkulima' ni kwamba utajikuta siku zote unageuka kuwa MTUMWA WA FIKRA ZA WASHAURI ambao pindi mambo yanapoharibika wao hucheka mtindo wa Jino-Pembe kwa kuwa siri yote wanayo kwamba wewe hauna input yoyote mle na kwamba hata zile perspective mikanganyiko walizokupa washauri mbali mbali wala haukuweza hata kujitengea muda wa peke yako with a BRUTALLY CRITICAL MIND.

Kama uliwahi kusikia Mheshimiwa Mwl Nyerere, Mkapa, Dr Shein na Dr Magufuli walipata kuheshimika sana ni kule katika wao kujitengea muda usioingiliwa hata na mama watoto pale nyumbani ili AKALIFIKIRIE TAIFA LAKE KWA UDHATI KABISA NA MOYO WA KIZALENDO ili ku-Question, kuomba ufafanuzi zaidi, uthibitisho wa maelezo na hata kule kufanya SUPRISE SELF-FACT FINDING MISSION bila kuwa pompus anda embarrassing to others kama Vijikamati Vya Bunge tunavyovishuhudia hivi leo viki-play both Police and Court roles together on their subordinate line ministries and related institutions whereas the costitution ONLY asks the to Oversee and Advise.

Wakati bado utafiti wetu juu ya Mtoto-wa-Mkulima na hasa kwa kumpima zaidi atakavyoshugulikia jambo la msingi zaidi kwa taifa (an immediate People-Centred Constitutional Overhaul call) au kuyaacha kwenye mikono ya wachache akina Oliver Mhaiki na Celina Kombani au atawaita wadau wote kuliweka sawa kabla ya kutinga nayo bungeni Aprili, mambo mengine yatakayoendelea kuangaliwa kwake ni pamoja na:

a. Pinda Leadership style and frame (Theories X and Y tools).

b. Whether Pinda is already at the Plateaue of his performance or not (Goal-setting & Abraham Maslow's Theory of Needs)

c. Jibu kama Mhe Pinda ni Innovative, Proactive or not

... na mjadala wa Uwezo Tunao family bado unaendelea juu ya kiongozi huyu kabla ya kuingia kwenye kuwachambu with a brutally critical mind mtu yeyote ambaye amewahi kutajwa kutamani kuwa kiongozi wetu ama wa kisiasa au technocrat kinamna fulani hivi.

Nyote mnakaribishwa kwenye huu mkutano endelevu wenye lengo la kukosoa hadi wale tunaowapenda ndani ya CHADEMA chenyewe ili kila mmoja aweze kupata marejesho jinsi tunavyomuona na mambo gani yafanyike huruka vihunzi kadhaa kuelekea kwenye mafanikio maridhawa kwa Wa-Tanzania tulio wengi.
 
Wanajamvi tujiulize swali hili maana kwa sasa linaonekana kuwa muhimu hasa baada ya kuonekana kwamba Chadema inakubalika kwa kasi sana hapa nchini -- hasa kwa vijana waliokata tamaa.

Hivi kati ya CCM na CUF ni chama kipi kitaanza kutokomea kutoka medani ya siasa za Tanzania?

hao woteni wafu. acha wazikane wenywe. watakubaliana nania aanze kuzikwa nani afuate
 
Mimi naona chadema ndio itakufa kwanza.fanya uchunguzi wa kina na uweze kuona ni vipi chadema imeweza kujiimarisha kuanzia ngazi ya matawi huko vijijini na ina wanachama wangapi ndo useme chama kipi kitakufa mwanzo.wako wapi nccr mageuzi walikuja juu kama moto wa kifuu na wamezimika.chadema kitakufa natural death na mutakuja kuona. Kujenga umaarufu kwa kupitia udini kuna mwisho wake.
 
Back
Top Bottom