Kasoro usafiri wa treni Dar zirekebishwe sasa

Adili

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
3,138
1,117
Kasoro usafiri wa treni Dar zirekebishwe sasa/Tanzania Daima

TUNAMPONGEZA kwa mara nyingine tena, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa kusimamia utekelezaji wa ahadi ya siku nyingi ya serikali, ya kuanzisha usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam.

Idadi ya wanaotumia usafiri huo ambao kwa kiasi fulani umesaidia wananchi kuwahi sehemu zao za kazi, imekuwa kubwa kuliko uwezo wa treni yenyewe, na hivyo kuonyesha dhahiri kwamba kuna haja ya kuongeza mabehewa zaidi kukidhi mahitaji hayo.
Pamoja na ubora wa huduma hiyo, kuna kasoro kadhaa ambazo zimeonekana kwa kipindi hiki cha wiki moja cha majaribio, na ni matarajio yetu kwamba zikifanyiwa kazi, hali ya usafiri huo itakuwa bora zaidi.
Mosi ni utaratibu za kukata tiketi. Hadi sasa hakuna utaratibu mzuri, na badala yake baadhi ya watu wamejikuta wakisafiri bila kulipia chochote na hali hiyo inaweza kusababisha treni hiyo ikashindwa kujiendesha.
Lakini kibaya zaidi ni stahili inayotumika na wafanyakazi wanaokatisha tiketi kuhifadhi fedha hizo. Tumeshuhudia wafanyakazi hao wakihifadhi fedha zao kwenye mifuko ya plastiki hali ambayo inatia shaka katika udhibiti wa fedha hizo.
Idadi ya watu wanaosafiri ni kubwa kupita kiasi, kwamba baadhi ya watu wa hadhi ya juu hawataweza kusafiri katika mazingira hayo.

Vibaka nao hawako nyuma kiasi kwamba hali ya usalama wa mali za abiria wawapo safarini iko shakani. Katika hili tunasisitiza ulinzi uongezeke.
Sisi tunashauri kuwe na idadi maalumu ya abiria kwa kila behewa ili kuwe na nafasi ya kutosha ya kufanya wananchi wasafiri kwa starehe.
Tatizo lingine kubwa ni kwamba wakati usafiri wa treni umeanza, hatukujiandaa kwa usafiri wa daladala. Hii maana yake ni kwamba Kituo cha Mabasi cha Ubungo, kimezidiwa na umati mkubwa wa watu wanaoshuka kwenye treni.
Idadi ya daladala imeonekana kuwa ndogo na kwa sababu hiyo, daladala nyingi husafirisha abiria kwa bei ya sh 1,000 kwani hakuna usimamizi wa magari hayo ya abiria.
Pamoja na changamoto zilizojitokeza, tunaamini kuwa zikifanyiwa kazi, usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam utakuwa mkombozi kwa wananchi wanaotumia muda mwingi kwenye daladala kufika sehemu zao za kazi.

Basi waanzishe madaraja tofauti - Waheshimiwa, Walionazo na Walalahoi

Tuko Kibamba wanasema kuna gari la mizigo limeanguka na kuziba barabara. Gari hazisogei kabisa na kesho kazini
 
Baadhi ya watu wenye hadhi ni watu gani hao, wenye hadhi wanatafuta nini kwenye treni zetu si wapande magari yao ya binafsi
 
Kasoro usafiri wa treni Dar zirekebishwe sasa/Tanzania Daima

TUNAMPONGEZA kwa mara nyingine tena, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa kusimamia utekelezaji wa ahadi ya siku nyingi ya serikali, ya kuanzisha usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam.

Idadi ya wanaotumia usafiri huo ambao kwa kiasi fulani umesaidia wananchi kuwahi sehemu zao za kazi, imekuwa kubwa kuliko uwezo wa treni yenyewe, na hivyo kuonyesha dhahiri kwamba kuna haja ya kuongeza mabehewa zaidi kukidhi mahitaji hayo.
Pamoja na ubora wa huduma hiyo, kuna kasoro kadhaa ambazo zimeonekana kwa kipindi hiki cha wiki moja cha majaribio, na ni matarajio yetu kwamba zikifanyiwa kazi, hali ya usafiri huo itakuwa bora zaidi.
Mosi ni utaratibu za kukata tiketi. Hadi sasa hakuna utaratibu mzuri, na badala yake baadhi ya watu wamejikuta wakisafiri bila kulipia chochote na hali hiyo inaweza kusababisha treni hiyo ikashindwa kujiendesha.
Lakini kibaya zaidi ni stahili inayotumika na wafanyakazi wanaokatisha tiketi kuhifadhi fedha hizo. Tumeshuhudia wafanyakazi hao wakihifadhi fedha zao kwenye mifuko ya plastiki hali ambayo inatia shaka katika udhibiti wa fedha hizo.
Idadi ya watu wanaosafiri ni kubwa kupita kiasi, kwamba baadhi ya watu wa hadhi ya juu hawataweza kusafiri katika mazingira hayo.

Vibaka nao hawako nyuma kiasi kwamba hali ya usalama wa mali za abiria wawapo safarini iko shakani. Katika hili tunasisitiza ulinzi uongezeke.
Sisi tunashauri kuwe na idadi maalumu ya abiria kwa kila behewa ili kuwe na nafasi ya kutosha ya kufanya wananchi wasafiri kwa starehe.
Tatizo lingine kubwa ni kwamba wakati usafiri wa treni umeanza, hatukujiandaa kwa usafiri wa daladala. Hii maana yake ni kwamba Kituo cha Mabasi cha Ubungo, kimezidiwa na umati mkubwa wa watu wanaoshuka kwenye treni.
Idadi ya daladala imeonekana kuwa ndogo na kwa sababu hiyo, daladala nyingi husafirisha abiria kwa bei ya sh 1,000 kwani hakuna usimamizi wa magari hayo ya abiria.
Pamoja na changamoto zilizojitokeza, tunaamini kuwa zikifanyiwa kazi, usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam utakuwa mkombozi kwa wananchi wanaotumia muda mwingi kwenye daladala kufika sehemu zao za kazi.

Basi waanzishe madaraja tofauti - Waheshimiwa, Walionazo na Walalahoi

Unashukuriwa sana kwa utafiti huo mzuri na wa haraka. Ni ushauri wa maana sana na ni kawaida kwamba kitu chochote kinapoanza kinakua na kasoro lakin la muhimu zaidi ni kiasi gani watendaji wako tayari kuzirekibisha kasoro hizo. Ushauri mzuri tunaomba wahusika wauthamini na waufanyie kazi kwa maslahi ya wananchi
 
Back
Top Bottom