Kasi na ari ya utendaji wa Rais Magufuli ndio mtoa roho wa CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo

Dec 13, 2018
30
140
KASI NA ARI YA UTENDAJI WA RAIS DR JOHN MAGUFULI NDIO MTOA ROHO WA CHADEMA, CUF NA ACT.

Leo 13:15pm,31/03/2019.

Hivi sasa wana Chadema na ACT wanavizia Boeing ikiwa imepark wanaipiga picha na kusema iko likizo haina vibali katika anga la kimataifa eti Serikali haina business plan,Airbus ikiruka na kutua Nairobi ama Entebbe, wana Chadema na ACT wanasema ndege yetu imeuzwa Kenya.

Wana Chadema na ACT na tabia yao na mwelekeo wao wa kushambulia watu kumsema Mh Rais kwa vitu vya ulongo ulongo ili mradi wamepata kiki badala ya kujadili sera,Siasa za ulongo ulongo kama zile za kujadili watu imeshawagharimu Chadema mfano kwa kutaja list ya mafisadi Papa na baadae wakala matapishi yao kwa kumkabidhi Chama mtu waliyemuita Fisadi Papa, hii ni namna Chadema na ACT wasivyo na maono hata kukosa vision japo ya miaka miwili, hivi ndivyo kinavyokufa Chadema na ndivyo kitavyokufa ACT, pengine CUF imestahimili jaribu la Nyakati, kama si Profesa Lipumba basi hivi leo CUF ingepotea kama ilivyopotea TLP na NCCR mageuzi.

Kasi na Ari ya Utendaji wa Dr Magufuli inatajwa kuwa ndio “mtoa roho” wa upinzani,tunaposema “Magufuli anaua Upinzani”. Ni kwa kuwa Magufuli ametimiza hitaji la Nyakati, hitaji hilo ni "Mabadiliko" toka Ufisadi na Nchi kutoendelea mbele hadi kumaliza Ufisadi na Nchi kuanza kupiga hatua za kimaendeleo, Yes anatumia silaha ile ile iliyobebwa na Upinzani kama ni Ak 47 basi nae kaibeba hiyo na bado ana Machine Gun na revolver ndio maana anaonekana `kuiba` ajenda za upinzani,Tunaweza kusema, ``Mh Magufuli ni Serikali na ni upinzani``.Hili ndilo lilikuwa hitaji la Watanzania kwa miaka mingi baada ya kuamka na kugundua kuwa tuna rasilimali zote ambazo Mwenyezi Mungu ametujalia lakini bado tu masikini, hivyo tulihitaji "Mabadiliko ya kiusimamizi wa Rasilimali,Uadilifu na Utendaji uliotukuka, Hii Ndio hofu ya Chadema na ACT kwa kuwa utendaji wa namna hii, unafifisha mng`aro wa upinzani na kubaki kuvizia matukio ya ulongo ulongo na udaku udaku na kuyafanya ajenda zao za msingi.

Leo Mgombea Uraisi wa Chadema 2015 na Mgombea Mwenza wao 2015 wote wameondoka Chadema,mmoja akirudi CCM na mwingine akitimkia ACT. Alianza Juma Duni Haji mgombea Mwenza kutoka Chadema na kurudi CUF na kutoa kijembe "Chadema kila mtu beberu ana ndevu "Sasa Mgombea Uraisi wa Chadema 2015 kamalizia .Kiutaalam wa Sayansi ya Siasa huwezi kubeza kuondoka kwa wapeperusha bendera ya Chama Kitaifa kuondoka na kuishia kusema hakuna kitu chochote kilichotokea.

-Kuibuka kwa Chadema na kudhohofika kwa CUF.

-Mizengwe iliyopata kuidhoofisha CUF ya Mwenyekiti Mapalala ndiyo mizengwe hiyo hiyo inayoendelea CUF hivi leo,labda sasa kinaweza kutulia kwa kuwa mleta mizengwe kaenda ACT, mizengwe yote kiini chake ni matokeo ya siasa za nafsi, siasa za kuchafuana na kupakana matope. Siasa za fulani na fulani. CUF kilichokuwa Chama kikubwa Tanzania na kushika hatamu baada ya kudhoofika kwa Chama Cha TLP na Nccr Mageuzi vilivyobebwa na umaarufu wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ndugu Augustino Mrema, CUF wakapoteza heshima kama Chama Kikuu Cha Upinzani Tanzania na nafasi yao kuchukuliwa na Chadema, CUF wanapoteza wanachama kwa kuwa walipoteza “HOJA YA MSINGI” kwa kuendekeza siasa za nafsi..siasa za Maalim Seif versus Mapalala, Maalim Seif Versus Lipumba na hivi sasa Maalim Seif kashindwa kwa Profesa Lipumba na kukimbilia ACT,ni Uchanga wa fikra,lakini tunaelekea kukomaa.

Mwaka 1994 ndio ulikua mwisho wa Mwenyekiti,Mzee James Mapalala baada ya viongozi wa CUF zanzibar kumuibulia hoja,

Serikali iliporejesha mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, ndipo kilipoanzishwa chama cha United Front kwa upande wa Zanzibar kikiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad na upande wa Tanzania Bara kulikuwa na chama kinaitwa Civic Party kikiongozwa na James Mapalala.

Mwaka huo huo vyama hivi viliungana na kuzalisha Chama Cha Civic United Front.Mwenyekiti akiwa Mapalala na Katibu Mkuu Maalim Seif. Sikio la kufa lilianza 1994 pale Mapalala alipovuliwa Uanachama wa CUF,na baadae Naibu Katibu Mkuu bara,Michael Nyaruba nae akavuliwa Uanachama wa CUF.Mwaka 2003 ,CUF ikamvua Uanachama Mwenyekiti wake wa bodi ya Wadhamini Bwana Naila Majid Jidawi, Sasa Mwaka 2016 ,Mwenyekiti Ibrahim Lipumba anarudi CUF baada ya kuomba kujiuzuru kwa sababu ya Chadema kuimeza CUF na baadae kabla ya kujibiwa akatengua uamuzi wake wa kujiuzuru akiungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mh Magdalena Sakaya na kurudi chamani kama Mwenyekiti.Mzunguko unajirudia Enzi za Mwenyekiti Mapalala na Naibu Katibu Mkuu bara Michael Nyaruba na hivi Sasa Mwenyekiti Profesa Lipumba na Naibu Katibu Mkuu, Mh Magdalena Sakaya.

-Kuimarika kwa Chadema Ubavuni kwa CUF ya Mwenyekiti Profesa Lipumba.

-Mkutano Mkuu wa kwanza wa Chadema chini ya Mzee Edwin Mtei (Arusha - mwenyekiti), Brown Ngwililupi (makamu mwenyekiti - Iringa) na Edward Barongo (Kagera).

Costa Shinganya (Kigoma), Evarist Maembe (Morogoro), Mary Kabigi (Mbeya), Menrald Mutungi (Kagera) na Victor Kimesela (Manyara).Desemba 1991, ukamchagua Bob Makani kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Chadema hata kabla Serikali haijarejesha kisheria mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Bob Makani alishikilia nafasi hiyo hadi mwaka 1998 alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chadema hadi mwaka 2004.

Katika kipindi chote, chama cha Chadema kilifaidi mengi kutokana na utumishi uliotukuka wa Bob Makani busara zake, kama si hivyo kabla ya mgogoro wa Mwenyekiti wa CUF na Katibu Mkuu Maalim Seif basi ingekuwa Mwenyekiti Edwin Mtei na Katibu Mkuu Bob Makani, zipo sababu nyingi hata wewe msomaji unaweza kuzihisi lakini Chama kilifaidika na busara za Katibu Mkuu Bob Makani aliyechukulia mambo kisomi zaidi kwa ajili ya amani ya Chama kwa utaalam wake wa Sheria ambao pamoja na busara zake zilikisaidia chama kutengeneza katiba na taratibu na kukipa uhalali zaidi.

-Mgogoro wa Chadema unaweza kuwa na taswira ya Mwaka 1995.

-Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, mwaka 1995,Mwenyekiti wa Chadema Edwin Mtei na Katibu Mkuu wake Bob Makani wote wawili walichukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wote walionekana kuwa na nguvu kweli kweli ndani ya Chadema hata kuanzishwa kwa makundi ndani ya Chadema ilihali nje ya Chadema katika siasa za Upinzani wakati huo Augustino Lyatonga Mrema,ndiye alikuwa na ridhaa ya Wananchi kupitia Upinzani.

Mpambano ndani ya Chadema ulileta sitofahamu kubwa, hata hivyo Mbowe akiwa mwanasiasa kijana alitoa ushauri kwa chama kwamba kisisimamishe mgombea urais ili kuepusha mpasuko ndani ya Chadema na badala yake wamuunge mkono Mgombea wa Urais kupitia NCCR Mageuzi Agustine Lyatonga Mrema ambaye wakati huo alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwa wananchi wengi.

Ushauri huo wa Kijana Mbowe enzi hizo uliungwa Mkono na wanachama na viongozi wa Chadema na kuwafanya Mwenyekiti Mtei na Katibu Bob Makani kuachana kabisa na mchakato huo wa kuwania urais na Chadema kumuunga mkono Augustino Mrema ambaye wakati huo alikuwa na nguvu kweli kweli hata afikapo mijini gari yake kusukumwa na Umati ama Mafuriko ya Wana -Mageuzi wa wakati huo.

Hatua hiyo ya mwaka 1995 ya kumuunga Mkono Augustino Mrema ikajirudia tena Mwaka 2000 kwa Mbowe kukishauri chama kutosimamisha Mgombea Urais ili kumuunga mkono mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ambaye nae alipendwa katika siasa za upinzani baada ya Augustino Mrema kudondokea pua katika uchaguzi wa mwaka 1995,Hatua ya Chadema kufuata shauri wa Freeman Mbowe kutosimamisha mgombea mwaka 1995,na 2,000 ndio ilikuwa hatua muhimu ya kumuinua Mbowe na Chadema na kuipiga kanzu CUF ya Profesa Ibrahim Lipumba kwa maana Freeman Mbowe alionesha uimara na misimamo na kukua katika Siasa na kuikomaza Chadema, na kuipa mtoko hasa Mwaka 2010 ambapo Katibu Mkuu, Dr Slaa aliipeperusha vyema bendera ya Chadema na kuipatia Chadema kura Milioni mbili na majimbo kadhaa na vita vya ubunge 20.

-Chadema kuiunga mkono ACT kwenye Uchaguzi Mkuu 2020.

Ni kama ilivyokuwa 1995 Chadema ilipomuunga mkono Augustino Mrema au 2000 Chadema ilipomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba, Safari hii 2020 Chadema kwa kuwa haina mgombea na ili kuepusha mpasuko wa Team Lissu na Team Mbowe basi Chadema itamuunga mkono Zitto Kabwe kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia ACT – Wazalendo,

ACT Wazalendo waliamua kuingia katika ulingo baada ya kuona Siasa za mipasho hazijaifanikisha Chadema wala CUF. Ingawa kwa mtazamo wangu ukuaji wa ACT – Wazalendo unategemea sana hatima ya CHADEMA. Kwa namna moja ama nyingine, kama CHADEMA itampata mgombea Urais mfano Membe ama kama Chadema itaimarika yenyewe na chini ya mwamvuli wa UKAWA,basi ACT – Wazalendo itaathirika mno. Na hivyo basi, kama hoja ni kufa kwa upinzani ,ACT itakuwa na hali ngumu zaidi hasa kwa kupata shida kuvutia wafuasi wapya, ikiwemo kutoka CCM au CHADEMA na vyama vingine ingawa ACT wameanza vyema kwenye mwelekeo mpya wa siasa za Hoja, changamoto ni kuwa kwa sasa hoja zote kerwa na kereketa kama vile Ufisadi na Uwajibikaji vinasimamiwa vyema kiasi cha kuwakosesha hoja vyama vyote vya Upinzani.

Nimalizie kwa kusema tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, si chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA,ama CUF ama ACT ambao wameibua hoja ya ukweli zaidi ya ulongo ulongo na udaku udaku, Chadema, ACT na CUF wameshindwa kabisa kufurukuta na kujenga hoja ya kuungwa mkono na Watanzania juu ya Utendaji wa Rais Magufuli. Ilizoeleka hapo awali kuwa Upinzani hasa Chadema walijikita katika kukosoa utendaji wa Serikali zilizopita. This time around, Chadema hawana tena nguvu wala tashwishwi ya kumshambulia Rais kwa muktadha wa utendaji wake.

Niwasihi ndugu zangu wa Chadema,tumieni busara na hekima kuunga mkono juhudi ndio okoka yenu kwa maana Rais Magufuli ni Serikali na ni Mpinzani, sasa ninyi kazi yenu ya Upinzani mtaifanya wapi?. Majungu na mipasho na ulongo ulongo na udaku udaku waachieni instagram, Muda unakwenda tunakaribia 2020. Magufuli na Serikali yake yupo busy kutekeleza Ilani na ahadi zake ili ikifika 2020 awe amezimaliza. Dalili zinaonesha atazimaliza kabla ya mwaka huo,na Katika kampeni za 2020 atakuwa akipunga mkono tu na kupita kwa kishindo,Viva Rais Magufuli, Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Back
Top Bottom