Kashfa ya Uzinzi: Lissu amsafisha Mbowe

Status
Not open for further replies.
Kiongozi kutembea nje ya ndoa si suala binafsi, rais wa Ufaransa kasababisha mkewe azimie kwa kuhusishwa na ngono nje ya ndoa baada ya gazeti kuandika uhusiano wake na mwigizaji wa kike nchini humo. Amebanwa na vyombo vya habari hadi kasema anaenda kwa Obama akirudi ndiyo atatoa uamuzi wake

Partner wa Rais wa Ufaransa anazimia nini, aache usanii. Yeye alimtoa mwenzake aliyekuwa amezaa watoto wa nne. Kuna usemi wa kidhungu usemao: If they have done it with you,they will do it to you. Cheaters dont see the problem.
 
Nimewahi kusoma humu JF kuwa Lissu ana matatizo ya akili. Jee, huo ni ukweli au wanampakazia tu?
 
Wazungu wana utamaduni wao na sisi tuna wa kwetu. Mzungu ni kawaida kumkaribisha rafiki wa binti yake nyumbani wakaendelea kupigana miti na ikiwa sawa tu.
 
Viongozi wa CHADEMA ni majanga tupu.

Kwa hiyo kumbe Mh. Mbowe ni mzinzi kwa maana nyingine, tuhuma hizi ni za kweli.

Sasa kama maswala ya Uzinzi ni private affairs. Vipi hili swala la kupewa millions pesa za Tanzania na wale wale kila mara alikuwa akipanda kwenye majukwaa alikuwa anawaita mafisadi.

Pesa za huyu kada wa CCM alizochukua nazo ni private affairs

View attachment 132573

Tunaomba tufahamu mipaka ya private affairs nchini

Kama ameweza kuijibu hoja ya uzinzi, kwa nini hakutaka kuijibu hoja ya "double agent" kwa maana kuwa, mchana ni mpiga vita mafisadi na usiku ni mpokea pesa za mafisadi

hilo nalo neno kamanda
 
Kimsingi hili ni suala ambalo ni personal, na kwamba ni mke wake mbowe tena nyumbani kwake ndio anaweza kulalamikia tabia hii binafi ya Mh. Mbowe. Ni vema jamii ikajikita zaidi katika kujadili mambo ynayolitesa taifakwa sasa kuliko ufuatilia mambo ya watu binfsi n ambayo hayana tija
 
Tatizo la Lissu haongei ukweli wote:

Angewaambia pia kuwa Clinton baada ya kutembea na Monica alikuwa impeached
Angewaambia pia kuwa mzee Mandela hakufanya yeye binafsi bali mke wake ndiye aliyefanya

Na angekuwa na Rekodi nzuri.
Angetueleza kuhusu Bob Livingston, mrepublican ambaye alitarajiwa kuwa Speaker of the house alipolazimika kujiuzulu baada ya ishu yake ya kuwa na kimada kuripotiwa

Angesema kuhusu Elion Spitzer gavana wa California aliyelazimika kujiuzulu kwa aibu baada ya kutembea na malaya

Angetueleza kuhusu Gary Hart mgombea uraisi wa Democrat aliyelazimika kujitoa kugombea uraisi mwaka 1988 baada ya picha kutoka akiwa katika style za kimahaba na msaidizi wa kampeni zake aitwaye Donna Rice.

Familia ni Unit kuu ya Taifa, Unapomuumiza mkeo kisaikolojia, Ukawaumiza watoto kisaikolojia, Wewe huwezi kuwa na uchungu kwa familia kubwa iitwayo "Taifa". MBOWE KWA JAMBO HILI HAFAI KUWA KIONGOZI

Msituletee habari, eti mbona fulani wa CCM naye anafanya. well kama CCM wanafanya basi CHADEMA si inabidi wajitofautishe nao?, au CHADEMA wanataka kuwa kama CCM?
Ndiyo maana tunasema Lissu anatumia taaluma yake kama muosha mashuka kwenye danguro.
 
Mijadala mingine ujinga mtupu! Mafuta juu, umeme juu, gas juu, hivi karibuni maji yatakuwa juu, ada za wanafunzi shule za binafsi juu, kipato cha mtanzania kilekile, badala ya kujadili hayo eti watu wameshupalia, uzinzi uzinzi uzinzi. Mkimaliza kujadili uzinzi Wachina watakuwa wamemaliza kuuwa tembo zenu huko Mbugani! Tuache kujadili mambo binafsi ya watu!!
 
Hayo ni mambo binafsi hatuwezi kuyaingilia tunaangalia uongozi wake na uongozi si elimu bali ni kipaji unaweza kuwa na elimu lakini usiwe na kipaji cha uongozi tungejadili mambo ya msingi kupanda kwa umeme gesi na gharama za kupiga cm tuache kumjadili mtu
 
Mbowe kama atakuwa na nyumba kubwa namna hii ya utitiri wa wanawake ruzuku ya chama itakuwa salama kweli? maana kila kimada atakuwa akidai matumizi tena marefu.
 
Poleni sana, ni kweli kabisa jambo hili limo ndani ya mambo binafsi ya mtu mwenyewe, nakubaliana. Lakini pia watanzania tujifunze kuwa utamaduni wa kuwasaidia viongozi wetu kuepukana na upotofu wa maadili na tusikimbilie tu kutangaza kasoro zao ili umma ujue kwani matokeo yake wanaotutazama toka nje wanaona kuwa sifa za viongozi pia zinafanana na sifa za wanaongozwa
 
Ametoka nje ya ndoa mlimuona?na alieanzisha hyo kashfa mbona asiseme kabla hawajatofautiana?huko ni kuchafuana kisiasa tu hakuna lolotee,pia ni maisha ya mtu binafsi hayatuhusu!
 
Haya sasa Pasco, yaleyale maneno ya jamaa yako. Hapa ina maana Mkono naye anahusishwa moja kwa moja kuwa Mkono pia alihonga fedha ili apite bila kupingwa. Jiwe la Lissu kweli kali sana na effect haitakwisha sasa hivi.
Kuna kitu kinaitwa "the right to privacy!", ambayo kila mtu anapaswa kuwa nao, ila kwa public officials who are paid by the taxpayers money, then they have to surrender their right to privacy kwa sababu the public has the right to know their public and private conduct because that is where their money goes and have to know and approve such conduct ndio maana wenzetu huwa wanaachia ngazi!.

Huku kwetu sifa!, hata ningekuwa mimi pale ningeshindwa!.
Pasco
 
Huyu lissu nahisi kama ana kaugonjwa flani kamemwingia! Maana matamko anayotoa siku za hivi karibuni yamekuwa ya ajabu sana! hata vitendo vyake havieleweki eleweki! Huyu siyo TL wa miezi kama sita iliyopita! I used to respect and like a guy.
 
Ametoka nje ya ndoa mlimuona?na alieanzisha hyo kashfa mbona asiseme kabla hawajatofautiana?huko ni kuchafuana kisiasa tu hakuna lolotee,pia ni maisha ya mtu binafsi hayatuhusu!
Hiyo kashfa haikuanzishwa na ZZK you dumb.... Ilianzishwa na Mwigulu
 
Clinton alikuwa impeached, Mandela alichapiwa kwa hiyo hakufanya jambo la kipuuzi kama alilofanya Mbowe.
Kama katiba ya CDM inatilia mkazo famili kama ndiyo kiini cha utawala (conservatives pillar) basi waonyeshe mfano na siyo kuweka vifungu kwenye katiba yao ili wapte wafadhili ilhali ni chma cha wasiooa na waasherati.

Tundu Lissu amejishusha.

soma vzr historia ujue kwa nini mke wa kwanza wa Madiba alimuacha na kuondoka, ukikosa kitabu tafuta movie ya Idris Elba Long walk to freedom utajua usikurupuke kumshambulia Lissu hapa...

take note sitetei ujinga wa mwenyekiti wao nakusahihisha kwenye historia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom