chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,009
- 20,683
Mnara wa Babeli?
Lissu anaonekana akiwa na furaha kubwa sana huko Ivory Coast akishangilia timu ya Msumbiji.
Lissu amegundua kwamba Mbowe anamuwekea mtego ili kumuonyesha kwamba aina ya siasa anazozitaka hazifanikiwagi, hasa Tanzania? Yaani anamuonyesha kwamba, si unataka siasa za maandamano? Haya nimeitisha, unamuona yoyote wa kuandamana?
Akiwa Marekani, Mbowe aliwahi kuongea na diaspora, akawaambia, siasa za Tanzania ni tofauti na za nchi nyingine, akatoa mfano wa Kenya ambapo maandamano yakiitwa hata usiku wa manane kila mtu atakurupuka na blanketi kwenda baranarani.
Wakati huo Mbowe alikuwa ametoka segere matata kwa kesi ya ugaidi, na kwa wakati wote huo, wanachadema hawakuandamana ili aachiwe, na wengi kama akina John Mrema walikuwa wanapiga kilauri tu mitaa ya Tabata na Sinza.
Kwa nini Lissu yuko bize na ya kwake katika wakati huu muhimu kuelekea tarehe yao ya maandamano? Kuna kitu kakistukia kuhusu chadema, chama ambacho ambacho amekitumikia mpaka karibu apoteze uhai wake?
Je, ameona "raha ajipe mwenyewe" na bora na yeye afanye ya kwake, na ya chama ni kupoteza muda kwa kuwa hakina malengo ya kisiasa zaidi ya kuchumia tumbo? Tamko lile la Mbowe hutolewa mbele ya viongozi wa chama wakiwa full cabinet.
Je, kushindwa kwa maandamano itakuwa ni aibu tosha kwa Mbowe kwamba ameshindwa kuonyesha uongozi, hivyo Lissu kaamua kujitenga na aibu hiyo, ili baadae akiwa anataka kumtoa katika nafasi ya uenyekiti "amzabue" Mbowe kisiasa vilivyo na awaaminishe wana CDM kwamba Mbowe ni "zilipendwa", hawezi kukusanya hata wana CDM 200 kwa jambo la chama?
Je kuna "joto" la kutosha la kisiasa linalofaa kuitisha maandamano? Maana ni kama nchi imetulia kabisa kama maji ya kisima chini ya uongozi wa Mwamba wa Kizimkazi, General Samia Suluhu Hassan.
Tanzania pia uhuru wetu hatukuupata kwa kuandamana, tulifanya mazungumzo, kwa hiyo, ili uupate moyo wa mtanzania, na akuelewe, jadiliana naye, huwa hapendi matata na mikiki mikiki.