Kashfa nyingine kwa Serikali ya JK: Wanafunzi Kidato cha I kufanya Qualifying Test

Bora serikali imeamua kuficha aibu, kuna wanafunzi kibao wasiojua kusoma na kuandika ilihali walifaulu mtihani wa darasa la Saba. SERIKALI IBANE, IRUDISHE HESHIMA YA MTIHANI WA STD VII
 
Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali ya JK imelazimika kuweka Mtihani wa aina yake kwa Sekondari zote za serikali kwa wanafunzi wa Kidato cha I kama Qualifying Test baada ya kutokuamini matokeo ya wanafunzi hao. Hii ni kashfa kubwa kwa maana mbili. Moja, wanafunzi hao wamefanya Mtihani wa Taifa- kwa kutumia fedha za umma; wakasahihishwa mtihani huo - kwa kutumia fedha za umma; matokeo yakatangazwa - kwa kutumia fedha za umma; Selection ikafanyika - kwa kutumia fedha za umma; wanafunzi na wazazi wakajiandaa kujiunga na sekondari, vifaa vikanunuliwa, madawati na karo vikalipwa kwa kutumia gharama kubwa. Leo hii, shule zote za sekondari zimeagizwa kufanyisha QT kwa watoto hao na wale wataoshindwa mtihani huo, watarudishwa majumbani. Hapo hasara inarudi tena kwa upande wa mtoto na wazazi. Huu ni uharibifu wa rasilimali fedha na muda.

Pili, ni kashfa kwa sababu, sekondari za yeboyebo (kata) zimesababisha hali hii maana, sasa kila mtoto aliyefika darasa la saba anaamini kuwa atajiunga na sekondari bila kujali amefaulu au la. Kipimo cha kupima uwezo halisi wa mtoto hakipo kama ilivyokuwa zamani na mitihani ya darasa la saba imerahishwa ili shule za kata zisipate aibu ya kukosa watoto. Kurahisishwa kwa mtihani kunafanywa kwa makusudi na serikali ili kupima indicator ya number of enrollment na siyo quality ya elimu inayopatikana. Hii ni aibu kwa serikali.

Wadau, hii Serikali ya zima moto inatupeleka wapi? Naomba kuwasilisha!!

Sasa wewe ulitaka hata asiyejua KUSOMA IRABU ZA KISWAHILI AINGIE KIDATO CHA 1 AKAFANYE NINI HUKO?Napongeza utaratibu huo ni mzuri ili KUWABAINI WACHAKACHUAJI WA ELIMU
 
sasa,walifaulu vp?maana wengine hata kuandika majina hawawezi,kulikuwa na wasimamizi,mpaka maaskari kama sio migambo,lakini bado watu walifanya udanganyifu,sawa watoto wafanye mtihani,lakini wasimamizi wawajibishwe,kuanzia msimamizi mkuu,ambaye ndo mkuu wa shule,
 
Chanzo cha tatizo hili ni mfumo mmbovu wa uongozi ulioharibu mfumo mzima wa elimu. Mbona zamani ama kipindi cha nyuma haya mambo hayakuwepo. Taaluma ya ualimu inadharauliwa sana kwa sasa haja ajira zao,maslai yao yanabezwa ndio maana nao walimu wakakata tamaa ni bora liliende kwa sasa au zima moto km serikali inavyowafanyia na mathara yake ndio haya kushuka kwa elimu tanzania. Serikali iwape kipaumbele walimu na maslai na mishahara inayokidhi na mazingira mazuri ya kazi hii taaluma itarudi km zamani ni itakuwa bora zaidi lasivyo hata form 4 hawajui kusoma wala kuandika kwenye mitihani wao wanajua bongo fleva tu.
 
Hapa serikali concedes imeboronga usimamizi mtihani wa taifa wa shule za msingi. Soon utasikia serikali decrees qualifying elections baada tume ya uchaguzi kuboronga. Baadaye qualifying sensa and the list of shame continues.
 
chanzo kingine cha uchakachuaji ni kuwatishia walimu wa shule za msingi,especially wakuu wa shule,kwamba wanafunzi wakifeli watakuwa demoted,kwa hiyo wanafanya wawezalo ili 2 wanafunzi wafaulu,halafu ujinga huu wanawauzia kesi walimu wa sekondari,sehemu zingine utakuta walimu wanitwa na mbunge ili kuwapongeza kwa kufaulisha
 
Mimi sioni tatizo hapa. Mwaka 1969 nilichaguliwa kuingia kidato cha kwanza na tulifanya mtihani mmoja wa Kiingereza. Sikuelewa mantiki yake mpaka tulipopungua darasani. Kwa kweli elimu yetu imekuwa tata. Policy zinabadilika kila baada ya masaa.

Kwa hapo kwenye red, bado una msimamo wa hapo kwenye blue??

Bila shaka wewe ni mmoja wa wanaofanya maamuzi ya kipuuzi hayo. Yaani mtoto amesoma miaka saba, hajui kusoma na kuandika. Lakini amefanya mtihani wa Taifa, walimu wamelipwa kwenda kusahihisha, amefaulu mtihani na wala hajakamatwa kwa kuiba mtihani... Amepewa shule, leo hii from no where eti hakustahili. Is the government serious????
 
sasa,walifaulu vp?maana wengine hata kuandika majina hawawezi,kulikuwa na wasimamizi,mpaka maaskari kama sio migambo,lakini bado watu walifanya udanganyifu,sawa watoto wafanye mtihani,lakini wasimamizi wawajibishwe,kuanzia msimamizi mkuu,ambaye ndo mkuu wa shule,

Hii ni yote ni udhaifu wa serikali.
 
kama mkuu wa nchi anapata GPA ya 2.3 unategemea anawaza nini kichwani mwake?ndo haya mautumbo yasiyo na mbele wala nyuma
 
Back
Top Bottom