Kashfa - Naibu Waziri Janeti Mbene ameanza kutumia madaraka yake vibaya

Ili kuelewa zaidi haya ninayoyasema unaweza kusoma baadhi ya nyaraka kuhusu mgogoro ambazo nakuwekea hapa baada ya muda mfupi ujao.
Mkuu Mzee wa Masaki, track record ya Janet Mbene kama M/Kiti wa Mtaa wa Masaki, inaeleweka, hivyo hivyo mimi ni mmoja tunaosubiri hizo nyaraka baada ya muda mfupi ujao!, Kwa vile ulipost saa 12:00 jioni, saa hizi ni zaidi ya saa 3:00 usiku, na huo muda mfupi ujao bado haujatimu, bado tunausubiria huo muda mfupi ujao wa kwako, hata kama ni kesho asubuhi, bado ni muda mfupi ujao na tunasubiria hizo nyaraka!.
 
Pasco si watu wote tunaofahamu track record ya mama mbene kama mwenyekiti wa mtaa. Unaweza kutupatia mbili tatu za kumhusu?
 
Last edited by a moderator:
CV nzuri lakini toka aungane na CCM, naye anekuwa Fisadi

Janet Mbene

jmbene.jpg
Janet Mbene is founder and Director of SIA Limited, a private firm that provides capacity-building support for small and medium enterprises.

Ms. Mbene has a rich history in development economics, banking, and international and regional trade. Her diverse background includes leadership positions in the private sector and in the United Nations before joining the non-profit sector. Prior to leading Mwengo, Ms. Mbene worked with Oxfam International, the UN Development Program, the International Labor Organization, and several international nongovernmental organizations. Her work focused on mobilizing producers and entrepreneurs into associations, building their capacity to improve production and manage their enterprises better, facilitating access to markets, campaigning for better conditions through dialogue with relevant authorities, and promoting fair trade policies. She has also led rights and empowerment programs for women and youth, particularly in advocacy, training in legal concepts and instruments, and microfinance and income-generation.
Ms. Mbene has also interspersed her career with short-term consultancies around entrepreneurship development (e.g. with TechnoServe in 2007); research and analysis around rural microfinance services (e.g. with the Economic and Social Research Foundation in Tanzania); and financial services to small and medial enterprises (e.g. with a project of the Austrian government in Tanzania).
Alongside her work with SIA Limited, Ms. Mbene is also the founder and chairperson of YATIMA Trust on HIV/AIDS in Tanzania, which provides support for children who were orphaned or partially orphaned by HIV/AIDS and advocates for policy changes protecting orphans and orphanages. She is also a founding Trustee of the Association of Women Economists in Tanzania, promoting economic literacy and empowerment of particularly rural women.
Ms. Mbene has a Master's degree in economics from the University of New England in Australia. SIA Limited aims to contribute to poverty eradication and sustainable growth support and promote entrepreneurs leading small and medium enterprises (SMEs) in Tanzania, and to contribute to the policy dialogue on SMEs and rural development in Tanzania. SIA targets start-up entrepreneurs in rural and urban areas, as well as local government bodies working with local communities in need of planning, implementation, and monitoring and evaluation capacities.
Additionally, Ms. Mbene serves as chairperson for Getting Old is to Grow (GOIG), an NGO involved in advocacy around aged-people, which also supports vocational training centers in handicraft work for youth, as well as a project for orphans left in the care of their grandparents. She co-founded an NGO to offer support to home based orphans living with relatives.

Huenda mavyeti yote hayo ni fake. katika kipindi cha kwanza cha JK kabla ya kuukwaa u-MP wa miezi sita aliwahi kutokea katika talkshow moja ya TV fulani (siikumbuki) akijitangaza kuomba kazi na kutaja hizo qualifications zake.

Na kabla ya hapo aliwahi kusota -- mapema mwaka 2003 aliwahi kufanya kazi pale habari Corporation (part time) kama proof reader wa gazeti la The African.
 
Kama sio mh. basi andiko hili ni la mtu wake wa karibu ambae kiswahili hakipandi, kwenye r anaweka l, shame!
my bigest qn, hivi hata kama sio la shomari open space ndo ujenge ofisi? open spaces are lungs of the city kama hujui. Mama Tibaijuka unatakiwa ubomoe hilo jengo full stop.
m
NDUGU WA JF NAOMBA KULITOLEA UFAFANUZI SWALA HILI LINALOONEKANA KUPOTOSHA UKWELI HALISI WA KIJANA SHOMARI KUTAPELI ENEO LA WAZI LA SERIKALI YA MTAA YA MASAKI(PENUSULA ROAD0 KARIBU NA DOUBLE TREE HOTEL.)

Ndugu shomari anayetajwa kupokonywa kiwanja na naibu waziri wa Fedha JanetI Mbene historia yake ipo hivi
SAKATA LA KUTOSWA BAHARINI
Ni kweli kijana shomari kwa mujibu wa maelezo yake alitoswa baharini akiwa anazamia kwenda nchi za nje,Kwa bahati nzuri aliokolewa na wavuvi wanaofanya kazi zao bandari ya salama(Feri)
Alipookolewa na wavuvi hao alianza kutafuta maisha hapa Dar es salaam kwa kujishughulisha na kazi mbalimbali.Mnamo mwaka 2004-2005 kijana Shomari alifika ofisi za serikali ya mtaa Masaki kwa lengo la kuomba eneo la wazi lililopo PENISULA ROAD karibu na Double T
 
Inasikitisha kuwa wapo wanaojiita great thinkers wamekubali kutumiwa kirahisi na huyu jamaa ambaye ni wazi anapigania maslahi yake. Sitashangaa kama ni mmoja wa watu wanaopiga mahesabu ama waliotapeliwa na huyu kijana ambaye amewaingiza mkenge (waliotapeliwa) watu wengi. Hii ni propaganda ya kulinda maslahi binafsi na sio haki ya mtu. Wenye haki hapa ni wananchi wa Masaki ambao wameamua kutumia eneo hilo ambalo ni eneo la wazi kwa shughuli za umma ikiwemo ofisi ya Mtaa. Mama Mbene amemvumiliamsana huyu mtu kwa muda mrefu sana. Ni wakati wa kuchukua hatua kama alivyochukua hatua katika maeneo mengine ya wazi yaliyokuwa yakinyemelewa na manyang'au wetu...

Wananchi wa masaki ni kina nani? Suala hapo ni kwamba open space yetu ibaki wazi ili diplomats na viongozi wetu wa serikali watakaokuja wapate hewa safi. Hawa wakazi wa muda wanaotumia nyumba zetu kwa madai ya kuzinunua ndo wanaleta hii migogoro, time wil come when al previous state property portifolio wil be returned with or without socialism ideology.
 
Inasikitisha kuwa wapo wanaojiita great thinkers wamekubali kutumiwa kirahisi na huyu jamaa ambaye ni wazi anapigania maslahi yake. Sitashangaa kama ni mmoja wa watu wanaopiga mahesabu ama waliotapeliwa na huyu kijana ambaye amewaingiza mkenge (waliotapeliwa) watu wengi. Hii ni propaganda ya kulinda maslahi binafsi na sio haki ya mtu. Wenye haki hapa ni wananchi wa Masaki ambao wameamua kutumia eneo hilo ambalo ni eneo la wazi kwa shughuli za umma ikiwemo ofisi ya Mtaa. Mama Mbene amemvumiliamsana huyu mtu kwa muda mrefu sana. Ni wakati wa kuchukua hatua kama alivyochukua hatua katika maeneo mengine ya wazi yaliyokuwa yakinyemelewa na manyang'au wetu...
Hao hao hao .... wapambe wake hao wameanza. Ole wenu, siku zenu za kuishi kwa kulamba vidonda kaa nzi zinahesabika. Mmezoea kuishi kwa kujipendekeza pendekeza ehe...
By the way nimeyasoma kwa kina maelezo ya huyu mama, anayoonyesha kabisa hili eneo alitaka kulipora/kuliuza kinamna, na hilo la kusema ''eti kujenga ofisi ya serikali za mitaa'' ni utetezi usio na mashiko. Hili la ofisi linaonekana linatumiwa tu kumwondoa huyu kijana. Maelezo yamepakwa rangi ili yangare... lakini kwa mjuaji utajua tu kuna agenda nyuma ya hiki kiwanja zaidi ya eti ofisi za serikali ya mitaa
 
my bigest qn, hivi hata kama sio la shomari open space ndo ujenge ofisi? open spaces are lungs of the city kama hujui. Mama Tibaijuka unatakiwa ubomoe hilo jengo full stop.

Mkuu Mjenda Chilo hata mimi nilikuwa nauliza swali hilo hilo. Kwanza kabisa ni vigumu kujua nani anasema ukweli kwa sababu ufafanuzi alioutoa fedha unapingana kabisa na taarifa ya Mzee wa Masaki. Hata hivyo, fedha ameghusia kuwa kulikuwa na kesi ambayo ilifunguliwa mahakamani na kijana Shomari ambapo alishindwa kesi bila kutoa ufafanuzi wa kesi yenyewe.

Nikirudi kwenye the biggest question, nakumbuka mwaka juzi wakazi wa Masaki wakiongozwa na Mwenyekiti wao Ms Janet Mbene walipigania hadi wizara ya ardhi kusimamishwa kwa ujenzi uliokuwa unafanywa na kampuni ya Ms Engineered Systems Solutions Ltd kwenye kitalu Namba 1832 kilichopo Masaki kwa kuwa kilikuwa ni eneo la wazi.

Sasa kama na hiki ambacho fedha anadai ni open space, inakuwaje tena wanataka kujenga ofisi hapo? Au kwa vile ni ofisi ya serikali ya mtaa basi ni ruksa kujenga ofisi yao kwenye sehemu ambayo imetengwa kuwa ya wazi? Kwa nini hawakuomba kujenga hiyo ofisi kwenye kitalu namba 1832 ambacho ni eneo la wazi pia? Hata hivyo, nilidhani kwa vile walikuwa wanapigania kitalu Namba 1832 kuwa ni sehemu ya wazi na hairuhusiwi kujengwa chochote pale basi ingekuwa hivyo hivo kwa hiki kitalu kingine kinachogombaniwa. Vinginevyo kutakuwa na mkanganyiko hapa.

Inasikitisha kuwa wapo wanaojiita great thinkers wamekubali kutumiwa kirahisi na huyu jamaa ambaye ni wazi anapigania maslahi yake. Sitashangaa kama ni mmoja wa watu wanaopiga mahesabu ama waliotapeliwa na huyu kijana ambaye amewaingiza mkenge (waliotapeliwa) watu wengi. Hii ni propaganda ya kulinda maslahi binafsi na sio haki ya mtu. Wenye haki hapa ni wananchi wa Masaki ambao wameamua kutumia eneo hilo ambalo ni eneo la wazi kwa shughuli za umma ikiwemo ofisi ya Mtaa. Mama Mbene amemvumiliamsana huyu mtu kwa muda mrefu sana. Ni wakati wa kuchukua hatua kama alivyochukua hatua katika maeneo mengine ya wazi yaliyokuwa yakinyemelewa na manyang'au wetu...
omarilyas mwaka juzi tuliambiwa na PCCB waliokuwa wanachunguza kitalu namba 1832 kilichopo Masaki kuwa kati ya viwanja 129 ambavyo vilitengwa kama sehemu ya wazi, ni vinane tuu vimebakia kama open space baada ya kuvamiwa. Kama kutajengwa ofisi kwenye hiki kitalu itakuwa ni kuendeleza uvamizi tena kwa serikali kuvamia na kujenga kwenye sehemu ambazo zimetengwa kuwa za wazi.

Kama wakazi wa Masaki na Mwenyekiti wao walikuwa wanapigania Kiwanja Namba 1832 kisivamiwe na kujengwa basi na hiki kisivamiwe na kujengwa pia. Hakuna excuse yoyote kuwa Kiwanja Namba 1832 kilivamiwa na mtu binafsi na kuwa hiki kinavamiwa na serikali ya mtaa na hivyo ni sawa kujenga ofisi yao. Vinginevyo kutakuwa na double standards hapa na wananchi wa Masaki wakiongozwa na mwenyekiti wao wa mtaa wataonekana ni wanafiki wakubwa.

Pia nikufahamishe kuwa wenye haki na hilo eneo sio wakazi wa Masaki peke yao bali ni Watanzania wote. That is is a public land, and the public does not mean Masaki residents only. Hivi mie mtu wa Tukuyu Mbeya nikija kupunga upepo hapo kwenye hiyo bustani ya wazi, wakazi wa Masaki watanitimua?
 
Mkuu unayejiita fedha bila shaka umejieleza kwa kirefu sana sijui ndiye Janet Mbene mwenyewe ama ni msaidizi wake huko wizara ya fedha.
Hapa bado mnajichanganya pamoja na maelezo ya mwanacuf ngunguri omarilyas mnajitahidi sana kumnasua naibu waziri na hii kadhia lakini bado, kuna maswali ya msingi itabidi muyajibu.
Kwamba kijana shomari ni tapeli, alipokwenda kulalamika ikulu wakagundua kwamba shomari amekuwa akitajwa katika matukio mengi ya utapeli. Kama kweli shomari ni tapeli na hata ikulu inafahamu mbona hajawahi kushitakiwa? Kwanini tusiamini kwamba ninyi ndio mnataka kumtapeli?
Unasema kwamba shomari alikuwa amefungua kesi mahakamani lakini hukumu imetoka akiwa ameshindwa. Unaweza kututajia ilikuwa kesi namba ngapi na mahakama gani ili tukajiridhishe na taarifa zako?
 
Last edited by a moderator:
Thanks mkuu FJM kwa kunikumbusha hilo sakata la kiwanja namba 1832 nimekumbuka mama mbene alivyowaongoza wakazi wa masaki kukipigania. Sasa inakuwa kichekesho kwamba mara hii ndiye tena anawaongoza wanamasaki kufanya uvamizi wa eneo la mtu (ama la wazi kama wanavyotaka wao tuamini) na kujenga ofisi ya mtaa. Hapa lazima kuna walakini...
 
Mkuu naona umechanganya madesa kati ya FJM na EMT. Be careful kuna MTM na jfm pia. Sisi zote ndugu, watoto wa baba mmoja, mama mbalimbali.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: FJM
Pasco si watu wote tunaofahamu track record ya mama mbene kama mwenyekiti wa mtaa. Unaweza kutupatia mbili tatu za kumhusu?
Mkuu Mwita Maranya, lets wait hizo nyaraka ziletwe "baada ya muda mfupi ujao", nitakuwekea track record ya Janet Mbene, kama Mwenyekiti wa Mtaa wa Masaki!.
 
Mkuu naona umechanganya madesa kati ya FJM na EMT. Be careful kuna MTM na jfm pia. Sisi zote ndugu, watoto wa baba mmoja, mama mbalimbali.

Ha ha ha nimekusoma mkuu long time no see you hapa uwanjani, kwema huko uliko? Msalimie sana MTM naye ameadimika sana.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Mkuu Mwita Maranya, lets wait hizo nyaraka ziletwe "baada ya muda mfupi ujao", nitakuwekea track record ya Janet Mbene, kama Mwenyekiti wa Mtaa wa Masaki!.
Pasco tunahitaji track records za Mbene kama Mwenyekiti wa Mtaa wa Masaki ili iwe nini? I thought the facts speak for themselves. Kama Mbene na wakazi wake wanadai hilo eneo ni open space, then kwa nini wanataka kujenga ofisi hapo? Should an open space just remain an open space?

Kwa muda mrefu sasa rushwa inaonekana kuwa sugu katika sekta ya ardhi ambapo imeonekana sehemu ya ardhi ambayo imeonekana katika gazeti la serikali kama sehemu za wazi zilizotengwa kwa matumizi ya umma kuwa vimegawiwa kwa njia za kushukiwa kwa waendelezaji binafsi wala rushwa na watafutao utajiri, bado si jambo lililoisha.

Katika hotuba aliyoitoa Mei 24, 2010 Rais Jakaya Kikwete wakati akifanya majumuisho ya ziara ya kukagua hali ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam alikiri kuwa yapo maeneo mengi ya wazi yaliyovamiwa na kuwa madiwani wanahusika na sakata hilo. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Kikwete na malalamiko ya umma Mkuu wa zamani wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alitembelea Manispaa ya Kinondoni tarehe 15 Juni 2010 na kubaini mapungufu kadhaa ya kiutendaji kuhusiana na masuala ya ugawaji wa ardhi yakiwemo maeneo ya umma yaliyozoeleka kuitwa viwanja vya wazi.

Bwana Lukuvi aliunda kamati maalumu ya kuchunguza maeneo yote ya wazi yaliyovamiwa katika mkoa wa Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa tarehe 18 Juni 2010 na pamoja na mambo mengine ilipewa hadibu za rejea ambazo ziliiongoza kamati tajwa kufanya kazi yake. Licha ya kwamba matokeo ya kamati hayajawahi kuwekwa wazi kwa umma, lakini imebainika kuwa manispaa ya Kinondoni ni miongoni mwa manispaa vinara katika uporwaji wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam.

Mfumo wa ufatiliaji wa rushwa Tanzania (CTS) uliona maeneo ya wazi yaliyo katika hatua mbalimbali za uendelezwaji batili kwa matumizi ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Haya maeneo ya wazi hayajumuishi yale yaliyovamiwa na watu binasfi.

  1. Kiwanja Na. 1022 Kitalu E Sinza ambacho kuna ofisi ya afisa mtendaji na banda lenye vyumba vitano vya biashara na msingi wa jengo ambalo halijakamilika.
  2. Eneo karibu na viwanja Na. 281, 282, 283 na 287 Sinza B. Eneo hili limejengwa ofisi ya Mtendaji kata Sinza D.
  3. Eneo karibu na viwanja Na. 411, 413,414 na upande mwingine kinapakana na 698 na 609 Sinza Block D, sehemu kubwa ya eneo hili ipo wazi na pia kimechimbwa kisima cha umma na kuna jiwe la msingi lenye shina la wakereketwa wa chama cha mapinduzi (CCM).
  4. Eneo jirani na kiwanja Na. 37 Sinza Block D ambalo kumejengwa msikiti na mmiliki wake hajulikani.
  5. Eneo linalopakana na viwanja Na. 63, 99 Sinza Block D ambalo limejengwa Kanisa la Assemblies of God, Shule ya chekechea, ofisi ya CCM, nk
  6. Eneo lililopo mkabala na kiwanja Na. 475 Sinza B ambapo kumejengwa shina la wakereketwa wa CCM.
  7. Eneo karibu na kiwanja Na. 23 Sinza C. Eneo hili hutumika limejengwa ofisi ya Afisa Mtendaji wa mtaa halmashauri.
  8. Eneo la wazi lililozungukwa na viwanja Na. 21, 23, 25, 27, 29 Sinza B. Eneo hili kuna shina la wakereketwa wa CCM
  9. Eneo la wazi lililozungukwa na viwanja Na.72-74. Eneo limewekwa shina la wakereketwa wa CCM Kawawa.
  10. Eneo la kiwanja cha michezo na Shule ya Msingi Sinza E. Kiwanja kimemilikishwa kwa CCM.
  11. Jirani na viwanja Na. 38, 40, 44, 46 na 48 Mtaa wa Kibesa Makurumla. Eneo hili limejengwa ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Makurumla.
  12. Eneo la wazi lililopo Mtaa wa Kagera Makurumla limevamiwa na kuna ofisi ya CCM Tawi la Karume Kata ya Makurumla.
  13. Nyuma ya jengo la RUBADA na Kanisa la KKKT na Anglikana. Eneo hilo limejengwa shule ya msingi Ubungo Plaza kwa mpango wa MMEM.
  14. Labda niongezee na hiki cha Masaki ambapo wanataka kujenga ofisi ya Mtaa wa Masaki?

Ifahamike maeneo tajwa yalitengwa kwa mujibu wa sheria (Public Recreation Grounds Cap. 320) na bado ni maeneo tegemewa na muhimu sana kwa umma mzima wa Watanzania na siyo kwa wakazi wa eneo husika tuu. Ucheleweshwaji wa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria unaathiri sana maslahi ya umma. Waendelezaji batili wanafanya kazi kwa ushirikiano na maafisa wa ardhi wala rushwa sambamba na vyombo vya kusimamia sheria kuchukua maeneo ya wazi kwa ujira wa fedha na marupurupu mengine.

Moja ya chama cha kisiasa imeonekana kikiwa pia kinaneemeka na biashara hiyo. Licha ya ari, mwamko, na vitisho aliokuja nao waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi, Prof Anna Tibaijuka, naona ameshondwa kwa sababu labda chama chake kinaongoza kwa kupora maeneo ya wazi. Zaidi ya viwanja 30 vya wazi katika manispaa ya Kinondoni pekee viko katika hatari ya kuwa katika mikono ya waendelezaji wasio halali.

Utembeleaji uliofanywa hivi karibuni unaonyesha bado mambo yanaendeshwa kikawaida, mchezo unaendeshwa kwa nguvu kubwa sana na kuna wanaonufaika na kuneemeka kutokana na matunda ya mchezo huo. Viwanja vya ukubwa huo vinasemekana kuwa kati ya TShs 50-300 milioni kutegemea ukubwa na eneo kiwanja kilipo.
 
Mkuu EMT, I'm just speechless!.
Nilifanya TV interview na Mama Prof. Tibaijuka kuhusu "restoration" ya maeneo ya wazi, nakumbuka specifikally nilimuuliza kama kweli ana guts, kuarejesha maeneo yote ya wazi, wakati defaulter mkuu ni CCM?. Alisisitiza kufuata sheria, taratibu na kanuni!, hata kama ni ikulu, kitarejeshwa!, she claimed to be fearless!. By now she is nothing more!, nothing less!. Kabla kipindi hakijarushwa hewani, kilisimamishwa na kuwa "withdrown!".
CCM ni chama dola, kiko over and above the law!. Tibaijuka by now has learned her lessons a hard way!, hamtamsikia tena kwenye hili!.
 
  • Shomari anawezaje kwenda mahakamani akiwa HANA document yeyote inayom'back up madai yake, kama kweli yeye ni mvamizi tu?
  • Kama kweli sio kwake, na nimvamizi tu, nini kiliwapa ikulu nguvu ya kufunga safari hadi pale kuona huo unaoitwa ukweli?
  • Kama ni tapeli, mwuza bangi, jambazi n.k bado hakumwondolei haki kama kweli hiyo sehemu ni yake. Iwaje mwalikwa ashindwe kutimuliwa na mwalika, kama serikali ya mtaa ndiyo iiliompa?

Mwenzenu naona chenga-chenga tu, aliyeko juu ya bati azungeshe antena tuone vizuri.....lol

Kibanga Msese
 
Nimewawekea attachment hapo juu angalienei wenyewe.
 
[/QUOTE

Angalia posti number 75
 
Back
Top Bottom