Kashfa - Naibu Waziri Janeti Mbene ameanza kutumia madaraka yake vibaya

Sep 30, 2012
21
15
Huyu Naibu Waziri wa Fedha Janeti Mbene ameanza kutumia vibaya madaraka yake kwa ajili ya kujinufaisha yeye binafsi. Hivi karibuni Naibu Waziri huyu ameuelekeza uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kwenda kubomoa nyumba ya kijana mmoja maeneo ya Masaki karibu na Double Tree hoteli kwa kusingizia eti anataka eneo hilo lijengwe ofisi za mtendaji wa mtaa. Eneo hilo limekuwa na mgogoro kwa siku nyingi kwani kijana Shomari ambaye huko nyuma aliwahi kutoswa baharini na kuokolewa amekuwa akiishi katika eneo na nyumba hiyo tokea bibi yake akiwepo. Bibi yake Shomari aliishi katika eneo hilo tokea enzi za ukoloni na eneo hilo inaonesha lilipimwa mwaka 1948 na kuwekwa katika mpango wa kujengwa barabara. Wanaoishi katika eneo hilo waliahidiwa kufidiwa lakini haikufanyika hivyo na badala yake wakawa wanaelekezwa wajenge makazi yasiyo ya kudumu ili Serikali ikiamua kutekeleza mradi wake wa kujenga barabara iwe rahisi. Kilichotokea bwana Shomari aliwahi kufuatwa na mmiliki wa Double Tree ili amuuzie hilo eneo. Shomari alipokataa huyo mmiliki wa Double Tree aliamua kumfuata Mwenyekiti wa Mtaa ambaye ni Janeti Mbene ili amsaidie kupata eneo hilo. Janeti Mbene akiwa kama Mwenyekiti wa Mtaa alikubali na kisha naye akawa ametamani eneo hilo ili wagawane na mmiliki wa Double Tree, ndipo wakaanza kufuatilia ili kulipata eneo hilo na kuzua mgogoro. Walipoona wanakwama wakamtumia mtu mwingine ajulikanaye kama Jaspreet ili amfungulie kesi Shomari kuwa amevamia eneo lake. Bwana huyu kaja na hati ya kufoji inayoonesha kama yeye ni lmmiliki wa eneo hilo tokea mwaka 1996. Hayo yote yameendelea kukwama kwa sababu ukweli kuhusu kiwanja hicho unabaki kuwa dhahiri kuwa Shomari ndiye mmiliki halali wa eneo hilo. Hivi karibuni kilichotokea mara baada ya Janeti Mbene kuteuliwa kuwa Naibu Waziri alienda kwenye uongozi wa Kinondoni na kuwaelekeza wakamtoe kwa nguvu bwana Shomari, ndipo hao watu wakampa notisi na kisha juzi wakaenda kutekeleza azma yao ya kubomoa na kuharibu haribu kila kitu. Wamewachukua hadi watoto wake ili kumlazimisha aondoke eneo hili. Ukibahatika kufika pale utahuzunika sana jinsi palivyo kwani kuna walinzi wanaolipwa na Janeti Mbene wanalinda eneo hilo ambalo tayri limewekwa uzio wa mabati kuonesha kuwa kuna nyumba itajengwa hapo. Bwana Shomari amebakishiwa banda ambalo analala yeye tu. Akiwa ndani ya uzio amezingwa, nje ya banda analolala kuna mbwa, bata kuku na makororo kibao, kitu ambacho kinasikitisha sana. Yaani huyu kijana kafanyiwa uonevu wa hali ya juu na hata hatima yake haijulikani kwani uongozi wa Kinondoni Manispaa unasema hautaki kabisa kumaliza mgogoro huo kwa sababu hawahusiki na anayehusika ni Naibu Waziri Janeti Mbene. Ili kuelewa zaidi haya ninayoyasema unaweza kusoma baadhi ya nyaraka kuhusu mgogoro ambazo nakuwekea hapa baada ya muda mfupi ujao.




View attachment 66928


Mlio online kwa sasa naomba mnielekeze namna ya kufanya attachment niwatumie documents

Sasa ukifungua hiyo attachment hapo juu utaona kuwa Manispaa walisema kuwa hilo eneo ni la barabara kwa mujibu wa upimaji wa mwaka 1948 wakati bibi yake Shomari akiwa anaishi eneo hilo, inakuwaje sasa Serikali ya Mtaa inalibadili eneo la barabara kuwa na Serikali ya mtaa. Inasemekana na ofisi za CCM zitajengwa hapo hapo karibu. Acheni uonevu jamani, hata aibu hamna. Wako wapi wapigania haki za binadamu, wanasheria wetu wanataka pesa tu. Pesa hii pesa itatutoa utumbo.
 
Ama kweli hujafa hujaumbika...
Huwa naamini hakuna viumbe wenye roho mbaya kama wanawake...
Sipati picha ndo awe mama wa kambo flani lazima madogo wafe njaa
 
mungu atamlipa huyu kijana. Sisi akina mama tukipata madaraka tu8jaribu kutulizana nayo kwanza maana kuna siku tutajaumbuka. Bibi Janeth hukuanza wewe kulikuwa na wenzio akina Monica Mbega ambao nao walikuwa hapohapo wakatumia madaraka yao vibaya leo unajua waliko. Be careful kilio cha wanyonge husikika zaidi na Mungu. Basi mlipeni haki yake akatafute kiwanja kinginw kule kwenye msitu wa mabwe pande.
 
Huyo kijana ajitokeze kwenye media umma wote ujue kuwa kuna dhuluma kubwa..dhidi ya mafisadi wa ardhi!tena wenye madaraka makubwa.....asiache haki yake ikapotea hivi hivi!!!!asikubalii kuna wanasheria wengii tuu watamsaidia tena bure tuu...watu waliokaribu nae wamshauri ajitokeze atasaidiwa
 
Nashindwa kuelewa uhusika wa Wizara ya fedha katika kushughulikia viwanja ama ofisi za watendaji wakati Manispaa ipo. haya ndiyo mambo yanayopelekea wananchi kuwa na chuki na serikali yao. UTAWALA WA SHERIA UPO WAPI?
 
Ndo serikali ya Jk hiyo. Hiyo ndo maana halisi ya NGUVU ZAIDI
 
Kidumu Chama cha Mapinduzi .Huyu yeye si mtu wa NEC ?Ashauriwe huyu aende mbele aseme Watanzania wajue ukweli wa maisha haya .
 
Ndiyo maana tunataka kuondoa CCM. CCM ikiondoka haya yote yatarudiwa na haki kutendeka. Tumeona juzi rais mstaafu wa Kenya akirejesha mali ya kijana mmoja wa kizungu aliyemdhulumu baada ya kupata madaraka. Hawa wajue arobaini yao imekaribia. Tukishindwa kuwaondoa kwa kura basi tuamua kujitoa mhanga ili watoto wetu wasiwe watumwa wa watoto wa vigogo hawa mafisi.
 
Usalama wa taifa umelala fofofo huku mlalahoi akinyang'anywa haki yake
 
Mama mbene, Mungu akupe hekima, busara, na huruna kwa viumbe wasio na nafasi kama yako. Naogopa kutabiri yajayo kwani sikupewa kipaji hicho ila ninacho amini ni kuwa dhuruma ni dhambi.
 
Pumbavu kabisa watanzania wanasheria wako wapi kutoka kumsaidia? watanzania wote ni watu wenye roho mbaya, huyu janet kwanza ni yule aliyehusishwa na wizi mkubwa kwenye miradi ya UN wakati akiwa sijui nini leo hii mnabakia kumchekea wako wapi wakina Francis Sitola wa Tanganyika Legal services? wanasheria mahiri wakina Alex Mgongolwa wameishia kujilimbikizia mali tu hakuna msaada wowote unaoenda kwa watu vikundi vya sheria kwa jamii, wakina NOLA si lazima mfuatwe huku kwenye AC zenu hizi ndio kesi za kushughulikia leo kafanyiwa shomari kesho watoto wenu, mimi naongea pia ningekua victim kama nisingefunguliwa na mungu kuniokoa tena kwa bei ndigo tu, shomari nenda magazetini kamtafute kubenea wa mwanahalisi simu yake ni 0653523282 hao manispaa achana nao ndio wezi wakubwa na wafoji makaratasi wakubwa sana, hebu rudi serikali ya mtaa pale msasani mtafute diwani wa zamani anaitwa mama tatu, hao ndio waliokua viongozi waadilifu watu wa mwalimu hawa wa JK ni genge moja
 
hapa ndio tutakapoona wale wanaokasirika tukisema pasipo mwanahalisi hakuna magazeti, tutaona kama watafuatilia maana mwanahalisi ingeshafika hapo na kubeba bango, tuone wako wapi wengine, wananchi piganieni mwanahalisi tupate haki zetu
 
huu ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu. Huyu mama kwanza tumeona anapendelewa pendelewa tuuu na sasa anaanza kudhulumu ardhi na mali za watu. Mtoa mada huwezi muunganisha jamaa na kituo cha sheri ya haki za binadamu jamaa apate msaada wa kisheria? Hii serikali imejaa wezi watupu
 
Janeth Mbene!! Kama ni kweli muogope Mungu wangu!!! Kwani uliyonayo hayakutoshi mpaka kuzunguka Serikali za Mitaa,this shows dhamira za watu hawa zilivyokufa!!! Wamebaki makapi tu!! Very Sad!!!
 
Duh, kwenye issie ya hela binadamu tunakuwa wanyama zaidi ya wanyama wenyewe, sasa hapo utakuta anaviwanya zaidi ya kumi, na fezaulole kigamboni lazima atakuwa alipata, bado anataka cha huyo kijana.......kweli?
 
Back
Top Bottom