Kashfa IMMIGRATION Dar Airport

.........
5.KABLA HUJATOKA MLANGONI UTAKUTANA NA WENGINE KAMA 5 HIVI HAWA HUWA WANAKUWA NA MASHATI MEUPE NAO HUJIITA IMMIGRATION OFFICERS AU SIKU NYINGINE UTAKUTANA NA MWINGINE ANAJIITA USALAMA WA TAIFA ATATAKA PASSPORT YAKO na ATAKUULIZA SAME QUESTIONS ULIOULIZWA KWENYE STAGE NUMBER 2 ..............

This is VERY TRUE..............imeshanitokea mara zote nilizokuwa natoka pale mlangoni (i.e.kutoka nje)

.........Uongo kama umekwisha gongewa passport hawawezi kukuuliza kitu huu ni uongo - Period!
 
Uongo huu..

GT umesafiri lini wewe? Mbona mimi nilikuwa na mizigo mingi tu na sikupata usumbufu?

GT huyo jamaa mwongo mimi sisafiri 1st class sina hiyo pesa. Tuwalaumu kwa mengine siyo hili na mie nabisha sio Uhamiaji walio karibu na mlangoni.

Wacha1.........watu hapa sio kwamba wanatunga.....ni mambo yaliyowakuta.........yaani ukitoka kwa Customs unapoelekea kwenye mlango wa kutoka nje pale mlangoni mara nyingi kunakuwepo Polisi......na sasa wapo pia hao jamaa wanaojiita siku nyingine Uhamiaji......siku nyingine Usalama wa Taifa.......yote hayo yamewahi kunifika mimi............. nilipoulizia inakuwaje....wakaniambia kuwa wanacheck passport za kugushi!!!!!!!!........na eti wana case nyingi tu wamezikamata kwa checking ya aina hiyo.......dah nilichoka kabisa............na kujiuliza maswali mengi sana kuhusu passport zetu...........
 
BTW Huyu jamaa kwani hajui sheria? Wewe tena umetoka majuu hujui sheria? Unababaishwa na procedural working routine?

Hebu tuambie Mkuu wengine hapa sheria imetupitia kando..........tukikutana na watu wa aina hiyo tuwaambieje?
 
Mkuu huyo mtoto sio mtanzania? Kama sio Mtanzania kwa nini hukuchukua viza kabla ya safari?

kwa njaa walionayo wale the so called UWT/IMMIGRATION/ASKARI KANZU/GESTAPO/MUKHABARAT etc

watamsimamisha tuuu awe na visa asiwe nayo
 
Sasa unaona mwenyewe hao sio uhamiaji ni :Uonevu unaofanywa na Maofisa wa polisi wa Upelelezi hapo Airport Dares-Salaam .

Mie nimepita sana pale sijui mara ngapi usumbufu unaosemwa hapa sijauona. Wizi kweli unaweza kutokea sio kusumbuliwa na askari uchwara wasiojua sheria.

GT kwa hiyo badili kichwa cha habari.

tatizo jamaa wanajiita majina yote, na mara nyingi huwa wanajitambulisha as immigration officers!!!

nibadili kichwa cha habari kumlinda nani?

acha asubuhi waamke wakute walivyo bandikwa
 
This is VERY TRUE..............imeshanitokea mara zote nilizokuwa natoka pale mlangoni (i.e.kutoka nje)

Wacha1.........watu hapa sio kwamba wanatunga.....ni mambo yaliyowakuta.........yaani ukitoka kwa Customs unapoelekea kwenye mlango wa kutoka nje pale mlangoni mara nyingi kunakuwepo Polisi......na sasa wapo pia hao jamaa wanaojiita siku nyingine Uhamiaji......siku nyingine Usalama wa Taifa.......yote hayo yamewahi kunifika mimi............. nilipoulizia inakuwaje....wakaniambia kuwa wanacheck passport za kugushi!!!!!!!!........na eti wana case nyingi tu wamezikamata kwa checking ya aina hiyo.......dah nilichoka kabisa............na kujiuliza maswali mengi sana kuhusu passport zetu...........
 
Hebu tuambie Mkuu wengine hapa sheria imetupitia kando..........tukikutana na watu wa aina hiyo tuwaambieje?

Mkuu nikitoka kwenye mlango wa Airport nipo Tanzania uraiani sheria za uraia zinaanza pale. Kama yeye ni askari ananiuliza chochote ni lazima:

1. Anionyeshe kitambulisho chake na mandate aliyonayo. Kama anataka kunipekua ni lazima awe na warrant iliyosainiwa na mkubwa wake na ina jina langu ili anipekue. Vile vile sitakubaliana naye hadi twende kwenye kituo chake cha kazi. Usikubali kupekuliwa hovyo na hawa vikaragosi wezi.
 
Mkuu nikitoka kwenye mlango wa Airport nipo Tanzania uraiani sheria za uraia zinaanza pale. Kama yeye ni askari ananiuliza chochote ni lazima:

1. Anionyeshe kitambulisho chake na mandate aliyonayo. Kama anataka kunipekua ni lazima awe na warrant iliyosainiwa na mkubwa wake na ina jina langu ili anipekue. Vile vile sitakubaliana naye hadi twende kwenye kituo chake cha kazi.

mhhhh

ku deal na waliopo nje si kazi, kazi ni wale wasumbufu pale mlangoni kabla hujatoka
 
kwa njaa walionayo wale the so called UWT/IMMIGRATION/ASKARI KANZU/GESTAPO/MUKHABARAT etc

watamsimamisha tuuu awe na visa asiwe nayo

tatizo jamaa wanajiita majina yote, na mara nyingi huwa wanajitambulisha as immigration officers!!!

nibadili kichwa cha habari kumlinda nani?

acha asubuhi waamke wakute walivyo bandikwa

Hao ni wezi wala wasikubabaishe sheria zipo usikubali kuibiwa kipuuzi. Ni sawa na kwenda kariakoo na kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Kama mambo yako yote yako mswano wafundishe adabu wataacha wenyewe.
 
Mkuu nikitoka kwenye mlango wa Airport nipo Tanzania uraiani sheria za uraia zinaanza pale. Kama yeye ni askari ananiuliza chochote ni lazima:

1. Anionyeshe kitambulisho chake na mandate aliyonayo. Kama anataka kunipekua ni lazima awe na warrant iliyosainiwa na mkubwa wake na ina jina langu ili anipekue. Vile vile sitakubaliana naye hadi twende kwenye kituo chake cha kazi. Usikubali kupekuliwa hovyo na hawa vikaragosi wezi.

Sawa Mkuu hilo linaeleweka....umemsoma huyu ndugu hapa chini......?

Ni Kweli hao ni Vikaragosi Askari wa Ofisa Upelelezi wa Mkoa (RCO) Bw. Nzowa wanao haribu jina lake Bw Nzowa ukifika hapo Aiport nje wanakusubiri na kuanza kukuliza Maswali ya kijinga Unatoka wapi,umeishi huko nje kwa muda gani,kwanini umerudi,umeleta kitu gani kusema kweli wana usumbufu wa kila aina na ndio hao wanao haribu jina zuri la Jeshi letu la Polisi na kulipa Jeshi letu la Polisi sifa mbaya na huyo Mkuu Ofisa Upelelezi wa Mkoa (RCO) Bw. Nzowa anayo habari lakini ananyamaza tu si unajuwa Nchi yetu ilivyoharibika Kwa Rushwa,na Ufisadi. Sasa hao Polisi wa Upelelezi wa Aiport wanakusumbuwa na kukutisha utafikiri wewe ni jasusi unayetafutwa na Amerika kazi yao hao Askari kanzu wa Upelelezi kukusumbuwa utafikiri huko ulikotoka hakuna Askari kuzidi hata wao. Mimi nakusimulia hivyo kuwa yalimtokea Rafiki yangu mwaka jana ikafika mpaka wakamzuia Vitu vyake alivyotoka navyo nje ya nchi na ikafika hatuwa ya kusema atowe Pesa (Rushwa) ya shilling Laki moja ndio watampa vitu vyake ikaenda mpaka miezi sita ikawa wanampa kidogo kidogo mpaka hii leo baadhi ya vitu vyake wamevizuia hapo hapo Aiport Dares-Salaam hii kweli imenisikitisha sana kuwa hao askari wa Bw Nzowa wanawasumbuwa wananchi wasiokuwa na hatia hayo yote wa kumlaumu ni Rais wetu anawapa watu vyeo hata na elimu navyo hivyo Vyeo hawana basi Rais akipenda Mtu amtakae anampa tu Cheo sawa ampe amtakae lakini itabidi Rais amuangalie huyo Mtu anaye taka kumpa cheo amesomea nini huyo mtu anayetaka kumpa Mheshimiwa Rais wetu cheo sio kila mtu ndio ampe cheo ama kweli Waswahili Husema kuwa (Miafrıka Bwana Ndivyo Ilivyo)

......Mkuu Wacha1

Wee sema tu kwa kuwa hayajakufika au ni "mwenzao".......Imagine this.......umetoka zako safari...umepita immigration.....kisha umepita customs......ndug zako wankusubiri pale nje ile unatoka tu......halafu unakutana na hao jamaa hapo mlangoni.......tena wanakuambia........utafikiri una ugomvi nao "leta passport yako"....."hii ni mali ya yetu" au siku nyingine wanasema "hii ni mali ya serikali".........ukiwaomba wajitambulishe......ndio mara utasikia Usalama wa Taifa au siku nyingine utasikia Immigration Officer na siku nyingine jamaa alinigomea kujitambulisha........eti akaniambia "serikali iko kazini"...............basi bana maswali yanaendelea unatokea wapi? uliondoka lini? ............"madhumuni ya safari yako?"......"ndio umerudi jumla au utaondoka tena?".....yaani basi tu ili mradi........anyway hii ndio bongo wanasema eti iko tambarare
 
Mimi nashanga yaani mtu akikwambia yeye ni usalama wa taifa basi unatetemeka? Au akikwambia yeye ni askari basi unaogopa? Tena kama yeye ni askari ndio vizuri kwa sababu yuko pale kwa usalama wako. Kama ni askari bandia wajulishe askari wa kweli achukuliwe hatua. Kama kweli wewe umetoka majuu kweli unaweza kubabaishwa na hawa askari bandia?

Jamani pamoja na majukumu mengi watanzania lazima tuelewe kazi za kila Idara. Kazi za polisi ni kulinda usalama wa raia na zina mipaka yake. Ni vizuri uelewe polisi ana nguvu kiasi gani kwa raia.

Kazi za immigration officer vile vile lazima ufahamu kwamba ukisha ingia kwenye nchi yoyote yaani ukigongewa muhuri huwa wanakuwa hawana power ya ku-arrest hiyo ni kazi ya polisi.

Askari kanzu au usalama wa Taifa hana power ya ku-arrest lazima atumie polisi.

Customer officer anaweza kuzuia mzigo wako kwa kutaka ulipe ushuru kutokana na sheria zilizopo. Unapoacha mzigo orodhesha kila kitu kama begi liko wazi au limefungwa na waweke sahihi ni vitu vipi wanabaki navyo na waandike kwa nini wanavizuia.

Sasa basi kama hizo sheria ndogo ndogo unazifahamu hakuna kimburu yoyote atakayekuonea kama yeye sio askari kweli kweli lazima aje kwako mzima mzima hata kama hujui sheria mwambie muongozane naye hadi kituoni kwake na kama hukubaliani naye unaweza kumuona mkubwa wake. It is as simple as that, na kama wanakuonea wafungulie kesi.

Ogah

Huyo jamaa hapo juu naona pengine katunga hiyo story. Mimi sio mwenzao kama unafikiria nafanya kazi huko nakupa experience yangu nimetumia sana DIA mara nyingi sana kwa regional na international flights for over 10 years now.
 
Nafikiri kuna tatizo lingine pale DIA nalo ni sehemu ya declaration haiko wazi. Pengine wangepanua na kuwa na milango miwili yaani green if you have nothing to declare na red kama unataka ku-declare some goods.

Kwa sababu unapotoka na mzigo ndio hapo jamaa wale mlangoni yaani Custom officers watakuuliza unatoka wapi? Umebeba vitu gani nk. Hili ni jukumu lao ku-asses kama una mzigo wa kulipia ushuru au la sasa hapa inawezekana ukaambiwa fungua mzigo wako - kisheria wana mamlaka hayo vile vile watakuuliza passport ili kuwa na uhakika kwamba wewe ndiye msafiri sio umeingia pale kwa njia za panya na kutaka kuiba mizigo ya watu nk. Lakini hawa hawana mamlaka yoyote na passport yako, wakati mwingine watakuuliza boarding pass yako ni kuthibitisha tu kwa sababu passport na boarding pass zote zina majina yako. Wanauwezo au mamlaka ya kuzuia mzigo wako ili ulipe ushuru.

Lakini hili siyo kila tom dick and harry can harass you. Kama unasafiri sana utawajua nani ni Immigration na nani ni Custom officer. Custom officer akiuliza passport ni verification tu.
 
Je na wale nchi jirani wanaoshukia hapo DIA na wenyewe inakuwaje??Maana na wenyewe wanasumbuliwa sana,Mfano kuna jamaa mmoja yeye kwao ni Uganda na yeye alikuwa anatokea Sweden kwa hiyo alikuwa anatumia Travel Document ya Sweden ambayo ni ya miaka 5 na anaruhusiwa kuishi kwenye hiyo nchi ya Sweden maishani yake yote,Sasa kwenye Pass yake ya Travel Document wameandika kwamba haruhusiwi kuingia Uganda,Sasa je inakuwaje mtu kama huyo anakuja kwenye nchi alafu anasumbuliwa na kuambiwa kwamba usipotoa hela tutakupeleka kwenye nchi yako ya Uganda ni kwa nini?Au kwa nini asumbuliwe kupewa Visa na aanza kuhojiwa maswali mengi?Kwanza hao Home office wana mamlaka hayo kuingilia Personal za watu??Au inakuwaje hapo??Au ndio usipotoa Rushwa ndio huna haki zaidi??
 
Mimi nadhani ni utaratibu au utawala wa kiwanja ambao ungekuwa katika sehemu kuu tatu. 1. Uhamiaji 2. TRA au customes 3. quarantite(Afya) na zingekuwa na wataalam wa taluma hizo wakisaidiwa na vitendea kazi(scanners), Sniff dogs na kadhalika. Kukagua bags ni kwa ajili ya customes kuona kitu gani unatakiwa kulipia kodi. Na qurantine wanakagua vitu ambavyo vinaweza kuleta magonjwa ya kuambukiza kama mafua ya nguruwe, vegetable quarantine yaani mimea inayoweza kuleta magonjwa ya kuambukiza kwenye mazao yetu. Na immigration wanaangalia hati zako za kusafiria na Visa yako kwa mgeni. Customes kuomba passport yako ni kuhakikisha kama bag hiyo ni yako ndiyo huendelea na ukaguzi. Si vibaya custome officer au qurantine officer kuuliza passport yako kwa ajili ya ukaguzi wa mzigo wako. Good luck naomba tushirkiane nao ili tusiweze kuleta au kuingiza vitu ambavyo vitatuletea madhara.
 
Ni kweli huduma za DIA ni za HOVYO..na mtu anayewatetea sielewi ana maana gani. Sio tu watu wa customs na uhamiaji, bali hata na attendants wabongo wa some of airliners. Nway, nchi inahitaji reshuffle kila pahala, na yanayotokea DIA is part tu of the bigger picture.
 
Wengineeeeeee wanaona wivuuu ukiwa unatoka mbele...wanasumbua sana sana naona ni wivu tuu wanakuwa hawana lolote la kukusumbua wala kudai passport yako...inawahusu nini??
 
Nafikiri kuna tatizo lingine pale DIA nalo ni sehemu ya declaration haiko wazi. Pengine wangepanua na kuwa na milango miwili yaani green if you have nothing to declare na red kama unataka ku-declare some goods.

Kwa sababu unapotoka na mzigo ndio hapo jamaa wale mlangoni yaani Custom officers watakuuliza unatoka wapi? Umebeba vitu gani nk. Hili ni jukumu lao ku-asses kama una mzigo wa kulipia ushuru au la sasa hapa inawezekana ukaambiwa fungua mzigo wako - kisheria wana mamlaka hayo vile vile watakuuliza passport ili kuwa na uhakika kwamba wewe ndiye msafiri sio umeingia pale kwa njia za panya na kutaka kuiba mizigo ya watu nk. Lakini hawa hawana mamlaka yoyote na passport yako, wakati mwingine watakuuliza boarding pass yako ni kuthibitisha tu kwa sababu passport na boarding pass zote zina majina yako. Wanauwezo au mamlaka ya kuzuia mzigo wako ili ulipe ushuru.

Lakini hili siyo kila tom dick and harry can harass you. Kama unasafiri sana utawajua nani ni Immigration na nani ni Custom officer. Custom officer akiuliza passport ni verification tu.

Asante Mkuu Wacha1 kwa maelezo yako safi kabisa...........

Customs hakuna tatizo sana........tatizo la customs ni kuwaogopa wadhungu na kuwabana wabongo...................standard ya ukaguzi inabidi ifanyike kwa wote.

swala ni pale ni wangapi wako sharp kujua hayo yote ukizingatia.....ndio umetoka safari (ukiwa kama wewe umepita pita mara kibao) walau waweza jua wale jamaa utapambana nao vipi........sasa mwenzangu na miye muongo mmoja hujafika nyumbani...........ghafla unakutana na mijamaa......lazima utashangaa shangaa....wakati huo huo ndio jamaa wana-take advantage of you.............hawa jamaa kusema ukweli wankera sana.............halafu kuna polisi pale wala hawasemi chochote............
 
Binafsi nishasimamishwa zaidi ya mara 4 na jamaa pale mlango wa kutoka

of course hawakunifanya kitu ni maswali waliuliza lakini ni ya kero na zaidi ya hayo wako watu wengi wanasumbuliwa

Hii issue ilishawahi kuzungwa kwenye JF ya zamani nikipata thread ntamwambia Steve aimerge maybe utapata idea na si JF tuu ni mpaka kwa michuzi watu washalalamika kuhusu usumbufu DIA

kataa tuu lakini usumbufu jamaa wa Immigration wanao mle ndani

Lakini kwa ajili ya usalama wa taifa Immigration, Police ama hata Customs na hata raia wa kawaida waadilifu wana haki ya kumshuku yeyote na kumdhibiti ama ama na kumriport kwa vyombo vya dola baada ya kuona na kujihakikishia kua hana mwenendo wa kawaida sehemu yeyote ndani mjengo wa airport.
Kitu cha kwanza utaombwa Pass na sioni kwa nini uulize maswali badala ya kuwapa tu waiangalie. Kwanza wanakuuomba Pass in public watu wengi wakiona. Hivyo basi kusimamishwa kwa ukaguzi wa passport mara tano au kumi labda ni mbinu yao tu ya kukuvunjavunja utulivu wako ili wajue ukweli wako, inawezekana si mbinu nzuri lakini ndio ya Kitanzania na ni cheap kwa airport zetu zisizokua busy. Usijishuku na kujilinda sana, waachie wafanye kazi yao na ukweli utajulikana.

Ni ukweli tu kua kuna watu wana forged passports ama ni criminals huko walikotoka ama wanategemea kuleta uhalifu hapa kwetu na ni kazi ya hivyo vyombo vya dola na raia wote wema kupitia vyombo vya dola kusaidia kudhibiti.
 
Wow Bro unless unasafiri na airport nyingine

the situation iko hivi pale DIA

1.UNAPOSHUKA TOKA KWENYE NDEGE YAANI KWENYE ZILE NGAZI PALE KWENYE CORRIDOR UTAKUTANA NA IMMIGRATION WAWILI WATATU WANAWASAIDIA WAGENI KWENYE MAMBO YA FORMS ZA VISA AND SO ON

2.KABLA HUJAENDA KWENYE DIRISHA IMMIGRATION UTAKUTANA NA JAMAA WA IMMIGRATION (WANAKUWA MINIMUM 5 OR 6 NA UNIFORM ZA IMMIGRATIONS) NA MMOJA AU WAWILI WATU WA AFYA WATAKUULIZA VACCINATION CARD ETC

3. BAADA YA HAPO UNAKUTANA NA MKANDA WA MIZIGO USOFANYA KAZI ...
PALE NAKO UTAKUTA IMMIGRATION OFFICERS KAMA 7 HIVI WANAZUNGUKA ZUNGUKA KUOTEA WATU

4 UKIMALIZA UTAKUTANA NA CUSTOMS OFFICERS AMBAO HUWA WANASIMAMISHA WATU WEUSI NA KUWAACHIA WAZUNGU

5.KABLA HUJATOKA MLANGONI UTAKUTANA NA WENGINE KAMA 5 HIVI HAWA HUWA WANAKUWA NA MASHATI MEUPE NAO HUJIITA IMMIGRATION OFFICERS AU SIKU NYINGINE UTAKUTANA NA MWINGINE ANAJIITA USALAMA WA TAIFA ATATAKA PASSPORT YAKO na ATAKUULIZA SAME QUESTIONS ULIOULIZWA KWENYE STAGE NUMBER 2

6.KUTOKA NJE SI SABABU KUWA UKO SALAMA, UNAWEZA KUKUTANA NA MTU YOYOTE YULE ANAYEJIITA USALAMA WA TAIFA AU IMMIGRATION SASA THAT WILL ALSO DEPEND ON A DAY!!!

Kama hujakutana nao hao then utakuwa na bahati kubwa sana na inawezekana huwa unasafiri VIP mwenzetu
Nakumbuka kuna safari moja wakati nawasili baada ya kumaliza kuclear immagration na custom, nilipotoka nje nikakutana na mtu akaniambie yeye ni usalama wa taifa, nikamuuliza so what? Akanywea, mtu mwenye alikuwa anaonekana kama tapeli au misheni town
 
Lakini kwa ajili ya usalama wa taifa Immigration, Police ama hata Customs na hata raia wa kawaida waadilifu wana haki ya kumshuku yeyote na kumdhibiti ama ama na kumriport kwa vyombo vya dola baada ya kuona na kujihakikishia kua hana mwenendo wa kawaida sehemu yeyote ndani mjengo wa airport.
Kitu cha kwanza utaombwa Pass na sioni kwa nini uulize maswali badala ya kuwapa tu waiangalie. Kwanza wanakuuomba Pass in public watu wengi wakiona. Hivyo basi kusimamishwa kwa ukaguzi wa passport mara tano au kumi labda ni mbinu yao tu ya kukuvunjavunja utulivu wako ili wajue ukweli wako, inawezekana si mbinu nzuri lakini ndio ya Kitanzania na ni cheap kwa airport zetu zisizokua busy. Usijishuku na kujilinda sana, waachie wafanye kazi yao na ukweli utajulikana.

Ni ukweli tu kua kuna watu wana forged passports ama ni criminals huko walikotoka ama wanategemea kuleta uhalifu hapa kwetu na ni kazi ya hivyo vyombo vya dola na raia wote wema kupitia vyombo vya dola kusaidia kudhibiti.

wawekeeni check point yao nyingine humo humo ndani......sio kuanza kusumbua sumbua watu wanapokuwa wanatoka nje tayari kupokewa na ndugu na jamaa halafu..........
 
2.Nilipomalizana na ukaguzi (sikukubali kulipa), nilisogea mlangoni ili sasa nikutane na familia yangu kwa ajili ya mahug lakini nkakutana na watu 4 wamesimama mstari mmoja. Mmojawao akaniambia 'hebu tuone passport yako'. Hapa ndio nataka niulize maswali zaidi.

Hivi hawa wanauliza umekwenda nje kufanya nini ni kazi yao?

Ni kweli huwa kuna watu wanauliza maswali hayo, hata mimi baada ya kumalizana na watu wa customs huku nikidhani sasa naenda kutoka kwenye geti la arrivals, nilisimamishwa na jamaa mmoja hapo mlangoni na akaomba passport yangu, nikampa akaikagua huku akiuliza ninafanya kazi gani Tanzania, na huko nilikotoka nilienda kufanya nini. Kwangu mimi alikuwa mmoja tu peke yake, na hakushughulika na mizigo yangu zaidi ya passport na maswali, then akaniruhusu. Kuna haja ya kujua hawa watu wanafanya kazi kwa ajili ya ofisi gani.
 
Back
Top Bottom