Kashfa IMMIGRATION Dar Airport

Tatizo Nchi yetu maskini, Mtu akipewa kazi anataka kula hapo hapo badala ya kufanya kazi aliyopewa..!! Kufungua mabegi ya watu ni tabia mbaya. Naeleza hili ili wajifunze kama hawakupata fundisho..

Mwaka Jana wakati natoka safari nikiwa hapo DIA alitokea dada mmoja wa kizungu na mizigo yake bahati mbaya wakamsimamisha na kumwomba afungue begi ili watazame mizigo aliyobeba. Huyu Dada Mmarekani alikuwa mkali kweli..Akamwambia jamaa kama unataka kufungua begi langu nenda kaoge kwanza ndipo nitakufungulia begi kwasababu hapa ndani kuna joto sana na najua unatoka jasho ambalo ni uchafu na sitaki vitu vyangu vichafuke...!!! Amini wale jamaa ilibidi wamwambie yule dada atoke tu..!!!

Sasa tabia za jinsi hii ni mbaya.. Naamini kabisa hawa watu wanayo haki ya kufanya hivyo pale tu wanapo kuwa na mashaka na mizigo uliyo beba!! Na hili halimaanishi kwamba kila mzigo uliyo bebwa na mtu mweusi una magendo au vitu vyenye kupaswa kulipia ushuru!!
Sipati kuamini na joto la Dar salaam mtu akusimamishe zaidi ya nusu saa kwenye ule mjengo usio na A/C , Na hii tabia ya kushika shika chupi za watu na mikono michafu kwa kweli ni mbaya ,Maana hawa watu wa Air port ni wachafu sana na sijui hata kama wananawaga mikono wakitoka maliwatoni !! Tabia ya kupenda rushwa na kusumbuana kwa vitu vidogo vidogo lazima ikemewe!!!
 
Ni kweli kua kuna matatizo dsm airport lakini tunapozungumzia suala hili lazima tujue tunazungumzia idara gani, zipo nyingi pale
kuna uhamiaji, immigration. Hawa wanahusika kuangalia kuwa wasafiri wanaoingia wana uhalali wa kuingia. Dili zao kubwa ni kuingiza wachina, wahindi na wasomali wasio na makaratasi rasmi
Halafu kuna watu wa ushuru, customs. Hawa kazi yao ni kutoza ushuru pale inapostahili. Dili zao kubwa ni kusaidia watu kukwepa ushuru.
Kisha kuna askari polisi wa madawa ya kulevya, mara nyingi hawavai sare. Kazi yao kubwa ni kukamata watu wa madawa ya kulevya na vitu vingine vya hatari. Dili zao zinafahamika.
Halafu kuna polisi anti terrorism, nao hawavai sare. Hawa hawana dili, kazi ni kuharasi wasafiri ili wapate kitu kidogo
kuna pia polisi wa kawaida wanaoangalia usalama wa jumla. Wako wa sare na wasio na sare. Hawa dili yao ni kusumbua wasafiri mwanzo mwisho.
 
Ni kweli hao watu wapo wanachukua passport na saa nyingine wanajiita kua wanaangalia madawa ya kulevywa. Wanasumbua sana wengi hawako prefssional na hata kama ni kweli wameamrizhwa kufanya hivyo lakin the manner wanavyofanya inaonekana kama uhuni fulani unaweza kudhani labda wana chuki na watu wa mavazi fulani.

Ukivaa suti poa lakini ukivaa kinyamwezi sidhani kama utapita pale. Sasa hilo pekeyake linaweza kubeba kesi ya ubaguzi kati ya passenger. Ni wasumbufu kupita maelezo ukizingatia abiria ametoka mbali saa nyingine amechoka, wengi anafuraha kua ninarudi nyumbani kwahiyo siwezi kunyanyaswa tena, baya zaidi familia yake imekuja kumpokea na ktk wanaompokea yuko baba mkwe au mama mkwe. Kwakweli inachanganya sana
 
Invisible kaamua kuhamisha thread toka kwenye siasa kwani anataka kuendelea kuficha ufisadi wa wale wapuuzi mlangoni

kweli tanzania tuna safari ndefu

sasa jf ina kampeni nini?

Lowassa na chadema wachukue nchi?

Acheni hizo nyie

hamuwezi kuwa pressure group huku mnawapepea akina mahingila na nundu
 
Hapa unajaribu kujibu nini?, mimi ni shuhuda, nilishahojiwa deatail za safari yangu baada ya kumlizana na migration na customs, huyu aliyenihoji hakukuwa na ID yoyote, so, usibishe-pale mlangoni(kwa ndani) kuna maofisa huwa wanakaa na kuchunguza PP.
Jamani unapoingia Airport Dar (Wageni wanaowasili kutoka nje) na kwenda nje (Uraiani) si kweli kwamba Immigration officers wanakuwa karibu na mlango wa kutoka huu ni uongo. Wanaokuwa karibu na mlango wa kutokea ni Custom officers ambao wao ndio huwa wanapekua ulichobeba. Lawama hapa ni za nani Customs au immigration?

Immigration kama wana swala na wewe utamalizana nao hata kabla ya kwenda kwenye mzigo wako.

Maswala mengine ni ulalamishi usiokuwa na msingi.

GT where are the facts?
 
safi sana. Kwanza jamaa ni mkorofi sana na anasema alipokaguliwa akaambiwa alipie kodi na akakataa, alipotoka ndio akakutana na hao jamaa. Hivi kama una kitu cha thamani kubwa hutakiwi kukilipia kodi kwa kuwa unaenda kutumia nyumbani? Pia kuhojiwa ulikuwa wapi na kwa shughuli ipi ni jambo la kawaida kabisa katika masuala ya usalama hata kama wewe ni mtanzania. mwenzetu, kukaguliwa nalo ni sahihi kabisa...na kwa taafifa yake ni kwamba Watanzania ndio tunaoongoza kwa ugaidi hapa A.mashariki, aliyelipua ubaloz wa Dar na juzi hapo Kampala ni watanzania, so tuwe wavumilivu kwa ajili ya usalama wa nchi yetu na si kutoa lawama kwa idara fulani.
 
Huu nadhani ni mwaka wa nne tangu tumekuwa tukizungumza na kutoa maoni kuhusu kadhia wanayopata wageni wanaoingia Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam DIA.

Sasa hebu someni hapo chini: hii nimeikuta Michuzi blog:

Nadhani its about time tukaacha kuongea na kuanza kuwataja kwa majina hawa jamaa.

Kwa kuanza nadhani ni muhimu tukajua Head of Immigration pale Airport ni nani? na anasemaje kuhusu malalamiko haya?

Wa pili ambaye anatakiwa kujibu hizi tuhuma ni Meneja wa Airport kwani pamoja na kuwa ni kituo cha kupokea wageni mbali mbali

1. CUSTOMER SERVICE pale ni poor na inatia kinyaaa kwanza wafanyakazi ni wajeuri na nishaona wanawafokea wageni bila sababu za msingi.

2. USAFI na UCHAFU wa mwili umeziachafu na wananuka jasho, pili whats so difficult kutengeneza escalators za kupanda kwenda juu na kushuka??

3. UCHAFU wa JENGO: Sijapata kuona International Airport iliyochafu kama ya Dar na kama imeshindikana yale matandabui yaliojazana mle nayo kazi kuondoa? yapo makampuni ya usafi left and right je wameshindwa hata kuwapa tenda ya kufanya usafi? maana wenyewe ndio weshashindwa.

4. CONGESTION: halafu aibu kubwa nyingine ni ile idara ya visa ambayo kusema kweli ule msomangano wa wale wageni kujaza form za visa unatisha na if anything ni kinyume cha health and safety.

5. IMMIGRATION: Its obvious wako understaffed na wako stressed na bila kusahau hawana vifaa vya kufanyia kazi. Lakini hiyo si sababu ya kujaza watu ambao wanapotezea wageni muda pale nje...hivi kuweka watu 8 baada ya customs kuuliza wageni maswali ni nini? I mean mtu keshamalizana na Immigration kisha keshamaliza na Cutoms kwa nini anakutana na watu ambao wanaficha vitambulisho huku wanajiita Immigration officials

6. JOTO: hivi how hard is it kutengeneza air condition mle ndani? kwa nini utawala wa DIA unawatesa watu kweli ile hali iliyo kama TANURI?

7.BAG BELTS MBOVU: I can live with the fact kuwa best labda mota imechakaa lakini ile sehemu inayotokea mzigo kwenye ukuta yaani ni CHAFU mpaka mtu unaogopa

Mwisho napenda kuwaomba waende kutembelea Airport ya Nairobi au Kigali waone wenzao wanavyofanya kazi kwa ufanisi.

Hapo hamna jambo lolote baya ulilofanyiwa zaidi ya kutaka kupondea tu. Kukaguliwa ni wajibu na kama ulivyobeba vina thamani kubwa lazima ulipe kodi hata kama unatumia nyumbani kwako na suala la matumizi binafsi au biashara ni lako, wewe lipia kodi. Kuhojiwa na maafisa walioficha vitambulisho ni cmpo 2, ulitakiwa kuwaambia nipelekeni ktk ofis yenu then ntawajibu maswali yenu au mnioneshe vitambulisho hapa nitawajibu. Lakini kujifanya kwako machinoo na ubabe koko wako ndio maana ukakoromewa. Tumia busara uheshimiwe brazaa.
 
Hapo kwenye joto,usiombe ufike muda mmoja na wanaotoka kuhiji,msongamano kwenye kusubiri mizigo,unaweza ukalia
 
Je na wale nchi jirani wanaoshukia hapo DIA na wenyewe inakuwaje??Maana na wenyewe wanasumbuliwa sana,Mfano kuna jamaa mmoja yeye kwao ni Uganda na yeye alikuwa anatokea Sweden kwa hiyo alikuwa anatumia Travel Document ya Sweden ambayo ni ya miaka 5 na anaruhusiwa kuishi kwenye hiyo nchi ya Sweden maishani yake yote,Sasa kwenye Pass yake ya Travel Document wameandika kwamba haruhusiwi kuingia Uganda,Sasa je inakuwaje mtu kama huyo anakuja kwenye nchi alafu anasumbuliwa na kuambiwa kwamba usipotoa hela tutakupeleka kwenye nchi yako ya Uganda ni kwa nini?Au kwa nini asumbuliwe kupewa Visa na aanza kuhojiwa maswali mengi?Kwanza hao Home office wana mamlaka hayo kuingilia Personal za watu??Au inakuwaje hapo??Au ndio usipotoa Rushwa ndio huna haki zaidi??

Jamani tuwe wawazi kidogo, hao Immigration wamefunzwa kitu Passenger Profiling, sasa wewe huna hata begi unasema utakaa miezi 3, ukiulizwa utafikia wapi, unasema Kempisky, hapo lazma maswali yatazidi kumiminika. Na huyo mswidish wa kuchovya inawezekana hatakiwi Uganda alifanya uhaini dhidi ya M7..na kuhojiwa maswali mengi ni kuhakikisha Tz haiwi uchochoro wa kupitisha mahaini kudhuru majirani zetu. Jiulize kwa nini hatakiwi kwao sie ndo tumkaribishe? Kama aliombwa rushwa hapo Maafisa walikosea. Nawasilisha
 
nilikutana pia na hawa watu pale airport siku niliyotua,kwa jinsi walivyonishupalia nimebeba madawa mpaka nikashangaa,mwisho waliishia kunipoora fedha baada ya kunisachi maana sikuwapa.baada ya kuchukua euro hizo ndio wakaanza kunibembeleza nikubali tu kuondoka ili wasinicheleweshe zaidi.hasira nilizotoka nazo pale airport zilinisababishia ajali mbaya siku hiyo hiyo usiku.nilijuta kuwa mtanzania.
Naandaa full story
 
sema uliwapa wakuachie bana. Ulikubali kuwaachia hivyo viyuro vyako kwa nini kama ww sio haramia?
 
Huu nadhani ni mwaka wa nne tangu tumekuwa tukizungumza na kutoa maoni kuhusu kadhia wanayopata wageni wanaoingia Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam DIA.

Sasa hebu someni hapo chini: hii nimeikuta Michuzi blog:

Nadhani its about time tukaacha kuongea na kuanza kuwataja kwa majina hawa jamaa.

Kwa kuanza nadhani ni muhimu tukajua Head of Immigration pale Airport ni nani? na anasemaje kuhusu malalamiko haya?

Wa pili ambaye anatakiwa kujibu hizi tuhuma ni Meneja wa Airport kwani pamoja na kuwa ni kituo cha kupokea wageni mbali mbali

1. CUSTOMER SERVICE pale ni poor na inatia kinyaaa kwanza wafanyakazi ni wajeuri na nishaona wanawafokea wageni bila sababu za msingi.

2. USAFI na UCHAFU wa mwili umeziachafu na wananuka jasho, pili whats so difficult kutengeneza escalators za kupanda kwenda juu na kushuka??

3. UCHAFU wa JENGO: Sijapata kuona International Airport iliyochafu kama ya Dar na kama imeshindikana yale matandabui yaliojazana mle nayo kazi kuondoa? yapo makampuni ya usafi left and right je wameshindwa hata kuwapa tenda ya kufanya usafi? maana wenyewe ndio weshashindwa.

4. CONGESTION: halafu aibu kubwa nyingine ni ile idara ya visa ambayo kusema kweli ule msomangano wa wale wageni kujaza form za visa unatisha na if anything ni kinyume cha health and safety.

5. IMMIGRATION: Its obvious wako understaffed na wako stressed na bila kusahau hawana vifaa vya kufanyia kazi. Lakini hiyo si sababu ya kujaza watu ambao wanapotezea wageni muda pale nje...hivi kuweka watu 8 baada ya customs kuuliza wageni maswali ni nini? I mean mtu keshamalizana na Immigration kisha keshamaliza na Cutoms kwa nini anakutana na watu ambao wanaficha vitambulisho huku wanajiita Immigration officials

6. JOTO: hivi how hard is it kutengeneza air condition mle ndani? kwa nini utawala wa DIA unawatesa watu kweli ile hali iliyo kama TANURI?

7.BAG BELTS MBOVU: I can live with the fact kuwa best labda mota imechakaa lakini ile sehemu inayotokea mzigo kwenye ukuta yaani ni CHAFU mpaka mtu unaogopa

Mwisho napenda kuwaomba waende kutembelea Airport ya Nairobi au Kigali waone wenzao wanavyofanya kazi kwa ufanisi.

Hakuna mahali pa kijinga kama DIA. Nilikuwa napanda Emirates wakati fulani eti uhamiaji mmoja anaiytwa Mbise kanisimamisha na kunitoa nje ya mstari. Unakwenda wapi? Nikamwambia naenda nchi ambayo hata wewe huwezi ukaingia na uofisaa wako. Nchi gani hiyo? nikamwambia hivi ulijifunza shuleni au vp? mbona maswali ya kijinga si usome pass na visa ni ya wapi?

Baada ya mwaka nikashuka na kumkuta hayupo nikaulizia manyoka wake wakasema shifti siyo yake leo. Nikaacha ujumbe kuwa nilitaka nimkute nimweleze mambo yake na kumwonyesha mambo fulani.

Pole sana ndugu hapo Dar mimi sipiti tena naingia nairobi hata KIA mara chache sana.
 
huu nadhani ni mwaka wa nne tangu tumekuwa tukizungumza na kutoa maoni kuhusu kadhia wanayopata wageni wanaoingia uwanja wa ndege wa dar es salaam dia.

Sasa hebu someni hapo chini: Hii nimeikuta michuzi blog:

Nadhani its about time tukaacha kuongea na kuanza kuwataja kwa majina hawa jamaa.

Kwa kuanza nadhani ni muhimu tukajua head of immigration pale airport ni nani? Na anasemaje kuhusu malalamiko haya?

Wa pili ambaye anatakiwa kujibu hizi tuhuma ni meneja wa airport kwani pamoja na kuwa ni kituo cha kupokea wageni mbali mbali

1. Customer service pale ni poor na inatia kinyaaa kwanza wafanyakazi ni wajeuri na nishaona wanawafokea wageni bila sababu za msingi.

2. Usafi na uchafu wa mwili umeziachafu na wananuka jasho, pili whats so difficult kutengeneza escalators za kupanda kwenda juu na kushuka??

3. Uchafu wa jengo: Sijapata kuona international airport iliyochafu kama ya dar na kama imeshindikana yale matandabui yaliojazana mle nayo kazi kuondoa? Yapo makampuni ya usafi left and right je wameshindwa hata kuwapa tenda ya kufanya usafi? Maana wenyewe ndio weshashindwa.

4. Congestion: Halafu aibu kubwa nyingine ni ile idara ya visa ambayo kusema kweli ule msomangano wa wale wageni kujaza form za visa unatisha na if anything ni kinyume cha health and safety.

5. Immigration: Its obvious wako understaffed na wako stressed na bila kusahau hawana vifaa vya kufanyia kazi. Lakini hiyo si sababu ya kujaza watu ambao wanapotezea wageni muda pale nje...hivi kuweka watu 8 baada ya customs kuuliza wageni maswali ni nini? I mean mtu keshamalizana na immigration kisha keshamaliza na cutoms kwa nini anakutana na watu ambao wanaficha vitambulisho huku wanajiita immigration officials

6. Joto: Hivi how hard is it kutengeneza air condition mle ndani? Kwa nini utawala wa dia unawatesa watu kweli ile hali iliyo kama tanuri?

7.bag belts mbovu: I can live with the fact kuwa best labda mota imechakaa lakini ile sehemu inayotokea mzigo kwenye ukuta yaani ni chafu mpaka mtu unaogopa

mwisho napenda kuwaomba waende kutembelea airport ya nairobi au kigali waone wenzao wanavyofanya kazi kwa ufanisi.

wapendwa katika bwana bwana yesu asifiwe

samahani nimesoma mpaka mwisho wa nukta naona ni vyema ukaandika mada anyingine ya kuwataka radhi immigration..kuanzia ulichoandika hadi nukta akuna sehemu immigration inahusika kwa minajili ifutayo

1...walikwambia ufungue mabegi hata kama ni nguo za hawara yako hao sio immigration wanaitwa customs
hawa ni kwa ajili ya wakwepa kodi ya serikali ya jamhuri ya kikwete..sasa basi wako pale kuhakiki kama unaleta vitu na kupita bila kutoa ama kulipa ushuhuru...ni haki yao kukufungua na mbaya zaidi kama walikusitiri wakihisi umeficha mzigo kwenye sehemu za siri wana chumba wanakuelekeza na unavua mpwa sikufichi

2..waliokuuliza passport ni usalama wa taifa wao wako kwa ajili ya kulinda usalama wa serikali na uwanja pia so sio kila mtanzania anaepita toka nje amekuja na mema ndio maana kuna watanzania wamekamatwa somalia wakienda kujiunga na alshabab..so wana haki ya kukuliza umetoka wapi umepita kwa nani na mengineyo

sijaona kosa lao mbaya zaidi nikusaidie hayo chini ulioyaandika yanahusu uwanja wa ndege na mamlka nzima ya uwanja yakiongozwa na taa..hawa ndio wadau wakubwa wa malalamiko yako

neno msamaha ni gumu sana lakini ni garama sana mwisho wa siku hasa kwenye hukumu ya mwisho si haba kuomba msamaha kwa kuwazalilisha ndugu zetu wa immigrwtaion ingawa wana matatizo yao binafsi
 
ni kweli kua kuna matatizo dsm airport lakini tunapozungumzia suala hili lazima tujue tunazungumzia idara gani, zipo nyingi pale
kuna uhamiaji, immigration. Hawa wanahusika kuangalia kuwa wasafiri wanaoingia wana uhalali wa kuingia. Dili zao kubwa ni kuingiza wachina, wahindi na wasomali wasio na makaratasi rasmi
halafu kuna watu wa ushuru, customs. Hawa kazi yao ni kutoza ushuru pale inapostahili. Dili zao kubwa ni kusaidia watu kukwepa ushuru.
Kisha kuna askari polisi wa madawa ya kulevya, mara nyingi hawavai sare. Kazi yao kubwa ni kukamata watu wa madawa ya kulevya na vitu vingine vya hatari. Dili zao zinafahamika.
Halafu kuna polisi anti terrorism, nao hawavai sare. Hawa hawana dili, kazi ni kuharasi wasafiri ili wapate kitu kidogo
kuna pia polisi wa kawaida wanaoangalia usalama wa jumla. Wako wa sare na wasio na sare. Hawa dili yao ni kusumbua wasafiri mwanzo mwisho.

umesahau wa pakistan wa kule mikocheni viwanda vya wahindi
naomba waniwie radhi kuwakumbusha
 
Tusilalamike sana. Kuhusu miundombinu ya uwanja ni kweli sehemu kadhaa ni mbovu na zinatakiwa marekebisho. Lakini kuhusu tight security nami naunga mkono vyombo vyetu vya usalama pale Airport. Kuna wakati Dar Airport ndio palikuwa njia kuu ya kupitishia kila takataka. Kwa sasa wamebanwa,wanatumia njia za barabara. Nawe unayesema ni vitu binafsi ulikuwa umebeba, inategemea ni bidhaa gani ulikuwa umebeba. Si kila private belongings huwa hazilipiwi kodi!.
 
mimi nilikutana na watu wao mlangoni baada ya kuchukua begi langu. nilitoka Nairobi na precision air mwezi wa saba 2011, jamaa akaniambia tuone passport yako nikamuuliza we nani? maana me nimegonga migration na nimeruhusiwa, akasema ooh tunakagua, hata nyumbani kwako twaeza kuja kupekua, mtu mwenyewe alikuwa haeleweki. kwa hili ni kero!..... Management ya Airport JKIA lazima itolee ufafanuzi wa kinachoendelea.

shame on them!...
 
kila mahali ktk nchi hii sasa ni blaaa, tunataka serekali ya wananchi sio mkuu wa nchi ni jeshi mkuu wa mkoa naye jeshi mkuu wa wilaya nae jeshi?
 
Back
Top Bottom