Geti la Airport lliivunjwa wakati wananchi wakitaka kumuaga Hayati Magufuli

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,126
22,619
Salaam, Shalom,

Baada ya tarehe 17 march 2021, Mh Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo Cha HAYATI Magufuli, Nchi ilizizima.

Binafsi, nilikuwa naendelea kufuatilia tetesi za kifo hicho baada ya taarifa nyingi kusambaa kutokana na ufinyu wa taarifa sahihi. Ilipothibitishwa taarifa hiyo, simanzi ilianza Rasmi.

Ilipowadia siku ya kusafirisha mwili baada ya kuaga pale uhuru, safari ya kuelekea Airport ilianza, mwili ulikuwa unapelekwa Airport Ili uende Zanzibar, Kisha Mwanza, kisha Chato Kwa maziko.

Wananchi sijui waliingiwa na nini, jamani sijui nini kiliwapata vijana wale baada ya kuambiwa kuwa hawaruhusiwi kuingia ndani ya uwanja wa ndege wa Dar Kwa sababu za kiusalama.

Nilichokishuhudia kwa muda mfupi ni uwanja wa ndege kujaa vijana wengi sana na hakuna aliyeweza kuwazuia, walikuwa wamelivunja gate Kwa sekunde chache Kisha kujaa ndani ya runways za airport na ndani ya uwanja wa ndege!

Kila mahala ulipopitishwa mwili wa HAYATI Magu, wananchi walitaka waone Kwa macho ndipo waamini Kweli Magu ameenda.

Niliona kijana mmoja akikimbiza jeneza lile, na alikiambia Kwa umbali mrefu sana, nilijiuliza Kwa jinsi chato kulivyo mbali, kijana yule asingeweza kufika Kwa kukimbia Kwa miguu. Ni kama aliona, tumaini na Imani alivyokuwa nayo kupitia kwa kiongozi wake linaondoka mbele ya macho yake😪

Nililia Kwa huzuni kuu, ndipo nikajua kuwa KAZI ya mtu Huwa inamfuata na kupaza sauti.

Alipofariki Mwl Nyerere, nilishuhudia vilio vile vya wananchi. Tofauti na msiba wa Mwl Nyerere na Magufuli ni kuwa Magufuli alifariki akiwa madarakani na ndoto alizopanga kuzitimiza hakuwa amekamilisha.

Asikwambie mtu, Nchi kuondolewa na Rais aliyepo madarakani, uchungu na taharuki Kwa wananchi Huwa haielezeki.

Taifa lilivuka salama katika msiba Ule, na hiyo ni Ishara kuwa Mungu anaipenda sana Nchi yetu.

Ahsante Mungu Kwa zawadi ya Rais na HAYATI Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen
 
Salaam, Shalom,

Baada ya tarehe 17 march 2021, Mh Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo Cha HAYATI Magufuli, Nchi ilizizima,

Binafsi, nilikuwa naendelea kufuatilia tetesi za kifo hicho baada ya taarifa nyingi kusambaa kutokana na ufinyu wa taarifa sahihi. Ilipothibitishwa taarifa hiyo, simanzi ilianza.
Sio poa
 
Jiwe kishakufa. Tena alikufa kizembe sana. Hata muandike mpk server ya jamiiforums ijae hafufuki.

Acheni uwongo. Watanzania kila Kona ya nchi walitaka kuchinja mbuzi ili kufurahia kifo cha dikteta jiwe lkn polisi wakaanza kuwakamata.
 
Hao waliochinja mbuzi kusherehekea kifo Cha mzalendo Magu, walifanya Kwa kificho.

Na TABIA hii ya kushangilia kifo Cha mtu afapo Si ya Watanzania.
 
Salaam, Shalom,

Baada ya tarehe 17 march 2021, Mh Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo Cha HAYATI Magufuli, Nchi ilizizima,

Binafsi, nilikuwa naendelea kufuatilia tetesi za kifo hicho baada ya taarifa nyingi kusambaa kutokana na ufinyu wa taarifa sahihi. Ilipothibitishwa taarifa hiyo, simanzi ilianza.

Ilipowadia siku ya kusafirisha mwili baada ya kuaga pale uhuru, safari ya kuelekea airport ilianza, mwili ulikuwa unapelekwa Airport Ili uende Zanzibar, Kisha Mwanza, kisha Chato Kwa maziko.

Wananchi sijui waliingiwa na nini, jamani sijui nini kiliwapata vijana wale baada ya kuambiwa kuwa hawaruhusiwi kuingia ndani ya uwanja wa ndege wa Dar Kwa sababu za kiusalama.

Nilichokishuhudia Kwa muda mfupi ni uwanja wa ndege kujaa vigana wengi sana na hakuna aliyeweza kuwazuia, Nchi ilizizima.

Kila mahala ulipopitishwa mwili wa HAYATI Magu, wananchi walitaka waone Kwa macho ndipo waamini Kweli Magu ameenda.

Niliona kijana mmoja akikimbiza jeneza lile, na alikiambia Kwa umbali mrefu sana, nilijiuliza Kwa jinsi chato kulivuo mbali, kijana yule asingeweza kufika Kwa kukimbia Kwa miguu.

Nililia Kwa huzuni kuu, ndipo nikajua kuwa KAZI ya mtu Huwa inamfuata na kupaza sauti.

Alipofariki Mwl Nyerere, nilishuhudia vilio vile vya wananchi. Tofauti na msiba wa Mwl Nyerere na Magufuli ni kuwa Magufuli alifariki akiwa madarakani na ndoto alizopanga kuzitimiza hakuwa amekamilisha.

Asikwambie mtu, Nchi kuondolewa na Rais aliyepo madarakani, uchungu na taharuki Kwa wananchi Huwa haielezeki.

Taifa lilivuka salama katika msiba Ule, na hiyo ni Ishara kuwa Mungu anaipenda sana Nchi yetu.

Ahsante Mungu Kwa zawadi ya Rais na HAYATI Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen
Kifo Huwa ni kiboko ya wababe,majeuri na wenye viburi wote.

Kifo kiheshimiwe.Na waswahilo husema ngoma ikivuma sana hupasuka.
 
Leo ni kumbukumbu,

Picha Ile inajirudia kichwani.

Tuvumiliane tu🙏
Leo kumbukumbu nyingi mbaya na nzuri zinapita vichwani mwa watanzania. Wapo wanaokumbuka baba zao na kaka zao waliouwawa kinyama katika uongozi wa hayati magufuli, wapo wanaokumbuka nafasi zao walizopoteza baada ya magufuli kufariki, wapo waliopoteza kazi zao wakati wa hayati magufuli nao wana kumbukumbu mbaya, wapo wanaokumbuka kasi ya maendeleo wakati wa awamu ya 5 nao wanaomboleza. Kwahiyo naungana na wewe Tuvumiliane wote ambao kila mmoja anakumbuka alivyoguswa na marehemu iwe kwa ubaya au kwa uzuri.
 
Yale mema na maono yake ni vyema Yaenziwe. pia ina staajabisha sana kuona wale waliokuwa wakikosoa Baadhi ya mambo yake mfano waliosema alimiliki kampuni za kandarasi na kujipa kazi wao wakifanya yaliyosawa wakati Huu naona Hawata kaa salama.

Sanjari na waliokuwa wakimshutumu kwa Ubadhirifu na Ufisadi.

Kwa kuwa Haki inakata pande zote sio moja.

Ni hayo tu.
 
Jiwe kishakufa. Tena alikufa kizembe sana. Hata muandike mpk server ya jamiiforums ijae hafufuki.

Acheni uwongo. Watanzania kila Kona ya nchi walitaka kuchinja mbuzi ili kufurahia kifo cha dikteta jiwe lkn polisi wakaanza kuwakamata.
mh!
 
Leo kumbukumbu nyingi mbaya na nzuri zinapita vichwani mwa watanzania. Wapo wanaokumbuka baba zao na kaka zao waliouwawa kinyama katika uongozi wa hayati magufuli, wapo wanaokumbuka nafasi zao walizopoteza baada ya magufuli kufariki, wapo waliopoteza kazi zao wakati wa hayati magufuli nao wana kumbukumbu mbaya, wapo wanaokumbuka kasi ya maendeleo wakati wa awamu ya 5 nao wanaomboleza. Kwahiyo naungana na wewe Tuvumiliane wote ambao kila mmoja anakumbuka alivyoguswa na marehemu iwe kwa ubaya au kwa uzuri.
Ungana na Mdude kwenye Uzi Ule kukumbuka hayo.

Uzi huu unakumbuka jinsi Watanzania walivyopata taharuki kumuaga Magufuli.

Tuvumiliane🙏
 
Back
Top Bottom