Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
najiuliza sina jibu, je kama kweli karume hakuwa na mchango wowote katika mapinduzi ya zanzibar kama baadhi ya post zinavyoashiria, ilikuwaje akaweza kumuondoa okello bila resistance kubwa kutoka kwa waliomuunga mkono okello? kwani kwa kuongoza mapinduzi kwenye "field" nina hakika alikuwa anao watu ambao walikuwa tayari kupoteza maisha yao kwa kumuunga mkono yeye. kwani nijuavyo mimi "bond" inayojengeka katika uwanja wa vita ni kubwa sana.
Kuna mambo inabidi uyaelewe. Kwanza, pamoja na Okelo kuunda serikali na kumteua Raisi Karume na baraza la mawaziri, hiyo serikali bado iliwajibika kwake. Neno lake lilikuwa la mwisho na yeyote ambaye hakutii, alishughulikiwa. Kwa mfano, Januari 13,1964, alitoa ujumbe huu kwenye redio:
Huu ulikuwa utawala wa kijeshi ambao haukuvumilia aina yoyote ya uasi. Januari 14, 1964 aliposikia kuna watu sehemu iliyoitwa Mtendeni, wanalalamikia sheria za ukandamizaji alitoa tangazo hili:The government is now run by us....should you be stubborn and disobey orders I will take measures 88 times stronger than at present." and, "If anyone fails to comply... and locks himself in a house, as others have done...I have no alternative but to use heavy weapons. We, the army have the strength of 99,099,000.
Huyo ndiye Okelo, aliogopwa labda zaidi ya Idi Amin wa Uganda baadaye na tamko lake lilikuwa kama sheria. Hakuna Mzanzibari aliyeweza kukohoa mbele ya Okelo. Kufanikiwa kwa haya mapinduzi kulileta hali ya hofu kubwa kwa serikali zote tatu za Afrika Mashariki Tanganyika, Kenya na Uganda. Hata hivyo Okelo alimheshimu sana kiongozi wa Tanganyika na hata alipopewa mwaliko kuja Dar es Salaam alikubali bila wasiwasi.Here is the Field Marshall of Zanzibar and Pemba....I am thinking of going to Mtendeni (village) to destroy it if the people there do not obey orders. After 40 minutes I am coming to finish you off, especially the Comorians". And "To all Arab youths living in Malindi; I will pass through Malindi armed with weapons of which I alone know. I want to see everyone stripped to his underpants and laying down. I want to hear them singing...father of Africans. God bless him in his task and that of the Field Marshall."
Hapa anaonekana Field Marshall wa Zanzibar na Pemba John G. Okelo siku alipofika Dar es Salaam
Kitu ambacho hakukijua ni kuwa huu ulikuwa ni mpango wa kumkamata na moja wa wasaliti wake ni Abeid Karume aliyeteuliwa Raisi lakini asiye na madaraka ya mwisho. Haya ndiyo nayaita mapinduzi ndani ya mapinduzi. Bila Tanganyika Zanzibar haingekuwa Zanzibar tunayoiona leo kwani juhudi kubwa ilibidi zifanyike kuifuta historia ya Okelo hadi kitabu alichoandika kupigwa marufuku ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Field Marshall wa Zanzibar na Pemba John G. Okelo alitisha ati.