Mzee Baraka - CCM IMESALITI, NIA NA SABABU ZA MAPINDUZI MATUKUFU YA 1964
View: https://m.youtube.com/watch?v=habiWXzPxFM
Mzee Baraka Shamte mwenye umri wa miaka 94 aliye na afya njema, katika mahojiano exclusive na Jambo TV akikumbuka mapinduzi matukufu na uongozi wa Mzee Abeid Amani Karume wa kuanzia 1964 hadi 1972 Mzee Karume alipouawa na wapinga mapinduzi ya makabwela, Mzee Baraka analia kwa uchungu na kutema nyongo kuhusu waliochukua madaraka ndani ya CCM sasa hawajali wanyonge kama serikali ya Mzee Abeid Karume
Mzee Baraka Shamte akiangalia nyuma mbali, anajiuliza vipi hakuna Kumbukizi ya Mzee Abeid Karume kama ilivyo Kumbukizi ya Mwl. Julius Nyerere kupitia Taasisi ya Mwalimu Nyerere kila mwaka kuendeshwa kwa makongamano yenye kuufanyia tathmini utawala wa Nyerere lakini kwa Zanzibar wamemtupa kiongozi wa mapinduzi ya 1964...
Mwanamapinduzi Mzee Baraka anasema kukosekana kwa kumbukizi ya Abeid Karume ni mwendelezo wa wapinga mapinduzi kwani wamefikia hadi kuuvunja uwanja wa Amani Karume ambao ni moja ya kumbukumbu nyingi wazee wanamapinduzi walio hai walikuwa wanavienzi kwa wivu mkubwa mzuri sasa kiwanja kimebomolewa, wakati wangeweza kujenga kiwanja cha kisasa chengine huku wakibakiza kumbukumbu mojawapo kubwa ya muasisi wa Zanzibar huru.
Mzee Baraka anakazia kuwa badala ya kuwakaribisha wanamapinduzi waliokuwepo wakati wa mapinduzi ya 1964 kuzungumzia hali ya siasa Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi, sasa wanaalika watoto wadogo kusoma historia kutokana na mabuku yaliyochakachuliwa badala ya kualika watu kama yeye walioishi katika kipindi halisi.
Mzee Baraka Shamte anaendelea kuelezea hujuma kibao dhidi ya wananchi wa Zanzibar zinazofanywa na viongozi walafi wa CCM wanaoshirikiana na wapinga mapinduzi ndani ya Tanzania na nje ....
Mzee Baraka anaongeza tuliungoa utawala wa kisultani uliokuwa unarithishana uongozi kifalme na sasa utawala wa CCM nao umetumbukia ktk kurithishana uongozi kindugu pia kifamilia na mbaya hawataki mtu achukue fomu kugombea nafasi hadi mtu amalize miaka 10 ikulu wakati katiba inasema kila miaka 5 uchaguzi ufanyike ...
Mzee Baraka azidi kuanika hulka za kibwanyenye zinazozidi kukita ndani ya chama kongwe dola cha CCM ....